Tangazo

Pages

Sunday, August 28, 2011

ZABU JUDAH AGONGA MWAMBA KURUDIANA NA AMIR KHAN

LAS VEGAS, Marekani
MIPANGO ya Amir Khan imepata kizuizi, baada ya bonsia alipigana naye mara ya mwisho, Zab Judah kutoa malalamiko dhidi ya bondia huyo Mwingereza.

Judah analalamika alipigwa chini ya mkanda wakati katika pambano ambalo alipoteza mkanda wake wa ubingwa wa IBF uzani wa light-welter, ambapo Khan alishinda kwa KO katika raundi ya tano mjini Las Vegas.

Gazeti la The Sun limesema, promota wa Judah ambayo ni kampuni ya Main Events, imekata rufaa katika Kamisheni ya Michezo Nevada na imetuba barua pamoja na ushahidi wa video ya pambano hilo la kuwania ubingwa wa mataji ya WBA na IBF na inataka kamisheni kuamuru lirudiwe.

Timu ya Judah inadai kuwa refa Vic Drakulich alikuwa hakuona jinsi Khan alivyopiga ngumi chini ya kanda, ambapo alimtangaza kuwa ni mshindi kwa KO.

Timu hiyo imemtuhumu Khan kwa kucheza faulo nyingine katika mechi hiyo.

Rais wa Main Events, Kathy Duva alisema: " Kulikuwa na ngumi zilizokuwa zikipigwa nyuma ya kichwa na kukumbatia na  Amir Khan hakuonywa kwa hilo. Video haisemi uongo."

Khan amepanga kupigana na bondia mkongwe wa Mexico, Erik Morales Desemba 10 lakini Judah anatumaini kuwa pambano hilo litazuiwa.

No comments:

Post a Comment