Tangazo

Pages

Monday, October 31, 2011

FRANSIC MIYAYUSHO AMTWANGA MBWANA MATUMLA KWA POINT

 Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupa masumbwi na Mbwana Matumla wakati wa mpambano wao Dar es salaam jana
 Jab Jab akuna kulala fransic akipiga jab jab kila wakati ndicho kilicho mfanya ashinde mpambano huo jana


 Kamanda wa Polosi Kanda Maarumu, Suleimani Kova akimvisha mkanda wa Ubingwa Bondia Fransic Miyayusho baada ya kushinda kwa pointu kulia ni Diwani wa KInondoni Kata ya Hananasifu, Abasi Tarimba na kiongozi wa kambi ya ngumi ya kinondoni Lazima Ukae, meneja ambaye ni mkurugenzi wa Kisangani Genalar Trades ya Kariakoo,Bobani

Masumbwi mawe kwa kwenda mbele

Saturday, October 29, 2011

MATUMLA, MIYAYUSHO WAPIMA UZITO LEO KWA AJILI YA MPAMBANO KESHO

 Ramadhani Shauli akipima uzito kulia ni mpinzani wake Issa Sewe

 Mbwana Matumla akipima uzito kwa ajili ya mpambano kesho jumapili
Mabondia Fransic Miyayusho kushoto na Mbwana Matumla wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito leo

makocha wamekutana

Kocha wa mchezo wa ngumi Nchini, Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' (kushoto) akisalimiana na mchezaji wa zamani  Bryan Robson ambaye ni kocha wa mchezo wa mpira wa miguu walipokutana  wakati wa clinic ya  Airtel Rising Stars kushoto ni mwandishi mwani nyangasa

Thursday, October 27, 2011

VIPAJI MCHEZO WA NGUMI VINAINULIWA HIVIKocha mkongwe wa mchezo wa ngumi Habibu Kinyogoli akimwelekeza mtoto Salim Mponda (5) jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi ya klabu ya ngumi ya Amana Dar es salaam

Wednesday, October 26, 2011

FRANCIS MIYAYUSHO NA MBWANA MATUMLA WATAMBIANA MPAMBANO JUMAPILI


Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) na Mbwana Matumla wakitunishiana misuri mbele ya waandishi wa habari katikati ni Mohamedi Bawaziri mratibu wa mpambano huo.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Mratibu wa mpambano wa ngumi Mohamedi Bawaziri katikati akiwa na mkanda wa ubingwa utakaogombaniwa na mabondia Fadhili Majia (kushoto) na Juma Fundi siku ya jumapili.(Picha na Linkwww.superdboxingcoach.blogspot.com)

FRANCIS MIYAYUSHO NA MBWANA MATUMLA WATAMBIANA MPAMBANO JUMAPILI

Mkurugenzi wa Kampuni ya Darworld Links Ltd,Mohamed Bawazir ambaye ndiye muandaaji wa pambano la ubingwa wa UBO INTER-CONTINENTAL BANTAM WEIGHT,akizungumza mapema leo asubuhi kwenye moja ya ukumbi wa hotel ya JB BELMONTE HOTEL,jijini Dar kuhusiana na pambano hilo litakalokuwa la aina yake. Bawazir amesema kuwa pambano hilo litawahusisha mabondia Mbwana Matumla pichani kulia na Francis Miyayusho pichani shoto,ambalo linatarajiwa kufanyika Oktoba 30 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar,aidha katika mpambano huo wa kukata na shoka kiingilio kimepangwa kuwa kati ya 10,000 na 5000 kwa kila kichwa. Bawazir amesema kuwa katika pambano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Kamishna wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam,Kamanda Suleiman Kova.Mbali ya mpambano huo,Bawazir alitanabaisha kuwa pia kutakuwepo na mapambano mengine ya utangulizi likiwemo pambano la akina Dada Asha Abubakar 'ASha Ngedere' na Salma Kiombwa.'cheka wa Moro

Saturday, October 22, 2011

DEO NJIKU NA JONAS SEGU WATAMBIANA BAADA YA KUPIMA UZITO


Bondia deo Njiku akimtambia mpinzani wake Jonas Segu kwa kumonesha vidole vitatu na kusema atamtwanga katika raundi hiyo katikati ni Kocha wa Mchezo wa Ngumi Mhamila Rajabu 'Super D Boxing Choach'
kocha wa mchezo wa ngumi Nchini Rajabu Mhamila ' Super D Boxing Coach' katikat akiwainua mikono juu mabondia Deo Njiku wa Morogoro kushoto na Jonas Segu wa Dar es salaam baada ya kupima uzito katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro LEO kwa ajili ya mpambano wa kuwania ubingwa wa taifa wa Oganaizesheni ya ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) utakaofanyika KESHO.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)Thursday, October 20, 2011

FRANSIC MIYAYUSHO AJIANDAA KUMKABILI MBWANA MATUMLA

 Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi na Badi Sachedina wakati wa mazoezi ya mwisho ya Miyayusho kabla ya kumvaa Mbwana Matumla katika mpambano wao wa ubingwa mwishoni mwa mwezi huu.( Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)
 Bondia Fransic Miyayusho (kulia ) akiongoza mazoezi katika kambi yake ya lazima ukae iliyopo Kinondoni Dar es salaam jana Miyayusho anajiandaa na mpambano wake wa ubingwa na Mbwana Matumla litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu.( Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)
 miyayusho aje huyo matumla nimchape
Bondia Fransic Miyayusho (kushoto) akielekezwa jinsi ya kutupa masubwi na Doi Miyayusho wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wa kuwania ubingwa na Mbwana Matumla utakaofanyika mwishoni mwa mwezi huu.( Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)

VIPAJI VYA MCHEZO WA NGUMI VYAIBURIWA ILALA

 Bondia Mkongwe Rashidi Matumla akimwonesha kuwa mshindi bondia chipukizi baada ya kumdunda mwezie


 Vipaji vikioneshwa wakati wa mpambano katika ukumbi wa Panandi panandi Ilakla


Sunday, October 16, 2011

NGUMI KULINDIMA ILALA BUNGONI LEO MBUNGE WAKE KUSHUUDIA

Mbunge wa Ilala Mussa Zungu atashuudi
ZAIDI ya mabondia 42 wanatarajia kushiriki katika mashindano ya mchezo wa ngumi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba16 mwaka huu Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha wa Klabu ya Ashanti ya Ilala, Rajabu Mhamila, 'Super D' alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha Klabu 12 kutoka katika maeneo mbalimbali.

Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.

Super D alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuhendeleza kuhamasisha mchezo wa ngumi nchini ikiwa ni pamoja na muendelezo wa mchezo huo unanaofanywa na Kinyogoli Foundation.

“Tumeandaa mashindano ya ngumi ambayo yatashirikisha vijana mbalimbali na lengo letu ni kuhamasisha mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuuendeleza ili uweze kutuletea faida hapo baaye” alisema.

Kocha huyo alisema kuwa vijana watakaoshiriki watakuwa katika uzito mbalimbali kuanzia Unyoya mpaka uzito wa juu.

Alisema kuwa pia wanatarajia kushirikisha mabondia wa kike kutoka katika klabu hizo hizo Aliongeza kuwa katika mapambano hayo mgeni mwalikwa ni Mbunge wa Ilala Mussa Zungu ambaye kwa mara ya kwanza atangalia mchezo huo ukipigwa katika jimbo lake


Aliongeza kwa kusema kuwa wanaitaji wadau mbalimbali wajitokeze kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya vijana ikiwemo maji kwa ajili ya mchezo huo kwa siku hiyo wenye nia ya kutaka kusaidia au kushiliki kwa kuchangia chochote wanaweza kuja katika ukumbi wa mazoezi uliopo Amana Ilala au kufika Ashanti Boxingi clabu kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwa siliana na Kocha Mkongwe, Habibu Kinyogoli kwa simu 0655928298 au unaweza kuwasiliana na Super D Boxing Coach O713,0787-406938 Email.superdboxingcoach@gmail.com wadau mbalimbali mnakalibishwa

Saturday, October 15, 2011

NGUMI KUPIGWA ILALA KESHO MABONDIA WAKUMBUSHWA SHERIA


Kocha wa mchezo wa ngumi Habibu Kinyogoli akiwaelekeza vijana toka klab mbalimbali jinsi sheria za mchezo wa ngumi zinavyokua wawapo ulingoni michuano ya mchezo wa ngumi inatarajiwa kulindima kesho jumapili katika ukumbi wa panandi panandi Ilala Bungoni
Babondia wakiwa katika picha ya pamoja na makocha wao wakati wa upimaji wa uzito kabla ya kupambana kesho
upimaji wa uzito ukiendelea

Baadhi ya mabondia wakiwa makini kumsikiliza kocha wa mchezo wa ngumi wakati wa kupima na kuelekezwa sheria za mchezo wa ngumi

DEO NJIKU AJIFUA KUMKABILI JONAS SEGU WIKI IJAYO


Kocha wa Mchezo wa ngumi, Boma Kilangi (kushoto) akimsimamia mazoezi bondia Deo Njiku wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake wa ubingwa zidi ya Jonas Segu litakalofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro wiki ijao.(picha www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Deo Njiku akijifua kikamilifu