Tangazo

Pages

Monday, August 29, 2016

MABONDIA NASIBU RAMADHANII NA IDDI ATHUMANI WASAINI KUZIPIGA OCTOBER 9 MABIBO

Bondia Nassibu Ramadhani kushoto akitunishiana misuli na Iddi Athumani 'Mchina' baada ya kutiliana saini ya kupambana novemba 9 Mabibo Dar es salaam katikati ni Promota wa mpambano uho Abdallah Kamanyani Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Nassibu Ramadhani wa pili kushoto na Iddi Athumani kulia wakiwa na promota wao Abdallah Kamanyani katikati kushoto ni kocha wa Nassibu Cristopher Mzazi na wa pili kulia ni kocha wa Athumani Yusuph Komba Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Nassibu Ramadhani kushoto akitunishiana misuli na Iddi Athumani baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga novemba 9 mabibo Picha na SUPER D BOXING NEWS
IDDI ATHUMANI 'MCHINA'
NASSIBU RAMADHANI
Bondia Iddi Athumani 'Mchina' kushoto akitia saini ya kuzipiga na Nassibu Ramadhani OCTOBER  9 mabibo Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Nassibu Ramadhani akisaini Mkataba wa kuzipiga na Iddi Athumani 'Mchina' OCTOBER  9 mabibo

Friday, August 26, 2016

MABONDIA IDDI MKWELA NA HASHIMU CHISORA KUGOMBANIA UBINGWA WA TAIFA WA TPBC


Mabondia Hashimu Chisora kushoto akitunishiana misuli na Iddi Mkwela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubngwa wa raundi kumi  KG 61 utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa agost 27 jumamosi Katikati ni kiongozi Ally Bakari 'Champion' Picha na SUPER D BOXING NEWSMabondia Abdallah Zamba kushoto akitunishiana misuli na Twalibu Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Hashimu Chisora kushoto akitunishiana misuli na Iddi Mkwela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubngwa wa raundi kumi  KG 61 utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa agost 27 jumamosi  Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Mabondia wa kike Halima Bandola kushoto na Ester Kazabe wakitunishiana misuli kwa ajili ya mpambano wao kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa katikati ni Mwenyekiti wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa
Bondia Iddi Mkwela ajiojiwa na mtangazaji wa ITV Jimmy Tala baada ya kupima Uzito
IDDI MKWELA
Mwenyekiti wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa kushoto akizungumza na mabondia pamoja na makocha wao kufata talatibu za kumwandaa bondia pamoja na sheria zake wa pili kushoto ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
Mabondia Hashimu Chisora na Iddi Mkwela wakitunishiana mishuli

ULINGO Briggs alimduwaza Klitschko


ILIKUWA ni ndani ya ukumbi wa Hamburg, nchini Ujerumani usiku wa kuamkia Oktoba 16,2010 pambano la kikatili lilipofanyika kwa kuwakutanisha ndani ya ulingo bingwa wa WBC, Vitali Klitschko raia wa Ukraine aishiye Ujerumani dhidi ya Shannon Briggs wa Marekani.
Utangulizi
Lilikuwa ni pambano la raundi 12, ambapo katika raundi zote hizo, pambano lilikuwa likipiganwa kinyama bila huruma likiwa ni pambano la kuwania ubngwa WBC uzani wa juu, huku Klitschko akitetea ubingwa wake kwa ushindi wa pointi.
Raia huyo wa Ukraine pamoja na kutawala pambano hilo kwa raundi zote akirusha ngumi nzito zilizotua kichwani kwa Mmarekani huyo, lakini alishindwa kabisa kumkalisha chini kwa makonde.
“Nimeshangazwa sana namna alivyostahimili, nilimchapa makonde mengi mazito na nimemchana lakini hakuanguka hata kidogo, Briggs anastahili sifa,”anaeleza Klitschko baada ya pambano hilo.
Katika pambano hilo, majaji wote walitoa alama 120-107, 120-107 na  120-105 kwa  Klitschko, ambaye kwa ushindi huo alijiwekea rekodi ya kushinda mapambano 41 akipigwa 2 wakati  Briggs alivurunda rekodi yake na kuwa 51-6-1.
“Nimepigana na George Foreman, nimepigana na Lennox Lewis, lakini Vitali ni zaidi, alinipiga ngumi nzito sana ana kasi ya ajabu katika mikono yake, kwangu mimi hili ni pambano bora,” anaeleza Briggs baada ya pambano hilo
Pambano ndani ya ulingo
Klitschko katika pambano hilo alikuwa akitumia ‘jab’ za kushoto kumwinda Briggs kisha akawa anamaliza na  ngumi kali ya kulia yaani ‘big right’. Ndiivyo alivyoanza hivyo pambano hilo, alikuwa akimtupia jab ndani ya dakika mbili za raundi ya kwanza kisha kuvurumisha konde kali la mkono wa kulia.
Kabla Briggs hajakaa sawa, akapigwa ‘left hooks’ mbili kidevuni kisha M-Ukraine huyo akaachia fataki jingine la mkono wa kulia, Briggs akawa anajaribu kujibu mashambulizi bila mfanikio.
Klitschko alikuwa akipiga ‘kombinesheni’ katika raundi ya tatu lakini Briggs akawa anatumia ngumi za hesabu yaani ‘counter-punches’.
Klitschko alipiga ‘right hook’ safi mwishoni mwa raundi hiyo ya tatu na akaendelea kutoa adhabu katika raundi ya nne.
Raundi ya tano, Briggs alijikakamua na kupiga ngumi kadhaa huku akiendelea kupokea kipigo kikali kutoka kwa Klitschko.
Katika raundi ya 10, Briggs aligeuzwa kuwa begi la mazoezi ya ngumi na Klitschko alikuwa akichagua pa kupiga lakini alimshitukiza Klitschko alipoachia ngumi kali ya kulia  katika raundi ya 11, lakini Klitschko akaibuka kwa ngumi mbili kali za kulia zilizofanya  kichwa cha Briggs kuvimba kwa nyuma.
Lakini Briggs alishika kichwa na kugoma kabisa kupigwa KO na kuendelea na pambano na hadi mwisho Klitschko akaambulia ushindi wa pointi.
Shannon Briggs aliwahi kupigwa na George Foreman kabla ya kudundwa na Lennox Lewis mwaka 1998.
**Mwandishi ni kocha wa mchezo wa ngumi anayefundisha klabu mbalimbali Dar es Salaam. Anapatikana kwa simu 0713/0787- 406938 au email: superdboxingcoach@gmail.com

SPF YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA JESHI LA MAGEREZA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM


Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimkabidhi seemu ya vifaa vya michezo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, Agosti 25, 2016. Vifaa hovyo ni vya michezo ya ngumi, mpira wa miguu na mpira wa pete.

 Afisa Masoko wa PSPF, Magira Werema, (kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umekabidhi vifaa vya michezo kwa wanamichezo wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam na kasha kufuatiwa na PSPF bonanza la michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Ngumi na Judo.

Akikabidhi vifaa hivyo vya michezo Agosti 25, 2016, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, alisema, PSPF imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua michezo nchini.

“Nyinyi mkiwa kama sehemu kubwa ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, tunayo furaha kutoa vifaa hivi vya michezo kwani baada ya kutekeleza majukumu mazito ya kitaifa mnahitaji kushiriki michezo ili kujenga afya lakini pia kuinua vipaji vyenu,” alisema na kuongeza,

 “Nichukue fursa hii kuwahamasisha mjiunge na PSPF kwani kuna faida nyingi mtapata kutokana na kutoa mafao mbalimbali yatakayoboresha maisha yenu kama ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema, PSPF ni chaguo lako sahihi na kamwe hutajutia uamuzi wako wa kujiunga na Mfuko huu.” Alisisitiza Njaidi.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya wanamichezo hao, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza-Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, aliishukuru PSPF kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwani vitawawezesha wanamichezo hao kushiriki michezo katika mazingira bora ya kiuanamichezo.

Baada ya makabidhiano hayo, wanamichezo hao walionyesha uwezo wao katika michezo ya mpira wa miguu, ngumi, mpira wa pete, na judo.
 Afisa Matekelezo (Compliance), wa PSPF, George Mnasizu, (kushoto), akigawa vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na Mfuko huo kwa baadhi ya wanamichezo wa Jeshi la Magereza
 Njaidi akiwa na Mkuu wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kikosi Maalum cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Rajabu Nyange Bakari, na wacheza judo wa kikosi hicho wakiwa katika picha ya pamoja na vipeperushi vya PSPF.
 Njaidi akimkabidhi sehemu ya vifaa hicho, Nahodha wa timu ya mpira wa pete (Netball), wa timu ya Magereza Ukonga, Pili Enzi
 Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo kocha wa soka wa timu ya Magereza, Sajenti Hassan Mulego
 N

 Hizi ndio Gloves na flana zilizotolewa kwa wana masumbwi (ngumi)
 Pambano la masumbwi likiendelea
  Pambano la masumbwi likiendelea
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akiwa na Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, wakati akitoa nasaha kwa wanamichezo

 Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo, Kocha na Afisa Michezo wa Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, Inspekta Francis Tabu

MABONDIA IDDI MKWELA NA HASHIMU CHISORA KUGOMBANIA UBINGWA WA TAIFA WA TPBC


Mabondia Hashimu Chisora kushoto akitunishiana misuli na Iddi Mkwela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubngwa wa raundi kumi  KG 61 utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa agost 27 jumamosi Katikati ni kiongozi Ally Bakari 'Champion' Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Abdallah Zamba kushoto akitunishiana misuli na Twalibu Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao kesho katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mabondia Hashimu Chisora kushoto akitunishiana misuli na Iddi Mkwela baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubngwa wa raundi kumi  KG 61 utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa agost 27 jumamosi  Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Mabondia wa kike Halima Bandola kushoto na Ester Kazabe wakitunishiana misuli kwa ajili ya mpambano wao kesho katika uwanja wa ndani wa Taifa katikati ni Mwenyekiti wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa
Bondia Iddi Mkwela ajiojiwa na mtangazaji wa ITV Jimmy Tala baada ya kupima Uzito
IDDI MKWELA
Mwenyekiti wa kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa kushoto akizungumza na mabondia pamoja na makocha wao kufata talatibu za kumwandaa bondia pamoja na sheria zake wa pili kushoto ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
Mabondia Hashimu Chisora na Iddi Mkwela wakitunishiana mishuli

Tuesday, August 23, 2016

JIFUNZE MASUMBWI NA SUPER D COACH

ULINGO..
 
Ngumi ya Chavez yakatisha uhai wa Johnson
Na Rajabu Mhamila

LEO katika safu yetu ya fahamu ulingo nitabadili aina ya mfululizo wa makala zangu kwa kuwaandikia mashabiki makala kuhusiana na moja ya athari za mchezo huu.
 
Nitazungumzia ngumi iliyopigwa katika raundi  11 ya pambano kati ya  Leavander Johnson wa Marekani mkazi wa Atlanta  dhidi ya Jesus Chavez wa Mexico.

Pambano hilo lilikuwa ni la kuwania taji lake la Shirikisho la Kimataifa la Ngumi za Kulipwa (IBF), ambapo Johnson alikuwa bingwa na alikuwa akitetea ubingwa wake dhidi ya raia huyo wa Mexico.

Pambano lilifanyika usiku wa Jumamosi ya Septemba, 2005 kwenye ukumbi wa  MGM Grand Hotel- Casino, Las Vegas Nevada huko Marekani.

Kwa hakika ilikuwa ni pambano kali, kumbuka walikuwa wakipigana katika uzito wa lightweight yaani uzito mwepesi, na walikuwa wakijibizana makonde na kufanya pambano hilo kuwa na msisimko mkubwa

Leavander Johnson alikuwa ameahidi mashabiki wake wakiwemo wazazi wake waliofika ukumbini kushuhudia pambano hilo kuwa angetetea vema ubingwa wake na kwamba angemgalagaza mpinzani wake.

Kumbuka kwamba kocha wake alikuwa ni baba yake mzazi huku meneja wake akiwa ni kaka yake. Ukumbini pia walikuwepo mama yake mzazi na ndugu zake wegine ambao waliishuhudia ngumi iliyowaachia majonzi

Kuanzia raundi ya kwanza Leavander Johnson alionekana kama angeweza kuibuka shujaa kwani alikuwa akirusha makonde yaliotua kichwani kwa mpinzani wake na umati ukawa ukishangilia kwa nguvu

Hata hivyo kufikia raundi ya tano, mambo yakaanza kubadilika, Jesus Chavez ambaye  alikuwa kana kwamba anausoma mchezo wa mpinzani wake, akaanza kujibu masambulizi kwa makombora ya nguvu na kufanya pambano kuwa gumu na lisilotabirika kirahisi.

Johnson, aliyekuwa akitokea Jiji la Atlantic  N.J. alikuwa amepigana karibu miaka 16 hadi alipopata ubingwa huo wa dunia katika uzito wa ratili 135 sawa na karibu kilo 58 na alitwaa taji hilo mwezi  Juni 2005 na sasa alikuwa akitetea ubingwa wake kwa mara ya kwanza.

Raundi ya sita, saba nane hadi kumi hazikuwa na mabadiliko makubwa sana kwa aina ya mchezo wao kwani pambano lilikuwa ni piga nikupige, lakini hata hivyo  Jesus Chavez ambaye ni mzoefu, alionekana kutawala pambano kwa muda mrefu kwa kumpiga ngumi nyingi mpinzani wake.

Ndipo ilipoingia raundi ya 11. Kengele ililia kuashiria kuendelea na pambano katika raundi hiyo, Chavez akipigana kwa  kujiamini zaidi alitoka kwenye kona yake na kumvaa moja kwa moja Johnson aliyekuwa bado na ulevi wa  makonde ya raundi ya kwanza.

Mwanzoni tu mwa raundi hiyo, Johnson akarusha jab yake, lakini ikapishana na ngumi  ya kulia ya Jesus Chavez, Johnson akapigwa ngumi ya kushoto na kumfanya ayumbe huku akiwa ameweka mikono yake yote usoni kujikinga na adhabu zaidi.

Jesus hakutaka kuiacha nafasi hiyo, akavurumisha ‘combination’ mfululizo kwa Johnsona na ngumi nyingi zikampata kichwani, wakati mwamuzi wa pambano hilo anaingilia kati kumwokoa Johnson, ngumi kali ya kulia ya Jesus ikatua kichwani kwa Johnson na kumfanya atake kuanguka,  ndipo mwamuzi alipofika na kusimamisha pambano.

Johnson akawa amepoteza ubingwa wake kwa Chavez, mwamuzi katikati ya ulingo akawashika mikono wote wawili kisha kunyanyua mkono wa Chavez na kumtangaza mshindi kwa Technical KnockOut (TKO).

Hata hivyo, Johnson alidondoka kwenye chumba cha kuvalia nguo na kukimbizwa haraka  Kituo cha Afya cha Chuo Kikuu na kufanyiwa upasuaji wa ubongo uliochukua muda wa dakika 40 kujaribu kuokoa maisha yake .

Alibaki akiwa hana fahamu kwa wiki nzima akiwa anapumulia mashine,  lakini baadaye akaanza kupata nafuu jambo lililowapa matumaini ndugu zake waliokuwa wameshakumbwa na hofu ya 'kuondokewa' na ndugu yao mpendwa.

Akiwa anaelekea kupata nafuu, ghafla  hali yake ikabadilika na kuwa mbaya. Hali ilikuwa mbaya zaidi na ndugu zake wakashikwa na uchungu kuona ndugu yao akiteseka na maumivu ya kupumua kwa mashine, wakaamua kuiondoa na  maisha ya Johnson  yakakoma milele.

"Hatukuwa na njia zaidi ya kumsaidia asife, kwa hiyo ndugu zake walikuwa sahihi kuamua kuondoa mashine ya kupumulia," alisema Dk. William Smith aliyemfanyia upasuaji

Promota wa Johnson  Lou DiBella  alisema:” familia ya  Johnson ilikuwepo wakati akikata roho, baba yake ambaye alikuwa kocha wake, kaka yake aliyekuwa meneja wake na mama yake walikuwepo, jambo ninaloweza kusema ni kwamba  amekufa akiwa bingwa, amefia mchezo alioupenda:” alisema " DiBella.
*
**Mwandishi ni kocha wa mchezo wa ngumi anayefundisha klabu mbalimbali Dar es Salaam. Anapatikana kwa simu 0713/0787- 406938 au email: superdboxingcoach@gmail.com

JIFUNZE MASUMBWI NA SUPER D COACH

ULINGO


SAFU hii inaendelea kuhusu sheria za mchezo wa ngumi, aina na staili za upiganaji na mambo mengi yanayouzunguka mchezo huu ambao unapendwa na wengi.
In-fighter/Swarmers
In-fighters/swarmers (wakati mwingine huitwa "pressure fighters") ni aina ya upiganaji ambapo bondia anakuwa hakai mbali na mpinzani wake, anakuwa ana kwa ana kila aendako.
Lakini jambo kubwa si kukaa ana kwa ana na mpinzani bali ni umahiri wao wa kurusha makombora mchanganyiko yaani ‘combinations’ hasa ‘hooks na uppercuts’.
Mpiganaji wa aina hii anahitaji kuwa mlinda kidevu chake mzuri kwani mara nyingi upiganaji huu hushambuliwa na ngumi ya mdonowo yaani ‘jab’ kabla ya wao kufanya kile wanachokusudia.
In-fighters hutumia staili hii ya upiganaji kwa kuwa wengi wao huwa ni wafupi kuliko wapinzani wao na hivyo kulazimika kupigana kwa makombora ya masafu mafupi na yenye kasi kupata ushindi.
Hata hivyo, baadhi ya mabondia warefu katika uzito mbalimbali wamekuwa pia wakipigana kwa staili hii, mfano ni Mike Tyson aliyewahi kuwa maarufu sana kwa ‘uppercuts’ zake zilizokuwa na madhara makubwa kwa wapinzani, pia Julio César Chávez, mabondia wengine ni Wayne McCullough, Amir Khan, Harry Greb, Jack Dempsey, Rocky Marciano, Joe Frazier, David Tua na Ricky Hatton.
Counter puncher
Counter punchers ni mabondia ‘wanaoteleza’ wenye kupigana kwa kujilinda zaidi na kutumia zaidi makosa ya mpinzani wake. Silaha yao kubwa ni kutumia makosa ya mpinzani na kuchukua pointi au hata kushinda kwa KO.
Hutumia muda mwingi kujikinga kuhakikisha wanazuia kila aina ya ngumi isiwapate na wakati huohuo kwa haraka kurusha makombora zaidi kwa kutegemea makosa ya mpinzani wake.
Mpinzani wake anaposhambulia yeye ndipo hupata mwanya wakati huohuo kulenga shabaha sehemu wazi iliyoachwa na mpinzani wake, kwa kuwa ni kawaida mtu anaposhambulia sehemu ya uso wake na nyingine huwa zinabaki wazi pasipokulindwa.
Hata hivyo, ili uwe mpiganaji wa staili hii, unapaswa kuwa na sifa zifuatazo. Uwe na mnyambuko (good reflexes), uwe mwenye kujaliwa akili ya upiganaji (intelligence), uwe na shabaha ya makonde (punch accuracy), lakini zaidi ya wepesi uwe  na mikono mwepesi yenye kasi ( good hand speed).
Baddhi ya mabondia katika kundi hili ni Jim Corbett, Jack Johnson, Laszlo Papp, Jerry Quarry, Anselmo Moreno, Chris Byrd, Bernard Hopkins, Vitali Klitschko, James Toney, Marvin Hagler, Evander Holyfield, Juan Manuel Márquez, Humberto Soto, Floyd Mayweather Jr, Roger Mayweather, Pernell Whitaker na  Max Schmeling.
·        Mchanganyiko wa staili
Mabondia wote duniani huwa na ujuzi wa msingi, ambapo kila bondia anapoanza ngumi hujikuta akitumia staili moja ambayo kwake inampa raha zaidi au inamfaa zaidi.
Lakini wanapokomaa katika fani hiyo lazima wawe na ujuzi wa zaidi ya staili hiyo waliyozoea ili wanapokutana na aina nyingine ya wapiganaji waweze kumudu pambano mfano, bondia wa staili ya ‘out-fighter’ atahitajika kutumia staili kukita miguu yake na kutumia staili ya ‘counter punch’, au kutumia mbimu za ‘slugger’ ili kuweza kumudu kupigana na bondia mwenye nguvu za mikono.
·        Staili dhidi ya staili
Je, kuna staili iliyo bora zaidi kuliko nyingine? Kinachokubalika na ambacho ni sahihi ni kwamba hakuna staili iliyo bora kuliko nyingine, zote zina faida yake na hasara yake lakini zaidi inategemea bondia mwenyewe anavyotumia staili yake isipokuwa kuna staili ambayo ina faida dhidi ya staili nyingine.
Mfano, mpiganaji wa staili ya ‘in-fighter’ ana faida anapopigana na mpiganaji wa ‘out-fighter’,  mpiganaji wa staili ya ‘out-fighter’ ana faida anapokutana na bondia wa staili ya ‘puncher’, bondia ‘puncher’ ana faida dhidi ya bondia ‘in-fighter’.
Huu ni mzunguko ambao unafanya kusiwepo na staili iliyo bora kuliko nyingine kwakua staili moja inaweza kuwa bora ya nyingine lakini ikawa dhaifu kwa nyingine.
Kwa asili sababu nyingine zinazochangia ubora wa staili husika ni kipaji, ujuzi na akili ya bondia mwenyewe pia aina ya mazoezi anayofanya na ndio maana kuna msemo kwamba staili hutengeneza upiganaji ("styles make fights"),
Ndiyo maana unakuta kwa mfano Joe Frazier alikuwa mzuri na kumsumbua sana Muhammad Ali, lakini alikuwa ‘nyanya’ kwa George Foreman ambaye naye alikuwa ‘nyanya’ kwa Ali.
**Mwandishi ni kocha wa mchezo wa ngumi anayefundisha klabu mbalimbali Dar es Salaam. Anapatikana kwa simu 0713/0787- 406938 au email: superdboxingcoach@gmail.com
 

JIFUNZE MASUMBWI NA SUPER D COACH

(Ulingo)
Na Rajabu Mhamila ‘Super D’
 
Aina za upiganaji masumbwi
 
Vifaa vya kukinga mwili
KWAKUWA ngumi ni mchezo unaotumia nguvu, ni lazima tahadhari za hali ya juu zichukuliwe kuhakikisha mifupa katika kichwa na mikono vinalindwa, lakini pia ubongo na athari nyingine.
 
Makocha wengi huwa hawaruhusu mabondia wao kufanya mazoezi ya kupigana (sparring) bila kuvaa clip bandage (wrist wraps) na glavu.
 
(Hand wraps) hutumika kwa ajili ya kulinda mifupa katika mikono na kichwani, na glavu hutumika kukinga mifupa ya mikono kutojeruhiwa.
 
Glavu zimekuwa zikihitajika na kutumika na katika mashindano tangu karne ya 19 ijapokuwa glavu za ngumi za kisasa ni nzito kuliko zile za mwanzoni mwa karne ya 20.
 
Kabla ya pambano, mabondia wote hukubaliana ni glavu zenye uzito upi zitumike wakiwa na uelewa kwamba glavu inavyokuwa nyepesi ndivyo ngumi zinavyopenya zikiwa na athari zaidi na kuweza kusababisha madhara.
 
Bidhaa ya glavu pia huathiri ngumi kwa namna moja au nyingine ikitegemea glavu imetengenezwa na kampuni gani na imetengenezwa kwa kiwango gani na hivyo kabla ya pambano lazima kuwe na makubaliano ya glavu zitakazotumika.
 
Kipira cha mdomoni ni muhimu kukinga meno na fizi visijeruhiwe na pia kuifanya taya muda wote kuwa na tahadhari, unapokuwa na mouthpiece taya muda wote huwa linakakamaa kwa kuwa unauma kile kipira na hii inasaidia kupunguza nafasi ya kupigwa KO.
 
Mabondia wote wanatakiwa kuvaa soksi na viatu maalumu vya mchezo huo wa ngumi (ring boots), hii ni tahadhari ya kujikinga na ajali inayoweza kutokea kama kugongana au kukanyagana kwa bahati mbaya.
 
Viatu vya mabondia wa kale vilikuwa vinafanana na vya wanamieleka wa kale lakini vya sasa vinafanana na vya ngumi za ridhaa au mieleka ya ridhaa.
 
Vifaa vya mazoezi
Mabondia hujifunza ujuzi wa ngumi katika misingi miwili; ya begi la kufanyia mazoezi (punching bags). Begi dogo linaloitwa "speed bag" ambalo kazi yake kubwa ni kulainisha misuli na kufanya ngumi au mikono kuwa na kazi na begi kubwa "heavy bag"  ambalo hujazwa mchanga na pumba  au vitu vingine, kazi yake kubwa ni kukomaza mikono na kuifanya iwe na guvu.
 
Vifaa vingine ambavyo hutumika katika mchezo wa ngumi ni vifaa ambavyo si maalumu katika mchezo wa ngumi ilimradi vinajenga nguvu, kasi na stamina, vifaa vinavyojulikana katika mazoezi ni vitu vya kunyanyua uzito, kamba ya kuruka, ‘medicine balls’ na dumb bells’.
 
Staili na mbinu
Unaweza ukawa na staili ya upigaji kama niliyoeleza hapo juu lakini ukakosa mbinu na ndio maana ni muhimu bondia kuwa mjuvi katika mbinu na staili ambazo tutaziangalia kama ifuatavyo:
 
Mkao (Stance)
Mkao au stance ni namna bondia anavyosimama akiwa anapambana, unaweza kuwa na mbinu lakini pia staili. Kwa bondia yeyote duniani kuna aina kuu mbili za usimamaji.
 
Kutangulia mguu wa kushoto mbele (orthodox)
Hii ni staili au mkao au msimamo ambao unatumika kwa mabondia karibu wote wanaotumia mkono wa kulia katika matumizi ya kawaida ya kila siku katika maisha yao.
 
Mkao huu, bondia anatanguliza mguu wa kushoto mbele, anatumia ngumi ya kushoto kama ‘jab’ yaani ngumi mdonowo hivyo silaha yake ya ‘kumaliza mchezo’ inakuwa ni ngumi ya kulia, mkao huu unaitwa ‘Orthodox’, KO yake hutokea kwenye mkono wake wa kulia.
·        Kutangulia mguu wa kulia mbele (southpaw)
Hii ni staili au mkao au msimamo ambao unatumika kwa mabondia wachache sana ambao wengi wao hata katika maisha ya kila siku hutumia mkono wa kushoto.
Mkao huu, bondia anatanguliza mguu wa kulia mbele, anatumia ngumi ya kulia kama ngumi mdonowo ‘jab’, hivyo silaha yake ya ‘kumaliza mchezo’ inakuwa ni ngumi ya kushoto,  mkao huu unaitwa ‘Southpaw’. KO yake hutokea kwenye mkono wake wa kushoto.
 
Kwa upande wa nchi ya Cuba ambayo ilipiga marufuku mchezo wa ngumi za kulipwa, mabondia wake wote ni ‘southpaw, kwa hiyo si lazima bondia wa aina hii awe ni ‘mashoto’ (lefted hand) au orthodox awe lazima mtumia mkono wa kulia (right-handed).  
 
Kuanzia hapo staili nyingine au mikao midogo huwa imeegemea katika misingi ya mikao hiyo miwili mikubwa. Hata hivyo mikao ya sasa inatofautiana na mikao ya zamani ya karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20.
 
Misimamo au mikao ya sasa (modern stance) bondia anakuwa wima zaidi na mikono akiwa ameiweka mbele kidogo ya uso wake, au chini (low guard) tofauti na mikao ya zamani ambapo bondia alikuwa akisimama na mikono katanguliza mbele na nundu za ngumi (knuckles) zikiwa zimeelekea mbele.
 
Mikao hiyo ilitumika katika karne ya 20 na mfano mzuri ni bondia Jack Johnson, na hapa nitaelezea mikao hiyo yaani ‘stance’ kwa mifano ya picha kama ifuatavyo. Itaendelea wiki ijayo.
*Mwandishi ni kocha wa mchezo wa ngumi anayefundisha klabu mbalimbali za ngumi za kulipwa Dar es Salaam. Anapatikana kwa simu 0713/0787- 406938 au email: superdboxingcoach@gmail.com

James ‘Buster’ Douglas alianzia kwenye soka


LONDON, England 
JAMES ‘Buster’ Douglas aliushangaza ulimwengu wa masumbwi pale alipomtwanga bingwa aliyekuwa akichukuliwa kwamba hapigiki, Mike ‘Iron’ Tyson.
Pengine hiyo ndiyo rekodi kubwa zaidi inayokumbukwa na wafuatiliaji wa mchezo wa masumbwi.
Pambano hilo lilifanyika Tokyo, Japan 1990  na kwa sasa Douglas ameshastaafu na anakisiwa kuwa na utajiri wa jumla ya dola milioni tatu.
Douglas (53) ni Mmarekani aliyezaliwa Columbus jimbo la Ohio, na ni mtoto wa bondia wa zamani, William ‘Dynamite’ Douglas.
Amejijengea heshima kwa masumbwi yake mazito, lakini pia kwa nidhamu ndani na nje ya ulingo.
Mbali na ngumi, tangu utoto Douglas alipenda sana michezo mingine na shuleni Linden McKinley aliwika katika mchezo wa soka na wa kikapu.
Alikuwa mzuri kwenye mpira wa kikapu unaopendwa zaidi na Wamarekani hivyo kwamba aliwaongoza wana Linden kwenye michuano ya kitaifa 1977.
Baada ya hapo aliendeleza kipaji chake hicho kwa kucheza mpira wa kikapu alipokuwa Chuo cha Coffeyville kwa timu yao iliyojulikana kama Red Ravens iliyopo Coffeyville, Kansas kati ya 1977 na 1978.
Alikuwa akicheza kama fowadi na urefu wake wa futi sita na akaja kujumuishwa kama mwanamichezo bora wa timu ya Coffeyville.
Aliendelea na kikapu ambapo kati ya 1979 na 1980, Douglas alichezea Chuo cha Sinclair kilichopo Dayton, Ohio kabla ya kwenda Chuo Kikuu cha Mercyhurst kwa skolashipu ya kikapu.
Hata hivyo, baada ya muda aliamua kurudi Columbus alikojikita zaidi kwenye ngumi na awali alijulikana zaidi kwa jina la Dessert Fox.
Pambano lake la kwanza la ngumi lilikuwa Mei 31, 1981 alipopigana na kumshinda Dan O’Malley kwenye kipute cha raundi nne.
Je, aliwekaje historia kwa kumpiga Tyson? Lilipotangazwa pambano lao, karibu kila mdau aliona kwamba Tyson angeshinda kirahisi tena kwa Knock Out (KO).
Hata jijini Las Vegas, miongoni mwa wacheza kamari na watabiri wa ushindi wa kwenye masumbwi pale Mirage Casino ni mtu mmoja tu aliweka dau lake kwa Douglas kwamba angeshinda.
Siku ya siku ilipowadia Douglas alipanda ulingoni kwa kujiamini na utulivu mkubwa.
Tyson kama kawaida aliingia kwa makeke, akitishia kwa jinsi anavyotazama lakini hali haikumwendea vyema ulingoni kwa sababu alikipokea kichapo.
Douglas alishikilia mkanda huo wa uzani wa uu duniani kwa miezi minane na wiki mbili, akaja kuupoteza Oktoba 25, 1990 alipokuja kupigwa na Evander Holyfield kwa KO ya raundi ya tatu.
Katika ngumi kwa ujumla, Douglas amecheza mapambano 46, akashinda 38, kati ya hayo 24 kwa KO, akapoteza sita, sare moja na jingine likafutwa matokeo.
Baada ya muda wake kwenye ngumi kumalizika aliingia kwenye uigizaji wa filamu, akaanza na ile ya sayansi kwa Artie Knapp iliyoitwa Pluto’s Plight ambapo alikuwa nyota katika video hiyo.
Inaelezwa kwamba pambano la Douglas dhidi ya Holyfield liingiza dola milioni 24.6 lakini Douglas anasema kwamba alichpopata hapo ni dola milioni 1.5 tu.
Nyingine zilitumiwa kwa ajili ya kulipa kodi, mameneja, wakufunzi wake na mengineyo na anasema alipopigana na Tyson alipata dola milioni 1.3 lakini baada ya makato akabakiwa na dola 15,000 tu.
Douglas alikuja kuongezeka uzito kiasi cha kutisha na kufikia karibu pauni 400. Alikuja kupata kisukari akakisogelea kifo ndupo akaamua kujaribu kurejea kwenye michezo.
Alianza tena mazoezi na alipopangiwa mapambano alishinda sita ya kwanza mfululizo. Hata hivyo 1997 alipigwa isivyo halali na Louis Monaco ambaye alimtwanga ngumi nzito ya mkono wa kulia baada ya kengele ya raundi ya kwanza kumalizika kupigwa.
Hakuweza kuendelea na pambano hata baada ya kupumzishwa kwa dakika tano ambapo ngumi ile batili ilimrusha kwenye zulia.
Alipatiwa ushindi kwa majaji kumfutia pointi zote Monaco. Alikuja tena kucheza na Roy Jones, Jr mwishoni mwa miaka ya ’90 halafu akapigwa kwa KO na Lou Savarese kwenye raundi ya kwanza. Hakukata tamaa, akacheza tena mapambano mawili kabla ya kuamua kutundika glavu zake moja kwa moja 1999.

Oscar De La Hoya na vituko kwa wanawakeNa Suit Jose, Madrid
BONDIA mstaafu wa Marekani mwenye asili ya hapa Hispania, Oscar De La Hoya anaweza kuwa na mali nyingi, lakini amefanya mambo ya ajabu sana.
Hoya anayetajwa kuwa na utajiri wa dola milioni 200 ametuhumiwa na wanawake kwa vituko vyake alipokuwa nao hotelini, ikiwa ni pamoja na kuvaa nguo zao za ndani.
Hoya alizaliwa Februari 4, 1973 mashariki mwa Los Angeles, California na ni mmoja wa mabondia wachache wa uzito wa juu kuwa mtu maarufu katika utamaduni wa pop.
Ametoka kwenye familia yenye historia ya ngumi, ambapo mwaka 1992 alilipatia taifa lake medali ya dhahabu baada ya kushiriki Michezo ya Olimpiki jijini Barcelona, Hispania.
Alikuwa ndio amehitimu masomo yake katika James A. Garfield High School na alikuja kujulikana kama ‘The Golden Boy’.
Amepanda ulingoni mara nyingi ambapo ameshinda mara 234 kati ya hizo kwa Knock Out (KO) ikiwa ni mara 163 na amepoteza mapambano sita tu katika ngumi za ridhaa na za kulipwa.
Alianza rasmi ngumi za kulipwa Novemba 1992 na kustaafu 2009 akiwa na amepigana katika uzani sita tofauti na kuwashinda mabingwa 17 wa dunia na ni mmoja wa mabondia waliotengeneza fedha zaidi.
Katika vituko vyake, Hoya anadaiwa kwamba akiwa kwenye hoteli ya Ritz Carlton jijini New York, alimbeba mwanamitindo wa jijini hapo Angelica Marie Cecora (25).
Hoya anadaiwa kuwa kama chizi, kwa jinsi alivyokuwa akicheza cheza chumbani humo, akavaa chupi ya Cecora na kuanza kuruka ruka kama mwanasarakasi na baadaye akavaa sketi yake.
Mwanadada huyo anadai walifanya ngono kabla ya Hoya kuagiza dawa za kulevya aina ya cocaine kuingizwa chumbani humo, kisha akaanza kumtisha.
Hii ni mara ya pili Hoya anatuhumiwa kuvaa chupi za kike, kwani mara ya kwanza alifanya hivyo kwa chupi ya mrembo wa Siberia, Milana Dravnel ambaye anadaiwa alilipwa dola milioni 20 mwaka 2008.
Hoya anadaiwa kuwasiliana na Cecora ili amliwaze baada ya safari ndefu ya kutoka Irak alikokuwa ameenda kuwasalimu wanajeshi wa Marekani.
Kwamba alikuwa anataka kustarehe baada ya kupitisha muda mrefu pasipo kutumia kilevi, mihadarati na wanawake.
Hata hivyo, Hoya alificha jina lake, akadaiwa kwamba alikuwa anaitwa Thomas Crown, jina la milionea aliyetumika kwenye filamu ya ‘Thomas Crown Affair’ iliyochezwa na Pierce Brosnan 1999.
Cecora aligundua jina la kweli la mwenzake huyo wakati wa chakula cha jioni baada ya kujisahau na kuiona kadi yake ya benki.
“Kuna vitu vingi alivyofanya ambavyo siwezi hata kuelezea … alivaa nguo yangu ya ndani tena ikamwenea vizuri tu, akavaa na sketi yangu,” mwanadada huyo aliliambia gazeti la The New York Post. 
Baadaye msichana huyo alimwalika rafiki yake wa kike chumbani wakakaa kabla ya kumtisha Hoya hadia kaondoka.
Hata hivyo ilipofika asubuhi, wasichana hao wawili walijikuta katika hali mbaya na deni la dola 1,500.
Hata hivyo, meneja wa Hoya alifika baadaye na kulipa deni hilo lililotokana na vitu walivyokula na chumba walichotumia.
Mwanasheria wa Cecora, Tony Evans anasema aliyofanya Hoya ni mambo mabaya na ni mfano anuai wa matumizi mabaya ya nguvu zake kwa kuwadhalilisha wanawake.
Hoya ana asili ya Hispania, ambapo babu yake, Vicente, baba Joel Sr. na kaka yake, Joel Jr wote walikuwa wana ndondi. Hoya alikuwa bondia wa mwaka 1995, akapewa tuzo.
Hoya alianzisha kampuni ya promosheni ya ngumi inayokwenda kwa jina la ‘Golden Boy Promotions’.
Huyu ni Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Hispania kumiliki kampuni ya promosheni ya ngumi kati ya mapambano aliyoshindwa ni mara mbili kutoka kwa mikono ya Shane Mosley.
Mama yake, Cecilia, aligunduliwa kuwa na saratani ya matiti na alifariki dunia 1990 na akiwa kwenye kitanda chake cha mauti alieleza matumaini kwamba mwanawe angekuja kutwaa medali ya dhahabu kwenye Olimpiki, na kweli ikawa hivyo.
Hoya anasema kwamba alijituma vilivyo kwenye mazoezi na pia katika ulingo kwa ajili ya kutimiza ndoto za mama yake, hata baada ya kufariki kwake dunia.