Tangazo

Pages

Thursday, May 30, 2013

Floyd Mayweather Jr KUPANDA ULINGONI September 14 NA Saul “Canelo” Alvarez

Floyd Mayweather Jr. (44-0, 26 KO’s) VS Saul “Canelo” Alvarez (42-0-1, 30 KO’s) step foot inside the ring on September 14th at the MGM Grand in Las Vegas, Nevada

Wednesday, May 29, 2013

KASEBA APANIA KUMKALISHA MMALAWINa Elizabeth John

BONDIA wa ngumi za mateke ‘Kick Boxer’ Japhet Kaseba amesema amejipanga kuweka rekodi nzuri katika tasnia hiyo kwa kumchapa Mmalawi, Rasco Chimwanza katika pambano lao la kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati linalotarajiwa kuchezwa Juni 8, mwaka huu.Akizngumza na Habari Mseto jijini Dar es Salaam, Kaseba alisema anajua kama bondia huyo ni nyota katika tasnia hiyo, lakini kutokana na maandalizi aliyoyapata atahakikisha anaweka heshima katika ngumi za mateke.
“Namshukuru mungu nina afya nzuri hadi sasa na naendelea na mazoezi kwajili ya pambano hilo naomba Watanzania wajitokeze kwa wingi katika ukumbi huo wa DDC Magomeni,” alisema Kaseba.
Naye Katibu Mkuu wa Oganizasheni ya ngumi ya za kulipwa Tanzania (TPBO), Ibrahim Kamwe alisema maandalizi ya pambano hilo yamekamilika, na tayari wamemtumia nauli Mmalawi huyo na kwamba anategemea kuingia nchini Juni 5.
Alisema TPBO imemtengenezea mazingira mazuri ya ushindani, Kaseba na kwamba wanategemea atafanya vizuri katika pambano hilo kutokana na maandalizi ambayo anaendelea kufanya.

 Nae kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia  wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
 
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila ,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe. 
 
 mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

Monday, May 27, 2013

KING CLASS MAWE KUPAMBANA NA BAUNSA JUNI 16 PANANDI PANANDI ILALA

KING CLASS MAWE
BAADA ya kumsambalatisha Amosi Mwamakula kwa point  bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' anakabiliwa na kibarua kizito kwa kupanda ulingoni na bondia  Patrick Anthony Kavako 'Baunsa' wa Morogoro  mpambano wa raundi 8 utakaofanyika katika ukumbi wa Panandi panandi Ilala Bungoni Juni 16 akizungumzia mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa mpambano huo ni wa kukata na shoka ambao si wa kukosa kwani kila mmoja amejitahalisha kivyake hivyo wasubili tu siku ya mpambano huo

Patrick  Kavako'Baunsa'
Unajua morogoro na Dar es salaam ni mahasimu katika michezo yote ukiangalia na sasa wamekutanishwa vijana katika masumbwi hivyo kila mmoja anaitaji ushindi ili ajiongezee rekodi yake kwani 'King Class Mawe' ato kubali kupigwa na Kavako ato kubali kabisa kupoteza mpambano wake kiraisi kwani na yeye anaitaji ajulikane katika ulimwengu wa masumbwi na kuiperekea sifa morogoro kama ilivyo kwa mabondia wengine wanao tamba mkoani hapo 

Mpambano huo ulioratibiwa na Kinyogoli Fondition kwa kushlikiana na PST itakuwa chachu kwa vijana kuendelea kuupenda na kuucheza mchezo huo unaopendwa na wengi nchini

mbali ya mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka bondia Abuu Mtambwe ataoneshana umwamba na Kassim Gamboo na Bondia mkongwe kabisa Yohana Robart atamenyana na Mussa Sunga

Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini,Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia  wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
 
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila ,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe. 
 
 mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
 HAMADUU MWALIMU ALIVYO MWONESHA UBABE COSMAS KIBUGA

Bondia Cosmas Kibuga kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamaduu Mwalim wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki mwalimu alishinda kwa pointi  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Cosmas Kibuga akimsubili kwa hamu hamaduu mwalim baada ya kudondoka chini wakati wa mchezo wao jana
Bondia Hamaduu Mwalimu kushoto akioneshana umairi wa kurushiana makonde na Cosmas Kibuga wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Mwalimu alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mpambano wa utangulizi kwa ajili ya kusafisha uwanja

DEO NJIKU ALIPOMSAMBALATISHA OMAR RAMADHANI MOROGORO

Bondia Deo Njiku kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Omari Ramadhani wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Taifa Njiku alishinda kwa TKO ya raundi ya pili na kuwa bingwa mpya wa Taifa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' akiwepo kushudia mpambano huo uliofanyika Morogoro

Mabondia wa Utangulizi wakisafisha jukwaa kabla ya mtanange wenyewe

Chembu Upcat Kidevu lazima ukae ndivyo inavyo someka picha hii

Omari Ramadhani kushoto akipambana na Deo Njiku wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Taifa Njiku alishinda kwa TKO ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, May 21, 2013

Sunday, May 19, 2013

TASWA FC YAWAFUNGA TIMU YA MPIRA YA MABONDIA KWA TABU 2.1Bonia Daudi Muhuzi akishindana na Mbuyu wa timu ya TASWA FC Majuto Omari wakati wa mpambano wao
Kocha wa kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila ' Super D' akisisitiza jambo wakati wa mapumziko
Mchezaji wa timu ya Taswa akipambana na bondia kuwania mpira
SUPER D BOXING COACH AKISISITIZA JAMBO WAKATI WA MAPUMZIKO WA MCHEZO HUO

JONAS SEGU ALETA HESHIMA YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA BAADA YA KUMWENYESHA MTHAILAND, LAKINI AUMIA MKONO RAUNDI YA 6

Tanzania imetengeneza historia mpya kwenye ngumi za kulipwa nchini Thailand baada ya mabondia wake kuwa wanapigwa kila mara wanapokwenda kuiwakilisha nchi na bara la Afrika. Safari hiiJEMBE, kijana mtanashati anayeinukia kwenye masumbwi Jonas Segu kutoka katika ukumbi wa mazoezi waRespect Gym Boxing Club ya Mabibo Loyola chini ya kocha Christopher Mzazi ameonyesha kipaji kikubwa cha kusukuma msumbwi alipoushangaza umati wa maelfu ya wananchi wa Thailand pamoja na nchi za ukanda wa Indo-China.
Segu alikuwa anachuana na bingwa wa IBF katika mara la Asia Pacific Patomsuk Pathompothong kutoka Thailand katika uzito wa Light Welter ambaye ni bondia namba 7 duniani katika viwango vya IBF. Mpambano wao ulifanyika katika jiji lenye mahekalu ya dhahabu la Bangkok na kurushwa na television katika nchi zote za ukanda wa Indo-Chinaza Laos, Myanmar, Cambodia, Vietnam na Thailand yenyewe.
Mpambano wa Segu na Pathompothong ulianza kwa bondia wa kitanzania kuchomoka kama upinde kwenye kona yake na kumshambulia Pathompothong kwa makonde mazito ya kumshikisha adabu. Segu alitupa makonde ya mchanganyiko na kumzidi Pathompothong kutokana na uzito na umakini wa ngumi zake. Kwa kipindi chote cha raundi ya kwanza ilimbidi Pathompothong ajilinde na kukimbia akizunguka ndani ya ulingo ili kudhoofisha masumbwi yaSegu aliyekuwa anayachanganya kama mashine ya kukomboa mpunga ambao unalimwa kwa wingi nchini Thailand!

Jonas Segu alikuwa chini ya uangalizi makini wa bondia maarufu mstaafu George “Lister” Sabuni ambaye aliweza kumpa maelekezo ya nini cha kufanya kwenye mpambano huo wa mwaka. Katika raundi ya 2, 3 na 4 Segu aliuonyesha umati wa mashabiki wa Thailand kuwa yeye kweli ni bingwa mtarajiwa na hakwenda Thailand kula wali wao ila kuiwakilisha nchi yake ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Segu alimhenyesha Pathompothong vilivyo kwa kumchakaza kwa makondde mfululizo hususan akiutumia mkono wake hatari wa kulia ambao ulionekana dhahiri kuwa unaleta madhara makubwa kwa Pathompothong.
Ilididi timu ya wataalam wa Pathompothong kutafakari namna ya kumdhibiti kijana huyo wa Kitanzania ambaye kweli alionekana kuwa alienda Thailand kuuchukua mkanda wa IBF Pan Pacific na sio kufuata ulaji! 
Raudi ta 5 Pathompothong aliingia ulingoni akiwa mtu tofauti kabisa akirusha msumbwi mfululizo na kutembea ulingoni kama siafu huku akimvuta Segu kenye kamba ili amkandamizie masumbwi yake. Kijana huyo nadhifu wa kitanzania (mwenye sura nzuri ya kuvutia na ambaye wasichana wengi wa Thailand walishinda karibu na hoteli aliyoshukia ili kuweza kuongea naye) alitumia wakati huo kumwonyesha Pathompothong kuwa yeye hababaishwi na masumbwi yake kwani amefanya mazoezi ya kutosha. Segu alibadilishana masumbi na Pathompothong vilivyo na kuufanya umati wa mashabiki waliojazana kwenye ukumbi huo kumshangilia kama vile yeye ndiye bondia wao wakiimba Tanzania, Tanzania, Tanzania!
Katika raundi ya 6 mabondia wote waliingia ulingoni kama vifaru na kubadilishana masumbwi ya mchanganyiko (combinations) wakitafuta kudhibiti harakati za mpinzani mwenza. Ni katika kubadilishana huku kwa masumbwi ambako Segu aliumizwa mkono na Mthailand Pathompothong. Inawezekana kuwa ni katika juhudi za kumzuia ili asiendelee kurusha masubwi ya nguvu na kudhoofisha nguvu zake.
Kuumia mkono kwa Segu ilikuwa dhahiri kwani mwanzoni mwa raundi ya saba wakati Pathompothong alipokuwa anamiliki ulingo dhidi ya kijana huyo mtanashati wa kitanzania. Katikati ya raundi ya saba Segu aliona kuwa hawezi kuutumia mkono wake vizuri na kumwashiria refarii wa mpambano kuwa anaacha!
Segu aliacha pambano hilo katika raundi ya saba wakati mashabiki wengi katika ukumbi huo wakiwa wanaimbaTanzania, Tanzania, Tanzania kwa jinsi alivyokuwa anapeperusha vyema bendera ya “Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”

Wednesday, May 15, 2013

MSANII DIPO AJIUNGA KWENYE MASUMBWI

Kocha wa mchezo wa masumbwi Klabu ya Amana CCM ,Kondo Nassoro Kulia akimwelekeza msanii wa michezo ya kuigiza kwenye Luninga, Haruna Mussa 'dipo' Dar es salaam jana jinsi ya kutupa makonde alipokwenda kufanya mazoezi ya ngumi kwa ajili ya kujiweka sawa sawa katika kuakikisha anafanya vizuri kwenye fani yake.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Msanii wa michezo ya kuigiza kwenye Luninga, Haruna Mussa 'dipo' akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Omari Bai wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika GYM ya Amana CCM Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa mchezo wa masumbwi Klabu ya Amana CCM ,Kondo Nassoro Kushoto akimwelekeza msanii wa michezo ya kuigiza kwenye Luninga, Haruna Mussa 'dipo' Dar es salaam jana jinsi ya kutupa makonde alipokwenda kufanya mazoezi ya ngumi kwa ajili ya kujiweka sawa sawa katika kuakikisha anafanya vizuri kwenye fani yake.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, May 10, 2013

SUPER D AFYATUA DVD TATU MPYA ZA MAFUNZO YA MASUMBWI

Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini,Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia  wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
 
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila ,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe. 
 
 mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

DVD MPYA ZA MASUMBWI HIZI HAPA

DVID MPYA ZA MASUMBWI KWA SASA ZIPO TAYARI KWA AJIRI KUPATA BURUDANI UKIWA NYUMBANI ZAID TUWASILIANE 0713406938 AU TEMBELEA www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, May 7, 2013

BONDIA SAID MBELWA AMGALAGAZA SAID MKONDE KWA K,O

Bondia Omari Zungu akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Sinondo wakati wa mchezo wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Sinondo alishinda kwa K,O raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Said Mkonde kushoto akioneshana uwezo wa kurushiana makonde na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbelwa alishinda kwa K,o raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Said Mkonde kushoto akioneshana uwezo wa kurushiana makonde na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Mbelwa alishinda kwa K,o raundi ya pil picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Chilambo Hemed kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana masumbwi na Boniface Urasa wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki Chanika Chilambo alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Said Mbelwa akipambana
Bondia Omari Zungu akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Haruna Sinondo wakati wa mchezo wao uliofanyika Chanika mwishoni mwa wiki iliyopita Sinondo alishinda kwa K,O raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Refarii Saidi Chaku akimwinua mkono juu Bondia saidi Mbelwa kuashilia ni mshindi katika mpambano huo

Monday, May 6, 2013

MAYWEATHER Jr AMCHAPA ROBERT GUERRERO KWA POINTI

 Bondia Floyd Mayweather Jr (kushoto) akimsulubu Robert Guerrero katika pambano la masumbwi kwenye Ukumbi wa MGM Grand Garden, jijini Las Vegas, Marekani. Mayweather Jr alishinda kwa pointi pambano hilo la kwanza tangu amalize kifungo cha miezi miwili jela.
 Mayweather Jr akiendelea kumuadabisha Guerrero, kiasi cha majaji wote watatu kumpa ushindi sawasawa wa pointi 117-111 na kutwaa ubingwa wa Dunia wa WBC uzani wa ‘welter.’ 
 Guerrero akiwa na jeraha juu ya jicho la kushoto lililotokana na makonde mazito ya Mayweather Jr.
 Guerrero akipewa maelekezo na kocha wake, wakati wa mapumziko ya moja ya raundi za pambano hilo, ambalo alipigwa kwa pointi na kukiri mpinzani wake ni mjanja na ana kasi kubwa ulingoni.
 Mayweather Jr (kushoto), akikwepa fataki la kushoto kutoka kwa Guerrero katika pambano hilo.
 Guerrero akiendelea kushambulia 'upepo' kutokana na Mayweather Jr kuwa mbunifu katika kukwepa makonde yake kama anavyoonekana pichani.
 Mayweather akaweka mzaha kando na kuanza kujibu mapigo, ambapo makombora yake yalikuwa yakitua sawasawa mwilini mwa Guerrero, ingawa hayakuweza kumdondosha na kuishia kumuumiza tu na kutokwa damu.
 Guerrero akipokea konde zito la Mayweather. Baada ya pambano, Guerrero alikiri kushindwa na kumsifia mpinzani wake: "Nilimpiga baadhi ya makonde mazuri. Lakini yeye ni bondia mkubwa na bora. Ni mjanja na mwepesi mno ulingoni"
 Mayweather Jr akiwa amebebwa baada ya kutangazwa mshindi kwa pointi 177-111 kutoka kwa majaji watatu wa mtanange huo ndani ya Ukumbi wa MGM Grand Garden, Las Vegas, Marekani.
 Mayweather Jr (kulia mwenye kapero) akishangilia ushindi wake na baba yake Mayweather Sr (kushoto), huku wapambe wake wakinyanyua juu mikanda anayoishikilia baada ya ushindi wake dhidi ya Guerrero.

Mayweather baada ya pambano hilo alisema: "Najisikia vibaya kwa sababu sikuweza kushinda kwa ‘knockout’ ambayo mashabiki wangu walikuwa wakitaka. Nilipigana kadri niwezavyo kuhakikisha nashinda kwa ‘knockout,’ lakini hilo halikutokea ulingoni"