Tangazo

Pages

Wednesday, July 31, 2013

BONDIA MTANZANIA OMARI KIMWERI ALIVYO MGALAGAZA Thailand kwa KO

 Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anaefanya shughuli zake Australia kulia akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wake baada ya kumtwanga  Ekkalak Saenchan  wa Thailand kwa KO raundi ya kwanza  PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anaefanya shughuli zake Australia kulia akinyooshwa akimsukumia makonde mazito mfululizi bondia Ekkalak Saenchan  wa Thailand na kufanikiwa kumtwanga kwa kwa KO raundi ya kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita picha kwa niaba ya Mtandao wa SUPER D

Bondia Mtanzania Omari Kimweri  anaefanya shughuli zake Australia akimsikilizia mpinzani wake baada ya kumtwanga kumi nzito na kuhesabilwa wakati wa mpambano wake ata hivyo mpinzani wake akuendelea na kufanikiwa kupata ushindi wa K,O ya raundi ya kwanza

Mabondia wa Tanzania huuza mechi zao Ulaya?http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2011/11/Rashid-matumla.png
Rashid Matumla 'Snake Man'

Benson Mwakyembe
 

http://www.ibn-tv.com/wp-content/uploads/2012/02/Nyilawila.jpg
Karama Nyilawila aliyetwaa ubingwa wa WBF Ulaya

MABONDIA Mada Maugo na Benson Mwakyembe Jumamosi walipokea vipigo nchini Russia katika mapambano yao ya kimataifa, huku kukiwa na tuhuma kwamba mabondia wengi wa Kitanzania wanaoenda kupigana nje ya nchi 'huuza' mechi zao.
Maugo alipokea kichapo cha TKO ya raundi ya 5 katika pambano la raundi 8 dhidi ya bondia asiye na uzoefu Movsur Yusupov aliyecheza mapambano manne tu kulinganisha na Mtanzania huyo aliyepigana michezo 25.
Mtanzania mwingine, Mwakyembe alidundwa kwa KO ya raundi ya 7 ya pambano lake la raundi 8 dhidi ya bondia mwingine asiye na uzoefu Apti Ustarkhanov, ambaye hilo lilikuwa ni pambano lake la tatu na la pili kushinda tangu aingie kwenye ngumi za kulipwa.
Kina Maugo walipambana dhidi ya wenyeji wao katika mapambano ya uzito wa Super Middle ya raundi nane yaliyofanyika katika ukumbi wa Trade & Entertainment Centre 'Moskva', Kaspiysk chini ya wakala Mkenya Thomas Mutua.
Vipigo vya mabondia hao vimekuja wakati wadau wa ngumi za kulipwa wakihoji sababu zinazofanya mabondia wa Kitanzania kushindwa kutamba kila waendapo nje huku ripoti mbalimbali zikiwatuhumu mabondia wa majuu kuwatumia mabondia kutoka Afrika kupandisha chati zao katika viwango vya ubora kwa kuwanunua wawaachie washinde.
Ripoti za kuuzwa mechi au kuwapo kwa mchezo mchafu ziliwahi kutolewa na baadhi ya mabondia akiwamo Pascal Ndomba na Francis Cheka aliyepokea kichapo cha kushangaza mapema mwaka huu nchini Ujerumani.

Ndomba anayepigana uzito wa juu wa (Cruiserweight), alisema baadhi ya mawakala wa nje hutaka mabondia dhaifu wa kwenda kupigana na mabondia wao ili kupata ushindi kirahisi na kuboresha rekodi zao.
"Hili ndilo linalofanyika, bondia mkali mara chache sana kupelekwa nje na hata akienda basi atahujumiwa ili apoteze mchezo kwa manufaa ya mabondia wanaoenda kupigana nao," Ndomba alisema hivi karibuni.
Naye Cheka alitoa maelezo ya kufanyiwa 'hila' katika pambano lake dhidi ya Uensal Arik aliloongoza kwa raundi sita za mwanzo kabla ya kurushiwa kitaulo katika raundi ya saba na kupoteza mchezo kwa TKO.

Pascal Ndomba
"Sikupoteza pambano lile, ila mwenyeji alibebwa na mwamuzi aliyemaliza pambano kana kwamba nimesalimu amri, ni vigumu mabondia wa Tanzania kushinda nje," alisema Cheka mara alipotua nchini.
Cheka alisema kambi ya mpinzani wake walimfuata hadi hotelini alipofikia kuelekea pambano lao kumshawishi awaachie pambano hilo kwa ahadi ya pesa lakini alipokataa ndipo alipokuja kuhujumiwa ulingoni kwa mtu aliyekuwa upande wa kona yake kurusha taulo ulingoni ilhali alikuwa akiongoza kwa pointi.
Bondia huyo anayeaminika kuwa bora zaidi nchini kwa sasa katika uzito wake, alisema hakuambatana na kocha wake wakati akienda katika pambano hilo hivyo hata kwenye kona yake walikuwa wenyeji wake na ndiyo waliorusha taulo ulingoni.
Hata hivyo, wapo waliomtuhumu kwamba huenda Cheka alicheza 'dili' na wakala wa pambano hilo ili kutotibua rekodi ya mpinzani wake ambaye alikuwa amepoteza pambano moja tu ya 18 aliyokuwa amecheza.
NIPASHE ilizungumza na Marais wa Mashirikisho ya Ngumi za Kulipwa Tanzania, Emmanuel Mlundwa wa PST na Yasin Abdallah 'Ustaadh' wa TPBO kutaka kujua ukweli kuhusu tuhuma hizo, ambapo walikuwa na maoni tofauti .
Mlundwa alisema kinachowaponza mabondia wa Tanzania siyo hujuma wala nini ila maandalizi duni wanayofanya kabla ya mapambano yao pia kuwa na viwango duni kulinganisha na wapinzani wao wanaoenda kucheza nao.

"Ngumi za kulipwa ni biashara, mabondia wa ngumi hizo wanapotafutiwa mechi wanapaswa kujiandaa, lakini hilo halifanyiki na hivyo kwenda kulitia aibu taifa na kujiharibia soko wao wenyewe bila kujua," alisema Mlundwa.
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa ngumi, alisema siyo kweli kama kuna rushwa zinazofanyika bali Watanzania wanaopewa nafasi kulingana na rekodi zao nchini huenda kupigana kichovu kwa kukosa maandalizi mazuri.
Ustaadh yeye alisema
Francis Cheka
linalowaangusha mabondia wa Tanzania nje ya nchi ni maisha wanayoishi kuwa kinyume na nidhamu ya ngumi za kulipwa na kwamba kutokuwa na mameneja ni tatizo jingine linalowakwaza.
"Mabondia wengi hawafanyi mazoezi mpaka wakati wa pambano, hapo unatarajia afanye vizuri? Pia hawaishi kwa kuzingatia miiko ya ngumi na hivyo wanapoenda nje ni rahisi kupigwa na kuhisiwa labda wanauza," anasema.

Alisema ni vyema mabondia wakafanya kazi chini ya mameneja kama ilivyokuwa kwa Rashid Matumla kwani itafanya ajikite kwenye mazoezi tu na mambo mengine kuwaachia meneja zao.
Ustaadh alisema majukumu wanayobeba mabondia ya kufanya kila kitu wakati mwingine huwafanya washindwe kujikita kwenye mazoezi na hivyo kujikuta muda wa pambano ukifika hawajajiandaa vizuri.
Rais huyo wa TPBO-Limited, alisema pia mabondia wengi hutoa visingizio kila wanapopigwa nje ya nchi bila kuangalia kama sheria za ngumi zinasemaje wanapokuwa kwenye ulingo na kutolea mfano pigano la Cheka na Arik.
"Cheka alipolalamika nilimuuliza vipi katika pambano lake na Arik, hakutupa ngumi yoyote katika raundi ya 7 na kupigwa makonde mfululizo na kunieleza mkono wa kulia ulimzingua, sheria zinasema bondia asipojibu mapigo kwa zaidi ya ngumi 10 alizorushiwa refa anaweza kuvunja pambano au wasaidizi wa bondia kuingilia kati kwa kurusha kitaulo na ndivyo ilivyotokea," alisema.
Mada Maugo

NGUMI KUPIGWA RUVUMA SIKU YA IDDI

MABONDIA OBOTE AMEME NA YUSUFU JIBABA WA DAR-ES-SALAAM WATAPANDA ULINGONI  KUZIPIGA NA MABONDIA WA MKOA RUVUMA SIKU ZA IDDI-MOSI NA IDDI PILI KATIKA VIWANJA TOFAUTI.

WAKATI BONDIA HATARI NA MKONGWE OBOTE AMEME ATAZIPIGA NA BONDIA MUSSA CHITEPETE WA SONGEA KATKA UWANJA WA MAJIMAJI ULIOKO SONGEA MJINI ,

YUSUFU JIBABA ATAKWAANA NA ROY MBUNDA KATIKA UWANJA WA NGURUDOTO ULIOKO WILAYANI MBINGA ,

OBOTE AMEME ATAZIPIGA NA MUSSA CHITEPETE KATIKA UZITO MWEPESI [LIGHT WEIGHT] RAUNDI SITA  NAYE  YUSUSFU JIBABA ATAZIPGA NA ROY MBUNDA KATIKA UZITO WA JUU MWEPESI [LIGHT HEAVY] PIA RAUNDI 6.

PROMOTA WA MAPAMBANO HAYA NI NDG GODFREY LUDOVICK ,MAARUFU SANA KWA JINA LA MGOGO ,MFANYABIASHARA WA MKOANI RUVUMA ,WILAYA YA SONGEA MJINI.

TPBO -LIMITED IMESHATOWA VIBALI  KWA PROMOTA HUYO ILI AWEZE KUANDAA MAPAMBANO HAYO, NA PIA INAMPONGEZA KWA KUHAMASISHA MCHEZO WA MASUMBWI KATIKA MIKOA YA KUSINI ,NA TPBO-LIMITED INAAHIDI KUMPA USHIRIKIANO MKUBWA PROMOTA HUYO KATIKA MAPAMBANO HAYA NA YAJAYO.

NA INAWATAKA WANANCHI WAKAAZI WA WILAYA HIZO KUJITOKEZA KWA WINGI SIKU HIZO ILI KUWASHUHUDIA MABONDIA HAO WAKIMENYANA VIKALI. PIA WAPENZI  WANAOMBWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU SIKU HIZO WAKATI WA MAPAMBANAO HAYO.

                                         IMELETWA KWENU NAMI;-

                                     yassni abdallah mwaipaya -ustaadh
                       rais- tanzania professional boxing organisation limited

MABONDIA WA BIGRIGHT BOXING GYM WAJIFUA KUWAKABILI WAPINZANI


Mabondia wa bigright boxing ya mwananyamala wapo kambini wakiendelea kujifua kwa ajili ya kuwakabili wapinzani  wao ambao watazichapa nao katika wakati tofauti na maeneo mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.
Mabondia hao ni  issa omar anaetarajiwa kuzipiga katika ukumbi wa Government complex nchini zambia na Pethias Chisonga wa Zambia chini ya uratibu wa Exodus Stable ya nchini humo. Hapa dare s salaam friends corner hotel Mustafa doto atazipiga na rajab mjeshi, martin Richard na mbena Rajab wao watakuwa mkoani Tanga huku zumba kukwe akizipiga kibaha na mabondia waliobaki watamsidikiza Daudi Anthony’odinga’ kuzipiga tom-po  katika ukumbi wa eagles  pub Bagamoyo. Katika mapambano ya bagamoyo yameratibiwa na Tan academy chini ya kiongozi wake Japhet kaseba yatakuwa  na ushindani mkali sana kwa wanafunzi watano wa kaseba watakapozipiga na wanafunzi wa bigright nje ya mkoa wao

mabondia wa DAR na songea -IDD MOSI NA IDDI PILI KUZITAWANGA

Bondia YUSUFU JIBABA kushoto akitunishiana masuri na Shabani Mhamila 'Star Boy; mpambano wake uliopita
 
 
 
 
 
MABONDIA OBOTE AMEME NA YUSUFU JIBABA WA DAR-ES-SALAAM WATAPANDA ULINGONI  KUZIPIGA NA MABONDIA WA MKOA RUVUMA SIKU ZA IDDI-MOSI NA IDDI PILI KATIKA VIWANJA TOFAUTI.

WAKATI BONDIA HATARI NA MKONGWE OBOTE AMEME ATAZIPIGA NA BONDIA MUSSA CHITEPETE WA SONGEA KATKA UWANJA WA MAJIMAJI ULIOKO SONGEA MJINI ,

YUSUFU JIBABA ATAKWAANA NA ROY MBUNDA KATIKA UWANJA WA NGURUDOTO ULIOKO WILAYANI MBINGA ,

OBOTE AMEME ATAZIPIGA NA MUSSA CHITEPETE KATIKA UZITO MWEPESI [LIGHT WEIGHT] RAUNDI SITA  NAYE  YUSUSFU JIBABA ATAZIPGA NA ROY MBUNDA KATIKA UZITO WA JUU MWEPESI [LIGHT HEAVY] PIA RAUNDI 6.

PROMOTA WA MAPAMBANO HAYA NI NDG GODFREY LUDOVICK ,MAARUFU SANA KWA JINA LA MGOGO ,MFANYABIASHARA WA MKOANI RUVUMA ,WILAYA YA SONGEA MJINI.

TPBO -LIMITED IMESHATOWA VIBALI  KWA PROMOTA HUYO ILI AWEZE KUANDAA MAPAMBANO HAYO, NA PIA INAMPONGEZA KWA KUHAMASISHA MCHEZO WA MASUMBWI KATIKA MIKOA YA KUSINI ,NA TPBO-LIMITED INAAHIDI KUMPA USHIRIKIANO MKUBWA PROMOTA HUYO KATIKA MAPAMBANO HAYA NA YAJAYO.

NA INAWATAKA WANANCHI WAKAAZI WA WILAYA HIZO KUJITOKEZA KWA WINGI SIKU HIZO ILI KUWASHUHUDIA MABONDIA HAO WAKIMENYANA VIKALI. PIA WAPENZI  WANAOMBWA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU SIKU HIZO WAKATI WA MAPAMBANAO HAYO.

                                         IMELETWA KWENU NAMI;-

                                     yassni abdallah mwaipaya -ustaadh
                       rais- tanzania professional boxing organisation limited

Monday, July 29, 2013

SUPER D SUPER COACH ALIPO JUMUHIKA NA NDUGU NA JAMAA ZAKE WA KARIBU KUFUTURU NYUMBANI KWAKE

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na jamaa na ndugu zake baada ya kupata futali ya pamoja  nyumbani kwake wakati wa chungu 20 Ramadhani
SUPER D AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA NDUGU ZAKE NA MARAFIKI

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D'  Katikati akiwa katika picha ya pamoja na jamaa na ndugu zake baada ya kupata futali ya pamoja  nyumbani kwake wakati wa chungu 20 Ramadhani

Super D akipata futari na Ibrahimu Kamwe
Super D akipata futari na Ibrahimu Kamwe

Super D akipata futari na Ibrahimu Kamwe

SUPER D

SUPER D KATIKA POZI

MPAMBANO MWINGINE WA MASUMBWI KUFANYIKA IDI MOSI
kocha kwame mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' jinsi ya kutupa makonde mazito mazito Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na SUPER D Bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Idi Mosi jijini Dar es salaam katika ukumbi wa friends Corner Manzese akizungumzia maandalizi ya mpambano huo mtaalishaji Waziri Rosta amesema mpambano huo wa uzito wa juu umekuwa gumzo katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kwani mabondia hawo wanatafutana kwa mda mrefu sana na sasa wamekutana kwa ajili ya mchezo huo Mpambano huo wa raundi 8 siwakukosa kwani ndio mpambano pekee kwa mwaka huu kukutanisha uzito wa juu kwani mabondia wa uzito huu  wanaotamba viwango vyao ni vidogo ukizingatia kuwa wapo wachache nchini aliongeza kuwa mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi na wanaotamba hapa nchini Na kwa upande wa kocha anaemnoa bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' amesema kuwa bondia wake alikuwa na manyama nyama mengi lakini kwa sasa akuna kutokana na mazoezi anayompatia kwani kwa sasa dozi yake ni kutwa mara tatu na mpaka siku ya mchezo naisi mambo yatakuwa safi Mpambano huo utakao sindikizwa na mabondia Hassani Mandula atakae pambana na Twalib Mchanjo na Fadhili Majia atakae menyana na Ally Mahiyo na Mustapha Doto atapambana na Hashimu Mjeshi mapambano yote ya utangulizi itakuwa ni ya raundi sita
Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
 
DVD hizo mpya ni kati ya  
mike tyson vs evander holyfield na felix trinidad vs roy jones jr

Felix 'Tito' Trinidad vs Pernell Whitaker

ambapo dvd hizo zilizo rekodiwa kwa ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mchezo wa masumbwi nchin


--
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
           mhamila1@gmail.com
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Sunday, July 28, 2013

MADA MAUGO NA BENSON MWAKYEMBE WACHEZEA VICHAPO TOKA KWA WARUSSIAMAUGO
BONDIA mada maugo  mwishoni mwa wiki iliyopita alichezea kichapo kutoka kwa  Movsur Yusupov wa Russia  katika mpambano uliopagwa kupigwa kwa raundi nane hata hivyo Maugo alipigwa kwa TKO ya raundi ya tano

ambapo Maugo alisalim amri kwa kupoteza mchezo huo ulifanyika katika viwanja vya Trade And Entertainment Centre "Moskva", Kaspiysk, Russia mwishoni mwa wiki iliyopita

Baada ya kupoteza mchezo uho August 30 atapanda tena uringoni kukabiliana na Thomasi Mashali mpambano wa ubingwa wa WBF Africa uzito wa kati mpambano utakaokuwa wa raundi 12
mwakyembe

Nae bondia benson mwakyembe alikuwa na kibarua kizito siku hiyo hiyo nae alikubali kichapo cha K,O ya raundi ya 7 katika mpambano wa raundi 8

Mabondia wote wawili walionesha kuwa na viwango vya kutosha ila walizidiwa ufundi na maarifa ya mchezo wa masumbwi uringoni
Mchezo wa masumbwi umekuwa ukipanda umaarufu siku adi siku baada ya mabondia wengi kutoka nje ya nchi kwenda kushiriki michezo mbalimbali katika nchi nyingine ambapo imeleta muhamko wa mchezo huo kupendwa na watu wengi zaidi ingawa wadhamini wanaukwepa kwa ajili ya kuwekeza katika mchezo huo

Hata hivyo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini   Rajabu Mhamila 'Super D' amekuwa akitoa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi akitumia mabondia kutoka mataifa yanayofanya vizuri katika mchezo huo ili kujua mbinu mbalimbali wanazotumia

Saturday, July 27, 2013

MPAMBANO MWINGINE WA MASUMBWI KUFANYIKA IDI MOSIkocha kwame mkuluma kulia akimwelekeza Bondia Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' jinsi ya kutupa makonde mazito mazito Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na SUPER D Bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' yupo kambini kwa ajili ya kupambana na bondia Bahati Mwafyela mpambano utakaofanyika siku ya sikukuu ya Idi pili jijini Dar es salaam katika ukumbi wa friends Corner Manzese akizungumzia maandalizi ya mpambano huo mtaalishaji Waziri Rosta amesema mpambano huo wa uzito wa juu umekuwa gumzo katika jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kwani mabondia hawo wanatafutana kwa mda mrefu sana na sasa wamekutana kwa ajili ya mchezo huo Mpambano huo wa raundi 8 siwakukosa kwani ndio mpambano pekee kwa mwaka huu kukutanisha uzito wa juu kwani mabondia wa uzito huu  wanaotamba viwango vyao ni vidogo ukizingatia kuwa wapo wachache nchini aliongeza kuwa mbali na mpambano huo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi na wanaotamba hapa nchini Na kwa upande wa kocha anaemnoa bondia  Iddy Kipandu 'Iddy Bonge' amesema kuwa bondia wake alikuwa na manyama nyama mengi lakini kwa sasa akuna kutokana na mazoezi anayompatia kwani kwa sasa dozi yake ni kutwa mara tatu na mpaka siku ya mchezo naisi mambo yatakuwa safi Mpambano huo utakao sindikizwa na mabondia Hassani Mandula atakae pambana na Twalib Mchanjo na Fadhili Majia atakae menyana na Ally Mahiyo na Mustapha Doto atapambana na Hashimu Mjeshi mapambano yote ya utangulizi itakuwa ni ya raundi sita
Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zitakazokuwa zikisabazwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
 
DVD hizo mpya ni kati ya  
mike tyson vs evander holyfield na felix trinidad vs roy jones jr

Felix 'Tito' Trinidad vs Pernell Whitaker

ambapo dvd hizo zilizo rekodiwa kwa ubora wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mchezo wa masumbwi nchin


--
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
           mhamila1@gmail.com
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

UCHAGUZI WA BFT KUFANYIKA MOROGORO SASA