Tangazo

Pages

Friday, March 12, 2021

BONDIA JONAS SEGE NA TWAHA KIDUKU KUPANDA ULINGO MMOJA MARCH 19 NA MABONDIA WA MATAIFA MENGINE


 Na Mwandishi Wetu


BONDIA Jonas Segu 'Black Mamba' ametamba kumpiga mpinzani wake Hanock Phili kutoka Malawi akizungumza mbele ya wahandishi wa habari kusiana na mpambano wake uho utakaofanyika March 19 katika ukumbi wa Ubungo Plaza


Segu amesema kuwa yeye alienda nchini Africa ya kusini na kuhishi uko kwa ajili ya mchezo wa ngumi na kufanikiwa kuchukuwa ubingwa wa  WBF ambao ata utetea siku hiyo ata hivyo amekuwa apati mapambano ya ndani kutokana na mabondia wengi kumkwepa baada ya kutembeza kipigo kwa mabondia kadhaa wa Tanzania

ambapo alishawai kumchapa Habibu Pengo Idd Pialali na alifanikiwa kumchapa Mfaume Mfaume ata hivyo kutokana na Figisu majaji wakatoa Droo sasa nimeruni nchini Tanzania na mpambano huu ndio utakuwa wa kwanza kwangu kucheza baada ya miaka mitano iliyopita ambapo sijacheza katika ardhi ya Tanzania naomba mashabiki wa ngumi morogoro dar es salaam pwani Tanga na mikoa mingine yote waje kuona ngumi ambazo zenye radha na manufaa katika mchezo huu wa tarehe 19 march


nae promota wa mpambano huo Evalist Elnest 'Mopao' amesema mbali na mpambano huo kutakuwa pia na mpambano wa Twaha Kiduku na Tishibangu Kayembe wa Kongo na mpambano wa kina dada utakao wakutanisha  Najma Isike na Halima Bandola pia kutakuwa na takribani jumla ya mapambano nane tu kwa siku hiyo


hivyo naomba wapenzi wa ngumi waje mapema kuangalia ngumi nzuri zilizo andaliwa vema kabisa kwa galama nafuu kabisa