Tangazo

Pages

Thursday, February 28, 2013

MNAMIBIA KUUMANA NA MGHANA UBINGWA WA IBF.


  Albinus (kushoto) akifanya vitu vyake
 Thursday, February 28, 2013 - Dar-Es-Salaam, TANZANIA- Siku kubwa na yenye matumaini mapya katika maisha ya bondia wa Namibai Albinus Felesianu (9(4)-2(1)-0) itawadia hivi karibuni wakati atakapokutana na bodia Herbert Quartey (10(7)-8(6)-0) wa Ghana kugombea ubingwa wa IBF wa dunai uzito wa Unyoya (Featherweight). Albinus alipata mshtuko mkubwa sana na kushangzwa na habari za hivi karubunI kuwa IBF imempa nafasi ya kugombea ubingwa wa dunia wa vijana jambo lililomfanya apate furaha ya ajabu. Albinus Felesianu Albinus (kushoto) akifanya vitu vyake Mtu pekee atakayeweza kuzima furaha yake na kumfanya asiweze kufikia malengo yake katika ngumi ni bondia Herbert Quartey kutoka Ghana ambaye ni moja kati ya mabondia wenye ujuzi mubwa wa kupigana ulingonI. Kama inavyosemwa kuwa "mtoto mtukutu aliyepotea kwenye ngumi anapoomba kurudi kundini na kukaa kufuata kanuni na shaeia za ngumi mchezo wa ngumi humpokea kwa shangwe na nderemo na kumpa mawaidha na ushauri wa kumwendeleza" ndivyo hivyo hivyo Albinus Felesianu na Herbert Quartey watakavyopokelewa na ngumi baada ya pambano lao la tarehe 29 Machi jijini Windhoek, Namibia. Bondia Albinus Felesianu yuko chini ya promosheni ya Kinda Nangolo ambaye anamiliki kampuni tanzu ya Kinda Boxing Promotion na ni promota anayeinukia kwa kasi sana katika tasnia ya ngumi nchini Namibia na barani Afrika

Wednesday, February 27, 2013

WATOTO WA NKRUMAH ISSAH SAMIR NA PHILIP KOTEY KUPANDA ULINGONI MACHI 30 KUWANIA UBINGWA WA AFRIKA UZITO WA MIDDLE
Philip Koyey akichapa makonde na bondia Kelly Brook wa Uingereza.

Nchi ya Ghana iko katika hekaheka za mapambano kadhaa ya ngumi mwezi wa Machi tarehe 30 wakati ubingwa maarufu wa middle weight utakapo gombaniwa na mabondia Issah Samir na Philip Kotey.

Mabondia wawili hao ni maarufu sana katika tasnia ya ngumi nchini Ghana na barani Afrika kwa ujumla, ambao watakutana wakati wanapogombea mkanda wa IBF AMEPG uzito wa middle.
Muziki wa aina ya Tangle unahitaji watu wawili kuucheza na ndivyo hivyo miamba hii miwili itakapokutana kwenye 'muziki wa masumbwi' ulingoni wakati mabondia hao watakapokuwa wakionyeshana umwamba na kuwadhihirishia mashabiki wa masumbwi katika bara la Afrika kuwa wanasifa hizo kama wanavyotambulika.
Pambano hilo linaandaliwa na GoldMike Boxing Promotions Syndicate, kampuni inayoongozwa na bw. Michael Tetteh pamoja na kigunge mmoja wa biashara za vyakula vilivyokaushwa wa Ghana bw. Henry Many-Spain ambaye pia ni Makamu wa Rais wa IBF Africa idara ya fedha.
Kwa maana hiyo miamba hiyo inatarajia kukutana na kupanda jukwaani Machi 30,katika mpambano uliopewa jina la “Watoto wa Nkrumah” jina lilaloheshimika sana katika nchi ya Ghana kutokana na Rais wake wa kwanza Mh. hayati Kwame Nkrumah.   
Nchi ya Ghana imetokeza kuwa maarufu katika michezo na inajizatiti kuendeleza michezo yote hususan mpira wa miguu na ngumi. Ni nchi ambayo imeshawahi kutoa mabingwa wengi wa dunia kama kina Azumah Nelson na Ike Quartey ambao walikaa na mataji ya ubingwa wa ngumi kwa miaka kadhaa na kulitangaza vyema bala la Afrika.
Sasa ni juu ya miamba hii miwili kufuata nyayo za akina Azumah Nelson, Ike Quartey, Joseph Agbeko na wengine wengi!
ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

Tuesday, February 26, 2013

RAMADHANI SHAURI KUZIPIGA 8-03-2013 JIJINI MOSCO -URUSI

        TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI-MICHEZO


NDUGU ZANGU WAPENDWA KATIKA MICHEZO ,

NINAYO FURAHA KUBWA SANA NA HESHIMA MBELE YENU KUWAARIFU KWAMBA BONDIA WETU

SHUJAA WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA RAMADHANI SHAURI ,BINGWA WA IBF-AFRIKA TAREHE 8-03-2013 ATAPANDA ULINGONI JIJINI MOSCO -URUSI KUZIPIGA NA BONDIA EDUARD TROYANOVSKY ,KATIKA PAMBANO LA RAUNDI KUMI NA MBILI [12]

BONDIA HUYU MTANZANIA ANAONDOKA NCHINI TANZANIA KESHO JUMATANO ALFAJIRI KWA USAFIRI WA BASI LA DAR-EXPRESS KUELEKEA JIJINI NAIROBI KUUNGANA NA WAKALA WAKE NDG FRANKLYN IMENZI TAYARI KWA MAANDALIZI YA MWISHO IKIWA NI PAMOJA NA KUJARIBU KUIZOWEA HALI YA HEWA YA BARIDI YA NAIROBI  AMBAYO ANALINGANA KABISA NA HALI YA HEWA YA URUSI.

HII NI MARA YA KWANZA KWA RAMADHANI SHAURI KIZIPIGA NJE YA TANZANIA ,NA TPBO ILIPENDEKEZA JINA LAKE BAADA YA KURIDHIKA NA KIWANGO ALICHONACHO ,

NI KIZURI SANA NA PIA ANAYO NIDHAMU YA HALI YA JUU SANA IKIWA NI PAMOJA NA KUTOKUTUMIA MADAWA YA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI IKIWEMO BANGI.


TPBO-LIMITED IMESHAMPATIA KIBALI BONDIA HUYO ILI AKAPAMBANE NA KUONYESHA UWEZO WAKE HUKO RUSSIA ,NA INAMTAKIA MAFANIKIO MAZURI.


KAMA TPBO-LIMITED ILIVYOAINISHA MIKAKATI YAKE KATIKA MWAKA HUU 2013 KWAMBA ITAJITAHIDI KUJENGA MAHUSIANO MAZURI NA MAWAKALA WA NGUMI ZA KULIPWA WA SEHEMU MBALIMBALI ZA ULIMWENGU ILI WAWAPATIE MAPAMBANO MENGI MABONDIA WA TANZANIA,

 TUNAMSHUKURU MUNGU KWAMBA MIKAKATI YETU IMEANZA KUZAA MATUNDA.


                    TAARIFA HII IMELETWA KWENU NAMI
                   YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                       RAIS -TPBO-LIMITED

Monday, February 25, 2013

IBRAHIMU MAOKOLA AJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO WAKE MARCH 2


Bondia Ibrahimu Maokola akifanya mazoezi ya kupiga panch bag wakati wa kujiandaa na mpambano wake na Rajabu Majeshi utakaofanyika katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa March 2  Mpambano huo utakua wa utangulizi kabla ya mpambano wa Maneno Osward na Japhert Kaseba,Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

VITA YA UBINGWA WA IBF AFRICA "RICHARD COMMEY NA BILAL MOHAMMED"
Kuna hekaheka nyingi kwenye jiji la Accra, nchini Ghana wakati wa pambano la kugombea ubingwa wa dunia kati ya bondia marufu Joseph Agbeko kutoka Ghana na Luis Mendenez bondia anayetoka katika nchi ya Amerika ya Kusini ya Columbia watakapokutana siku ya jumamosi tarehe 8 Machi.

Kati ya mapambano ya utangulizi bondia anayeinukia kwa kasi Richard Commey atakutana na bondia mwenzake wa Ghana Bilal Mohammed kugombea mkanda wa IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika uzito mwepesi (Lightweight).

Wawili hao wanatoka katika kambi mbili zinazohasimiana kwa siku nyingi na mpambano wao unategemea kuwa wa kasi, ufundi na wenye kusisimua katika raundi zote 12.

Mpambano wa Richard Commey (khttp://www.youtube.com/watch?v=IBG5a9LtIhU) na Bilal Muhammed umekuwa gumzo kubwa katika jiji la Accra pamoja na majiji mengine katika Afrika ya Magharibi. Hii inatokana na umaarufu wa promota na meneja wa Ruchard Commey Mghana Michael Amoo Bediako anayeishi barani Ulaya akiwa na makazi yake nchini Uingereza kuwa mtu aneyeshughulika na mabondia wenye vipaji vya hali ya juu.

Richard Commey atapenda kuwadhihirishia wapenzi wake kuwa yeye ndiye Mfalme wa Afrika katika uzito wa mwepesi (Lightweight) na hakuka atakayeweza kumzuia katika mipango yake ya kupanda ngazi. Naye Bilal Muhammad atapenda kuudhihirisia ulimwengu kuwa sio bondia anayeweza kusukumwa sukumwa na kwamba ubingwa wa IBF AMEPG katika uzito wa Lightweight na wake.

Imetolewa na:

ISSUED BY:
INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)

DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

Friday, February 22, 2013

MANENO OSWARD ATAMBA KUMCHAKAZA KASEBA MARCH 2


Bondia Maneno Osward akijifua kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa dhidi ya Japhert Kaseba March 2 katika ukumbi wa DDC Madomeni Kondoa Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' akifanya mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa dhidi ya Japhert Kaseba March 2 katika ukumbi wa DDC Madomeni Kondoa Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Maneno Osward kushoto na Japhert Kaseba walipokutana kwa ajili ya kuzungumzia mpambano wao utakaofanyika March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni Kondoa Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Maneno Osward ametamba kumchakaza mpinzani wake Japhert Kaseba kunako raundi za awali akizungumza na mwandishi wa habari hizi maneno maarufu kwa jina la Mtambo wa Gongo amesema yeye yupo fiti na anasubili hiyo March 2 katika ukumbi wa DDC Magomeni kondoa apate kumshikisha adabu 

Kaseba ni bondia mchanga sana kwangu nilimkaribisha katika masumbwi na sasa nitamstafisha masumbwi mimi mwenyewe kwa kipigo nitakacho mpa na atajua kwa nini nimepewa jina la mtambo wa Gongo

Katika mpambano huo kutakuwa na mpambano wa uzito wa juu kati ya Josefu Marwa na Alphonce Mchumiatumbo mpambano unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wa ngumi za uzito wa juu nchini 

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.

--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Thursday, February 21, 2013

MAKOCHA WA MASUMBWI WAHITIMU KOZI YA HAWALI

Meja Charles Mbuge wa pili kushoto akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya Hawari ya ukocha wa mchezo wa masumbwi,Charles Muhilu wakati wa kumalizika kwa kozi hiyo Dar es salaam leo kushoto ni mjumbe wa BFT, Koba Kimanga na Rais wa shirikisho hili, Michael Changalawe.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya makocha wa mchezo wa masumbwi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimu mafunzo ya awali yaliyomalizika Dar es salaam (Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Meja Charles Mbuge akihojiwa na wana habari wakati wa kufunga mafunzo hayo leo
Mmoja ya wakufunzi Kulwa Kindondi akiojiwa na wandishi wa habari
kocha Charles Muhilu kushoto akihojiwa kuhusu kozi hiyo
Mmoja ya wakufunzi Kulwa Kindondi kushoto akiwa na Patric Nyembela wa EATV picha na  www.superdboxingcoach.blogspot.com

Wednesday, February 20, 2013

Floyd Mayweather alamba mkataba mnono


Floyd Mayweather
 
BONDIA bingwa wa Dunia mkanda wa WBC Floyd Mayweather Jr  ambaye ajawai kupigwa wara kutoka droo rekodi yake won 43 (KO 26) + lost 0 (KO 0) + drawn 0 = 43  ameingia mkataba wa kumwezesha kupigana hadi mara sita zaidi ya kipindi cha miezi 30. mkataba uho mnono utakao mfanya awe mwana michezo wa kwanza duniani kuingia mkataba mkubwa kuliko mwana michezo yoyote 

Mkataba uho utanza kwa mara ya kwanza kwa kupambana na Robert Guerrero Mei 4 ambapo kuna mfanya awe na mpambano mmoja tangia mwaka jana mei 5 kumtwanga bondia Miguel Cotto na kuamliwa kwenda jela baada ya kuitalifiana na mpenzi wake tangia atoke jela ajawai kucheza na ndipo anapokutana na Robert Guerrero mwenye rekodi won 31 (KO 18) + lost 1 (KO 0) + drawn 1 = 35 

Mkataba huo utausisha matangazo mbali mbali ya kwenye TV yatakayo muwezesha kumiliki mlungula kwa kwenda mbele kwa kipindi chote hicho bondia huyo anayekubalika kwa sasa hususani kwa stayl yake ya kujikinga na kupiga kumi kwa kushtukiza

MCHEZO WA Taichi Kung-fu WAENDELEA KUHAMASISHWA


Mkufuzi wa mchezo wa Taichi Kung-fu, Jumanne Wilsoni 'Masta Jumanne' (kulia) akitoa mafunzo ya mchezo huo Dar es salaam jana katika jengo la CCM Ilala Dar es salaam jana.
(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mkufuzi wa mchezo wa Taichi Kung-fu, Jumanne Wilsoni 'Masta Jumanne' (kulia) akitoa mafunzo ya mchezo huo Dar es salaam jana katika jengo la CCM Ilala Dar es salaam jana.
(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Monday, February 18, 2013

MAPAMBANO MAWILI YA IBF AFRIKA KUFANYIKA MWEZI UJAO

Likiwa limetokea kwenye wiki la mafanikio makubwa katika majijini ya Johannesburg nchini Africa ya Kusini na Tunis, Tunisia ambako iyalifanyika mapambano mawili ya ubingwa wa dunia kwa vijana na ubingwa wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, ambako Illunga Makabu wa Jamhuri ya Watu wa Kongo
(DRC) aliukwea ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito wa Cruserweight baada ya kumsambaratisha Gogito Gorgizadze kutoka nchini Georgia. Aidha bondia Ayolub Nefzi wa Tunisia anayeishi nchini Belgium kumkata ulimi bondia Ishmael Tetteh kutoka nchi ya Ghana,  Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa)  linajiandaa tena kwa mapambvano mawili makubwa mwezi ujao.

Safari hii vita kubwa itafanyika katika nchi ya iliyowahi kujulikana kama Pwani ya Dhababu au Gold Coast (Ghana) katika jiji la Accrah wakati bondia anayechipukia kwa kazi Richard Commey wa Ghana anayeishi katika jiji la London nchini Uingereza atafuana na Mghana mwenzake Bilal Mohammed ambaye anatoka katika moja na viunga maarufu kwa kutoa mabingwa wa dunia cha Lenanon katika jiji la Accrah nchini Ghana kugombea mkanda wa IBF Africa katika uzito mwepesi  au lightweight.

Wawili hao wanakutana katika pambano la utangulizi wakati bondia bingwa wa dunia wa zamani wa IBF katika uzito wa Bantam Joseph Agbeko atakapochuana na Luis Melendez kutoka nchini Columbia iliyoko Amerika ya Kusini kugombea ubingwa wa dunia katika uzito wa Bantam.

Mpambano mwingine ambao utawakutanisha mabondia wawili wa Ghana wenye uzoefu mkubwa ni wa kugombea uzito wa Welter wakati bondia maarufu Frederick Lawson atakapokutana na bondia chipukizi Issac Sowah wakigombea ubingwa wa IBF katika bara la Afrika.

Ukweli utajulikana wakati huu ni nani kati ya mabondia hawa wanne watakaoibuka na mikanda ya ubingwa wa IBF.
 
ISSUED BY:

INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA

WATOTO WA NKRUMAH WAWANIA UBINGWA WA IBF


Bondia Franisic Cheka kushoto na Thomasi Mashali wakiwa wameushika mkanda wa ubingwa wa IBF Africa watakaogombania mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba wakati wa kutambulisha mpambano huo katikati ni Promota wa mpambano huo Tanaka Adam na Khalid Kibavu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 
Likiwa limetokea kwenye wiki la mafanikio makubwa katika majijini ya Johannesburg nchini Africa ya Kusini na Tunis, Tunisia ambako iyalifanyika mapambano mawili ya ubingwa wa dunia kwa vijana na ubingwa wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, ambako Illunga Makabu wa Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) aliukwea ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito wa Cruserweight baada ya kumsambaratisha Gogito Gorgizadze kutoka nchini Georgia. Aidha bondia Ayolub Nefzi wa Tunisia anayeishi nchini Belgium kumkata ulimi bondia Ishmael Tetteh kutoka nchi ya Ghana,  Shirikisho la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa)  linajiandaa tena kwa mapambvano mawili makubwa mwezi ujao.

Safari hii vita kubwa itafanyika katika nchi ya iliyowahi kujulikana kama Pwani ya Dhababu au Gold Coast (Ghana) katika jiji la Accrah wakati bondia anayechipukia kwa kazi Richard Commey wa Ghana anayeishi katika jiji la London nchini Uingereza atafuana na Mghana mwenzake Bilal Mohammed ambaye anatoka katika moja na viunga maarufu kwa kutoa mabingwa wa dunia cha Lenanon katika jiji la Accrah nchini Ghana kugombea mkanda wa IBF Africa katika uzito mwepesi  au lightweight.

Wawili hao wanakutana katika pambano la utangulizi wakati bondia bingwa wa dunia wa zamani wa IBF katika uzito wa Bantam Joseph Agbeko atakapochuana na Luis Melendez kutoka nchini Columbia iliyoko Amerika ya Kusini kugombea ubingwa wa dunia katika uzito wa Bantam.

Mpambano mwingine ambao utawakutanisha mabondia wawili wa Ghana wenye uzoefu mkubwa ni wa kugombea uzito wa Welter wakati bondia maarufu Frederick Lawson atakapokutana na bondia chipukizi Issac Sowah wakigombea ubingwa wa IBF katika bara la Afrika.

Ukweli utajulikana wakati huu ni nani kati ya mabondia hawa wanne watakaoibuka na mikanda ya ubingwa wa IBF.
 
ISSUED BY:

INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA)
DAR-ES-SALAAM, TANZANIA


For Immediate Release                                                 Media Contact: Onesmo Ngowi
IBF/Africa Notes 13                                                      Tel: (+255) 754- 360828

Friday, February 15, 2013

DVD MPYA ZA SUPER D BOXING COACH ZINAZOTARAJI KUINGIA SOKONI MWEZI UJAO

DVD YA MUHAMED ALI AMBAYO ITAKUWA NA HISTORIA YAKE MBALIMBALI KUHUSIANA NA MCHEZO WA MASUMBWI  DVD ZA MAFUNZO YA MCHEZO WA NGUMI ZIPO MTAANI KWA AJILI YA MAFUNZO YA MCHEZO HUO HIVI SASA KWA MATAJI YA JUMLA NA REJAREJA PIGA SIMU 0787/0774/0715/0754/0733/0713-406938 AU FIKA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI 0652755838
DVD ITAKAYOHUSISHA MIPAMBANO YA JUAN EMANUEL MARQUEZ
MPAMBANO HUNAO HUSISHA MAHASIMU WAWILI KATIKA MASUMBWI WANAOTAMBA DUNIANI MIGUEL COTTO VS ANTONIO MARGARITO ITAKUWA INAHUSISHA MIPAMBANO YAO YOTE MIWILI NA MINGINE KIBAO
DVD ITAKAYOMUHUSISHA MKALI WA MASUMBWI DUNIANI MANNY PAQUAIODVD INAYOHUSISHA MABONDIA WA TANZANIA AKIWEMO MMBWANA MATUMLA VS FRANSIC MIYEYUSHO NA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' VS SAID MUNDI NA ROGERS MTAGWA

MPAMBANO WA MASUMBWI ULIVYOFANYIKA SIKU YA WAPENDANAO

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila  'Super D' kushoto akipiga picha ya pamoja na Godfrey Silva baada ya kocha huyo kumzawadia vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo Flana ya SUPER D BOXING COACH Kikingia kinywa na DVD zenye mafunzo ya mchezo wa masumbwi kama zawadi kutoka kwa kocha huyo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Dkt, Milhael Arraham kushoto akimpima Afya Iddy Mnyeke kabla ya mpambano wake na Sadiki Momba jana

Bondia Cosmas Kibuga kulia akimshambulia kwa makonde Makali mawe wakati wa mchezo wao uliofanyika jana

Mashabiki na wapenzi wa mchezo wa masumbwi kutoka kambi ya Ilala akifatilia mpambao huo

Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Iddyt Mnyeke wakati wa mpambano wao uliofanyika jana momba alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Sadiki Momba kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Iddyt Mnyeke wakati wa mpambano wao uliofanyika jana momba alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Ramadhani Kumbele kushoto akioneshana kazi na Shabani Kilumbelumbe wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Kumbele alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mashabiki wa bondia toka kambi ya ilala Iddy Mnyeke wakiwa katika picha ya pamoja na bondia wao

Bondia Omar Ramadhani akishangilia ushindi baada ya kumpiga Deo njiku kwa point jana na kutawazwa kuwa bingwa wa taifa PST

Bondia Adamu Yahaya kushoto akipambana na Godfrey Slva wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Taifa unaotambuliwa na PST Silva alishinda kwa Point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Ibrahimu Class ' Kking Class Mawe' akifatilia mpambano wa masumbwi uliokuwa ukifanyika manzese Dar es salaam jana na Aasha Kamnyanga ' Mama Iikota' Mrs Super D Boxing Coach. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' akimkabidhi bondia Godfrey Silva vifaa vya mchezo wa masumbwi ikiwemo Flana, vikingia kinywa na DVD kwa ajili ya mafunzo ya mchezo uho picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila  'Super D' kushoto akipiga picha ya pamoja na Godfrey Silva baada ya kocha huyo kumzawadia vifaa mbalimbali vya michezo ikiwemo Flana ya SUPER D BOXING COACH Kikingia kinywa na DVD zenye mafunzo ya mchezo wa masumbwi kama zawadi kutoka kwa kocha huyo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Omary Ramadhani kushoto akijaribu kumkwepa bondia Deo Njiku wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana Ramadhani alishinda kwa point na kutangazwa kuwa bingwa wa Tanzania PST ,Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Deo Njiku wa Morogoro akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Omary Ramadhani wakati wa kugombania mkanda wa ubingwa wa Tanzania PST Ramadhani alishinda kwa Point .picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia wakisubili matokeo ya mchezo

Tuesday, February 12, 2013

MASHALI VS CHEKA WASANI KUCHEZA MEI MOSI


Mabondia Thomas Mashali kushoto akitunishiana misuli na Fransic Cheka wakati wa kutangaza mpambano wao wa masumbwi wa kugombea ubingwa wa IBF Africa utakaofanyika Mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Rais wa TPBO  Yassin Abdallah kulia akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa ubingwa Wa IBF kati ya Thomasi Mashali kushoto na Fransic Cheka ayupo pichani katikati ni Promota wa mpambano huo Tanaka Adam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Thomas Mashali kushoto akitunishiana misuli na Fransic Cheka wakati wa kutangaza mpambano wao wa masumbwi wa kugombea ubingwa wa IBF Africa utakaofanyika Mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam katikati ni Promota wa mpambano huo Tanaka Adam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Thomas Mashali kushoto akitunishiana misuli na Fransic Cheka wakati wa kutangaza mpambano wao wa masumbwi wa kugombea ubingwa wa IBF Africa utakaofanyika Mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Thomas Mashali kushoto akitunishiana misuli na Fransic Cheka wakati wa kutangaza mpambano wao wa masumbwi wa kugombea ubingwa wa IBF Africa utakaofanyika Mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Franisic Cheka kushoto na Thomasi Mashali wakiwa wameushika mkanda wa ubingwa wa IBF Africa watakaogombania mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba wakati wa kutambulisha mpambano huo katikati ni Promota wa mpambano huo Tanaka Adam na Khalid Kibavu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Thomas Mashali kushoto akitia saini mkataba wa makubaliano wa kucheza mpambano na Fransic Cheka kulia katikati ni Promota wa mpambano huo Tanaka Adam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Promota wa Mpambano wa ubingwa wa IBF Tanaka Adam katikati akiwaelekeza mabondia Thomas Mashali kushoto na Fransic Cheka jinsi ya kusaini ya mkataba wa makubaliano wa mpambano wao utakaofanyika mei mosi mwaka huu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Monday, February 11, 2013

BONDIA IBRAHIMU MAOKOLA AJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO

Bondia Ibrahimu Maokola akipiga beg wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mpambano wake utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia maneno Oswald kulia akimsimamia Ibrahimu Maokola wakati akipiga begi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Saturday, February 9, 2013

DEO NJIKU KUGOMBANIA UBINGWA WA TAIFA NA OMARY RAMADHANI February 14


Mabondia Omary Ramadhani kushoto na Deo Njiku wakitunishiana misuri baada ya kusaini mkataba kupigania ubingwa wa Tanzania PST siku ya February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Deo Njiku wa Morogoro na Omary Ramadhani wataingia uringoni  February 14 katika ukumbi wa Friends Corner Hotel Manzese 14 kuwania Ubingwa wa Tanzania PST 

Mpambano huo wa aina yake unatarajiwa kuwa wa kusisimua kutokana kila mtu kuwa na rekodi nzuri mpambano uho utakaosindikizwa na mpambano mwingine wa ubingwa kati ya  Godfrey Silver na Adam Yahya ambapo mipambano hiyo itakuwa ya raundi kumi
Huku kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' atampandisha kwa mara ya kwanza bondia wake mpya Iddy Mnyeke kuvaana na Sadiki Momba mpambano utakaopigwa kwa raundi nne

Mgeni rasmi siku hiyo anatsrahjiwa kuwa ni Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela atakaewafisha mikanda ya ubingwa

Super D, alisema katika mpambano huo atasambaza DVD zake mpya tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio,Juan Emanuel Marquez, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina.  michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition ” alisema.
 Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia  hii watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.   
Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana