Tangazo

Pages

Saturday, February 25, 2012

MATUMLA AMSAMBALATISHA MTAMBO WA GONGO

)
Refarii Antoni Luta katikati akimnyoosha mkono juu bondia Rashidi Matumla Snake Man kuashiria ushindi dhidi ya mpinzani wake maneno Osward Mtambo wa Gongo kushoto wakati wa mpambano wao uliochezwa Jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Matumla alishinda kwa point.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/


Mabondia Maneno Osward Mtambo wa Gongo (kushoto) na Rashid Malumla Snake Man Wakioneshana umwamba wa kutupa masumbwi wakati wa mpambano wao uliochezwa Jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Matumla alishinda kwa point.(Picha na www.superd boxingcoach.blogspot.com)

Date: 2012-02-25Venue: PTA Hall, Dar es Salaam , TanzaniaCommission: Pugilistic Syndicate of TanzaniaPromoter: Issa Malanga Promotion [1] Lightfly weight Moses Musa WPTS 4 rounds of a 4 rounder VS Fred Cloud- Referee: Ramadhan Basta 39 - 37 [2] Super Featherweight 6 roundsShomari Mirundi DREW 4 rounds of a 4 rounder VS Mohammed Kashinde- Referee: Pembe Ndava 38 - 38 [3] Super Bantamweight 4 roundsMuhidini Ndolanga WPTS 4 rounds of a 4 rounderVS Shukuru Said- Referee: Ramadhan Basta 40 - 36 [4] Light Welterweight Hamis Mputeni WKO round 2 of a 6 rounder VS Rashid Makali- Referee: Pembe Ndava; Judges:Ramadhan Basta, Emmanuel Mlundwa, Anthony Ruta [5] Flyweight 6 roundsHassani Kiwale WTKO round 2 of a 6 rounder VS Mawazo Kanju- Referee: Emmanuel Mlundwa Judges: Pembe Ndava , Ramadhan Basta, Anthony Ruta [6] Super Middleweight 6 roundsIdd Kigula WTKO round 4 of a 6 rounder VS Shabani Kaineko- Referee: Emmanuel Mlundwa Judges: Pembe Ndava , Ramadhan Basta, Anthony Ruta [7] Female Boxing Middle/Super MiddleMonica Mwakasanga WPTS 4 rounds of a 4 rounder VS Furaha Nganda - Referee: Emmanuel Mlundwa 40 - 36 [8] Super Middleweight 10 roundsRashid Matumla WPTS 10 rounds of a 10 rounder VS Maneno Oswald- Referee/Judge: Anthony Ruta 97 - 93; Judges: Pembe Ndava 95 - 95, Ramadhan Basta 97 – 95

MATUMLA AMSAMBALATISHA MTAMBO WA GONGO


)
Refarii Antoni Luta katikati akimnyoosha mkono juu bondia Rashidi Matumla Snake Man kuashiria ushindi dhidi ya mpinzani wake maneno Osward Mtambo wa Gongo kushoto wakati wa mpambano wao uliochezwa Jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Matumla alishinda kwa point.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/

Mabondia Maneno Osward Mtambo wa Gongo (kushoto) na Rashid Malumla Snake Man Wakioneshana umwamba wa kutupa masumbwi wakati wa mpambano wao uliochezwa Jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Matumla alishinda kwa point.(Picha na www.superd boxingcoach.blogspot.com)

RASHIDI MATUMLA VS MANENO OSWARD KUPAMBANA TENA LEO FEBRUARY 25 UKUMBI WA PTA SABASABA DAR...!!!MAANDALIZI ya pambano lisilo la ubingwa kati ya mabondia Rashid
Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’ lililopangwa
kuwa Februar 25 mwaka huu leo yanaenda vizuri.Promota wa mpambano huo Issa
Malanga, alisema pambano hilo limeandaliwa ili kumaliza ubishi baina
ya mabondia hao, ambao pambano la mwisho walitoka sare ya point 99.99

Hata hivyo Oswald aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki.
Mabondia hao wamewahi kupambana mara nne, Oswald akishinda mara moja
na Matumla mara mbili na kutoka sare mara moja.

Alisema pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati,
litafanyika kwenye ukumbi wa PTA sabasaba Dar es salaam


Mpambano huo wa kumaliza ubishi baada ya kila mmoja wao kudai
alishinda katika mpambano wao wa mwisho

Aidha aliwataja wakali watakaosindikiza mpambano huo ni Shomali
Mirundi na Mikidadi Abdallah 'Tatson', na Iddy Mkenye atapambana na
Shabani Mtengela ' Zunga Boy', Abdallah Mohamedi na Saleh Mkalekwa
mbali na hayo mpambano mwingine ni Ramadhani Mashudu na Hassani Kiwale
'Moro Best

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye
mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Roy Jonas,Evander holyfield,Lenox Lewis, Manny Paquaio, Floyd Maywherth,
Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali
ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila
‘Super ‘D’.
“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika
pambano la Cheka na Maugo ili kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’

Friday, February 24, 2012

MABONDIA MANENO OSWARD NA RASHIDI MATUMLA KUMALIZA UBISHI KESHO FEB 25 UKUMBI WA PTA SABASABA

 Mabondia Furaha Nganda na Monica Mwakasanga wakitunishiana misuri baada ya kupima uzito leo

Bondia Furaha Nganda akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika jumamosi feb 25 na bondia Monica Mwakasanga kushoto kulia ni Katibu wa Shilikisho la ngumi za Kulipwa Tanzania PST Anton
 Bondia Maneno Osward akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika katika ukumbi Wa PTA sabasaba jumamosi ya Feb 25 (kushoto) ni mpinzani wake Rashidi Matumla kulia ni katibu wa PST, aNTON Luta.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
 Bondia Shabani Kaineko akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Antoni Mwakapalila utakaofanyika katika ukumbi wa PTA sabasaba kesho kulia ni Katibu wa Shilikisho la ngumi za Kulipwa Tanzania PST Anton Luta(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Mabondia Antoni Mwakapalila akitunishiana misuri na bondia Shabani Kaineko baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao wa kirafiki utakaofanyika Kesho katika ukumbi wa PTA Sabasaba(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Thursday, February 23, 2012

SALEH MKALEKWA VS ABDALLAH MOHAMED PRINCE NASIM WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO

 Bondia Salehe Mkalekwa akipima uzito kushoto ni mpinzani wake Abdallah Mohamedi
Bondia Abdalla Mohamed Akipima uzito kushoto ni mpinzani wake Sasehe Mkalekwa na kulia ni Katibu wa PST Anton Luta

Wednesday, February 22, 2012

MCHUMIA TUMBO AMTWANGA MKENYA BILA HURUMA

Bondia aliyejitambulisha kwa jina la Obadia Mwangi  akiwa oi baada ya kudundwa na bondia Alifonce Mchumia Tumbo
 Refarii Said Chaku akimwonesha Mchumiatumbo baada ya kumtwanga Mkenya

Tuesday, February 21, 2012

MABONDIA SALEHE MKALEKWA NA ABDALAH MOHAMED (PRINCE NASEM) WATAMBIANA

Bondia Salehe Mkalekwa (kushoto) na Abdalah Mohamed (Prince Nasem) wakitunishiana misuri Dar es salaam jana wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa KG 67 Watel weight litakalofanyika feb 24.katikati ni mratibu wa mpambano huo Shabani Adiosi (Mwaya Mwaya)

BINGWA wa mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST) Abdalah Mohamed 'Prenc Naseem' atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa PST Februari 24 mwaka huu dhidi ya Salehe Mkalekwa

Pambano hilo la ubingwa wa PST litakuwa ni pambano la uzito wa kg 67 na litashirikisha mapambano mengine manne ya utangulizi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Shaban Adiosi 'Mwayamwaya' alisema pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa New Kibeta uliopo mbagala kuu Dar es Salaam.

Alisema pambano hilo la ubingwa wa PST ni muendelezo wa shirikisho hilo kuendelea kuinua mabondia ambao hawajawa na majina makubwa ili nao waweze kufikia kiwango kizuri cha mchezo huo.

"Ubingwa huu wa PST ni maalum kwa ajili ya mabondia chipkizi na ndio maana mabondia wanaoshirikishwa wengi ni chipkizi na lengo ni kuendeleza vipaji vyao,"alisema Mwayamwaya.

Aliyataja mapambano ya utangulizi yatakayopamba pambano hilo yatakuwa kati ya Shaaban Zungu na Hasan Debe watakaopigana uzito wa kg 55,Safari Mbeyu na Ibrahim Maokola watakaopigana uzito wa kg 67, Jofrey Pacho atakayetwangana na Dickson Kawiani na Kulwa Kindondi atakayepigana na Khaji Hamisi.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones, Lenox Lewis,David Haye na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Ngumi, Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.

“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

Sunday, February 19, 2012

Vitali Klitschko adunda Dereck Chisora

TSE Exclusive: Klitschko retains WBC heavyweight boxing crown
MUNICH, Germany (The Sports Encounter) Ukrainian heavyweight boxer Vitali Klitschko proved too big for Dereck Chisora of Great Britain on Saturday night as he successfully defended his WBC Heavyweight title in German city of Munich.
Vitali Klitschko upheld the legacy of his boxing family as he outscored his British challenger as referees made a unanimous points decision in favor of the Ukranian boxing powerhouse.
Klitschko never found it a hard task to defend his title on Saturday night as packed Olympiahalle in Munich witnessed sheer class and charisma of the Ukrainian boxer as he unleashed his fearsome punches on Chisora who had literally no answers in his kitty.
Vitali Klitschko, 40, and his brother Vladimir Klitschko now hold the WBO, WBA, IBO, IBF, and WBC titles among them as the Klitschko family had all the reasons in the world to feel proud of the two Klitschkos inside the Olympiahalle.
With this victory, Vitali Klitschko has now bettered his professional boxing record to 44-2 but it was never a walk in the park despite of the fact that the British Chisora always fell short of the target.
Chisora, a former Commonwealth champion, did try his luck to turn the bout into a controversial one but his gimmicks also fell short of the targets, just like his punches.
A pumped up Vitali Klitschko, while talking to media persons in a ringside interview, said, “Chisora put in a solid performance today but as a person, I have no respect for him”.
Vitali had an upper hand right from the start of the long-awaited bout and his dominance paid off in the paid in a big way as all the three judges had better numbers for the Ukrainian pugilist as they gave 118-110, 118-110, and 119-111 in his favor.
Not happy with the scores, British boxer Dereck Chisora clearly showed his opposition and demanded a rematch but the 12500-crowd in Olympiahalle had already witnessed the best in the business in the ring and started booing and jeering him.
Chisora told reporters, “This booing, I don’t mind as long as they paid money to watch the sport I love, I don’t mind. I want another fight. There will be a rematch or I will fight his younger brother”.
It is important to mention here that this was Chisora’s third loss in his last four fights as his record is now 15-3.
Vitali Klitschko was taller of the two, better of the two, more aggressive of the two, and in the end the ultimate winner in the Olympiahalle which was a perfect revenge for him against Chisora who had earned a bad name before the bout as he had slapped the Ukrainian at the weigh-in on Friday and also splashed water into his face during the pre-fight events.
Now Chisora is also demanding a fight against the younger Klitschko, Vladimir, who acted as a buffer during tonight’s bout.

MABONDIA WALIOTEULI​WA TIMU YA TAIFA WATAJWA LEO BAADA YA KUMALIZIKA MASHINDANO

jumla ya mabondia 17 kutoka timu ya taifa ya ngumi wamechaguliwa kuendelea kubakia katika
kikosi cha timu ya taifa
katika mashindano ya mchujo yaliyo malizika tarehe 17.2.2012 Mabondia waliochaguliwa ni 49kg
L-fly.John Christian na Said Pume.52kg fly.Abdalah Kassimu na George Costantinee 56kg
bantam.Emilian Patrick na Undule Langson 60kg i-weight.Denis Martine na Fabian Gaudence  64kg
L-welter.Victor Njaiti na Hamisi Kitenge 69kg welter.Mohamed Mhibumbui 75kg middle.Selemani
Kidunda na Abdul Rashid 81kg l-heavy. Mhina Morris 91kg heavy.Haruna Swanga na Nuru Ibrahim
91-kg super heavy.Maxmillian Patrick.wote wanatakiwa kulipoti Ofisini katika shirikisho la
ngumi za Ridhaa Nchini BFT tarehe 21.2.2012 ili wapewe taratibu za kuanza mazoezi .

IMETOLEWA NA KATIBU MKUU WA BFI MAKORE MASHAGA

Saturday, February 18, 2012

MABONDIA WA UZITO WA JUU KUONESHANA KAZI MANZESE KESHO

Mabondia wa Uzito wa juu, Obadia Mwangi kutoka Kenya (kushoto) na Alphpnce Mchumiatumbo wa Tanzania, wakitunishiana misuri baada ya kupima uzito, Dar es salaam mabondia hawo watapambana kesho katika ukumbi wa Frensi Kona Manzese katikati ni Mratibu wa pambano hilo Huseni Omari.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

TANGAZO KWA WANAFUNZI WA QT NA PRIVATE CANDITATE ULIPAJI WA ADA


Friday, February 17, 2012

big mechi

 

Chisora atamba kumtwanga Vitali

 
kwa KO
LONDON, Uingereza
DERECK Chisora ametamba kuwa anaweza kutwaa ubinga wa dunia kwa kuwa hatabiriki na kwamba hajui ni kitu gani kitatokea, umesema mtandao wa The Sun.
Del Boy atapambana na bingwa mtetezi wa WBC, Vitali Klitschko mjini Munich kesho Jumamosi ambapo ameahidi kuibuka na ushindi wa KO katika raundi ya nane.
Chisora anatumaini kuwa atafuata nyayo za mpiganaji mahiri wa zamani wa Uingereza, Lennox Lewis ambaye limtwanga Vitali mwenye urefu wa futi sita na ichi saba.
Alisema: " Ninaahidi kuwa ninasonga mbe kuanzia kengele ya kwanza, katika raundi ya nane atakwua mepigwa kwa KO.
"Kwanini raundi ya nane 8? ninaipenda namba nane kwa ubora . Timu ya Klitschko hainipendi kwa kuwa ni sitabiriki na sugu. Ni mwisho wa Vitali, ninaahidi."
Chisora mwenye umri wa miaka 28, yuko fiti sana kwa jili ya kupambana na mpinzani wake mwenye umri wa miaka 40, Klitschko ambaye ni kaka wa Wladimir.
Vitali, alipigwa na Lewis mwaka 2003, lakini alisema: "Waingereza wanapenda sana kuchonga. Nitamfundisha somo. Hakuna mtu wa kunizuia."

Wednesday, February 15, 2012

MASHINDANO YA KUTAFUTA TIMU YA TAIFA YA MASUMBWI YAANZA LEO

Mabondia peter Stanley kushoto akipambana na Doto Shoka wakati wa mashindano ya kutafuta mabondia watakaoliwakilisha taifa katika mashindano ya kufunzu Olimpic mapema hivi karibuni (picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)Monday, February 13, 2012

KAMISHENI YA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TPBC YAFANYA MABADILIKO KIUTENDAJI

Hivi karibuni kumekuwepo na ulazima wa mabadiliko katika Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) yanayotokana na changamoto zifuatazo:

1. Kuajiriwa kwa Boniface Wambura aliyekuwa Msemaji wa TPBC kuwa Msemaji

wa TFF. Wambura amefanya kazi nzuri sana tangu achukue jukumu la kuwa

Msemaji wa TPBC na ndiko alikoonekana kwa kazi nzuri na kuajiriwa TFF. Lakini

kwa kutambua kuwa kunaweza kuwa na mgongano wa maslahi, tumelazimika

kumpunguzia majukumu yake ili aweze kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi TFF.

Tunasikitika kumwachia mtendaji mzuri huyu! Msemaji wa Kamisheni sasa

atakuwa Rais wa Kamisheni Onesmo Ngowi.
2. Ukuaji wa mtandao wa ngumi kitaifa na kimataifa3. Matatizo kadhaa wa kadha katika medani ya ngumi za kulipwa Ili kukabiliana na changamoto zilizotajwa hapo juu, TPBC ilimteua Godfrey Madaraka Nyerere kuwa Makamu wa Rais December mwaka jana. Pia kitengo cha Fedha na Mipango kitakuwa chini ya makamu wa Rais. Uteuzi wa Madaraka ulifuatia mchango wake mkubwa kwenye medani ya ngumi za kulipwa kama Kromota, Kamaisha wa TPBC kanda ya Ziwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TPBC kwa kipindi kirefu. Pamoja na mabadiko haya, TPBC inaendelea kifanya mabadiliko yafuatayo kwa kuunda Kanda Mpya ya Ngumi za Kulipwa ya Dar-Es-Salaam na kumteua bondia wa siku nyingi na bingwa wa kwanza wa dunia toka Tanzania Rashid "Snake Boy” Matumla kuwa Kamishna wa Kanda Mpya ya Dar-ES-Salaam. Aidha, TPBC imeunda Kamati zifuatazo:


Kamati ya Viwango na kumteua Boniface Wambura kuwa Mwenyekiti wake.


Kamati ya Ubingwa na kumteua John Chagu kuwa Mwenyekiti wake. Chagu amekuwa Referii na jaji wa ngumi za kulipwa wa siku nyingi anayetambuliwa na mashirikisho mengi ya ngumi duniani kama vile IBF. WBC, WBA na WBO.TPBC imeteua Makamishna wa Kanda kama ifuatavyo:1. Kanda ya Dar-Es-Salaam: Rashid “Snake Boy” Matumla
2. Kanda ya Kaskazini: Mh. Justine Nyari
3. Kanda ya Kusini: Nicholas MallyaJustine Nyari ni Diwani wa Mererani kwa tiketi ya CCM na ni mtu aliyefanya kazi na TPBC katika miaka ya nyuma na anapenda kusaidia maendeleo ya ngumi nchini.TPBC imeteua pia Makamishna wa baadhi ya Mikoa kama ifuatavyo:
1. Mkoa Dar-Es-Salaam: Issa Maranga 2. Mkoa wa Tanga: Ibra Steke 3. Mkoa wa Kilimanjaro: Henry Mfinanga 4. Mkoa wa Arusha: Roman Chuwa
5. Mkoa wa Morogoro: Rauriti Bazi


Issa Maranga mwalimu wa shule ya St. Anthony na mpenzi wa ngumi wa muda mrefu.

Abra Steke ni bondia wa muda mrefu na mfanyakazi wa benki ya CRDB Tanga.

Henry Mfinanga ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TPBC na ni mfanyabishara. Roman Chuwa ni mfanyabishara wa Utalii mjini Arusha na mpenzi na mfadhili wa TPBC. Rauruti Bazi anafanya kazi Kampuni ya Tumbaku na amekuwa mpenzi na mfadhili wa TPBC kwa muda mrefu.Tutaendelea kufanya mabadiliko jinsi siku zinavyokwenda ili kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa TPBC 2012 - 2013 wa kuleta maendeleo ya Ngumi hapa Tanzania.


Aidha, TPBC imetoa vibali kwa mabondia Francis Miyeyusho na Fadhili Majia kucheza ngumi nchini Uingereza mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika mapambano yasiyo ya ubingwa.


Francis Miyeyusho atapambana 17 March katika ukumbi wa Sheffield katika jiji la London, ambapo bondia Fadhili Majia atapambana na Ashye Sexton tarehe 2 March Sheffield pia katika jiji la London.
Imetolewa naOnesmo A.M.NgowiIBF/USBA President for Africa
Director, Commonwealth (British Empire) Boxing Council (CBC)
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)Tel: 0754-360828

Sunday, February 12, 2012

RASHIDI MATUMLA AOMBA KUSAPOTIWA NA KAMBI YA ILALA AFULIWA KWA AJILI YA MPAMBANO WAKE MWINGINE NA MANENO OSWARD


Kocha Mkongwe wa mchezo wa masumbwi Nchini , Habibu Kinyogoli (kushoto) akimwelekeza bondia Rashidi Matumla 'Snake Man' jinsi ya kurusha Ngumi wakati bondia huyo alipotembelea kwa ajili ya kujifua katika Kambi ya ILala, Dar es salaam jana Matumla anajiandaa na mpambano wake mwingine dhidi ya Maneno Osward litakalofanyika tareha 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)Kocha Mkongwe wa mchezo wa masumbwi Nchini , Habibu Kinyogoli (kulia) akimwelekeza bondia Rashidi Matumla 'Snake Man' jinsi ya kurusha Ngumi wakati bondia huyo alipotembelea kwa ajili ya kujifua katika Kambi ya ILala, Dar es salaam jana Matumla anajiandaa na mpambano wake mwingine dhidi ya Maneno Osward litakalofanyika tareha 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Kocha Mkongwe wa mchezo wa masumbwi Nchini , Habibu Kinyogoli (kulia) akimwelekeza bondia Rashidi Matumla 'Snake Man' jinsi ya kurusha Ngumi wakati bondia huyo alipotembelea kwa ajili ya kujifua katika Kambi ya ILala, Dar es salaam jana Matumla anajiandaa na mpambano wake mwingine dhidi ya Maneno Osward litakalofanyika tareha 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Kocha Mkongwe wa mchezo wa masumbwi Nchini , Habibu Kinyogoli (kulia) akimwelekeza bondia Rashidi Matumla 'Snake Man' jinsi ya kurusha Ngumi wakati bondia huyo alipotembelea kwa ajili ya kujifua katika Kambi ya ILala, Dar es salaam jana Matumla anajiandaa na mpambano wake mwingine dhidi ya Maneno Osward litakalofanyika tareha 25 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

VIJANA WA MCHEZO WA MASUMBWI WAKIJIFUA KATIKA KAMBI YA ILALA

Baadhi ya vijana wakifanya mazoezi katika kambi ya ilala
 Mazoezi yakiendeleaa

Thursday, February 9, 2012

www.mamapipiro.blogspot.com yarejea Hewani


Kufuatia tatizo la kiufundi lililojitokeza hapo nyuma blogu yako ya Mamapipiro ilishindwa kuendelea na utendaji wake, nawaomba radhi wadauwangu wote ambao mlikosa kupata matukio muhimu ya michezo na burudani kwa zaidi ya wiki moja,hivyo kwa sasa mambo yamekaa sawa hivyo endeleeni kuperuzi blogu yenu kwa habari kem kem za michezo na burudani kupitia www.mamapipiro.blogspot.com.

Tuesday, February 7, 2012

Rashidi MATUMLA VS MANENO OSWARD KUPAMBANA TENA Februar 25 UKUMBI WA PTA SABASABA DAR
BONDIA wa ngumi za kulipwa Rashid Matumla 'Snek man' amesema kukutana ulingoni mara kwa mara na bondia Maneno Osward 'Mtambo wa gongo' hawachezei njaa isipokuwa ni mapenzi ya ngumi aliyokuwa nayo.

Matumla na Maneno wanakutana ulingoni kwa mara ya tano sasa ambapo baadhi ya wadau wamekuwa wakihisi labda mabondia hao hupigana kwa sababu ya kutafuta fedha.

Akizungumza kwa njia ya simu Dar es Salaam jana, Matumla alisema yeye binafsi bado anauwezo wa kupigana katika mchezo huo na kama angetaka kustaafu angeweza kufanya hivyo ila bado anayo nafasi ya kufanya vizuri katika mapambano yake.

Alisema pambano lake dhidi ya Maneno litakalopigwa Februari 25 mwaka huu katika ukumbi wa PTA Sabasaba litakuwa ni pambano lake la tano kukutana na bondia huyo.

"Mimi na Maneno tumeshakutana mara nne ulingoni hadi sasa na hili litakuwa ni pambano letu la tano kupigana,"alisema Matumla na kuongeza kuwa.

"Katika mapambano hayo nimemshinda Maneno mapambano mawili, amenipiga pambano moja na tumetoka sare pambano moja lakini kama itawezekana nitamtwanga katika pambano lijalo,"alisema Matumla.

Alisema kwa sasa anajifua chini ya kocha wake Habibu Kinyogoli ambaye ameingia naye mkataba wa kumnoa na anainami atafanikiwa kumtwanga Maneno katika mchezo huo.

Pambano hilo la Februari 25 litakuwa ni pambano la marudiano kwa mabondia hao baada ya kutoka sare katika pambano la kwanza lililofanyika katika ukumbi wa Henken Mtoni Desemba 25 mwaka jana.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.


“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

Sunday, February 5, 2012

SUPER D BOXING COACH ASHANTI NA ILALA

Kocha wa KImataifa wa Mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super d' akiwa ameshika cheti chake alichopewa baada ya kufuzu mafunzo ya ukocha kimataifa yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpic Tanzania kwa kushirikiana na chama cha ngumi cha Dunia 'AIBA'

FRANCIS CHEKA MADA MAUGO KUGOMBEA UBINGWA WA IBF RAUNDI 12 APRIL 28 PTA SABASABA
Makamu Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) , Madaraka Nyerere (Kushoto) akiwaelekeza mabondia Fransc Cheka kulia na Mada Maugo jinsi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

SUPER D BOXING COACH AJIDHATITI KUENDELEZA MCHEZO WA NGUMI 2012

Baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Olimpic Tanzania 'TOC' na viongozi wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa Nchini 'BFT' wakiwa katika picha ya pamoja na makocha wa mchezo wa ngumi toka mikoa mbalimbali nchini Tanzania baada ya kupatiwa vyeti vya kutambulika kimataifa baada ya kuhitimu kozi kwa makocha hao
Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti vyao wakati wa mafunzo ya kimataifa ya mchezo huo yaliyomalizika Kibaha Mkoa wa Pwani jana huku wakiwa wameng'arishwa na fulana zilizotolewa na SUPER D BOXING COACH kama zawadi kwa makocha hao.Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti vyao wakati wa mafunzo ya kimataifa ya mchezo huo yaliyomalizika Kibaha Mkoa wa Pwani jana huku wakiwa wameng'arishwa na fulana zilizotolewa na SUPER D BOXING COACH kama zawadi kwa makocha hao.
Mkufunzi Mkuu wa Makocha wa Ngumi kutoka Chama cha Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Duniani ( AIBA), Josephe Diouf, akimkabidhi cheti cha kufuzu ukocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa, Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani
Kocha wa KImataifa wa Mchezo wa Ngumi Rajabu Mhamila 'Super d' akiwa ameshika cheti chake alichopewa baada ya kufuzu mafunzo ya ukocha kimataifa yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpic Tanzania kwa kushirikiana na chama cha ngumi cha Dunia 'AIBA'

MASHINDANO YA KWANZA YA MCHUJO KUTAFUTA MABONDIA WATAKAOWAKILISHA TAIFA LA TANZANIA


                                                                                              3 February 2012
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Yah;- MASHINDANO YA KWANZA YA MCHUJO KUTAFUTA MABONDIA
                     WATAKAOWAKILISHA TAIFA LA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA
              KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO YA OLIMPIKI CASABLANCA
MOROCCO APRIL 2012. 
Mashindano ya kwanza ya mchujo kwa ajili ya kuwapata wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo wa ngumi.yatafanyika jijini Dare s salaam katika ukumbi wa uwanja wa taifa wa ndani tarehe 15-18/02/2012.
Watakao husika katika mchujo huo ni mabondia ambao wapo mazoezi,katika vituo vilivyoainishwa  na BFT kwa ajili ya mazoezi ya awali kwa wachezaji walioteuliwa kwa kuzingatia vigezo vya kuwa wamefanya vizuri sana katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yaliyoandaliwa au kutambuliwa na BFT.
Vituo hivyo ni uwanja wa ndani wa Taifa,Magereza Ukonga,mwenge JWTZ,mgulani JKT na kituo kilichopo jijini Mwanza.
Kwa umuhimu na ubora wa mashindano BFT inawaomba wale wote ambao wanahitaji kucheza na kujima na wachezaji walioteuliwa awali waende kujiandikisha katika vituo hivyo kwa kuwa watakao ruhusiwa kucheza ni wale tu ambao watakuwa wamepitishwa na makocha wa timu ya taifa waliopo katika vituo hivyo.

Katika mashindano hayo tunategemea kupata ufadhiri kutoka katika mamlaka ya usajiri wa biashara na makampuni (BRELA)
Hali ya mazoezi katika kambi zote inaendelea vizur hadi kufikia leo hakuna majeruhi na katika kituo cha mwenge leo watakuwa na zoezi la kucheza wao kwa wao kwa nia ya kujiimalisha zaidi na kuzoea hali ya mashindano kwa maandalizi ya tarehe 15.

Mako.re Mashaga
KATIBU MKUU
                              Mob;0713588818

klabu ya Bigrayt Mwananyamala yaendelea kuwanowa vijana


Kocha wa mchezo wa Ngumi Ibrahimu Kamwe 'Bigrayt' (kulia) akimwelekeza bondia Issa Omari jinsi ya kutupa masumbwi katika klabu ya Bigrayt Mwananyamala Dar es salaam jana (PIcha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

FRANCIS CHEKA MADA MAUGO KUGOMBEA UBINGWA WA IBF RAUNDI 12 APRIL 28 PTA SABASABA
Makamu Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) , Madaraka Nyerere (Kushoto) akiwaelekeza mabondia Fransc Cheka kulia na Mada Maugo jinsi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kupigania ubingwa IBF raundi 12 litakarofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Aprilo 28.(picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Thursday, February 2, 2012

Abdalah Mohamed 'Prins Naseem KUTETEA UBINGWA WAKE NA Salehe Mkalekwa .Februari 24BINGWA wa mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST) Abdalah Mohamed 'Prins Naseem' atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa PST Februari 24 mwaka huu dhidi ya Salehe Mkalekwa.
Pambano hilo la ubingwa wa PST litakuwa ni pambano la uzito wa kg 57 na litashirikisha mapambano mengine manne ya utangulizi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Shaban Adiosi 'Mwayamwaya' alisema pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa New Kibeta uliopo mbagala kuu Dar es Salaam.
Alisema pambano hilo la ubingwa wa PST ni muendelezo wa shirikisho hilo kuendelea kuwainua mabondia chipkizi ambao hawajawa na majina makubwa ili nao waweze kufikia kiwango kizuri cha mchezo huo.

"Ubingwa huu wa PST ni maalum kwa ajili ya mabondia chipkizi na ndio maana mabondia wanaoshirikishwa wengi ni chipkizi na lengo ni kuendeleza vipaji vyao,"alisema Mwayamwaya.

Aliyataja mapambano ya utangulizi yatakayopamba pambano hilo yatakuwa kati ya Shaaban Zungu na Hasan Salehe watakaopigana uzito wa kg 55, Safari Mbeyu na Ibrahim Maokola watakaopigana uzito wa kg 67, Jofrey Pacho atakayetwangana na Seleman Shaaban na Abdalah Yusuph atakayepigana na Omari Kijepa.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.


“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.