Tangazo

Pages

Sunday, February 5, 2012

MASHINDANO YA KWANZA YA MCHUJO KUTAFUTA MABONDIA WATAKAOWAKILISHA TAIFA LA TANZANIA


                                                                                              3 February 2012
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Yah;- MASHINDANO YA KWANZA YA MCHUJO KUTAFUTA MABONDIA
                     WATAKAOWAKILISHA TAIFA LA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA
              KUFUZU KUSHIRIKI MASHINDANO YA OLIMPIKI CASABLANCA
MOROCCO APRIL 2012. 
Mashindano ya kwanza ya mchujo kwa ajili ya kuwapata wachezaji wa timu ya taifa ya mchezo wa ngumi.yatafanyika jijini Dare s salaam katika ukumbi wa uwanja wa taifa wa ndani tarehe 15-18/02/2012.
Watakao husika katika mchujo huo ni mabondia ambao wapo mazoezi,katika vituo vilivyoainishwa  na BFT kwa ajili ya mazoezi ya awali kwa wachezaji walioteuliwa kwa kuzingatia vigezo vya kuwa wamefanya vizuri sana katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yaliyoandaliwa au kutambuliwa na BFT.
Vituo hivyo ni uwanja wa ndani wa Taifa,Magereza Ukonga,mwenge JWTZ,mgulani JKT na kituo kilichopo jijini Mwanza.
Kwa umuhimu na ubora wa mashindano BFT inawaomba wale wote ambao wanahitaji kucheza na kujima na wachezaji walioteuliwa awali waende kujiandikisha katika vituo hivyo kwa kuwa watakao ruhusiwa kucheza ni wale tu ambao watakuwa wamepitishwa na makocha wa timu ya taifa waliopo katika vituo hivyo.

Katika mashindano hayo tunategemea kupata ufadhiri kutoka katika mamlaka ya usajiri wa biashara na makampuni (BRELA)
Hali ya mazoezi katika kambi zote inaendelea vizur hadi kufikia leo hakuna majeruhi na katika kituo cha mwenge leo watakuwa na zoezi la kucheza wao kwa wao kwa nia ya kujiimalisha zaidi na kuzoea hali ya mashindano kwa maandalizi ya tarehe 15.

Mako.re Mashaga
KATIBU MKUU
                              Mob;0713588818

No comments:

Post a Comment