Tangazo

Pages

Saturday, January 9, 2021

BONDIA AMOSI MWAMAKULA KURUDI KIVINGINE KUZIPIGA FEB 6

Kocha wa mchezo wa masumbwi na mateke /kicki Boxing Esmail Abdallah 'Van Dame' kushoto akimwinua mkono juu bondia Amosi Mwamakula kwa ajili ya kumtambulisha katika mpambano wake wa kuzipiga Feb 6 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na Hashimu Kilaga

 Kocha wa mchezo wa masumbwi na mateke /kicki Boxing Esmail Abdallah 'Van Dame' kushoto akimtambulisha bondia Amosi Mwamakula kwa ajili ya  mpambanmo wake wa kuzipiga Feb 6 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na Hashimu Kilaga

Na Mwandishi Wetu

BONDIA AMOSI MWAMAKULA ametambulisha mpambano wake wa kuzipiga na Hashimu Kilaga mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Saba saba SIKU YA FEB 6 Dar es salaam

akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpambano uho kocha wa masumbwi na Mateke Kicki Boxing Esmail Abdallah 'Van Dame' amesema kuwa mwamakula amejiandaa vya kutosha hivyo mpinzani wake nae ajiandae vya kutosha kwani kwa sasa amerudi kivingine

ameongeza kwa kusema kwa sasa wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya pambano hilo ambalo linandaliwa kwa ubora wa aina yake kwani maandalizi ya mpambano uho sasa yamepamba moto

alieleza kuwa mbali na pambano hilo la masumbwi pia kutakuwa na mapambano mengine ya ngumi ambapo bondia Lulu Kayage atazipiga na Agnes Kayange na Jitu Rajabu kutoka kwa Super D Coach atazipiga na Daniel Mwakafyale na Shabani kaoneka atazipiga na Butel Obedi mambano huo unaletwa na Jamukaya kwa kushilikiana na Black Panda utakuwa na kingilio cha shilingi 10,000 TU kwa siku hiyo 

pia kutakuwa na ngumi za mateke kick Boxing na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa Sanaa Michezo Na Utamaduni 

Friday, January 1, 2021

SUPER D BOXING PROMOTIOBN KUMRUDISHA HAMISI MAYA ULINGONI APRIL 2 SABASABA

                                                  BONDIA HAMISI MAYA

Hamisi Maya ambaye ni bingwa wa GBC mkanda unaotambulika Duniani  akwa amevalishwa mkanda baada ya kumdunda Piergiulio Ruhe wa ujerumani na kufanikiwa kurudi na mkanda

NA MWANDISHI WETU

BONDIA HAMISI MAYA sasa kupanda ulingoni rasmi April 2 katika ukumbi wa Sabasaba Hall uliopo katika viwanja vya Sabasaba akimvaa bondia Alvin Omondi wa Kenya mpambano wa Raundi 8 utakaopigwa katika uzito wa KG 66

Akizungumza kuusu mpambano uho Mratibu wa pambano hilo Chaurembo Palasa amesema kuwa baada ya muda mrefu kukaa kimya kwa bondia huyo sasa anaibuliwa upya na kampuni tanzu ya kizarendo ya Super D Boxing Promotion ambao ndio waandaaji wa mpambano uho kwa sasa

Hamisi Maya ambaye ni bingwa wa GBC mkanda unaotambulika Duniani ambapo mpaka sasa anasifika kwa kuwapiga mabondia mbalimbali akiwa nje ya nchi ambapo alishawai kumpiga K,O mbaya sana Jems Onyango wa Kenya mpambano uliofanyika Charter Hall, Nairobi  Kenya na kurudi na ubingwa wa Afrika na kumgalagaza bila ya huruma bondia Piergiulio Ruhe wa ujerumani na kufanikiwa kurudi na mkanda

Alisema Palasa ata hivyo mapromota wengi wamekuwa wakimkwepa Maya kutokana na uchezaji wake awapo ulingoni ni kama bondia aliyekusudia kuuwa mtu akiwa mchezoni ndio mana ajapata mapambano tangu mwaka 2019 hata hivyo kupitia kampuni yetu ya Super D Promotion tunampa nafasi ya kuonesha Kipaji chake kwa mara nyingine kwa mwaka uhu 2021

aliongeza kwa kusema kuwa mbali na mpambano uho pia kutakuwa na mapambano mengine ya lkukata na shoka ambapo bondia machachali awapo ulingoni Vicent Mbilinyi atazipiga na George Onyango na Fransic Miyeyusho atazipiga na Gabriel Chola wakati Hamidu Kwata atazidunda na Jems Kibazange na juma Abdul wataoneshana kazi na Hamza Mchanjo na Bakari Magona atazipiga na Emanuel Mwakyembe

SUPER D BOXING PROMOTIOBN KUMRUDISHA HAMISI MAYA ULINGONI APRIL 2

 NA MWANDISHI WETU

BONDIA HAMISI MAYA sasa kupanda ulingoni rasmi April 2 katika ukumbi wa Sabasaba Hall uliopo katika viwanja vya Sabasaba akimvaa bondia Alvin Omondi wa Kenya mpambano wa Raundi 8 utakaopigwa katika uzito wa KG 66

Akizungumza kuusu mpambano uho Mratibu wa pambano hilo Chaurembo Palasa amesema kuwa baada ya muda mrefu kukaa kimya kwa bondia huyo sasa anaibuliwa upya na kampuni tanzu ya kizarendo ya Super D Boxing Promotion ambao ndio waandaaji wa mpambano uho kwa sasa

Hamisi Maya ambaye ni bingwa wa GBC mkanda unaotambulika Duniani ambapo mpaka sasa anasifika kwa kuwapiga mabondia mbalimbali akiwa nje ya nchi ambapo alishawai kumpiga K,O mbaya sana Jems Onyango wa Kenya mpambano uliofanyika Charter Hall, Nairobi  Kenya na kurudi na ubingwa wa Afrika na kumgalagaza bila ya huruma bondia Piergiulio Ruhe wa ujerumani na kufanikiwa kuruni na mkanda