Tangazo

Pages

Saturday, January 9, 2021

BONDIA AMOSI MWAMAKULA KURUDI KIVINGINE KUZIPIGA FEB 6

Kocha wa mchezo wa masumbwi na mateke /kicki Boxing Esmail Abdallah 'Van Dame' kushoto akimwinua mkono juu bondia Amosi Mwamakula kwa ajili ya kumtambulisha katika mpambano wake wa kuzipiga Feb 6 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na Hashimu Kilaga

 Kocha wa mchezo wa masumbwi na mateke /kicki Boxing Esmail Abdallah 'Van Dame' kushoto akimtambulisha bondia Amosi Mwamakula kwa ajili ya  mpambanmo wake wa kuzipiga Feb 6 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na Hashimu Kilaga


Na Mwandishi Wetu


BONDIA AMOSI MWAMAKULA ametambulisha mpambano wake wa kuzipiga na Hashimu Kilaga mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Saba saba SIKU YA FEB 6 Dar es salaam


akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpambano uho kocha wa masumbwi na Mateke Kicki Boxing Esmail Abdallah 'Van Dame' amesema kuwa mwamakula amejiandaa vya kutosha hivyo mpinzani wake nae ajiandae vya kutosha kwani kwa sasa amerudi kivingine


ameongeza kwa kusema kwa sasa wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya pambano hilo ambalo linandaliwa kwa ubora wa aina yake kwani maandalizi ya mpambano uho sasa yamepamba moto


alieleza kuwa mbali na pambano hilo la masumbwi pia kutakuwa na mapambano mengine ya ngumi ambapo bondia Lulu Kayage atazipiga na Agnes Kayange na Jitu Rajabu kutoka kwa Super D Coach atazipiga na Daniel Mwakafyale na Shabani kaoneka atazipiga na Butel Obedi mambano huo unaletwa na Jamukaya kwa kushilikiana na Black Panda utakuwa na kingilio cha shilingi 10,000 TU kwa siku hiyo 


pia kutakuwa na ngumi za mateke kick Boxing na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa Sanaa Michezo Na Utamaduni 

No comments:

Post a Comment