Tangazo

Pages

Friday, October 31, 2014

MABONDIA WAZIPIGA MAZOEZINI

Bondia Shabani Kaoneka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Obago Kamata wakati wa mazoezi yaliyofanyika shule ya uhuru uwanja wa basket yakisimamiwa na Super D Boxing Coach Dar es salaam jana picha na SUPER D BLOG
Bondia Shabani Kaoneka kulia 
akimtupia konde  Obago Kamata wakati wa mazoezi yaliyofanyika shule ya uhuru uwanja wa basket yakisimamiwa na Super D Boxing Coach Dar es salaam jana picha na SUPER D BLOG
Bondia Shabani Kaoneka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Obago Kamata wakati wa mazoezi yaliyofanyika shule ya uhuru uwanja wa basket yakisimamiwa na Super D Boxing Coach Dar es salaam jana picha na SUPER D BLOG
Bondia Jumaa Rashid akioneshana ubavu na Juma Biglee wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika uwanja wa shule ya uhuru uwanja wa basket yaliyokuwa yakisimamiwa na Super D Boxing Coach Dar es salaam jana picha na SUPER D BLOG

Bondia Omari Bai kushoto akipambana ya Kelvin Majiba wakati wa mazoezi yaliyofanyika katika uwanja wa basket shule ya uhuru yaliyokuwa yakisimamiwa na Super D bOXING coach Dar es salaam jana picha na SUPER D BLOG
Bondia Shabani Kaoneka akipambana na Omari Bai wakati wa mazoezi yaliyofanyika shule ya uhuru uwanja wa basket yakisimamiwa na kochas Super D picha na SUPER D BLOG
Bodia Obaga Kamata kushoto akipambana na Idrisa Mweta wakati wa mazoezi yaliyofanyika shule ya uhuru uwanja wa basket yakisimamiwa na Super D Boxing Coach picha na SUPER D BLOG

BONDIA THOMAS MASHALI KUPAMBANA NA HENRY WANDELA FRENDS CORNER MANZESE NOVEMBA MOSI

Bondia Thomas Mashali kushoto ankinyooshwa mkono juu na Yassin Abdallah katikati na mpinzani wake Henry Wandela kutoka Kenya baada ya upimaji uzito kwa ajili ya mpambano wao picha na SUPER D BLOG

MABONDIA MBALIMBALI WATAKAOCHEZA KESHO WAKITUNISHA MISULI
BONDIA SHABANI KAONEKA AKITUNISHA MSULI BAADA YA KUPIMA UZITO
Bondia Ramadhani Alfani kushoto akitambiana na Shabani Kaoneka baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa novemba mosi picha na SUPER D BLOG
Bondia Ramadhani Alfani kushoto akitambiana na Shabani Kaoneka baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa novemba mosi picha na SUPER D BLOG
mabondia baada ya kupima

Thursday, October 30, 2014

MPAMBANO WA KWANZA KUZAMINIWA NA RAIS WAENDELEA KUWEKA HISTORIAMpambano  wa kwanza kabisa kuzaminiwa na Rais wa Zaire Mabutu Seseseko mwaka 1974 ambapo historia mpaka leo hii inasomeka na aito futika duniani
super d boxing coach and promotion news leo ni siku muhimu sana katika masumbwi ya kukumbukwa duniani kote ambapo mabondia muhamed ali na george formen walicheza kwa mara ya kwanza afrika na kuweka historia ambayo bado aijavujwa mpaka leo ni miaka 40 tangia lifanyike pambano hilo dvd zake zipo SUPER D 0787406938 uhuru na msimbazi kariakooTuesday, October 28, 2014

BONDIA FADHILI MAJIHA AONESHA MAAJABU KWA KUPIGWA KWA POINT THAILAND MCHEZO WA RAUNDI 12


Bondia Pungluang Sor Singyu wa Thailand kushoto akipambana na Fadhili Majiha wa Tanzania  wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title   uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point
Bondia Fadhili Majiha wa Tanzania kushoto akipambana na Pungluang Sor Singyu wa Thailand  wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title   uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point

 Na Mwandishi Wetu


akizungumzia matokeo hayo ya kupigwa kwa point bondia huyo amejigamba na kusema kuwa yeye alistaili ushindi hivyo wamempa kwa kuwa kacheza kwao na mcheza kwao utunzwa mana nilicheza kwa ustadi wa ali ya juu na wapenzi wote wa ngumi walikuwa upande wangu wakitafakali kwa nini nilinyimwa ushindi

bondia huyo ambaye anatamba sana hapa nchini kuwa akuna wa kumbabaisha ambapo anadai kukimbiwa mara mbili na bondia Fransic Miyeyusho pamoja na Nassibu Ramadhani ambao wote amewapa onyo ole wake mmoja wao akaingia anga zake atakiona cha moto kwa kuwa mechi zao nyingi wanapenda kupangiana wenyewe kwa wenyewe

nimerudi nyumbani nipo fit sina ata kovu la aina yoyote hile hivyo nitahakikisha nafanya mazoezi kuendeleza ufiti niliokuwa nao na napenda kutoa tahadhali kwa bondia yoyote mtanzania atakayejitokeza kwa sasa mbele yangu yeye atakuwa halali yangu 
nae  Kocha wake Waziri Chara amejigamba kwa kusema kuwa bondia wake ni wa kimataifa ambapo michezo yake karibia mitatu kacheza
Philippines na mwingine Thailand hivyo wao ni wa kimataifa zaidi mana mapambano aliyocheza nje yote yalikuwa magumu na raundi ni 12 ambapo zote alimaliza kwa kuwa nilimjenga katika mazingira mazuri mabondia wengi wakienda nje ya nchi wengiwao wanapigwa raundi ya kwanza ya pili awafiki ya nne

CHEKA AONA NGUMI HAZILIPI, SASA ARUDI KUOKOTA CHUPA

Francis Boniface Cheka 'Maputo'
Na Imani Makongoro, Mwananchi
Nyumbani kwa bondia Francis ‘SMG’ Cheka hakuishi pilika ambazo zinatokana na kazi ya chupa za plastiki anayofanya bingwa huyo wa zamani wa dunia wa WBF.
Nje ya nyumba yake kuna mafurushi kila kona yakiwa na ‘bidhaa’ tofauti ikiwamo chupa za plastiki, chupa za konyagi, chibuku na plastiki ngumu (ndoo na madumu) yaliyopasuka.
Cheka anavyookota chupa
“Mimi ndiyo mwanzilishi wa biashara hii hapa Morogoro, niliianza 2004 baada ya kuamua kuingia mtaani kuokota na kuziuza mwenyewe, wakati huo kilo moja niliuza kwa Sh100 na nilikuwa nikizunguka kutwa nzima kutafuta chupa mtaani,” anasema Cheka.
Anasema wakati anaanza kuokota chupa alikuwa na miaka mitano tangu aingie kwenye ngumi za kulipwa, lakini hakuwa maarufu.
“Nilikuwa nina uwezo wa kuzunguka na kuokota hadi kilo 100 kwa siku, japo ilikuwa kazi ngumu, lakini nilipata fedha nikanunua kiwanja maeneo ya Kilimahewa na kujenga nyumba kwa kazi ya kuokota chupa.
“Pia niliweza kujiandalia mapambano peke yangu kwa kazi hii, ambayo yalinijenga na kunipa umaarufu kwenye ngumi, nimejiandalia mapambano zaidi ya 15 kwa fedha niliyopata kwa kuokota chupa,” anasema Cheka.
Anasema vijana wengi wa Morogoro walianza kuokota chupa baada ya kuona Cheka amejenga nyumba kwa kazi hiyo, hivyo hakuwa na hiyana aliwafundisha kazi hiyo na wengine aliingia nao mtaani kuokota.
“Nilipoanza kucheza mapambano ya ubingwa wa Afrika nilisimama kuokota chupa nikawaachia wengine na mimi kuelekeza nguvu zangu kwenye ngumi, kijiwe changu nikamweka mtu wa kufanya hiyo kazi na nikawa na nanunua kwa watu wengine kisha mimi nauza tena.
“Kwa kipindi chote ambacho nilikuwa nimebanwa na masuala ya ngumi, mradi wangu huu uliyumba kwani kila niliyemwachia alikuwa na fikra za kuniibia, ilifikia mahali nikakwama kwani nilikopa fedha benki kuongezea nguvu kwenye biashara yangu ya makopo hivyo nilipaswa kulipa,” anasema Cheka.
Anavyookota chupa mtaani
“Watu wanashangaa mtu kama mimi kuokota chupa, lakini ndiyo kazi inayoniweka mjini, wiki iliyopita nilikuwa Msamvu (stendi kuu ya Morogoro) nakusanya chupa kwa bahati nikakutana na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alishangaa kuniona naokota Chupa.
“Hakuamini kama mimi bingwa wa dunia na bondia namba moja Tanzania ndiyo naokota chupa mtaani, lakini ukweli nisipofanya kazi hii na nikabaki kutegemea ngumi, maisha yatakuwa magumu kwangu,” anasema Cheka.
Anasema haoni aibu kufanya kazi hiyo kwani ni kazi iliyompa mafanikio na kujenga nyumba mbili, moja ikiwa Kilimahewa ambako anaishi hivi sasa na nyingine Kihonda alikowapangisha watu wengine.
“Muda wangu mwingi nimeelekeza kwenye chupa, mazoezi sasa sifanyi kwani nina muda sijafanya mazoezi ya ngumi, nasimamia mwenyewe biashara yangu ya chupa ambayo mbali na kuokota mwenyewe pia kuna watu ambao wanaokota na kuniuzia.
“Chupa za maji nanunua kilo moja Sh250 na mimi nauza 700 baada ya kusaga, kwa mwezi nina uhakika wa kuuza kilo 4,500 mpaka 6,000 na plastiki ngumu nanunua Sh350 na mimi nauza Sh 2,000 baada ya kusaga hivyo kwa mwezi nauza zaidi ya kilo 3,000, pia naokota chupa za konyagi na chibuku ambazo naziosha na kuwauzia watu wa kampuni hizo,” anasema Cheka.
Ameamua kuingia mtaani kutembeza CD
“Sijapata mafanikio yoyote kwenye ngumi hadi sasa hivyo nimeona nijaribu kuuza CD za mapambano yangu labda nitafanikiwa,” anasema Cheka.
Anasema kazi hiyo anaifanya kwa kutembeza CD zake mkononi na kuwapelekea watu kwenye maeneo tofauti mjini Morogoro na amekwishauza CD 200 hadi sasa.
“Nilitoa CD 200 ambazo niliziuza kwa kutembeza mwenyewe mkononi zikaisha na sasa nimetoa nyingine 200, najitangazia biashara mwenyewe kwani napeleka kwenye mkusanyiko wa watu, vituo vya daladala, Stendi ya Msamvu na maeneo ambayo najua nikienda sikosi wateja, CD moja nauza Sh 3000,” anasema Cheka.
Fedha nyingi aliyowahi kupata katika ngumi
“Fedha nyingi niliyopata ni Sh10 milioni ambayo nilicheza pambano Russia mwezi Desemba 2012 na kupigwa kwa Knock Out (KO) raundi ya nne, pambano lile nilicheza bila kujiandaa na nilipata fedha hiyo kwa kuwa sikuitumia kwenye maandalizi,” anasema Cheka.
Anasema mapambano mengi anayocheza nchini amekuwa akiambulia Sh3 milioni mpaka Sh4 milioni baada ya kutoa fedha za maandalizi, kumlipa kocha na kununua vifaa.
“Pambano nililocheza na Mmarekani la ubingwa wa dunia nilipewa Sh4 milioni za maandalizi, nikaweka kambi Nairobi kila kitu nalipa mwenyewe mpaka kumlipa kocha, hadi narudi sina fedha baada ya pambano nikapewa Sh3 milioni, nilikuwa na madeni nikalipa na kubaki sina kitu.
“Hata wakati nafanyiwa sherehe ya kupongezwa Morogoro, sikuwa na hata shilingi, siku nawekewa dau la Sh10 milioni nikacheze Russia, sikukataa japo nilijua sina mazoezi, nilipigwa KO kihalali na kuvuliwa ubingwa wa dunia,” anasema Cheka.
Mkakati wake wa kurudi shule
Cheka alipewa ofa ya masomo kwenye Chuo cha St Joseph cha mjini Morogoro na aliingia darasani siku moja kisha akatokomea hadi leo hajawahi kurudi.
“Mimi ni baba wa familia ambayo inanitegemea, siyo kama sipendi kusoma, lakini nikiwa shule majukumu ya familia nitayatekeleza vipi? Hivi sasa nimeamua habari ya kusoma niiweke kando niboreshe biashara yangu, Mungu akiniweka hai, nitasoma miaka ijayo,” anasema Cheka.
Kwa nini anaitwa Kazimoyo?
Akiwa Morogoro, Cheka anajulikana pia kwa jina la Kazimoyo.
“Hili jina nimepewa na marafiki zangu ambao wananiita Kazimoyo kutokana na kazi ninazozifanya, ambazo wanasema nina moyo mgumu ndiyo sababu nazifanya, hivyo kazi ninazofanya sasa na nilizowahi kufanya nimefanya kwa moyo tu,” anasema Cheka.
Historia fupi ya maisha yake
Cheka alizaliwa miaka 32 iliyopita jijini Dar es Salaam, akiwa mtoto wa kwanza kwa baba yake, Boniface Cheka na alisoma Shule ya Msingi Kinondoni Hananasifu.
Alianza kucheza ngumi akiwa darasa la tatu na wakati huo baba yake alipenda kumfundisha ngumi.
“Nilipohitimu shule ya msingi, nilipata kazi kwenye gari la taka la Manispaa ya Kinondoni, nilifanya kazi hiyo pia nikijifua ngumi kwenye Ukumbi wa Arnautoglu, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
“Baada ya kuona maisha magumu Dar es Salaam, Nilikwenda Morogoro, sikuwa na mahali pa kufikia hivyo nikaomba kazi ya kufagia Stendi ya Msamvu na usiku hapo ndipo nikawa nalala,” anasema Cheka.
Anasema alilazimika kutandika maboksi na kulala kituoni hapo usiku ulipoingia na asubuhi anaamkia kwenye kibarua cha kufagia kituo hicho.
“Nilipata fedha kidogo na kupanga chumba, nakumbuka kitanda changu nilinunua kwa fedha niliyopata kwenye kazi ya kuzibua choo, sikuwa na ujuzi huo, lakini rafiki zangu waliponiambia kuna kazi hiyo nilienda kufanya na kulipwa Sh50,000 ambayo ilikuwa fedha nyingi kuwahi kulipwa,” anasema Cheka.
Anasema baada ya muda ndipo aliingia mtaani kuokota chupa, kazi iliyompa mafanikio na kujenga nyumba, na kutumia fedha aliyopata kujitangaza kwenye ngumi.
CREDIT: MWANANCHI

Sunday, October 26, 2014

BONDIA SAIDI MBELWA APIGA GEORGE DIMOSO KWA POINTBondia Georger Dimoso kushoto akipambana na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamoso iliyopita Mbelwa alishinda kwa point mpambano huo wa raundi nane Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Said Mbelwa kushoto akioneshana umwamba na Geore Dimoso wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi jana Mbelwa alishinda kwa point Picha na SUPER D BLOG


 Mashabiki wa mchezo wa masumbwi wakifatilia kwa makini mchezo huo
Bondia Said Mbelwa akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wa mpambano huo

S
Bondia Hamza Mchanjo kushoto akipambana na Juma Fundi wakati
wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Fundi alishinda kwa point mpambano huo wa raundi sita picha na SUPER D BLOG
Baadhi ya mashabiki kutoka Tanzani Boxing Fans Group Watssup wakijadili jambo na bondia Thomasi Mashali wa pili kushoto anae ongea nae ni Rajabu Mkamba mwenye tai
Bondia Aman Bariko 'Manny Chuga' akioneshana umwamba na Ally Bugingo wakati wa mpambano wao Bariki alishinda kwa point picha na SUPER D BLOG

Bondia Zamoyoni Mbishi kushoto akipambana na Sadiq Nuru wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Mbishi alishinda kwa pointi picha na SUPER D BLOG


Bondia Hassan Mandula kulia akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mohamed Jaka Mandula alishinda kwa TKO ya raundi ya pili picha na SUPER D BLOG

Friday, October 24, 2014

NGUMI KUPIGWA KESHO OKTOBER 25 FRENDS CORNER MANZESE

Bondia Ally Bugingo akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Amani Bariki 'Manny Chuga' mpambano utakaofanyika Oktoba 25 katika ukumbi wa Frends corner Manzese Dar es salaam katikati ni Antony Rutta picha na SUPER D BLOG
Bondia Sadiki Nuru akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa kesho jumamosi
Bondia Said Mbelwa akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika kesho oktoba 25 katika ukumbi wa frends corner manzese ambapo anapambana na George Dimoso mpambano wa raundi nane picha na SUPER D BLOG
Bondia Fadhili Boika kushoto akitunishiana misuli na Robinson Msimbe baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utajkaofanyika jumamosi ya oktoba 25 katika ukumbi wa Frends Corne Manzese Dar es salaam picha na SUPER D BLOG

 Mwandishi Wetu

MPAMBANO wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika

October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'


amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi'  na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo


pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver  na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi


katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika


mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani


Wednesday, October 22, 2014

BONDIA THOMAS MASHALI AJIFUA KUMKABILI MKENYA HENRY WANDERA NOVEMBA MOSI FRENDS CORNEBondia Tomas Mashali  kushoto akijifua wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Henry Wandera kutoka kenya novemba 1 katika ukumbi wa frends corner manzese, akisimamiwa na Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Na Mwandishi Wetu
BON DIA Thomasi Mashali  yupo katika maandalizi mazito ya kumkabili bondia kutoka kenya Henry Wandera Novemba mosi katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam

akizungumza wakati wa mazoezi yake juzi Mashali amesema kuwa yupo fiti wakati wowote yeye kufanya kazi hivyo aofii ata kiogo mpambano huo na kuwataka mashabiki wake waje waone anavyo mgalagaza vibaya sana siku hiyo mkenya Wandera

mbali na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi yatakayo wakutanisha Mbayo Ilunga na Fred Sayuni wakati Joseph Mbowe ataoneshana umwamba na Saidy Salum na Ramadhani Johncena ataoneshana ubabe na Baina Mazola

na mipambano mingene mikali zaidi siku hiyo kutakuwa na michezo ya utangulizi zaidi ya nane yenye raundi sita sita

katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 7000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali 

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

Monday, October 20, 2014

BONDIA FADHILI BOIKA AJINOA KUMKABILI GODFREY SILVE OKTOBA 25 FRENDS CORNER MANZESE


Bondia Fadhili Boika kushoto akipambana na Shomari Milundi wakati wa mazoezi yake yaliyofanyika katika ukumbi wa garden mburahati ya kujiandaa na mpambano wake wa Oktoba 25 kumkabili bondia Godfrey Silve katika ukumbi wa frends corne manzese Dar es salaam Picha na
SUPER D BLOG
Bondia Fadhili Boika kushoto akipambana na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi yake yaliyofanyika katika ukumbi wa garden mburahati ya kujiandaa na mpambano wake wa Oktoba 25 kumkabili bondia Godfrey Silve katika ukumbi wa frends corne manzese Dar es salaam Picha na
SUPER D BLOG
Msimamizi wa mazoezi kutoka 'King Class Team' Bilali Ngonyani kushoto akimsimamia kupiga gab bondia Fadhili Boika wakati wa masoezi yake ya kujiandaa kupambana na Godfrey Silve mpambano utakaofanyika oktoba 25 katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaa 
 ambaye ni msimamizi wa gym ya garden iliyopo kigogo mburahati walipokuwa wanafanyika mazoezi jana Picha na
SUPER D BLOG

Kocha Mohamed Mbadembade kushoto akiwaelekeza mabondia godfrey Mbwalu kulia, Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Shomari Malundi na Fadhili Boika baada ya kumaliza mazoezi katika ukumbi wa Garden Kigogo Mburahati Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
MABONDIA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA BAADA YA KUMALIZA MAZOEZI YAO KATIKA UKUMBI WA GARDEN KIGOGO MBURAHATI DAR ES SALAAM

BONDIA MANNY PAQUAIO KATIKA MATUKIO MBALIMBALI AKISHILIKI KATIKA MCHEZO WA BASKET BALL

Manny Pacquiao plays basketball with Cebu sports reporters at the Cebu City Sports Club in 2007. (CDN FILE PHOTO)
MANILA, Philippines—From being an eight-time world boxing champion and then a congressman, Manny Pacquiao can now call himself a basketball head coach.
Newly-approved PBA team Kia officially named Pacquiao its coach Monday in a press conference held at the Pacific Star building in Makati.
“I’m very happy to be named head coach of Kia,” said Pacquiao
- See more at: http://cebudailynews.inquirer.net/32311/its-official-new-pba-team-kia-names-pacquiao-head-coach#sthash.iDlyxtRE.dpuf
Manny Pacquiao plays basketball with Cebu sports reporters at the Cebu City Sports Club in 2007. (CDN FILE PHOTO)
MANILA, Philippines—From being an eight-time world boxing champion and then a congressman, Manny Pacquiao can now call himself a basketball head coach.
Newly-approved PBA team Kia officially named Pacquiao its coach Monday in a press conference held at the Pacific Star building in Makati.
“I’m very happy to be named head coach of Kia,” said Pacquiao
- See more at: http://cebudailynews.inquirer.net/32311/its-official-new-pba-team-kia-names-pacquiao-head-coach#sthash.iDlyxtRE.dpuf