Tangazo

Pages

Saturday, October 11, 2014

NGUMI KALI KUPIGWA OCTOBA 25 KATIKA UKUMBI WA FRIENDS CORNER MANZESE



MPAMBANO wa mchezo wa masumbwi mkali utakaokutanisha mabondia mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania utafanyika

October 25 katika ukumbi wa friends Corner manzese jijini Dar es salaam akizingumza na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'


amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mpambano wa mahasimu katika mchezo wa ngumi kati ya bondia Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi'  na George Dimos mpambano mwingine utawakutanisha Amani Bariki 'Manny Chuga' na Ally Bugingo mpambano unaosubiliwa kwa hamu kila kona ya jiji la Dar es salaam ambapo mabondia hawo wamejizolea umaarufu mkubwa kupitia mchezo huo


pambano jingine ni kati ya Juma Fundi atakaezichapa na Hamza Mchanjo wakati Hasani Mandula ataonyeshana kazi na Mohamedi Jaka na Shabani Kaoneka atazipiga na Ibrahimu Maokola anaejiandaa kuwania kucheza ubingwa wa taifa mwishoni mwa mwaka huu Fadhili Boika atazipiga na Godfrey Silver  na Habibu Pengo atazidunda na Abdallah Luanje, Kashinde Mohamedi atazidunda na Mohamed Kibaga wakati Sadiki Nuru atakumbana na Mohamed Mbishi


katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na ulinzi wa kutosha kabisa kutokana na kujipanga vizuri katika swala hilo  kingilio ni shilingi, 5000; kwa kila mtu mchezo huu utapambwa na burudani mbalimbali 



siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika


mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani


No comments:

Post a Comment