Tangazo

Pages

Wednesday, November 30, 2011

UBWA SALUMU AJIFUA KUMKABILI MUSTAFA DOTO DESEMBA 25


Bondia Ubwa Salum (kushoto) na Omari Bayi wakioneshana umwamba wa kutupa masubwi wakati wa Mazoezi ya Kambi ya Ilala Dar es salaam jana Ubwa anajiandaa na mpambano wake na Mustafa Doto Desemba 25 mwaka huu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

DAVID Haye amethibitisha kuwa kambi yake iko kwenye mazungumzo na Vitali Klitschko

LONDON,
DAVID Haye amethibitisha kuwa kambi yake iko kwenye mazungumzo na Vitali Klitschko kujadili uwezekano wa kufanyika pambano kati yao Machi mwakani.
Mpiganaji huyo wa London alitangaza kustaafu ngumi Oktoba mwaka huu lakini amesema kuwa yuko tayari kupigana tena kama atapata nafasi ya kurudiana baada ya kupoteza pambano lake Julai dhidi ya Wladimir Klitschko ambaye ni kaka wa Vitali.
Haye mchezo huo alisema: " Sijaona mkataba lakini kuna mazungumzo yanayoendelea.
"Nilisema kabla kabla ya kustaafu ningependa pambano hilo na kuna tarehe katika Machi ambayo imekuwa ikizungumziwa."
Mabondia hao wazaliwa wa Ukraine wamekuwa wakisema kwua mabalkuanalino yanafanyika ili kuwepo pambano la kuwania ubingwa wa WBC unaoshikiliwa na Vitali, baada ya Haye kupoteza pambano ambalo lilifanya apokwe ubingwa wa IBF/WBO dhidi ya Wladimir mjini Hamburg Julai mwaka huu.
Haye mwenyewe alisema amestaafu ngumi lakini yuko tayari kurejea ulingoni kama atajitokeza mmoja kati ya wanamasumbwi wa familia ya Klitschko.
Kumekuwa na mazungumzo kuwa huenda pambano hilo likafanyike Machi mwakani katika mji wa Dusseldorf Ujerumani.

BONDIA Amir Khan amethibitisha kuwa atapandisha

BONDIA Amir Khan amethibitisha kuwa atapandisha


WASHINGTON, Marekani

BONDIA Amir Khan amethibitisha kuwa atapandisha uzito baada ya pambano lake dhidi ya Lamont Peterson litakalofanyika Washington mwezi ujao kama Timothy Bradley atakataa kupigana naye.

Kwa mujibu wa Dail Mail Khan, ambaye ni bingwa wa dunia uzito wa Light-welter atataka kutwangana na Bradley katika mechi ya kuunganisha mataji.

Bondia mwenye miaka 28, Bradley nsiye anaonekana anaweza kutoa upinzani mkubwa kwa Khan katika uzito wao, lakini amekuwa akionesha kuwa hataki kupigana naye.

Khan mwenye miaka 24, anaamini kuwa kama
Bradley ataendelea kugoma kupigana hatakwua na uamuzi mwingine ataacha na mapambano ya light-welter na mikanda yake na kuhamia katika uzani wa welter ili kupata mechi kubwa.

Kama pambano dhidi ya Bradley litakuwepo kwangu nitabaki katika uzito nilio nao lakini kama halitakuwepo nitahamia katika uzito wa welter,"alisema Khan.
Alisema anataka kupigana na mabondia wapya na na lihi ndilo linamsukuma kwa sasa.

"Tutaona kitu gani kitatokea baada ya mechi hii na kama pambano dhidi ya Bradley litafanyika. kama sivyo nitapandisha uzito."
Khan atapigana Desemba 10 kwenye ukumbi wa Convention Center, Marekani dhidi ya Peterson atakayekuwa nyumbani.

Khan alisema: "Nina mtindo ambao watu wanapenda, kasi na ngumi kali na kweli anamini kuwa ingawa Peterson atakwua nyumbani nitaaungwa mkono zaidi kuliko yeye siku hiyo.
"Hawajapata pambano la kusisimua Washington kwa muda mrefu kwa hiyo itakwua kitu kizuri kwao. Kila wakati nimekuwa nikitamani kupigana katika miji tofauti ili watu kupata nafasi ya kuniona mimi jukwaani.
"Nilitaka kupigana na Bradley na nikaja kupiugana na Marcos Maidana na Zab Judah na kuwapiga wote."

Monday, November 28, 2011

Rashid Matumla VS Maneno Osward KUPIMA UKIMWI SIKU KUMI KABLA YA MPAMBANO

Rashid Matumla VS Maneno Osward KUPIMA UKIMWI SIKU KUMI KABLA YA MPAMBANO


Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.
Pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .

Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki wakati walishawai kupigana mara mbili nyuma ambapo Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kashinda mara moja mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.

UTasindikizwa na mabondia Venas Mponji atakayezichapa na Tumaini Maguno 'SMG' na bondia mkongwe Rashidi Ally atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet Kalulu na Saleh Mtalekwa

Siku kumi kabla ya mpambano huo mabondia Rashidi Matumla na Maneno Osward wameshauliana kupima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi na madawa ya kuongeza nguvu kama wanatumia sheria za mchezo huo azirusu kutumia dawa za aina yoyote ya kuongeza nguvu
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

Monday, November 21, 2011

Ngumi kupigwa Desemba 18,MZALENDO PUB
Na MWANDISHI WETU

WASANII mbali mbali hapa nchini wanatarajiwa kutoa burudani katika pambano la mchezo wa ngumi lisilo na ubingwa litakalowakutanisha bondia, Mada Maugo na mpinzani wake Suleimani Saidi 'Toll' Desemba 18 mwaka huu katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama JIjini Dar es Salaam.

Akizungumza na kona hii ya burudani Raisi wa shirikisho la ngumi za kulipwa hapa nchini (PST) Emanuel Mlundwa alisema, maandalizi kwa ajili ya pambano hilo yamekamilika.


Aliwataja wasanii watakaotoa burudani siku hiyo kuwa ni Kundi la mapacha watatu Khalid Chokoraa (Halidi Chuma)pamoja na msanii wa mziki wa bongo fleva Mwana FA (Hamisi Mwinjuma).

Alisema licha ya kuwepo kwa burudani hizo vile vile atakuwepo kocha wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila Super D kwa ajili ya kutoa mafunzo kupitia Dvd pamoja na kuzisambaza.

Aliwataka mashabiki wao wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani hiyo, licha ya kuwa mchezo huo haupewi kipaombele watahakikisha wanasonga mbele katika kuazimisha miaka 50 ya uhuru.

aidha katika mapambano ya ngumi ya utangulizi mabondia Yohana Miyayusho na Shadrack Juma, Doto Kipacha atazidunda na Saidi Muhidini na kwa upande wa mchezo wa Kick Boxing ambao utatuwakilisha kimataifa Tanzania Muaythai Academy of Combat watawaletea mpambano kwa mara ya kwanza nchini kati ya bondia Emanuel Shija kutoka Tanzania na Munyeshyaka Vincent kutoka Rwanda Mpambano huo utakuwa wa kimataifa kutokana na ushiriki wake wa nchi hizo mbili nchini zitakuwa zikipeperusha bendera zao.

Sunday, November 20, 2011

ngumi kupigwa Desemba 9 DDC Keko Dar es Salaam

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Ramadhan Nassib, anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na mpinzani wake Antony Kariuki wa Kenya, katika pambano la maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru litakalopigwa kwenye Ukumbi wa DDC Keko Dar es Salaam, Desemba 9 mwaka huu.

Akizungumza  Mratibu wa pambano hilo, Pius Aghaton, alisema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na rekodi zilizopo kwa mabondia wote.

Alisema kuwa pambano hilo litakuwa la uzito wa Fly ambalo litapigwa katika raundi 10.

“Tumeandaa pambano la aina yake kwa ajili ya kusherekea miaka 50 ya Uhuru na pia kuweza kuwajengea mabondia wetu uwezo wa kucheza mapambano ya kimataifa” alisema.

Mratibu huyo alisema kuwa katika pambano hilo, kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo bondia Juma Fundi atazichapa na Juma Seleman katika pambano la uzito wa Fly la raundi sita, Fred Sayuni atazipiga na Bakari Dunda katika pambano la uzito wa Feather la rfaundi sita.

Pambano jingine litawakutanisha mabondia Rashid Ally pamoja na Daud Mhunzi katika pambano la uzito wa Feather la raundi sita na Faraji Sayuni atazichapa na Alpha George katika pambano la uzito wa Fly la raundi nne.

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
Mob;+255787 406930
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Saturday, November 19, 2011

mashindano ya ngumi ya kova cup yamalizika

 Bondia Mussa Mohamedi (kulia) akimfulumusha makonde mfululizo, Fadhili Hassani wakati wa mpambano wa mashindano ya Kova Cup yaliyomalizika, Dar es salaam jana Mussa alishinda kwa K,O ya raundi ya tatu.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

 Mabondia wa kike Mariamu Edwer (kushoto) na Matha George wakipambana wakati wa mashindano ya Kova Cup yaliyomalizika, Dar es salaam, jana Matha alishinda kwa ponti.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Friday, November 18, 2011

KOZI YA MAKOCHA WA NGUMI MKOA WA PWANI YAOTA MBAWA

 Baadhi ya makocha wa mchezo wa ngumi wakiwa Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuuzuria kozi ya makocha iliyotarajia kuanza jumamosi ya kesho
ata hivyo kozi hiyo iliota mbawa baada ya mkufuzi alieteuliwa na chama cha ngumi cha dunia (AIBA) kupata dharura kozi hiyo iliyoandaliwa na kamati
ya Olimpic (TOC) iliota mbawa na kufanyika kwa makocha hawo kutojua hatma yao baada ya kufika Pwani bila kupewa stahiki zao walizoaidiwa katika
barua ikiwemo usafiri wa kwenda na kurudi pamoja na chakula ambavyo awajapatiwa na kujitafutia usafiri kwa njia yao wenyewe kurudi mikoani
kwao.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)


Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa NChini (BFT), Michael Changalawe (kulia) akizungumza na makocha wa ngumi nchini wakati
walipowasili, Kibaha Mkoa wa Pwani Juzi kwa ajili ya kozi ya mchezo huo na kuambiwa kozii hiyo iliyoandaliwa na kamati ya Olimpic (TOC)  imealishwa
kutokana na mkufuzi wake alieteulia kupata dhalura hata hivyo, makocha hao kutoka mikoa mbalimbali ya nchi walinyimwa stahiki zao hususani
maradhi na posho za nauli za kuwaludisha mikoa walikotoka na kupatiwa kwa makocha wachache tu kinyume na barua walizopewa makocha ya kuwa
watalipiwa garama zote za kwenda na kuwarudisha mikoani kwao.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)

Wednesday, November 16, 2011

MASHINDANO YA NGUMI YA KOVA CUP YAENDELEA

Bondia Sunday Elius akipambana na Abdallah Kasimu wakati wa mashindano ya Kova Cup Dar es salaam jana Kasimu alishinda kwa point
Bondia Mussa Mohamedi (kulia) kushoto akioneshana ufundi wa kutupa makonde na John Christian wakati wa mashindano ya Kova Cup Dar es salaam jana Mussa alishinda kwa pointFuraha ya ushindi
musa mohamedi na
JOhn Christiani wakioneshana ubavu
Monday, November 14, 2011

MABONDIA WAPIMA AFYA ZAO LEO


Daktar wa Mchezo wa ngumi Josefu Magesa akiwapima mabondia watakaoshiriki mashindano ya kova Cup yanayoanza Dar es salaam leoMsimamizi wa mchezo wa ngumi Antoni Mwangonda akiakiki uzito wa bondia Mustafa Mtolo leo

Sunday, November 13, 2011

BONDIA MANNY PAQUAIO AMDUNDA JUAN MANUEL KWA POINTI

Manny Pacquiao celebrates his majority decision victory against Juan Manuel Marquez in the WBO world welterweight title fight at the MGM Grand Garden Arena on November 12, 2011 in Las Vegas, Nevada. Photograph: Ethan Miller/Getty

Saturday, November 12, 2011

TAARIFA YA KUPIMA UZITO NA AFYA WACHEZAJI NA WAAMUZI

                         BOXING FEDERATION OF TANZANIA (BFT)
                                       SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA
                                                                                                                             SLP 15558                
                                                                                                                              DA ES SALAAM
                                                                                                                                       12/11/2011
                                                                                                                        Email;bft.tanania2009@gmail.com
           VYOMBO VYA HABARI.

                        YAH; TAARIFA YA KUPIMA UZITO NA AFYA WACHEZAJI  NA WAAMUZI
                                   WATAKAOSHIRIKI MASHINDANO YA KOVA CUP 14/11/2011
                                                  PR STADIUM HOTEL..
 
           SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA(BFT)LIMEPEPANGA  KUWA UPIMAJI WA AFYA NA UZITO KWA WACHEZAJI NA WAAMUZI  WATAKAO SHIRIKI KATIKA MASHINDANO YA  KOVA BOXING CUP UTAFANYIKA TAREHE 14/11/2011 SAA 1.00 HADI SAA 4.00 ASUBUHI ,PR STADIUM HOTEL KATIKA UKUMBI  WA HOTEL HIYO WA IJUMBI GRILL.

UPIMAJI WA AFYA NA UZITO UTASIMAMIWA NA WAAMUZI WALIOTEULIWA NA CHAMA CHA WAAMUZI WA NGUMI  TANZANIA WAKISIMAMIWA NA KATIBU WAO JUMA SELEIMAN.

JUMLA YA WAAMUZI 8  NA DAKITARI  1 WAMETEULIWA KUJA KUCHEZESHA MASHINDANO HAYO BAADHI YAO NI JUMA SULEIMANI,SALEHE MWINYIKHERI,MANENO OMARI,RIDHAA KIMWELI,MARCO MWANKENJA,MAFURU MAFURU,MOHAMED BAMTULAH ,MOSHI MAKALI NA DAKITARI JOSEPH MAGESA,

ZAIDI YA TIMU 15 ZIMETHIBISHA  KUJA KUSHIRIKI MASHINDANO HAYO BAADHI YA TIMU HIZO NI  ASHANTI YA ILALA,NGOME, JKT,MAGEREZA,URAFIKI,MABIBO ,SIFA,MBAGALA,MIEMBENI,NDAME,MBEZI,LUAHA ,TEMEKE,KEKO,POPUILAR NA TIMU ILIYOOMBA KUSHIRIKI KUTOKA DODOMA

Katika Michezo hiyo ya siku mbili kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach'  kabla ya kwenda kuhudhulia kozi ya kimataifa ya mchezo huo ambayo itaongozwa na mkufuzi ambaye ameteuliwa na Chama cha Ngumi cha Dunia (AIBA) Ndg Azzedin Aggoune kutoka Algeria
DVD HIZO kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi. Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali. '' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani, DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
Mob;+255787 406930
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

--

MAKORE MASHAGA
KATIBU MKUU BFT

                                    MOB;+255713588818
                                    EMAIL; mashagam@yahoo.com--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Friday, November 11, 2011

RASHIDI MATUMLA NA MANENO OSWARD KUZIPIGA Desemba 25

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni  kuzichapa Desemba 25  mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.

Pambano hilo linatarajia kuwa  la raundi 10 uzito wa kati  litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .

Akizungumza Dar es Salaam jana  Ofisa habari wa Kampuni Adios Promotion ambao ndio waandaaji wa pambano hilo, Mao Lofombo alisema  pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki.

Alisema tayari mabondia hao wamekubali kucheza pambano hilo ambalo litakuwa la marudiano na kwamba  wameshaanza maandalizi  ambapo kila mmoja amejigamba kumstaafisha mwenzie ngumi.

Mao alisema, licha ya pambano hilo linalotarajia kuvuta hisia za mashabiki wa ngumi, pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ambapo Rashidi Ally atachapana makonde na Hassan Sweet, Kalulu Bakari na  Athuman Kalekwa na  Shabani Kazinga na Kashinde
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D Boxing Coach' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

'' Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi '' alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.

Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
Mob;+255787 406930
+255774406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania


Jina: Rashid Matumla

Nafasi Yake: Bingwa wa dunia wa uzito wa kati (WBU)
Historia Fupi

Rashid Matumla alizaliwa mkoani Tanga hapo Mei 6, 1968. Aliingia katika masumbwi mwaka 1979 ambapo ameshiriki mashindano mbali mbali kama vile ile ya olimpiki ya Seoul 1988. Amewahi kuwa bondia bora Afrika mashariki na kati hapo mwaka 1990, na mwaka huo huo alikuwa bingwa wa ridhaa Afrika mashariki na kati .

Mwaka 1997 alitwaa ubingwa wa Afrika na kutwaa taji la mabara linalotambuliwa na WBU mwaka huo huo. Mwaka 1998 alitwaa taji la kimataifa WBU na mwaka hou huo alitwaa ubingwa wa dunia wa WBU uzito wa lightmiddle.

Amecheza michezo 24 katika ndondi za kulipwa na ameshindwa mara moja. Kati ya hiyo 14 ameshinda kwa knockout.


Makutano ya Rockers na familia ya Matumla January 1999
"Mafanikio ya akina Matumla ni jitahada za muda mrefu"

Kitu kilichochukuliwa kama burudani ya kawaida na Mzee Matumla miaka mingi iliyopita leo hii kimegeuka kuwa sifa kwa taifa zima la Tanzania. Bondia huyo wa zamani, Mzee Matumla anasema enzi hizo hakukuwa na chama ngumi hivyo mchjezo huo ulikuwa ni kwa ajili ya burudani hasa kwa siku za jumapili huko katika mashamba ya mkonge Tanga.

Lakini mzee huyo alianza kubadili muelekeo wake katika ndondi pale pale alipoanza kuwafundisha watoto wake mchezo huo. Si kwamba wanawe walikuwa wakiupenda mchezo huo ila nia yake ilikuwa ni kuwaepusha na makundi ya kihuni. Hii iliwafanya wawe na nidhamau na taratibu nao walianza kuvutiwa na mchezo huo. "Ilikuwa ikifika Jumapili kila mtu
anakasirika kwani siku hiyo itamaanisha kukimbia sana na mazoezi" anasema bingwa wa dunia Rashid Matumla. Mzee Matumla aliendelea kuwakazania wanae katika masumbwi.
Lengo lake likiwa siku moja nao waje kuliletea taifa la Tanzania sifa, lengo ambalo limetimia hivi karibuni. Mzee Mataumla anasema katika kupata mafanikio ni lazima rasilimali itumike. "Lazima ugharamie mazoezi ili kupata timu nzuri, mimi niliwagharamia sana hawa vijana kimazoezi, vifaa na kuwapa lishe ya kutosha. Kama huwapatii lisha ya kutosha basi hujengi bali unaumiza". Mzee Matumla anaendelea kusema kuwa siri ya mafanikio katika ngumi ni uvumilivu. "Kumbuka umapompata mwenzio, na yeye anakupata, mvumilivu ndiye anashinda". Mzee Matumla anatoa wito kwa viongozi kuitumia vizuri sera ya michezo vizuri, kuzingatia na kuweka mbele maslahi ya wanamichezo katika maandalizi ya awali ili kutoa mabingwa kila wakati. "Kama hujala vizuri, utatetemeka tu".

Mzee Matumla anavutiwa na juhudi za bondia Marwa chni ya promota Madaraka Nyerere na anasema kuwa vijana wengi wakipatiwa nafasi basi taifa litakuwa na mabondia wegi katika nyanja za taifa na kulipwa.

Mzee Matumla anamshukuru sana promota Jamal Malinzi wa DJB Promotions kwa kuwapeleka wanae katika anga za kimataifa. "Mimi niliwafikisha ngazi ya taifa, yeye kawapeleka ngazi ya kimataifa". Hadi leo pamoja na kuwa Rashidi na Mbwana wanashikilia mikanda ya dunia, Mzee Matumla bado hachoki kukagua mazoezi yao wawapo nyumbani. "Nawakazania kuwa tayari wakati wowote kwani anaweza mtu kuja wakati wowote kutaka kuwa challenge, hivyo lazima wawe tayari wakati wote", anamalizia mzee Matumla.

Rashidi Matumla anasema yeye bado hajaridhika kabisa na mafanikio aliyoyapata hivi karibuni. Anasema lengo lake ni kushinda mataji yanayatambuliwa na vyama vingine kama IBF, WBC au WBA. Anasema bidii yake katika WBU itamwenzesha kucheza WBC au WBO.
"Nikiweza kutetea taji hili mara mbili au tatu naweza kuomba kucheza kupitia vyama vingine kama WBC au WBO" anasema Rashid. Anaendelea kusema kuwa katika ngumi kinachohitajika ni nafasi, bila kupewa nafasi ya kupigana hautaendelea wala kutambulika.

Mafanikio ya akina Matumla yanatokana kwa kiwango kikubwa na kocha wao Norman Hlabane wa Afrika ya Kusini. Rashid anasema wanapokuwa Afrika ya kusini huwa wanapata mazoezi mazito sana. Ansema anapokuwa nje ndio anakuwa makini zaidi hivyo hategemei kuweka kambi yake ya mazoezi
hapa Tanzania. Akiwa Afrika ya Kusikni huwa anakuwa na program nzuri ya mazoezi. Hii yote inatokana na kuwa na kocha mzuri na mwenye kuipenda kazi yake. "Kocha wangu ni mtu mkali sana kuhusu mazoezi" anaongeza Rashid. Kocha huyo huwajenga ki boxing na kisaikolojia. "Tukiwa nyumbani tunakuwa kama watoto wake lakini mazoezini anabadilika kabisa". Rashid anamsifia kocha wake kwa kusema kuwa ni mtu makini na ndio maana ametoa mabingwa wa dunia kama watatu auwnne hivi. "Kila siku atakuotoa makosa, ukifanya vizuri anakwambia na vibaya anakwambia". Kutokana na mazoezi ya kocha wake huyo hivi sasa anajisikia nguvu zaidi tofauti na mwanzo ambapo alikuwa mwepesi lakini hana nguvu. "Ukipata mafunzo Afrika ya kusini una uwezo wa kupigana na mtu yeyote duniani", anasema Rashid.

Anavutiwa na mchezo wa Moses Marwa na ndiye bondia ambaye anamuona anaweza kufanya vizuri katika ndondi za kulipwa, pamoja na umri wake. "Mbona Foreman alirudi kama mtu mzima na alifanya mavitu ?" anauliza Matumla.
Kimataifa alikuwa anavutiwa na Mohammed Alli na Sugar Ray Leonard. Hivi sasa anavutiwa na Roy Jones.

Nukuu muhimu
"Huwa sina makeke. Mimi ni wa vitendo sio mtu wa porojo".

"Ubingwa wa dunia haunifanyi nijione tofauti na watu wengine. Ninafurahia heshima ninayoipata kutoka kwa watanzania wenzangu. Hata hivyo mimi bado ni mtu yule yule, naishi kule kuloe nilikokuwa nikiishi, naongea na watu wale wale na natembelea sehemu zile zile".

"Mbwana ni bondia mzuri anaachohitaji ni nafasi tu. Kule Afrika ya Kusini watu walikua wakihama hata Gym kumkimbia. Ni mwepesi sana."

"Mzee wetu alifanya boxing kama elimu. Akiwa off kazini, tulikuwa tunaenda nae mazoezini, wakati mwingine tulikuwa tunamkimbia. Tulikuwa tukiwasikia akina Nassor Michael na Isangura tulitamani kuwa kama wao na baba yetu alikuwa akitupa moyo sana."

"Jioni tulikuwa tunatembea toka klabu ya Simba mpaka nyumbani (keko) kwa miguu na njia nzima anakuwa akitutoa makosa. Ulikuwa unafanya bidii ili nyumbani usikosolewe".