Tangazo

Pages

Friday, March 27, 2015

MUDY MATUMLA MCHINA KUPAMBANA LEO IJUMAA DIAMOND JUBILEE


 Bondia Wang Xin Hua kutoka China 'kushoto'  wakitunishiana misuli na Mohamed Matumla baada ya kupima uzito Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wao leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee (Picha Zote  na Super D Boxing News)
Wang Xin Hua kutoka China 'kushoto'  wakitazamana kwa usongo  na Mohamed Matumla baada ya kupima uzito Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wao leo katika ukumbi wa Diamond jubilee katikati ni Jay Msangi Promota wa mpambano huo.
Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Jay Msangi 'Jiwe Gumu' katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Mfaume Mfaume kushoto na Cosmas Cheka baada ya kupima uzito jana kwa ajili ya mpambano wao wa leo.

 

 

NGUMI KUPIGWA KESHO JUMAMOSI MANYARA PARCK CCM TANDALE JUMAMOSI MARCH 28

Bondia Yusuph Mkali kushoto akitunishiana misuli na  Vicent Mbilinyi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho jumamosi ya march 28 katika ukumbi wa manyara parck uliopo tandale ccm Picha na SUPER D BOXING NEWS
Chirstopher Mzazi katikaki akiwainua juu mabondia Julius Kisalawe kushoto na Said Uwezo kwa ajili ya mpambano wao wa kesho jumamosi ya march 28 utakaofanyika katika ukumbi wa manyara parck ccm tandale Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Yusuph Mkali kushoto akitunishiana misuli na  Vicent Mbilinyi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho jumamosi ya march 28 katika ukumbi wa manyara parck uliopo tandale ccm Picha na SUPER D BOXING NEWS


Na Mwandishi Wetu

Mabondia Julius Kisalawe kutoka Ndame Clab na Said Uwezo kutoka Mzazi GYM wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa utakao fanyika katika ukumbi wa manyara parck ccm tandale march 28 jumamosi

mpambano uho utakuwa chini ya oganaizesheni ya mchezo wa ngumi za kulipwa T.P.B.O ambapo msimamizi wa upimaji uzito Ibrahimu Kamwe alitoa taharifa kuwa bondia Uwezo alikuwa kazidi uzito na kumfanya apewe mda wa kukata uzito kwa masaa matano zaidi ili afikie lengo lake la kugombanmia ubingwa uho ambao unashikiliwa na Kisalawe

bondia huyo alikata uzito kwa mda unaotakiwa na kurusiwa kuwania ubingwa uho wa kg 52

mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kusindikiza mtanange uho ambapo bondia kutoka Super D GYM iliyopo shule ya Uhuru Vicent Mbilinyi atapambana na Yusuph Mkali mpambano wa raundi sita ambapo kiingilio katika mpambano uho ni silingi. 5000 tu na wanawake ni bule kabisa 
 siku hiyo kutakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwa watu na mali zao 

siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
 

Tuesday, March 24, 2015

BONDIA WANG XIN HUA KUTOKA CHINA AWASILI KUMKABILI MUDY MATUMLA IJUMAA


Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassini Abdalla kushoto akisalimiana na bondia Wang Xin Hua kutoka China mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wake na mohamed Matumla utakaofanyika march 27 katika ukumbi wa diamond jubilee katikati ni Rais wa ngumi za kulipwa nchini PST Emanuel Mlundwa na kulia ni promota wa mpambano uho Jay Msangi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassini Abdalla kushoto akisalimiana na bondia Wang Xin Hua kutoka China mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam jana kwa ajili ya mpambano wake na mohamed Matumla utakaofanyika march 27 katika ukumbi wa diamond jubilee katikati ni Rais wa ngumi za kulipwa nchini PST Emanuel Mlundwa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Wang Xin Hua kutoka China akilakiwa na mwenyeji wake Rais wa ngumi za kulipwa nchini PST Emanuel Mlundwa

bondia Wang Xin Hua kutoka Chinabondia Wang Xin Hua kutoka China
Bondia Wang Xin Hua kutoka China akiwasili nchini kwa ajili ya mpambano wake na Mohamed Matumla utakaopigwa March 27 katika ukumbi wa Diamond jubilee kulia ni promota wa mpambano uho Jay Msangi

Thursday, March 19, 2015

MPAMBANO WA MASUMBWI KUFANYIKA 28/3/2015

Na Mwandishi Wetu 
Mabondia Julius Kisarawe kutoka 'Ndame Club' na Saidi Uwezo kutoka 'Mzazi GYM' watapanda uringoni march 28 kugombania ubingwa wa taifa wa kg 54 katika ukumbi wa manyara park uliopo CCM Tandale Manzese mpambano uho wa raundi kumi wenye upinzani wa hali ya juu utasindikizwa na mabondia mbalimbali kutoka katika kambi tofauti

ambapo bondia Ibrahimu Tamba atapambana na George Dimoso na Vicent Mbilinyo kutoka kwa 'Super D Boxing Coach' atapambana na Yusufu Mkari na kasimu Gamboo atakabiliana na Mustafa Dotto na Mohamed Kibanga atapambana na Bakari Dunda wakati Karim Mura  atamkabili Eddy Baguo


Bondia Cosmas Cheka kushoto akitunishiana misuli na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika jumamosi ya feb 28 uwanja wa ndani wa taifa picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Cosmas Cheka wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa raundi kumi kugombania ubingwa wa U.B.O Africa utakaofanyika jumamosi hii katika uwanja wa ndani wa taifa mpambano huo mkali utatanguliwa na ngumi kali kutoka kwa bondia Fransic Miyeyusho atakaezipiga na Fadhili Majiha mpambano wa raundi nane mpambano mwingine wa ubingwa ni kati ya Alibaba Ramadhani na Jacobo Maganga na katika kusindikiza mapambano hayo makali bondia machachari na chipkizi Vicent Mbilinyi ataoneshana umwamba na Epson John wa Morogoro na Shomari Milundi atapambana na Mwinyi Mzengela huku Husein Mbonde atakabiliana na Shedrack Ignas katika kuhakikisha mpambano huo unakuwa wa kihistoria na kuacha gumzo nchini bondia Said Mundi wa Tanga atapambana na Ramadhani Shauli na mapambano mengine mbalimbali
mpambano huo unaosimamiwa na P.S.T chini ya rais wake Emanuel Mlundwa yamekuwa gumzo mjini na kusababisha taflani za mabondia kutaka kupigana kavukavu uku makocha wao pia wakikunjiana ngumi
siku hiyo kutakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwa watu na mali zao 

siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.


NGUMI KUPIGWA MARCH 28 KATIKA UKUMBI WA MANYARA PARKBONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE'MATUMLA AMPANIA KUMMALIZA MCHINA


Mwandishi Wetu
Wakati bondia Mohamed Matumla Jr akiwa katika mazoezi ya mwisho mwisho
kumkabili Wang Xin Hua wa China, wenzake Thomas Mashali na Karama
Nyilawila wametoleana uvivu huku kila mmoja akijigamba kutwaa ubingwa
watakapozichapa Machi 27 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar
es Salaam.
Matumla Jr atazichapa na Hua pambano la super bantam la ubingwa wa
dunia wa (WBF World Eliminate) pambano maalumu kwa mabondia hao la
kutafuta tiketi ya kucheza pambano la utangulizi kwenye lile la nguli
wa masumbwi duniani, Manny Pacquiao na Floyd Mayweather la Mei 2.
Kama Matumla atampiga Hua kwenye pambano lao la Machi 27 na kuonyesha
kiwango kizuri atapata nafasi ya  kucheza pambano la utangulizi
kuwasindikiza nguli hao wa masumbwi duniani watakapovaana Mei 2 jijini
Las Vegas.
Akizungumza katika mazoezi yake yanayoendelea kwenye gym ya Oil Com,
Keko jijini Dar es Salaam chini ya kocha wake ambaye ni baba yake
mzazi, Rashid 'Snake Man' Matumla, bondia huyo alisema hataki kupoteza
nafasi ya kucheza kwenye pambano la Mayweather na Pacquiao.
"Najua ugumu wa pambano langu na Hua hivyo sitaki kufanya mzaha, niko
fiti na sasa nafanya mazoezi mepesi ili kumkabili lakini pia sitaki
kupoteza nafasi ya kuwasindikiza nguli wa masumbwi duniani kwani ni
pambano ambalo 'litanitoa'," alisema Matumla Jr.
Kocha wake alisema, hivi sasa bondia huyo anajifua katika mazoezi ya
mwisho mwisho ambayo ni ya wepesi na kumweka tayari kumkabili Hua.
"Mudy yuko fiti, nimekuwa naye katika mazoezi, kiwango chake
kinaridhisha na sasa yuko katika hatua ya mwisho kabisa ambayo ni ya
mazoezi mepesi ya kumuweka tayari kwa pambano," alisema kocha wa
bondia huyo.

Promota wa pambano hilo, Jay Msangi alisema ili Matumla Jr apate
nafasi ya kuwasindikiza Pacquiao na Mayweather ni lazima aonyeshe
kiwango kwenye pambano lake na Hua.
"Tayari tumemwambia Matumla Jr vigezo hivyo kwani si ili mradi
kushinda bali aonyeshe kiwango kama ni ngumi ziwe ngumi kweli kwani
hawezi akacheza kwa kukumbatia na kushinda kwa pointi alafu apewe
nafasi ya kucheza Las Vegas, kule mashabiki wanataka waone ngumi hivyo
Matumla Jr anapaswa kupambana Machi 27 ili apate nafasi hiyo,"
alisema.
 
Siku hiyo pia, Japhet Kaseba atazichapa na Mada Maugo wakati Karama
Nyilawila akionyeshana ubabe na Thomas Mashali ambapo mabondia hao
kila mmoja amejigamba kutwaa ubingwa.
"Sina hofu na mpinzani wangu kwani kiwango chake nakijua na amekuwa
bondia wa kukimbia kimbia ulingoni hivyo ajiandae, cha msingi ni
mashabiki wangu kujitokeza kwa wingi kunipa sapoti," alisema
Nyilawila.
Wakati Mashali akijinadi kuwa yeye ataonyesha vitendo ulingoni siku
hiyo kwani nafasi ya kupigwa na Nyilawila haipo kwake na kusisitiza
kuwa yuko fiti na hatarajii kama mpinzani wake atamaliza raundi zote
siku hiyo.

Saturday, March 14, 2015

MUDY MATUMLA NA MCHINA KUTABILI RUKSA


WAKATI homa ya pambano la ubingwa wa dunia wa WBF kati ya mabondia, Mohamed Matumla na Wang Xin Hua wa China ikipamba moto, wadhamini wa pambano hilo wametoa nafasi kwa mashabiki wa ndondi kubahatisha 'kubeti' mshindi.

WAKATI homa ya pambano la ubingwa wa dunia wa WBF kati ya mabondia, Mohamed Matumla na Wang Xin Hua wa China ikipamba moto, wadhamini wa pambano hilo wametoa nafasi kwa mashabiki wa ndondi kubahatisha 'kubeti' mshindi.

Pambano hilo la raundi 12 la uzani wa Bantam limepangwa kufanyika Machi 27 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa pia na bingwa wa zamani wa dunia wa uzani wa juu, Francois Botha ambaye atakuwa mgeni rasmi.

Promota wa pambano hilo, Jay Msangi alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na pambano litasimamiwa na Shirikisho la ngumi la dunia la WBF ambaye rais wake atawasili nchini Machi 21.

Akizungumza jijini jana, Meneja Masoko wa Casino za Iplay 8, Le Grande na Palm beach, Ezekiel Lyal alisema wameamua kutoa nafasi ya bahati nasibu ya kushinda fedha'Kubeti' kwa mashabiki wa ndondi kwenye pambano hilo.

"Shabiki anachotakiwa ni kuingia kwenye tovuti ya www.iplay8casino.com ambapo kama ni mara ya kwanza atajisajili kwa kufuata maelekezo ambapo ni bure na atafungua akaunti ambapo ataanza kubeti na anaweza kufanya hivyo kwa wakala yoyote wa mtandao wa simu au benki na anaweza kuweka kiasi chochote cha fedha kuanzia elfu moja na kuendelea," alisema Lyal.

Mbali na pambano la Matumla, siku hiyo pia mabondia wenye upinzani, Mada Maugo na Japhet Kaseba na Karama Nyilawila na Thomas Mashali watazichapa mapambano ya kumaliza ubishi nani mkali kati yao huku bondia wa uzito wa juu kutoka Zanzibar akizichapa na bondia kutoka Marekani.

"Maandalizi yote yamekamilika na kuanzia wiki ijayo mabondia kutoka nje ya nchi na viongozi wa WBF sambamba na Botha wataanza kuwasili kwani tayari tiketi zao zimekamilika," alisema Msangi.
Mshindi wa pambano hilo, atashuhudia pambano la wakali hawa, Manny Pacquiao (kushoto) na Floyd Mayweather.
 

NGUMI KUPIGWA MARCH 15 UWANJA WA NDANI WEA TAIFA

Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakikunjana baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakikunjana baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Thomas Mashali akipima uzito
Bondia Japhert Kaseba akipima uzito kulia ni mpinzani wake Said Mbelwa akishudia kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Said Mbelwa akipima uzito kulia ni mpinzani wake Japhert Kaseba akishudia kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Said Mbelwa na Japhert Kaseba wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Abdallah Pazi Akipima uzito
Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Mada Maugo na Kalama Nyilawila nusula wazipige kavu kavu wakati wa upimaji wa uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kesho jumapili mpambano utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa wakati wa upimaji uzito

Maugo alienda kumtambia Kalama na kumpiga kibao pamoja na teke kali sana lililompiga Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakati akiamulizia ugomvi uho hapo ndipo lilipozuka songombingo kali kwa mashabiki wa kambi zote mbili wakitaka kuzipiga kavu kavu uku maugo akiwa ameshapanda moli wa kupigana nje ya uringo

mpambano uho ambao utakuwa na michezo mingine ya kumaliza ubishi ni kati ya Thomas Mashali atakaemkabili Abdallah Pazi na Japhert Kaseba atapambana na Saidi Mbelwa mipambano hiyo yote yatafanyika siku ya jumapili march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa


ambapo baadhi ya mashabiki wameomba baadhi ya daladala zinazofanya kazi usiku kwenda kuwa chukuwa pindi wamalizapo kuangalia mapambano hayo yaliyo na ushindani wa kweli

siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

Thursday, March 12, 2015

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' ANYAKUWA UBINGWA WA U.B.O AFRICA KWA KUMTWANGA COSMAS CHEKA


 

 

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa kugombea ubingwa wa U.B.O Africa mpambano uliofanyika jumamosi ya jana Class alinyakuwa ubingwa huo kwa kushinda kwa Point na sasa Class anashikilia mikanda miwili ya ubingwa wa Africa W.P.B.F na U.B.O Africa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' askiwa na mikanda yake ya ubingwa wa Africa wa U.B.O na WPBF
Bondia Fadhili Majiha kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fransic Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Majiha alishinda mpambano huo kwa point Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Cosmas Cheka wakati wa kugombea ubingwa wa U.B.O Africa mpambano uliofanyika jumamosi ya jana Class alinyakuwa ubingwa huo kwa kushinda kwa Point na sasa Class anashikilia mikanda miwili ya ubingwa wa Africa W.P.B.F na U.B.O Africa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Cosmas Cheka akipambana na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa U.B.O AFRICA
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' akishangilia ushindi na mashabiki wake baada ya mpambano wake na Cosmas Cheka na kufanikiwa kumdunda kwa point


Na Mwandishi Wetu

BONDIA machachali wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ametwaa ubingwa wa U.B.O Africa mwishoni mwa wiki iliyopita kwa kumtwanga bondia Cosmas Cheka wa Morogoro kwa point mpambano wa raundi kumi lililofanyika katika uwanja wa ndani wa taifa Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita

katika mpambano uho ulioanza kwa mashambilizi kwa kila bondia kumtupia makonde mwenzie kwa ufundi wa  ali ya juu na ulikuwa wa vuta nikuvute kwa kila upande baada kila mmoja kujiandaa kwa mda mrefu ata hivyo class alibuka mbabe baada ya raundi kumi kwisha

katika mipambano mingine iliyopigwa siku hiyo bondia Fadhili Majiha alimsambalatisha Fransic Miyeyusho kwa point mpambano mwingine uliowakutanisha bondia chipkizi Vicent Mbilinyi aliyepambana na Epson John wa Morogoro mpambano uliomalizika kwa sale

wakati bondia Shedrack Ignas alimpiga bila ya huruma bondia Husein Mbonde kwa K,O ya raundi ya nne ya mpambano wao nae Saidi Mundi akimpiga kwa point bondia Ramadhani Shauri

aidha wadau wa mchezo wa ngumi waliofulika kuona mpambano huo wa kistoria wameomba kuwa mapambano hayo yanatakiwa kuanza mapema kuondoa hadha ya usumbufu wa usafili wakati wa kutoka na kwenda majumbani kwao kwani wapenzi wa mchezo wengi wa masumbwi wanategemea daladala kwa usafiri wa kurudi makwao ambapo ikifika zaidi ya saa sita daladala zinatoweka barabarani

IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' NA VICENT MBILINYI WALIVYOKONGA MOYO WA KOCHA WAO SUPER DBondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwa na Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Promota Jay Msangi 'Jiwe Gumu' kushoto baada ya bondia huyo kutwaa mkanda wa U.B.O Africa baada ya kumdunda Cosmas Cheka
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi akiwa na bondia Vicent Mbilinya wakati wa mpambano wake na Epson John
Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akipambana na Epson John mpambano uliomalizika kwa sale
Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akipambana na Epson John mpambano uliomalizika kwa sale


Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe

MAYWEATHER NA PAQUAIO WAKUTANISHWA KWA MARA YA KWANZA
LAS VEGAS, Marekani
TIKETI ya bei ya chini katika pambano la ngumi za kulipwa kati ya Floyd Mayweather pamoja na Manny Pacquiao zinapatikana kwa pauni 1,000 (sh mil 2.7.
 
Mabondia hao wanatarajia kupanda ulingoni Mei 2 mwaka huu katika Ukumbi wa GMG Las Vegas katika pambano linalosubiriwa kwa hamu na mashabiki na wapenzi wengi wa mchezo huo ulimwenguni.
Katika pambano hilo tiketi za kuzunguka katika ulingo zinatarajiwa kuuzwa kwa pauni 5,000 kwa tiketi sawa na sh. Milioni 13.5.
Pambano hilo ndilo linatarajiwa kuwa la ghali na la historia zaidi kuliko mapambano yoye yaliyopita.
Juzi mabondia hao walikutana kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa Habari juu ya pambano hilo.
Pacquiao alisema kuwa anashukuru Mungu kutokana na kufikia mpaka siku hiyo, ambapo anatarajia kuwapa raha mashabiki wake ambayo walikuwa wanaisubiri kwa kipindi cha miaka mitano sasa.
Mayweather alisema kuwa pambano hilo linatarajiwa kuwa la kipekee na ndio pambano bora zaidi kwake tofauti na mapambano 47 aliyowahi kucheza ambapo hana historia ya kupoteza hata moja.

KOCHA SUPER D AMZAWADIA BONDIA 'KING CLASS MAWE' VIFAA VYA MASUMBWI


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kumdunda bondia Cosmas Cheka na kunyakuwa ubingwa wa U.B.O Africa Class kwa sasa anamiliki mikanda miwili ya Africa ukiwemo wa WPBF na U.B.O Africa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kumdunda bondia Cosmas Cheka na kunyakuwa ubingwa wa U.B.O Africa Class kwa sasa anamiliki mikanda miwili ya Africa ukiwemo wa WPBF na U.B.O Africa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' baada ya kumdunda bondia Cosmas Cheka na kunyakuwa ubingwa wa U.B.O Africa Class kwa sasa anamiliki mikanda miwili ya Africa ukiwemo wa WPBF na U.B.O Africa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiangalia mkanda wa bingwa mpya wa U.B.O Africa Ibrahimu class 'King Class Mawe' aliopata hivi karibuni baada ya kumdunda bondia Cosmas Cheka Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiangalia mkanda wa bingwa mpya wa U.B.O Africa Ibrahimu class 'King Class Mawe' aliopata hivi karibuni baada ya kumdunda bondia Cosmas Cheka Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametimiza ahadi yake ya kumzawadia bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' endapo atanyakua ubingwa wa U.B.O kwa kumtwanga bondia Cosmas Cheka kwa point

ahadi hiyo ameitekeleza jana baada ya bondia huyo kumfata katika GYM ya Super D iliyopo karikoo Shule ya Uhuru Dar es salaam na kumkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi

akipokea vifaa hivyo bondia huyo ameaidi kuendelea na mazoezi ili afike juu zaidi kuliko ata mabondia waliotamba nchini bondia huyo anaemiliki mikanda miwili ya ubingwa wa Africa ikiwemo ya WPBF na U.B.O aliyouchukua hivi karibuni ametamba kumdunda bondia yoyote yule atakae jitokeza kutaka kutetea mikanda hiyo

nae kocha wa kimataifa wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D' ameseme kuwa kutoa ni moyo hivyo amewaomba wadau wengine kumpa sapoti ya aina mbalimbali kwa nguwa mchezo wa masumbwi auna wadhamini hivyo wadau wanatakiwa wachangie maendeleo ya mchezo wa masumbwi iwe kwa mtu mmojammoja au kampuni kwa ujumla

Super D ambaye ujishulisha na usambazaji wa vifaa mbalimbali vya masumbwi nchini amekuwa akiuza na kugawa msaada kwa vijana wanaochipukia kwa ajili ya kuhamasisha mchezo uho ambao umekosa wafadhili

Floyd Mayweather vs Manny Pacquiao

Floyd Mayweather vs Manny Pacquiao
 Pambano la ngumi linalosubiriwa kwa hamu
Bingwa kulamba Euro mil 160
 Pambano kupigwa Mei 2
LOS VEGAS, Marekani
MCHEZO wa ngumi ni kati ya michezo ambayo inapendwa sana ulimwenguni kutokana  na kuwa uhalisia kwa kiasi kikubwa.
Ni mchezo wa hatari ambao umeshawapa vilema vya baadhi ya viungo wachezaji wa mchezo huo kutokana na kutokuwa makini.
Kwa sasa pambano ambalo ndio limekuwa gumzo kwa mashabiki wa ngumi ulimwenguni, ni kati ya Floyd Mayweather, Jr dhidi ya Manny Paquiao.
Pambano hilo na uzito wa middle linatarajiwa kufanyika Mei 2 mwaka huu katika Ukumbi wa MGM Grand ndani ya Los Vegas.
Kwa kiasi kikubwa mashabiki wa mchezo wa ngumi wanalisubiria kwa hamu pambano hilo kutokana na rekodi zilizopo kati ya mabondia hao.
Ukiangalia kwa upande wa Mayweather ameshapigana mapambano 47 na kushinda yote na kati ya hayo 26 ameshinda kwa KO.
Kwa upande wa Paquiano, ameshacheza mapambano 64 na kushinda 57, K) 38 ambapo amepoteza matano na kutoa sare mawili.
Katika pambano la mwaka huu, lilianza kuadaliwa tangu mwezi Januari baada ya masupastaa hao kukutana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu Miami na kuamua kukaa pembeni kwa ajili ya kuongelea mpambano huo mkali.
Baadaye walikubaliana kwa kubalilishana namba za simu ambapo pia baadaye ilifahamika kuwa wamefikia muafaka.
Pamoja na kuwa walifikia muafaka lakini awali Mayweather hakuwa tayari kulizungumzia pambano hilo kutokana na kuamua kuweka siri, lakini baadaye ilibainika kuwa wameshainishana na kupanga siku ya pambano ambapo waliamua kuanza kuitangaza katika vyombo mbalimbali vya Habari.
Pambano hilo ambalo ndilo litakalokata ngebe za mabondia hao linatarajiwa kuhudhuriwa na umati wa mashabiki ambapo mpaka sasa tiketi zimeshaanza kuuzwa.
Pambano hilo limegubikwa na utata ambapo awali walikuwa wazipige mabondia hao lakini pambano liliahirishwa baada ya Pacquiao kukataa kupima matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu.
Hata hivyo kwa sasa Pacquiao ametamka mwenyewe kuwa anatarajia kumlipa faini ya pauni milioni 3.2 kwa Mayweather kama yeye atashindwa kufaulu katika kipimo hicho safari hii.
Mkataba waliongia kati ya mabondia hao ni pamoja na bingwa kuondoka na dau la Euro milioni 160.
Hata hivyo kwa sasa kumekuwa na tambo za hapa na pale kwa mabondia hao kwa kila mtu kudai kuwa atafanya vizuri, lakini cha msingi ni kusubiria Februari 2 kwa ajili kuona uhondo.