Tangazo

Pages

Saturday, March 14, 2015

MUDY MATUMLA NA MCHINA KUTABILI RUKSA


WAKATI homa ya pambano la ubingwa wa dunia wa WBF kati ya mabondia, Mohamed Matumla na Wang Xin Hua wa China ikipamba moto, wadhamini wa pambano hilo wametoa nafasi kwa mashabiki wa ndondi kubahatisha 'kubeti' mshindi.

WAKATI homa ya pambano la ubingwa wa dunia wa WBF kati ya mabondia, Mohamed Matumla na Wang Xin Hua wa China ikipamba moto, wadhamini wa pambano hilo wametoa nafasi kwa mashabiki wa ndondi kubahatisha 'kubeti' mshindi.

Pambano hilo la raundi 12 la uzani wa Bantam limepangwa kufanyika Machi 27 kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa pia na bingwa wa zamani wa dunia wa uzani wa juu, Francois Botha ambaye atakuwa mgeni rasmi.

Promota wa pambano hilo, Jay Msangi alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na pambano litasimamiwa na Shirikisho la ngumi la dunia la WBF ambaye rais wake atawasili nchini Machi 21.

Akizungumza jijini jana, Meneja Masoko wa Casino za Iplay 8, Le Grande na Palm beach, Ezekiel Lyal alisema wameamua kutoa nafasi ya bahati nasibu ya kushinda fedha'Kubeti' kwa mashabiki wa ndondi kwenye pambano hilo.

"Shabiki anachotakiwa ni kuingia kwenye tovuti ya www.iplay8casino.com ambapo kama ni mara ya kwanza atajisajili kwa kufuata maelekezo ambapo ni bure na atafungua akaunti ambapo ataanza kubeti na anaweza kufanya hivyo kwa wakala yoyote wa mtandao wa simu au benki na anaweza kuweka kiasi chochote cha fedha kuanzia elfu moja na kuendelea," alisema Lyal.

Mbali na pambano la Matumla, siku hiyo pia mabondia wenye upinzani, Mada Maugo na Japhet Kaseba na Karama Nyilawila na Thomas Mashali watazichapa mapambano ya kumaliza ubishi nani mkali kati yao huku bondia wa uzito wa juu kutoka Zanzibar akizichapa na bondia kutoka Marekani.

"Maandalizi yote yamekamilika na kuanzia wiki ijayo mabondia kutoka nje ya nchi na viongozi wa WBF sambamba na Botha wataanza kuwasili kwani tayari tiketi zao zimekamilika," alisema Msangi.
Mshindi wa pambano hilo, atashuhudia pambano la wakali hawa, Manny Pacquiao (kushoto) na Floyd Mayweather.
 

No comments:

Post a Comment