Tangazo

Pages

Tuesday, October 27, 2020

SUPER D AMNOWA VICENT MBILINYI KUMKABILI SHEDRACK IGNAS NOVEMBA 28 MASAKI


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimfundisha bondia Vicent Mbilinyi kupiga ngumi yenye mkunjo wa chini 'UPCAT' kwa ajili ya maandalizi yake na Shedrack Ignas litakalofanyika Novemba 28 katika ukumbi wa Nexrt Door Arena

 Na Mwandishi wetu


BONDIA Vicent Mbilinyi yupo katika maandalizi mazito sana katika kujiandaa kwake kwa mpambano wake na Shedrack Ignas utakaofanyika Novemba 28 katika ukumbi wa Nextri Door Arena Masaki Dar es salaam

akizungumza wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na pambano hilo Mbilinyi amesema kuwa yeye ngumi ni kazi yake hivyo anaiheshimu kwa kufanya mazoezi kwa bidii na wakati muhafaka kabisa kwani ndio moja na yaisha yake ya kila siku

alivyo ulizwa amejipangaje kumkabili bondia Shedrack Ignas ambaye ni mgumu pia ni nunda kwa uvumilivu wa ngumi hapa nchini

amesema ajakutana na ngumi kali hivyo ajipange kwa kipigo kitakatifu ambacho atampatia bila huruma yani hakika katika ngumi nimejifunza mambo mengi hususani nilivyokwenda safari za nje hivyo siwezi kukubali kupigwa kizembe na kwa uraisi hapa Tanzania

Nae kocha wake ambaye ni kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kwamba ana shaka na bondia wake huyo kwani yupo fiti na mtiifu wa mazoezi hivyo ushindi kwake kama kumsukuma mlevi kwani ngumi ni kipaji nae anacho hivyo anatumia kipaji 


Saturday, October 3, 2020

IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' NA SIMON NGOMA WATAMBULISHA MPAMBANO WAO WA NOVEMBA 27 PTA

Promota Ernest Evarast kutoka kampuni ya Mopao katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Simon Ngoma kutoka Zambia kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa Dunia wa GBC utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es salaam novemba 27

 Mabondia pamoja na makocha wao wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutambulisha mpambano wao wa novemba 27 katika ukumbi wa PTA Sabasaba  kulia bondia Simon Ngoma kocha wake Antoni Mwaba Kocha wa wa kimataifa wa mchezo wa ngumi Tanzania Rajabu Mhamila 'Super D' Bondia Ibrahimu Class King Class Mawe Dkt Hadija Hamisi Promota  Everist Ernes na Ubwa SalumuNA MWANDISHI WETU

BONDIA Ibrahimu class 'King Class Mawe' amekutanishwa uso kwa uso na mpinzani wake Simon Ngoma kutoka Zambia ambaye alikuja kusaini mkataba wa kuzipiga Novemba 27 katika ukumbi wa PTA Sabasaba

akizungumzia mpambano huo Class amesema kuwa yeye yupo fit ata kwa sasaivi kwa kuwa moto wake bado aujazimika unajua hivi karibuni nimetoka kucheza mchezo na Nassibu Ramadhani na nikafanikiwa kumtwanga bila huruma hivyo na huyu nampiga kama bag naomba watanzania wani sapoti kwa hali na mali na sito wahangusha

ata hivyo naomba wadhamini wajitokeze kwa wingi kwani kwa sasa mchezo wa ngumi unaonekana live katika Luninga na umekuwa kwa kira hidara hivyo wadhamini mjitokeze kupromoti mpambano wa masumbwi nchini usonge mbele

nae Simoni Ngoma kutoka Zambia amesema kuwa kati ya Tanzania na Zambia ni ndugu hila kwa hili udugu utakaa pembeni na nitamtwanga bila huruma Class

nae promota wa mpambano huo Evarist Elnest aliongeza kwa kusema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine yenye upinzani zaidi ya hiro ambapo bondia Said Chino atapambana na Haidari Mchanjo na Abdi Kivu atapigana na Maisha Samsoni

ameomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili waujaze ukumbi pia ameomba wadhamini wajitokeze kwa wingi kwani nafasi zipo kwa ajili ya udhamini na mpambano bodo tuna utangaza  nae kocha wa bondia Class Kocha wa Kimataifa  Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa sasa class yupo vizuri na tunaitaji kumbadilisha kidogo katika upiganaji wake ili arete furaha kwa nchi ya Tanzania unajua amebeba watanzania wote watakuwa wanamuangalia Dunia nzima kwa njia mbalimbali hivyo tunategemea ushindi wa mapema alisema Super D