Tangazo

Pages

Thursday, November 29, 2012

BOB CHORA AMNG'ARISHA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE'

Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake unaokuja zidi ya bondia Saidi Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake wa DESEMBA 9
MOJA YA BANGO LILILOCHOLWA NA BOB CHORA
Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake unaokuja zidi ya bondia Saidi Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Msanii wa Sanaa ya Uchoraji Jeremia Makimata 'Bob Chora' akichora moja ya bango la kumuhamasisha bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya mpambano wake unaokuja zidi ya bondia Saidi Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba jijini Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, November 27, 2012

SUPER D APANIA KUPELEKA VIJANA WAKE OLIMPIKI 2016


Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiwa katika picha ya pamoja na vijana waliojitokeza katika mazoezi ya ngumi ufukwe wa GYKHANA Dar es salaam jana Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


KLABU ya ngumi ya Ashanti Ilala imeota kuwa moja ya klabu itakayotoa wawakilishi katika michezo ya Olimpiki itakayofanyika mwaka 2016  nchini Brazil.

Klabu hiyo ambayo kwa sasa inaundwa na chipkizi 18 pamoja na mabondia wakongwe imepania kufanya hivyo huku ikijitapa kuwa itaanza kufanya maajabu kupitia mashindano ya taifa ya mchezo huo yatakayofanyika Januari mwakani.

Akizungumza na gaazeti hili Dar es Salaam jana, Kocha wa ngumi wa klabu ya Ashanti  pamoja na timu ya Mkoa wa Ilala Kimichezo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kwa sasa klabu yake imejikita katika maandalizi kabambe kuhakikisha inaingiza mabondia wengi katika timu ya taifa ambao baadaye wataingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi za kufuzu kucheza Olimpiki.


Alisema tayari jumla ya vijana 18 wanajifua katika Ufukwe wa Gymkhana Dar es Salaam kwa ajili ya mapambano mbalimbali ikiwemo ya ubingwa wa taifa ambayo yanaandaliwa na Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT).


Alisema vijana wengi waliopo kwenye klabu hiyo ni wenye umri chini ya miaka 12 na chini ya miaka 20 ambapo amewataja kuwa umri huo ni mzuri kwani kijana atakuwa mwepesi wa kuelewa kile ambacho atakuwa anafundishwa na makocha wake
Super D ambaye anafundisha kwa kutumia mbinu mbalimbali zikiwemo kwa njia ya DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.
Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani
Super D ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi

BONDIA TYSON FURY KUMVAA WLADIMIR KLITSCHKO MWAKANILONDON, England
“Nimezungumza mara kadhaa na kocha wa Wladimir, Bernd Boente kuhusu pambano hilo na Tyson yu tayari sasa kwa hilo. Ni mpambano ambao unaweza kuwa katika uwanja wa soka katika kipindi cha kuanzia Mei, Juni au Julai
BONDIA mahiri Tyson Fury amepania kupanda ulingoni kupimana ubavu na Wladimir Klitschko kuwanuia ubingwa wa dunia kiangazi kijacho.
Fury, 24, bondia asiyepigika katika uzani wa ‘heavyweight,’ Jumamosi hii anapanda ulingoni kumvaa Mmarekani Kevin Johnson jijini Belfast, Ireland ya Kaskazini.
Na promota wa pambano la Jumamosi Mick Hennessy amedai kuwa, ushindi kwa Fury mwenye urefu wa futi 6.9, utampa fursa ya kuandaliwa pambano dhidi ya Klitschko - bingwa wa mikanda ya WBA, IBF, na WBO.
Hennessy alisema: “Nimezungumza mara kadhaa na kocha wa Wladimir, Bernd Boente kuhusu pambano hilo na Tyson yu tayari sasa kwa hilo.
“Ni mpambano ambao unaweza kuwa katika uwanja wa soka katika kipindi cha kuanzia Mei, Juni au Julai.
“Ujerumani ni nchi inayoweza kuwa kipaumbele chetu kupigwa pambano hilo, lakini nimeshazungumza na wamiliki wa Uwanja wa Old Trafford au Croke Park,” alisema Hennessy.

TIKETI ZA VIP SASA ZINAPATIKANA

Promota  wa mchezo wa masumbwi Mohamed Bawazir katikati akiwainua mikono juu bondia Fransic Miyayusho kushoto na Nassibu Ramadhani wakati wa kutambulisha mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba siku ya DECEMBER 9, 2012. Tiketi za VIP za mpambano huo kwa sasa zipo tayali kwa maitaji ya kuwai kununua mapema kabla azijaisha wasiliana na Promota kupitia namba  0715 666686 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam  Tiketi za VIP za mpambano huo kwa sasa zipo tayali kwa maitaji ya kuwai kununua mapema kabla azijaisha wasiliana na Promota kupitia namba  0715 666686   Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mwandaji wa mpambano wa ubingwa wa WBF Mohamed Bawazir katikati akiwa ameshika mkanda na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Fransic Miyayusho kulia wengine kulia ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa ambao na wasimamizi wa mpambano huo na Kushoto ni Mratibu Paul Kunanga na Kocha wa Nasibu Christopher Mzazi

Mabondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho wakitunishiana misuri wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa WBF utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MICHAEL YOMBAYOMBA KUPAMBANA NA SAID OMAR 'GOGO POA' KUCHANGIA WAGOJWA WA MOYO

 Saidi Omari 'Gogo Poa' .kushoto na Rajabu Mhamila'Super D' 
MABONDIA wazamani walioiletea nchi Medali katika mashindano ya All Africa Games na Jumuiya ya Madola miaka ya 1998, Michael Yombayomba na Said Omari 'Gogo Poa' wamejitolea kupanda ulingoni na kutwangana kwa ajili ya kuchangia watoto wenye matatizo ya Moyo.

Yombayomba ambaye alitwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya Jumuia ya Madola katika miaka hiyo ya 1998 na Gogo Poa wameamua kutwangana ikiwa ni sehemu ya mchango wao kwa watoto hao huku wakisisitiza wadau kuunga mkono tukio hilo.


Akizungumza na gaazeti hili Gogo Poa alisema pambano hilo litafanyika Januari 25 mwakani ambapo pia litasindikizwa na mapambano ya mabondia mbalimbali wenye viwango vya juu nchini.


"Tumeguswa sana na tatizo hili la watoto wanaougua ugonjwa wa moyo ambao wengi wao hukosa fedha kwa ajili ya matibabu hivyo sisi kama sehemu ya jamii tutahamasisha uchagiaji wa fedha kwa kujitolea kupanda ulingoni na chochote kitakachopatikana itakuwa ni sehemu ya mchango wetu,"alisema Gogo Poa.

Aliwaomba wadhamini na wadau mbalimbali kujitokeza kuzamini mchezo huo ambao una tija ya kuchangia watoto hawo kwani ata wao walikuwa watoto ndio mana wamekuwa katika afya nzuri na kucheza mchezo huo na kuiletea sifa taifa hili kwa kuleta Medali

Hivyo na watoto hawo wanatakiwa wawe na AFya njema ili wapate kuja kurithi nyayo zetu bila afya ya mtoto michezo yote akuna kwa kuwa vipaji vingi vinangaliwa ukiwa mtoto

Monday, November 26, 2012

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TPBC TAREHE 12 JANUARI, 2013

                                                                                   WANACHAMA,
                                                                   TANZANIA PROFESSIONAL BOXING COMMISSION,
                                                                    S. L. POSTA 6058,
                                                                    DAR ES SALAAM.
 
Kumb. Na: CP/MO/3                                                 24 Novemba, 2012
 
Msajili wa Vyama,
Wizara ya Mambo ya Ndani,
S. L. Posta 9223,
DAR ES SALAAM.
 
Ndugu,
 
YAH: TAARIFA YA KUFANYA MKUTANO TAREHE 12 JANUARI, 2013.
 
Rejea barua yako Kumb. Na: S.O. 6446/17 ya 23 Agosti, 2011 iliyotujibu kuhusu mwongozo wa kukufufua chama chetu, kwa kutufahamisha kuwa ombi hilo haliwezi kushughulikiwa kabla haijalipwa ada ya usajili na adhabu ya kutolipa kwa miaka ya fedha 1998 mpaka 2012. Aidha rejea pia barua yako Kumb. Na: S.O. 6446/20 ya
13 Septemba, 2011 iliyosisitiza barua yako Kumb. Na: S.O. 6446/17 ya 23 Agosti, 2011.
 
Malipo yamekwisha kufanywa na wanachama hivyo tumepanga kufanya mkutano tarehe 12 Januari, 2013 wa kuhakiki wanachama na kufanya uchaguzi wa viongozi wa muda:
 
[1] UONGOZI WA CHAMA:
 
       Chama hakijawahi kufanya uchaguzi wowote ule kikiwa hai au kimekufa    
       tangu mwaka 1998 kilipowachagua viongozi :
            [a] Emmanuel Salehe       – Rais wa chama
            [b] Onesmo Ngowi           - Makamu wa rais wa chama
            [c] Fidel Haynes                 - Katibu Mkuu
            [d] Titus Kadyanji              - Mweka Hazina
            [e] Habibu Kinyogoli        - Mjumbe
            [f] Bakari seleman                        -  Mjumbe
 
        Tarehe 12/01/2000 mkutano mkuu wa chama ulimthibitisha Onesmo Ngowi
        kama rais wa chama.    
 
        Viongozi wote aliochaguliwa 1998 wapo hai kasoro Bakari Selemani ambaye
   ni marehemu lakini hawajishughulishi na maswala ya chama. Badala yake
   Onesmo Ngowi amekuwa akitoa madaraka anavyotaka yeye hata kwa watu
   ambao hawana sifa ya kuwa wanachama. Chama hiki ni cha mabondia.
 
[2] OFISI YA CHAMA
      Chama hakina ofisi wala mahali maalum pa kukutania.
 
      Mabondia wapokuwa na shida huambiwa na Onesmo  
      Ngowi kuwa wakamtafute Boniface Wambura ambaye kama mwandishi wa  
      habari hana sifa za kuwa mwanachama.
 
[3] MIKUTANO YA CHAMA:
 
      Mkutano Mkuu wa mwisho wa chama ulifanyika mwaka 2001 ambao
      ulizungumzia mabadiliko ya katiba ambayo ilitaka kuwaondolea mabondia
      uwanachama.
      Kwa pamoja walipinga hili kwa kuwa hiki ni chama kilichosajiliwa na mabondia
      kwa ajilia ya mabondia na wala siyo kampuni ya mtu.
 
[4] MAPATO NA MATUMIZI:
 
Taarifa ya mwisho ya mapato na matumizi ililetewa kwa wanachama tarehe
31 Desemba, 2000. ( AMBATANISHO NA: 1 )
 
Lakini katika miaka yote hii 12 mabondia wamekuwa wakikatwa asilimia kumi
( 10%) ya malipo yao kila waposhindana nje ya nchi aidha mapromota wamekuwa wakilipia vibali vya kuandaa mapambano.
 
[5] WANACHAMA:
 
       Chama tulikianzisha kwa ajili ya mabondia mwaka 1984 na orodha ya
       wanachama mpaka mwaka 1998 ambayo ndiyo iliyofanya uchaguzi wa 
       mwisho ( AMBATANISHO NA:2 )
 
[6] DHANA YA KUITISHA MKUTANO
Wanachama tuliona kuwa sababu ya malimbikizo ya ada ya usajili ni kuwa hakukuwa na mtu wa kuwajibika kuhusu hili. Ndio maana tukalipia.
 
     Aidha kukosekana kwa [a]  ofisi [b] takwimu ya  mapato na matumizi [c]
     orodha ya wanachama na [ d] viongozi wa chama wa kuwajibishwa.
 
Hivyo basi iwapo una pingamizi kuhusu mkutano huu basi tunaomba mwongozo wako.
 
Wako mtiifu,
 
_______________                                              __________________
Chaurembo Palasa                                              Agapeter Mnazareth
MWENYEKITI WA MKUTANO                           MJUMBE
 
Nakala kwa: [1] Vyombo vya Habari