Tangazo

Pages

Sunday, September 30, 2012

CHEKA AENDEREZA UBABE KWA KARAMABINGWA wa ngumi za kulipwa anayetambuliwa na vyama vya ICB, IBF na WBC, Francis Cheka 'SMG' usiku wa kuamkia leo amedhihirisha kwamba hana mpinzani katika ngumi hizo nchini baada ya kumchapa kwa KO mpinzani wake mkubwa, Karama Nyilawila na kuongeza taji jingine.
Cheka alimpiga Nyilawila katika raundi ya sita ya pam,bano hilo lililokuwa la uzani wa Super
BINGWA wa ngumi za kulipwa anayetambuliwa na vyama vya ICB, IBF na WBC, Francis Cheka 'SMG' usiku wa kuamkia leo amedhihirisha kwamba hana mpinzani katika ngumi hizo nchini baada ya kumchapa kwa KO mpinzani wake mkubwa, Karama Nyilawila na kuongeza taji jingine.
Cheka alimpiga Nyilawila katika raundi ya sita ya pam,bano hilo lililokuwa la uzani wa Super Middle la raundi 12 lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA, Temeke jijini Dar es Salaam na kutwaa ubingwa wa Mabara wa UBO uliokuwa wazi.
Pambano hilo lililohudhuriwa na mashabiki lukuki, lilishuhudia raundi zote tano za kwanza Nyilawila akionyesha kumdhibiti Cheka kwa kumchezea 'kibabe' akitumia nguvu nyingi kujihami na baadhi ya watu ukumbini kuamini mwisho wa tambo za Cheka zilikuwa zimewadia.
Hata hivyo raudni ya sita ilipoanza Cheka alionyesha amebadilika na hasa baada ya kocha wake Abdallahj Saleh 'Komando' kupanda ulingoni na kuzungumza na bondia huyo na kumshushia kipigo Nyilawila, ambapo moja ya makonde matatu ya mfululizo yalimpeleka chini mpinzani wake.
Mwamuzi wa pambano hilo, Jerome Waluza alimhesabia Nyilawila ambaye alijitahidi kuinuka, lakini ghafla akaonyesha ishara kwamba asingeweza kuendelea na pambano hilo na ukumbi mzima kuripuka kwa shangwe akishangiliwa Cheka ambaye hiyo ni mara ya pili kumpiga Nyilawila.
Kabla ya pambano hilo lililoanza majira ya saa 3;40 usiku, kulikuwa na mapambano saba ya utangulizi pamoja na burudani ya muziki toka bendi ya Mashujaa ambao hata hivyo sio wapenzi wengi walioweza kuishuhudia kutokana na kuondoka ukumbini mapema.
Katika pambano la kwanza la utangulizi Said Mbelwa alimpiga kwa pointi Dickson Mwakipesile, Juma Kihiyo alipigwa kwa pointi na Ibrahim Mahokola katika pambano lililovutia kwa namna mabondia hao walivyoonyeshana kazi.
Pia mdogo wa Cheka, Cosmas Cheka alifanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi dhidi ya Fadhil Awadh katika pamnbano jingine lililosisimua wengi kwa ufundi uliokuwa ukionyesha na mabondia hao, naye Shaaban Kilumbelumbe alimpiga kwa pointi Anthony Mathias kabla ya Safari Mbiyu kumpiga kwa KO ya raundi ya kwanza Khalfan Jumanne.
Michezo minginme iliwakutanisha Stan Kessy na Seba Temba, pambano lililoisha kwa mabondia hao kutoka sare na Hassani Kidebe alitolewa nishai na Deo Samwel kwa kupigwa kwa pointi.
Mgeni rasmi katika pambano hilo alikuwa Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam ambaye aliutangazia umma kwamba kama Mlezi wa Ngumi za Kulipwa amefanikiwa kuwafuta wafadhili katika mchezo huo na kumtambulisha raia mmoja wa kigeni kwamba ni miongoni mwao.
Middle la raundi 12 lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA, Temeke jijini Dar es Salaam na kutwaa ubingwa wa Mabara wa UBO uliokuwa wazi.

Saturday, September 29, 2012

CHEKA AENDELEA KUWA MBABE KWA MABONDIA WATANZANIA

CHEKA AMGALAGAZA KARAMA RAUNDI YA SITA

Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Refarii wa mpambano akiwaelekeza mabondia wasicheze kwa kukumbatiana

Bondia Fransic Cheka kushoto akipepesuka baada ya kupigwa ngumi na Karama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K.O raundi ya sita na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Fransic Cheka kushoto akimshambulia Karama Nyilawila kwa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi Cheka alishinda raundi ya sita baada ya kumpiga na kudondoka chini baada ya kuesabiwa akashindwa kuendelea picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Karama Nyilawila  kulia akijitaidi kukwepa makonde ya mpinzani wake Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Karama Nyilawila kushoto akionesheana umwamba wa kutupa masumbwi na Fransic Cheka wakati wa mpambano wao cheka alishinda kwa K,O Raundi ya sitapicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Fransic Cheka kushoto na Karama Nyilawila wakiwa uringoni kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi Cheka alishjnda kwa K,O ya Raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Fransic Cheka wakionesheana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MTANZANIA KUPIGANA URUSI

                    TAARIFA KWA VYMBO VYA  HABARI -MICHEZO.

BONDA WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA CHUPAKI CHIPINDI KUTOKA IRINGA ,
TAREHE 13-10-2012 ATAPANDA ULINGONI NCHINI URUSI KUZIPIGA NA BONDIA- RODION PASTUKH,WA URUSI KATIKA UZITO WA CRUISERWEIGHT ,PAMBANO LA RAUNDI 12.

TAYARI ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO],TUMESHAPOKEA BARUA ZA KUMUALIKA BONDIA CHUPAKI CHIPINDI KUTOKA  SHIRIKISHO LA NGUMI LA URUSI [RUSSIA FEDERATION OF PROFESSIONAL BOXING ].

CHUPAKI CHIPINDI ANATARAJIWA KUONDAKA NCHINI TANZANIA TAREHE 04-10-2012 KUELEKEA JIJINI NAIROBI [KENYA] KWENDA KUUNGANA NA WAKALA WAKE NDG THOMAS MUTUA TAYARI KWA SAFARI YA KELEKEA RUSSIA. HAPO TAREHE 07-10-2012

TPBO INAMTAKIA KILA LA HERI BONDIA CHUPAKI CHIPINDI KTK SAFARI YAKE NA AKAJIWAKILISHE VIZURI KWENYE BIASHARA YAKE YA MASUMBWI ILI AWEZE KUPATIWA MAPAMBANO ZAIDI NJE YA TANZANIA.

IMELETWA KWENU NAMI;-

YASSIN ABDALLAH -USTAADH

RAIS -TPBO

CHEKA AMGALAGAZA KARAMA RAUNDI YA SITA

Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Refarii wa mpambano akiwaelekeza mabondia wasicheze kwa kukumbatiana

Bondia Fransic Cheka kushoto akipepesuka baada ya kupigwa ngumi na Karama Nyilawila wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K.O raundi ya sita na kufanikiwa kunyakuwa ubingwa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Fransic Cheka kushoto akimshambulia Karama Nyilawila kwa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi Cheka alishinda raundi ya sita baada ya kumpiga na kudondoka chini baada ya kuesabiwa akashindwa kuendelea picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Karama Nyilawila  kulia akijitaidi kukwepa makonde ya mpinzani wake Fransic Cheka wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Karama Nyilawila kushoto akionesheana umwamba wa kutupa masumbwi na Fransic Cheka wakati wa mpambano wao cheka alishinda kwa K,O Raundi ya sitapicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Fransic Cheka kushoto na Karama Nyilawila wakiwa uringoni kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi Cheka alishjnda kwa K,O ya Raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Karama Nyilawila kushoto na Fransic Cheka wakionesheana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa jumamosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Cheka alishinda kwa K,o raundi ya sita picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Fransic Cheka akinyooshwa mkono juu na mmoja wa mashabiki wa Kigeni waliokuja kuangalia mpambano wake dhidi ya Karama Nyilawila Cheka alishinda katika raundi ya sita baada ya karama kusalimu amri kushoto ni Rais wa PST Emanuel Mlundwa na wa pili kulia ni mgeni rasmi Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es salaam Suleiman Kova.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, September 28, 2012

CHEKA VS KALAMA WAPIMA UZITO LEO

Bondia Fransic Cheka akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba na Kalama Nyilawila siku ya jumamosi .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Kalama Nyilawila akipima vipimo mbalimbali wakati wa kupima uzito leo
Bondia Kalama Nyilawila akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Fransic Cheka utakaofanyika siku ya jumamosi hii

KALAMA NYILAWILA FRANSIC CHEKA USO KWA USO JUMAMOSI HII

MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na aliyekuwa bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni Jumamosi mwaka huu kuoneshana umwamba.
Cheka na Nyilawila walitwangana mbambanmo wao uliofanyika morogoro ata hivyo ulizua utata baada ya mpambano wao kugubikwa na alama za mshangao ambalo cheka aliibuka na ushindi wa point  mashabiki kuhisika wa mabondia hao wanaogopana na kutafutana kwa mda mrefu watapoza kiu yao kwa mpambano huo jumamosi ya kesho.

Akizungumza Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo Oswald Mlay alisema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa PTA Sabasaba
.
Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 12 uzito wa kg 72 ambapo leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano uho utakaoamua nani zaidi

Katika Mchezo huo kutakua na Uhuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Tuesday, September 25, 2012

SEHEMU YA KWANZA YA HISTORIA YA NGUMI ITAKAYOKUWA INALETWA KWENU KILA WIKI

MCHEZO WA MASUMBWI, TAA INAYOZIZIMA

UNAPENDWA NA KUOGOPWA NA WATU WENGI DUNIANI

UKO HATARINI KUPOTEZA ASILI YAKE KABISA
 
Na Onesmo NgowiMasumbiwi au kwa majina mwengine ndondi au ngumi na kwa majina ya mitaani ndogwa, mawe n.k. ni mchezo unapoendwa sana na watu wengi. Aidha mchezo huu ni kati ya michezo inayoogopwa sana duniani. Mchezo wa ngumi uko hatarini kupoteza maana yake ya asili yaani kucheza kama burudani, kuwakilisha nchi na kujenga ushupavu wa mchezaji. Mamilioni ya watu wanaojazana kuutazama wasingependa kabisa kujiingiza kuucheza mchezo wa ngumi.

Japokuwa katika maisha ya kawaida watu wengi hupigana kwa sababu mbalimbali kama vile kuwa na hasira, kujilinda au kuwaonea tu wengine kwa sababu mbalimbali lakini kwa kawaida ni watu wachache sana walio tayari kujiingiza katika kuucheza mchezo huu.

Kama tulivyokwisha ona kwenye makala zilizotangulia, ngumi ni mchezo ambao ulianza wakati wanadamu walipoanza tu kukunja ngumi na kurushina kama mchezo. Mchezo wa ngumi upo wa aina mbalimbali.

Japokuwa kumbukumbu nyingi zinaonyesha kwamba chimbuko haswa la mchezo huu linakubalika kuwa ni nchi za kusini mwa Ulaya hususan Uyunani (leo Ugiriki) na Urumi (Italia ya leo) lakini kuna mataifa au dola nyingine nyingi zilizokuwa na aina yao ya michezo iliyofanana na ngumi.  Wanazuoni wa maswala ya michezo wanaifananisha michezo yote ya kupigana iwe ni kwa kutumia mikono na miguu au kutumia silaha za aina mbalimbali na mchezo wa ngumi.

Aidha mchezo wa ngumi ni kati ya michezo inayojenga ushupavu wa wachezaji na kuwafanya washujaa wa jamii. Wachezaji wa ngumi mara nyingi ni watu wanaoonekana kama mashujaa kutokana na ujasiri wanaoonyesha katika mchezo wenyewe. 

Wakati wa utawala wa Marcus Aurelius, mtawala shupavu wa iliyokuwa dola ya Roma (Italia ya leo) na aliyepata mafanikio makubwa ya kuipanua dola ya Warumi (Italia) toka ukanda wa bahari ya Mediterania hadi jangwa la barafu la Siberia huko Urusi, mashujaa wengi wa michezo walichuana kwenye mashindano yaliyofanyika Coliseum (uwanja mkubwa uliokuwa umejengwa katika jiji la Roma). 

Mashujaa hawa ni pamoja na wapiganaji ngumi na wengine walioshiriki kwenye michezo yenye hatari na kujijengea umaarufu mkubwa kwenye jamii ya Warumi. Dola ya Warumi ilikuwa na nguvu sana katika bara la Ulaya na ilienea hadi kaskazini mwa bara la Afrika. Hivyo utamaduni wao hususan michezo iliyochezwa baada ya ushindi wa vita ulienea kwenye himaya yao yote.

Kwa mfano katika dola ya Manchuria (China ya leo) iliyotawala kutoka Uchina na nchi nyingi za mashariki ya kusini mwa Asia ngumi zilijulikana kama Kung-Fu ambazo japokuwa kuchezwa kwa ngumi hizi huchanganywa na mateke.

Maaskari wengi walitakiwa wawe wamejifunza kupigana Kung Fu na waujue mchezo wenyewe kwa kiwango kikubwa. Kwao Kung Fu ilikuwa ni aina nyingine ya silaha na walizitumia ipasavyo kwenye kukabiliana na maadui kwenye vita.  Baada ya ushindi wa vita walikusanyika katika viwanja vikubwa na kucheza michezo hii kama isahara ya kusheherekea ushindi wao.

Dola ya Kijapani iliyotawala nchi nyingi za Asia ikiwa ni mpinzani mkubwa wa dola ya Manchuria katika karne ya 12 nayo ilikuwa na mchezo wa ngumi uliojulikana kama Karate. Mashujaa wengi wa Kijapani walitakiwa wawe na ujasiri wa hali ya juu wa kupigana Karate.

Kwao Karate ilikuwa sio mchezo tu bali ni ufundi wa kumshinda adui kwenye vita. Ushindani mkubwa kati ya Wachina na Wajapani uliifanya michezo ya Karate na Kung Fu kupata umaarufu mkubwa sana. Kila upande uliuona mchezo wake kama bora kuliko mwingine.

Katika miaka ya karibuni watawa wengi katika ukanda huu wanaojulikana kama Monks (monki) waiijifunza Karate na Kung Fu kwa kiwango cha juu ili kujilinda na Maharamia waliokuwa wanawavamia na kuiba mali zao.

Mtawala Genghis Khan wa dola ya Mongolia (Mongol Empire) ambayo ilitawala kuanzia Mongolia yenyewe hadi Persia (Irani), Babilon (Iraki) na baadhi ya nchi za Balkan (Ulaya ya Kati) aliwachagua wapiganaji wake kwa ustadi na uangalifu mkubwa. Kwa kutumia wapiganaji waliosheheni kila aina ya ushupavu aliweza kushinda majeshi mengi na kuwa kati ya watawala walioogopewa sana wakati wa enzi yake.

            Dola ya Otoman ya Kituruki iliyotawala katika karne ya 19 ilitumia mchezo ulioulikana sana na wengi kama Mieleka ukichanganya na utumiaji wa farasi. Mara nyingi wachezaji wa mchezo huu walifariki kutokana na ugumu wa mchezo wenyewe na watanzamaji walisisimka sana kuona damu ikimwagika. Kwao huu ulikuwa ndio ushujaa tosha.

Nazo dola za Mafarao wa Misri zilikuwa na aina yao ya michezo iliochezwa haswa na watumwa kwa minajili ya kuwafurahisha Mafarao na familia zao hata katika kujitetea au kushambulia maaduni! Kwa dhati kabisa mchezo wa ngumi ulivyojulikana na Wanafalsafa wa zamani katika ukanda wa Mediterania katika dola nilizotaja hapo juu ulikuwa ni mojawapo ya vipimo vya ujasiri wa mtu.

            Sio vibaya watanzania wakaelewa kuwa ngumi ni mchezo wa zamani sana kuchezwa hata kabla nchi yetu haijatawaliwa na wakoloni katika karne ya 19. Michezo hii iliyochezwa katika viwanja vikubwa vyenye mikusanyiko mikubwa ya watu (Coliseum) huko Roma na (Arena) huko Athina, iliyokuwa katika hekalu kubwa la ufalme wa Wayunani (Ugiriki) la Akropolis.

Viwanja hivi vilikuwa ndio mwanzo wa ulingo wa kisasa kwani japokuwa ulingo wa kisasa ni wa mraba lakini mwanzo wake ni Arena ya mduara.
Mwandishi wa makala haya ni: Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Shirkisho la Ngumi za Kulipwa Afrika Mashariki na Kati (ECAPBF), Shirikisho la Ngumi la Kimataifa bara la Afrika (IBF/AFRICA) na Mkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC). E-mail: ibfafrica@yahoo.cm
                              
BFT NA TPBC KUUNDA KAMATI YA KUFUFUA NA KUENDELEZA MASUMBWI TANZANIARais wa TPBC, Onesmo Ngowi
Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC} zimekubaliana kuunda Kamati ya watu kumi (lO) ili kufufua na kuundeleza mchezo wa ngumi Tanzania.
Kamati hiyo ambayo itajumuisha wajumbe watano (5) kutoka BFT na watano (5) kutoka TPBC itakuwa chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais wa TPBC, Godfrey Madaraka Nyerere, ambayo itajulikana kwa jina la 'Kamati ya Nyerere ya Kufufua nKuendeleza Ngumi Nchini'
'Kamati ya Nyerere ya Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini'  itafanya kazi ya kuandika hadidu rejea za rasimu ya makubaliano ya pande zote mbili ili ziweze kutumika kama mwongozo wa makubaliano hayo.
Ushirikiano kati ya BFT na TPBC utaratibiwa na Katibu Mkuu wa BFT  Makore Mashaga pamoja na Katibu Mkuu wa TPBC Nemes Kavishe
Wawili hawa watakuwa ndio wakuu wa Sekretariet ya 'Kamati ya Nyerere ya Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini', ambacho ndicho chombo cha kusimamia na kuratibu makubaliano haya.
Ushirikiano kati ya vyama hivi viwili ambavyo kimoja kipo kwenye ngumi za ridhaa na kingine kipo kwenye ngumi za kulipwa ni ushirikiano unaolenga kubadili mwelekeo wa mchezo wa ngumTanzania.
Kwa muda mrefu sasa mchezo wa ngumi umekuwa ukikumbwa na matatizo mbalimbali ambayo yamepelekea kutokuwepo na maendeleo yanayotegemewa na wadau wa ngumi Tanzania.
Ushirikiano wa vyombo vyote vinavyoratibu ngumi nchini Tanzania utakuwa ni msingi imara wa kujenga ari ya maendeleo ya ngumi kwa Tanzania.
Tanzania imekuwa ikivurunda kwenye mashindano ya kimataifa karibu kila michezo ya kimataifa na hivyo ushirikiano wa vyombo hivi viwili vya ngumi utakuwa ndio msingi imara wa kuendeleza na kuondoa aibu hiyo ya muda mrefu ya mchezo huo Tanzania .

Monday, September 24, 2012

MOBONDIA WA KULIPWA WANAVYOPOTOSHWA.NA VIONGOZI

NDG WAANDISHI  WA HABARI- MICHEZO

NI MASIKITIKO YANGU MAKUBWA SANA NINAPOONA JINSI BAADHI YA VIONGOZI WENZANGU WA NGUMI ZA KULIPWA [ SIYO ONESMO NGOWI ] JINSI WANAVYO WAPOTOSHA BAADHI YA MABONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA ,KIASI CHA KUWAFANYA WAJENGE TABIA ZA KUDHARAU MABONDI WENZAO.

MNAMO MWEZI WA SABA MWAKA HUU 2012 WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA WALIINGIZWA KTK MGOGORO MKUBWA WA MAWAZO PALE LILIPOTANGAZWA PAMBANO KATI YA BONDIA FRANCIS CHEKA NA JAPHET KASEBA,

KATIKA HALI YA KUUSHANGAZA ULIMWENGU WA MASUMBWI NA WAPENZI WAKE KUINGIA KTK FADHAA KUBWA  ,BAADA YA KUMUONA BONDIA FRANCIS CHEKA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI AKIPIMA UZITO NA AFYA KWA AJILI YA PAMBANO LAKE LA TAREHE 07-07-2012 PALE UWANJA WA TAIFA NA KISHA KUGOMEA KUPAMBANA KWA KIGEZO AMBACHO HAKINA NAFASI KATIKA TARATIBU ZA NGUMI ZA KULIPWA.

KTK MAELEZO YAKE CHEKA ANADAI NA BADO ANAENDELEA KUMPONDA KASEBA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI[BAADHI]KWAMBA KASEBA NI KIBONDE NA ANA POINT 13 TU NA YEYE AKIWA NA POINTS 90. KWA KWELI UTARATIBU WA KUDHARAULIANA WAKATI HAKUNA PAMBANO LINALOWAHUSU ,HAUPO- NA  INARUHUSIWA TU WAKATI WA KUTANGAZA PAMBANO LINALOWAHUSU MABONDIA HUSIKA NA,BAADA YA PAMBANO KWISHA UHUSIANO MWEMA UNADUMISHWA NA KUENDELEA KAMA KAWAIDA.

NDG WAANDISHI KWANZA NI LAZIMA MJUWE KWAMBA KUPANDA KTK UBORA WA VIWANGO KWA BONDIA WA NGUMI ZA KULIPWA ,NI BUDI BONDIA AMBAYE REKODI YAKE NI NDOGO APATE NAFASI YA KUPAMBANA NA BONDIA MWENYE REKODI BORA.ILI AONYESHE UWEZO WAKE

NA IWAPO BONDIA MWENYE REKODI NDOGO ATABAHATIKA KUMSHINDA BONDIA MWENYE REKODI BORA ,BASI HUYU BONDIA MWENYE REKODI NDOGO ATAPANDISHWA KWENYE VIWANGO ,NA POINTS ZAKE ZITAPANDA VILEVILE KUWA NYINGI,  NA POINT ZA HUYU BONDIA MWENYE REKODI BORA ATASHUSHWA KTK VIWANGO NA POINT PIA.

NA IWAPO BONDIA MWENYE REKODI BORA NA PONT NYINGI AKISHINDA YEYE HAONGEZEWI KITU BALI ATABAKI NA POINT ZAKE ALIZOKUWA NAZO NA ATABAKIA KTK NAMBA ILEILE ALIYONAYO KTK VIWANGO .

NDIYO MAANA HAPO JUU NIMESEMA KWAMBA SABABU ALIZOZITOWA BONDIA FRANCIS CHEKA HAZINA NAFFASI KABISA KTK NGUMI ZA KULIPWA BALI ALIHOFIA KUWA ENDAPO ANGEPOTEZA PAMBANO HILO BASI ANGEKUWA AMEMPANDISHA KATIKA VIWANGO BONDIA JAPHET KASEBA .

                      MUHHAMAD ALI-THE GREATEST

 BONDIA MAARUFU DUNIANI MOAHAMED ALI, ALIPOANZA KUPIGANA NGUMI ZA KULIPWA HAPO TAREHE 29-10 -1960 KTK UKUMBI WA FREEDOM -HALL STATE FAIR GROUND-USA ,PAMABNO LAKE LA WANZA ALILIPAMBANISHWA NA BONDIA TUNNY HUNSURKER

RAIA WA MAREKANI ,NA MKAZI WA FAYELLEVILLLE, WEST VIRGINIA-USA

NA WAKATI HUO HUYO TUNNY HUNSAKER ALIKUWA TAYARI AMEPAMBANA MAPAMBANO 1SHIRIN NA TANO [25] AKIWA AMESHINDA MAPAMBANO 15 AMEPOTEZA 9 NA SARE 1 , [ingia boxrec.com  -then search -andika tunny last name hunsaker] UTAONA REKODI YAKE YOTE NA ALIOPAMBANA NA MOHHAMD ALI UTAONA.

SASA KAMA TARATIBU HIZO ZA KUMKATAZA MABONDIA WENYE POINT NYINGI KUCHEZA NA WENYE POINT CHACHE ZINGEKUWEPO BASI HATA HUYU MUHAMMAD ALI TUJINGEMJUWA . NA ASINGEJULIKANA

                             JAPHET KASEBA

TAREHE 02 -10 -2009 FRANCIS CHEKA ALIKUBALI KUPAMBANA NA BONDIA JAPHET KASEBA  WAKATI HUO MLUNDWA/PST AKIJUA WAZI KWAMBA JAPHET KASEBA ALIKUWA NJE YA ULINGO WA NGUMI ZA BILA MATEKE KWA KIPINDI CHA MIAKA 12, NA AKIWA NA PAMBANO MOJA TU LA NGUMI BILA MATEKE ALILOPIGANA NA ERNEST BUJIKU PALE -PTA HALL, NA HALI YA KUWA YEYE FRANCIS CHEKA ALIKUWA TAYARI AMEPIGANA MAPAMBANO ISHIRINI NA TATU [23]

NDIYO MAANA HAPO KTK SOMO  ,NIMESEMA MABONDIA WA KULIPWA WANAVYOPOTOSHWA NA VIONGOZI ,

PAMBANO LA CHEKA MWENYE REKODI YA 23 NA JAPHET KASEBA MWENYE REKODI YA PAMBANO MOJA LA TAREHE 02-10-2009 LILIIDHINISHWA NA EMANUEL MLUNDWA /PST

NA PAMBANO AMBALO ALITAKIWA FRANCIS CHEKA ACHEZE NA KASEBA LILIKUWA CHINI YA USIMAMIZI WA TPBC , TENA WAKATI HUU KASEBA AKIWA NI BINGWA WA PST ,CHEKA AKAPOTOSHWA KWAMBA POINT ALIZONAZO NI NYINGI HIVYO HARUHUSIWI KUCHEZA NA JAPHET KASEBA .NAYE KWA KUWA HAJUWI ALIKUBALIANA  NA USHAURI WA KIJINGA , ULIOMHARIBIA HESHIMA YAKE MBELE YA JAMII.

SASA TUJIULIZE HATA NAFASI YA JAPHET KASEBA KUPIGANIA UBINGWA WA PST DHIDI YA MKONGWE MANENO OSAWLD MWENYE MAPAMBANO ZAIDI YA 60 ALIIPATAJE HALI YA KUWA JAPHET KASEBA AKIWA NA MAPAMBANO MAWILI TU ? LA CHEKA NA BUJIKU ?NA KISHA ETI KWA CHEKA AWE HANA SIFA ZINAZOSTAHILI? KWA PAMBANO LINALOSIMAMIWA NA TPBC?

SISI ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO] TUNAAMINI KABISA KWANBA KUNA BAADHI YA VIONGOZI WA NGUMI ZA KULIPWA NI WAPOTOSHAJI WA TARATIBU ZINAZOTAWALA NGUMI ZA KULIPWA NA TUTAENDELEA KUWAELIMISHA WAANDISHI WETU MARA ZOTE ILI KUONDOWA DHANA NZIMA YA KUWA KUNA MIGOGORO KTK NGUMI ZA KULIPWA. KUMBE NI UJINGA WA BAADHI YETU SISI VIONGOZI.

 ,NAPO BAADHI YA VIONGOZI WANAOJIFANYA WANAJUWA SAAANA NA KUWAPOTOSHA MABONDIA KWA MASLAHI YAO BINAFI.

KATIKA PAMBANO LILOANDALIWA NA KITWE GENERAL TRADERS KUGOMBEA UBINGWA WA IBF-AFRIKA BAINA YA MTANZANIA RAMADHANI SHAURI NA MGANDA SANDE KIZITO
LILIPANGWA PAMBANO LA UTANGULIZI KATI YA BONDIA FRANCIS MIYEYUSHO ACHEZE NA BONDIA BORA WA TASWA NASIBU RAMADHANI ,

 KUNA KIONGOZI MMOJA [SIYO NGOWI] ALIMKATAZA BONDIA FRANCIS MIYEYUSHO ASIPIGANE PAMBANO LA UTANGULIZI ETI MIYEYUSHO ALISHAWAHI KUMPIGA RAMADHANI SHAURI PALE TEXAS, KWA HIYO SHERIA INAMKATAZA KUCHEZA UTANGULIZI KWA PAMBANO KUU ANALOCHEZA  BONDIA ALIYEWAHI KUMSHINDA / NA KWELI FRANCIS ALIKATAA HUKU AKIWA AMESHACHUKUWA MALIPO YA AWALI KUTOKA KWA PROMOTA. NA KIONGOZI HUYO ALIJUWA KWAMBA BONDIA AMESHALIPWA ADVANCE.---HUU NI UPOTOSHAJI MKUBWA SANA NA UNAFAA ULAANIWE.

KWA KIFUPI NDG WAANDISHI WA HABARI HAKUNA KIPENGELE KINACHOMPA RUHUSA BONDIA KUKATAA KUCHEZA NA BONDIA MWINGINE ETI KWA KUWA ANA POINT CHACHE , ILA NI CHAMA NDIYO CHENYE MAMLAKA YA KUAMUWA KWA MAPAMBANO YA UBINGWA TU. NDIPO HUTAFUTWA MABONDIA WENYE VIWANGO VINYOKARIBIANA ILI KULETA USHINDANI MKUBWA KWENYE MAPAMBANO YA UBINGA ,NA SI KTK PAMBANO AMBALO SIYO LA UBINGWA.

NA KIUTARATIBU BONDIA ANAPOKUWA BINGWA ANAYETAMBULIWA NA CHAMA CHOCHOTE CHA NCHI AU CHA KIDUNIA ,NA ANATAKA KUCHEZA PAMBANO LISILO LA UBINGWA AU LA UBINGWA WA CHAMA KINGINE NI LAZIMA AOMBE KIBALI KUTOKA KWENYE CHAMA ANACHOSHIKILIA UBINGWA HUO . HASA KAMA CHAMA HICHO ANACHOSHIKILIA UBINGWA WAKE HAKISIMAMII PAMBANO HILO.

NATOWA WITO KWA VIONGOZI WENZANGU KWAMBA HUU SIYO WAKATI WA KUWADANGANYA WAANDISHI , KWA KUWAPA HABARI POTOFU , KWANI KUWA KIONGOZI WA CHAMA HAKUKUPI WEWE NAFASI YA KUPOTOSHA WAANDISHI ,NA KAMA KUNA BAADHI YA MAMBO HATUYAJUWI TUWE NA UTARATIBU WA KUULIZANA ,KWANI MAMBO HUBADILIKA KILA MARA.

                    IMEANDIKWA NAMI[-
         YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH

   RAIS -TPBO & WPBF-USBC [WORLD PROFESSIONSL BOXING FEDERATION -REPRESENTATIVE -TO TANZANIA

       +255-713-644974 -752-335584