Tangazo

Pages

Tuesday, September 11, 2012

MASHINDANO YA TAIFA YA MASUMBWI KUANZA SEPTEMBA 17

Kocha wa mchezo wa ngumi Hasan Mzonge akiwaelekeza mabondia wa timu ya taifa ya masumbwi jinzi ya kupiga ngumi zilizonyooka wakati wa mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika katika GMY ya Gmykhana Klabu.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
                                 SHIRIKISHO LA NGUMI LA TAIFA (BFT)
                                                                                                        S.L.P 15558                                                                             

       DAR ES SALAAM
                                                                                                               September 10, 2012
                                                                                 Email:-bft.tanzania2009@gmail.com
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
          YAH:-MASHINDANO YA UBINGWA WA TAIFA 17-22/09/2012.
Shirikishi la ngumi Tanzania (BFT)limeandaa mashindano ya ngumi ya ubingwa wa Taifa 2012 yatakayofanyika kuanzia jumatatu ya tarehe 17-22/09/2012 uwanja wa ndani wa taifa (indoor stadium) kila siku kuanzia saa 9.00 alasiri.
Awali mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kuanzia tarehe 15/09/2012 lakini kutokana na uwanja wa ndani wa taifa kuwa na shughuri nyingine ya kimichezo ya ligi ya mpira wa kikapu,sasa mashindano hayo yataanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 17/09/2012.
Lengo la mashindano hayo ni kupata timu ya taifa ya ngumi yenye sura ya kitaifa ,itakayoshirikisha mikoa yote ya Tanzania bara.ili kuanza maandalizi ya mapema na ya uhakika kwa ajili ya kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola 2014,mashindano ya Afrika 2015,mashindano ya olimpiki 2016,ubingwa wa dunia na mashindano mbalimbali tutayopata mwaliko kwa ajili ya kuwakilisha taifa.
Hadi  leo jumla ya mikoa kumi na nane (18) imethibitisha kuja kushiriki katika mashindano hayo,mikoa hiyo ni mikoa ya kimichezo ya Temeke,Kinondoni  na Ilala.Mingine ni Ngome ya JWTZ,JKT,Magereza na Polisi.Mingine ni Pwani,Morogoro,Mbeya,Ruvuma,Dodoma,Kigoma,na Bukoba.mikoa mingine ni Tanga,Arusha ,Tabora na Mwanza.
Uongozi wa BFT licha ya kutopata udhamini wa uhakika wa kufanikisha mashindano haya,kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumejipanga vema kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha hali ya juu ili kufikia lengo la kupata timu ya taifa kwa wakati kwa maandalizi ya mapema.mashindano hayo yana takiwa kufanyika kwa bajeti ya milioni ishirini na sita (26,000,000/=).
Sasa Mabadiliko ya ratiba ya mashindano itakuwa kama ifuatavyo:-

TAREHE    MUDA    TUKIO      
16/09/2012        Timu zote kuwasili dare s salaam.      
17/09/20123    1.00-4.00 Asb
4.00-5.00 Asb
5.00-7.00 Mch    Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa wa ndani.
Zoezi la draw na bye na ratiba ya mashindano.
Semina kwa waamuzi,timu manaja,makocha kwa ajili ya kupatiwa kanuni na sheria za mashindano.      
18/09/2012    1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk    Kupima uzito na afya,uwanja wa taifa wa ndani.
Gwaride la ufunguzi na kuanza mashindano hatua ya mtoano      
19/09/2012    1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk    Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea hatua ya mtoano      
20/09/2012    1.00-2.00 Asb
9.00-2.00 Usk    Kupima uzito na afya
Mashindano kuendelea kwa hatua ya robo fainali      
21/09/2012    1.00-2.00 Asb
2.30-8.45Mch
9.00-2.00 Usk    Kupima uzito
Mkutano mkuu  wa BFT(indoor stadium)
Mashindano kuendelea hatua ya nusu fainali      
22/09/2012    1.00-2.00 Asb
8.00-2.00 Usk    Kupima uzito na afya.
Gwaride la kufunga na kuendelea kwa mashindano hatua ya fainali.      
23/09/2012        Timu zote kuondoka   
Aidha ajenda za mkutano mkuu wa wanachama wa bft ni mbili tuambazo ni kupitia na kupitisha rasmu ya katiba ya BFT na maandalizi ya uchaguzi wa BFT wa kuwapata viongozi makiniwa kuongoza BFT kwa kipindi cha miaka mine kuanzia marchi 2013 kwa mujibu wa katiba .
Makore Mashaga
Katibu Mkuu BFT.,
   Mob:-0713/0784/0763/0773 -58 88 18
Email:- mashagam@yahoo.om

No comments:

Post a Comment