Tangazo

Pages

Thursday, September 13, 2012

TPBO YAMFAGILIA IDDI AZANI

Ndugu waandishi ,na wadau wakuu wa mchezo wa ngumi za kulipwa tanzania.

hivi karibuni mbunge wa kinonondoni ndg iddi azani aliwakabidhi vifaa vya mchezo wa ngumi mabondia wa ngumi za kulipwa nchini ,


ni jambo la kupongezwa sana hasa inapotokea wabunge kuanza kuona umuhimu wa kusaidia wanamichezo bila ubaguzi wa aina ya michezo.



imekuwa ni jambo la kawaida sana ktk nchi yetu ya tanzania kuona wabunge na makampuni mbalimbali yakitowa misaada ya vifaa vya michezo kwa upande wa mpira wa miguu tu ,na si jambo la kawaida kwa wabunge hata makampuni kuona wakitowa misaada ya vifaa kwa wanamasumbwi ,IDD AZAN umefunguwa ukurasa mpya na TPBO inaamini kabisa kwamba mfano wako utaigwa na wabunge wanzako.



TPBO inakutuma rasmi mara uingiapo bungeni uishawishi serikali ya jamhuri ya tanzania ibadil sera zake za michezo ,kwa KUTAMBUWA RASMI MICHEZO ya kulipwa ili watanzania wapate ajira zaidi kupitia michezo.



mpaka sasa hakuna taasisi yoyote ya ngumi za kulipwa inayoweza kujinadi na kujigamba eti wao ndiyo wamepewa mamlaka na serikali ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini tanzania ,


kwa sababu hata ktk orodha ya vyama vya michezo vinavyotambuliwa na baraz la michezo la taifa ,ni BFT tu ndiyo inayotambuliwa kwa ngumi za ridhaa tu.



na ngumi za kulipwa hazimo ktk orodha hiyo, hivyo hata hizi taasisi tulizonazo zimetokana na ubunifu wa watu tu kuziunda ili kuwasaidia vijana kuishi kwa nguvu kazi michezo.



TUNAHITAJI IDDI AZAN AWE MWAKILISHI WETU BUNGENI KWA KUISHIONIKIZA SERIKALI ITAMBUWE MICHEZO YA KULIPWA NA HATIMAYE SERIKALI IUNDE BOXING BOARD OF CONTROL AMBAKO TAASISI ZOTE ZA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA ZIWAJIBIKE KWA BOARD OF CONTROL itokeapo kutokuelewana miongoni mwa taasisi hizi.



NA NI BUDI WAANDISHI MJUWE WAZI KATIKA TAASISI HIZI ZA NGUMI ZA KULIPWA MPAKA SASA ZINATAMBULIWA KWA MSAJILI ALIYEZISAJILI TU ,



HIVYO IELEWEKE WAZI HAKUNA TAASISI YEYOTE ILIYO NA MAMLAKA JUU YA TAASISI NYINGINE ,WALA HAKUNA SERA YA SERIKALI YA MICHEZO ILIYOIPATIA NGUVU TAASISI NYINGINE ETI NDIYO ISIMAMIE NGUMI ZA KULIPWA , KWANI SERA YA SERIKALI YA MICHEZO BADO HAIJABADILISHWA ,NA INATAMBUWA MICHEZO YA RIDHAA TU.


                              IMELETWA KWENU NA
            YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA---  USTAADH

RAIS -- TANZANIA PROFESSIONAL BOXING ORGANISATION -TPBO


WPBF -USBC -world professional boxing federation -representative to TANZANIA

No comments:

Post a Comment