Tangazo

Pages

Sunday, September 9, 2012

VITALI KLITSCHKO AMCHAPA MANUEL CHARR WA UJERUMANI


Bondia Manuel Charr wa Ujerumani akiokolewa na mwamuzi baada ya kupigwa na Vitali Klitschko na kuchanika jichoni na kutokwa damu nyingi kama anavyoonekana.
 
MOSCOW, Russia

Manuel Charr, ambaye alshinda katika raundi kama hiyo alipoumana na Danny Williams, juzi alilazimika kutoendelea na pambano lake dhidi ya Vitali, kutokana na konde zito lililomchana juu ya jicho lake la kulia

BINGWA wa WBC Vitali Klitschko, alifanya kazi rahisi ulingoni kumuwezesha kuibuka na ushindi pasipo changamoto kubwa kutoka kwa Mjerumani Manuel Charr, katika dakika ya mwisho ya raundi ya nne jijiji hapa. 

Klitschko, 41, ameibuka mbabe wa pambano hilo dhidi ya mpinzani wake ambaye hakuwahi kupigwa huko nyuma.

Charr, ambaye alipata ushindi wa raundi kama hiyo alipoumana na Mwingereza Danny Williams, alilazimika kutoendelea na pambano hilo kuokana na konde zito lililomchana juu ya jicho lake la kulia na kumsababishia kumwagika kwa damu nyingi.

Hata hivyo Charr alikuja juu kupinga maamuzi – kufuatia majibu ya uchunguzi wa madaktari kuwa alikatwa na kitu na kwamba jeraha lake halikutokana na ngumi, hivyo kupinga matokeo.

Klitschko kwa mara nyingine anaingia katika ushindi wa utata, baada ya Februari mwaka huu kumchapa Dereck Chisora kwa pointi, na kusababisha mgogoro baina yam kali huyo na David Haye wakati wa mkutano na vyombo vya habari.

Haye, ambaye alipigwa kwa pointi na ndugu wa kuzaliwa wa Vitali, Wladimir mwaka jana, alifanikiwa kumchapa Chisora KO Julai mwaka huu nma kuamua kuomba pambano dhidi ya mkongwe huyu Vitali.

Pambano baina ya Haye na Vitali, linaweza tu kufanyika kama raia huyo wa Ukraine atashindwa uchaguzi wa nchi yake ambako anawania ubunge, ambapo kama akishinda atalazimika kustaafu masumbwi.

No comments:

Post a Comment