Tangazo

Pages

Tuesday, September 25, 2012

BFT NA TPBC KUUNDA KAMATI YA KUFUFUA NA KUENDELEZA MASUMBWI TANZANIA



Rais wa TPBC, Onesmo Ngowi
Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC} zimekubaliana kuunda Kamati ya watu kumi (lO) ili kufufua na kuundeleza mchezo wa ngumi Tanzania.
Kamati hiyo ambayo itajumuisha wajumbe watano (5) kutoka BFT na watano (5) kutoka TPBC itakuwa chini ya uenyekiti wa Makamu wa Rais wa TPBC, Godfrey Madaraka Nyerere, ambayo itajulikana kwa jina la 'Kamati ya Nyerere ya Kufufua nKuendeleza Ngumi Nchini'
'Kamati ya Nyerere ya Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini'  itafanya kazi ya kuandika hadidu rejea za rasimu ya makubaliano ya pande zote mbili ili ziweze kutumika kama mwongozo wa makubaliano hayo.
Ushirikiano kati ya BFT na TPBC utaratibiwa na Katibu Mkuu wa BFT  Makore Mashaga pamoja na Katibu Mkuu wa TPBC Nemes Kavishe
Wawili hawa watakuwa ndio wakuu wa Sekretariet ya 'Kamati ya Nyerere ya Kufufua na Kuendeleza Ngumi Nchini', ambacho ndicho chombo cha kusimamia na kuratibu makubaliano haya.
Ushirikiano kati ya vyama hivi viwili ambavyo kimoja kipo kwenye ngumi za ridhaa na kingine kipo kwenye ngumi za kulipwa ni ushirikiano unaolenga kubadili mwelekeo wa mchezo wa ngumTanzania.
Kwa muda mrefu sasa mchezo wa ngumi umekuwa ukikumbwa na matatizo mbalimbali ambayo yamepelekea kutokuwepo na maendeleo yanayotegemewa na wadau wa ngumi Tanzania.
Ushirikiano wa vyombo vyote vinavyoratibu ngumi nchini Tanzania utakuwa ni msingi imara wa kujenga ari ya maendeleo ya ngumi kwa Tanzania.
Tanzania imekuwa ikivurunda kwenye mashindano ya kimataifa karibu kila michezo ya kimataifa na hivyo ushirikiano wa vyombo hivi viwili vya ngumi utakuwa ndio msingi imara wa kuendeleza na kuondoa aibu hiyo ya muda mrefu ya mchezo huo Tanzania .

No comments:

Post a Comment