Tangazo

Pages

Monday, March 31, 2014

SUPER D AMPIKA JUMA BIGLEE KUPAMBANA APRIL 15 CHALINZE


Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Juma Biglee wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala amana CCM Dar es salaam jana Biglee anajiandaa na mpambano wake april 15 Chalinzo mkoa wa pwani picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Juma Biglee wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala amana CCM Dar es salaam jana picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Juma Biglee wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala amana CCM Dar es salaam jana Biglee anajiandaa na mpambano wake april 15 Chalinzo mkoa wa pwani picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Saturday, March 29, 2014

WBO WATOA UJUMBE MASHALI AKIMGALAGAZA KASEBA KWA POINT

Mabondia Japhert Kaseba na Thomas Mashali wakipambana wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba kugombania ubingwa wa UBO Africa Mashali alishinda kwa Pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mtoto Zainabi 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkata wa Ubingwa wa UBO Africa katika kona ya bondia Japhert Kaseba kabla ya kuanza kwa mpambano wao mkanda uho aliubeba kwa ajili ya kuwaonesha mashabiki pamoja na mabondia waliokuwa wakiwania mkanda huo

Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akiwa na mkata wa Ubingwa wa UBO Africa kabla ya mpambano kuanza katika kona ya Thomas Mashali ambaye alishinda na kuunyakuwa mkanda huo kwa kushinda kwa point

Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo uku Rais wa ngumi za kulipwa nchini Emanuel Mlundwa akiwakumbusha mabondia Thomas Mashali kushoto na Japhert Kaseba sheria zitakazotumika katika mpambano huo www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Kalage Suba kushoto akipambana na Alan Kamote wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO katika ukumbi wa PTA Sabasaba Kamote alishinda kwa TKO ya raundi ya saba oicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Alan Kamote akiwa na ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO
Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo
Baadhi ya watoto ambao wanafanya mazoezi katika GYM mbalimbali walijitokeza kuamasisha ujumbe wa World Boxing Ordanization 'WBO'  kushoto nio Rashidi Matumla na kulia ni Promota kutoka tanga Ally Mwazoa ambaye anakuja kwa kasi uku akiwa na mapasmbano matatu mfululizo yatakayofanyika PTA Sabasaba

Mabondia wakongwe Jock Hamisi kushoto akipambana na Said Chaku wakati wa mpambano wao waliotoa droo

Katika kuhakikisha ujumbe wa WBO unazingatia mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akipiga padi huku akisimamiwa na Emanuel Mlundwa

Baadhi ya watoto waliojitokeza katika kampeni ya kufanya mazoezi watoto wasipewe madawa wakiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali uku wakiwa na zawadi zao walizopewa mabegi flana na glove zenye ubora wa ali ya juu

Zainabu 'Ikota' Mhamila

Friday, March 28, 2014

KASEBA NA MASHALI WAPIMA UZITO KUPIGANA JUMAMOSI MARCH 29 PTA SABASABA

Bondia Japhert Kaseba akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa na Thomasi mashali kushoto mpambano utakaofanyika PTA Sabasaba siku ya jumamosi march 29 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Thomasi Mashali kushoto na Japhert Kaseba wakiwa na mkanda ambao wataugombania katika ukumbi wa PTA sabasaba siku ya jumamosi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Promota wa mpambano huo Ally Mwazoa akizungumza mbele ya waandishi wa habari
Mabondia Alani Kamote wa Tanga kushoto pamoja na Karage Suba wakiwa na mkanda watakaougombania kesho kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Ally Mwazoa akisisitita jambo

Thursday, March 27, 2014

Super D: Kocha anayejitolea kuinua mchezo wa ngumi nchini


  Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akikabizi vifaa vya mchezo wa masumbwi Gloves pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo kwa Kocha wa GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo  Mohamed Chipota kwa ajili ya kuamasisha mchezo  wa masumbwi katika eneo ilo na kuwapa moyo wa kuendelea na mazoezi wanaoshudia wengine wa pili kushoto ni Atanasi kibwe,Omari Bai, Raymond Mbwago na Mussa Sindano Vifaa hivyo pamoja na Dvd vina thamani ya shilingi laki mbili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi clip bandeji na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa bondia Mussa Mchopanga baada ya kumdunda Anton Idoa kwa K,o ya raundi ya pili bondia huyo ndie bingwa kwa sasa wa mkoa wa Dar ers salaam na anajiandaa na mashindano ya Majiji yatakayofanyika katikati ya mwaka huu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.comKIU kubwa aliyonayo katika mchezo wa ngumi ndiyo unaomfanya bondia wa zamani wa klabu za
Simba,  Reli  na Amana, Rajabu Mhamila 'Super D' ndiyo iliyomfanya kujitolea kwa hali na mali kuwasaidia na kuendeleza vipaji vipya vya mchezo huo.
Mwishoni mwa mwaka jana kocha huyo anayetambuliwa kimataifa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Duniani (AIBA) alifanya ziara mikoani ili  kuhamasisha ngumi akigawa pia DVD zenye (clips) za mapambano ya mabondia mbalimbali nyota ili watu wajifunze mchezo huo.
Pia mapema mwaka huu amejitolea akigawa vifaa vya michezo kwa baadhi ya klabu za ngumi lengo likiwa kuwahamasisha vijana kujifunza na kuucheza mchezo huo bila ya matatizo ya ukosefu wa vifaa.
Aligawa vifaa hivyo katika klabu ya Uhuru Gerezani, pia amekuwa akisaidia na kuuza vifaa vya ngumi kwa bei rahisi katika michuano na mapambano mbalimbali za ngumi za ridhaa na zile za kulipwa ili kusaidia kuendelea mchezo huo.
Super D, pia amekuwa akiendelea kuwanoa mabondia chipukizi katika klabu za Amana akisaidia na wazoefu wa kazi hiyo Habib Kinyogoli na Kondo Nassor na klabu yake ya Ashanti iliyoshirikina kufanya vyema michuano ya Kombe la Taifa na Klabu Bingwa ya ngumi.

Super D anasema japokuwa kazi ya ukocha wa ngumi imekuwa hailipi na pengine ndiyo sababu ya mabondia wengi wa zamani waliostaafu mchezo huo kutopenda kuifanya, lakini yeye anafurahia kwa kuona vijana waliopitia mikononi mwake wakipata mafanikio na kuwa tishio.
Baadhi ya vijana wanaotamba wakipitia mikononi mwake ni Erck Magana,Husein Pendeza, Mussa Mchopanga,Juma Bigrii, Ibrahim Class 'King Class Mawe', Idd Mnyeke, Mussa Sunga na wengineo.
"Nafarijika kuona vijana niliowaibua kupitia klabu ya Ashanti Boxing wakizidi kuwa tishio, nadhani muda si mrefu watavaa viatu vya akina Rashid Matumla, Joseph Marwa na wakali wengine," anasema.
Anasema bila kujali kama ananufaika au la, furaha yake ni kuona mchezo wa ngumi ukizidi kusimama na kuendelea kuibua vipaji vipya ambavyo anaamini watakuja kuwa faida ya baadaye kwa taifa.
Super D   baba wa watoto wawili, Zainabu Mhamila 'Ikota' (11) na Saada Swedi (16) mtoto wa kuasili, anasema kumekuwa na vikwazo vingi katika kuendeleza ngumi nchini hasa suala la wafadhili na wadhamini.
Anasema wafadhili na wadhamini wamekuwa wazito kujitokeza kuupiga tafu mchezo huo na mabondia kwa ujumla kitu ambacho hakujua kinasababishwa na nini ilihali huo ni mchezo kama michezo mingine.
"Tatizo kubwa katika ngumi ni suala la udhamini, ngumi zimesahauliwa sana na hata wafadhili kwa mabondia nalo ni tatizo, japo inaelezwa ubabaishaji unaofanywa na wasimamizi wa ngumi ni sababu," anasema.
Anasema ni wajibu wa wasimamizi wa ngumi na wadau kwa ujumla kupigana kurekebisha hali ya mambo ili kutoa ushawishi kwa wadhamini na wafadhili kujitokeza kuwapiga tafu.
Rajabu Mohammed Mhamila 'Super D' alizaliwa mwaka 1977 jijini Dar akiwa mtoto wa pili kati ya wanne wa familia yao na alianza kupenda michezo tangu akiwa mdogo.
Mwenyewe anasema aliyemuingiza kwenye ngumi ni baba yake mzazi, Mzee Mhamila 'Chuck Norris, aliyekuwa mnyanyua vitu vizito na 'gateman' wa ukumbi wa DDC Kariakoo aliyekuwa akiwalazimisha kufanya mazoezi bila kupenda akidai anataka wawe fiti.

Mazoezi hayo na kule kumuona akinyanyua vitu vizito vilimfanya taratibu ayafurahie mazoezi kabla ya kuanza kupenda ngumi kwa kuvutiwa na mabondia Muhammad Ali na George Foreman.
Anasema mwanzoni mwa miaka ya 1980 alipelekwa klabu ya Simba na mjomba wake aliyewahi kuwa bondia tishio nchini, Iraq Hudu 'Kimbunga' na ikawa mwanzo wa safari yake ndefu katika ngumi mpaka
Super D anasema mbali na yeye pia kaka yake Shaaban Mhamila "Star Boy',  na wadogo zake Rashid Mhamila 'Nature Fire' na 'Mohamed Hemed' 'Kadogo Ninja' wote walitamba kwenye ngumi enzi zao wakipigwa tafu na mazoezi ya baba yao aliyekuwa pia mwanamieleka.
Baada ya kupata mafanikio akiwa Simba akishiriki michezo kadhaa, alihama kujiunga klabu ya Reli kisha baadae Amana, ingawa hakupata mafanikio makubwa.
Anasema kati ya michezo yote aliyocheza hawezi kusahau pambano dhidi ya Roger Mtagwa anayeishia kwa sasa Marekani, ambapo anakiri aklichakazwa isivyo kawaida.
"Siwezi kumsahau Mtagwa kwani alinipa kichapo  kutokana na jamaa alijua ngumi na alileta yupinzani wa ali ya juu kwani nilipofika raundi ya tano
nilikuwa nimeumia taya," anasema.
Anamshukua kocha wake, Habib Kinyogoli pamoja na mabondia mahiri nchini kama  Maneno Osward, Japhet Kaseba, Kalama Nyilawila,Fransic Miyeyusho pamoja na uongozi Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT)  kwa kumtia moyo katika juhudi zake za kuendeleza mchezo huo.

Kaseba, Mashali nani kucheka Jumamosi?


* Wanawania mkanda wa UBO-Afrika
(PIX-Ngumi)
Kaseba, Mashali

BAADA ya tambo za muda mrefu kila moja akitamba kuwa ni zaidi ya mwenzake, mabondia Japhet Kaseba 'Champion' na Thomas  Mashali 'Simba Asiyefugika' wanatarajia kukata mzizi wa fitina mwishoni mwa wiki hii watakapopanda ulingoni kuzipiga.
Mabondia hao machachari wanaoshikilia ubingwa wa Taifa kila mmoja wa vyama 'hasimu' vya ngumi za kulipwa nchini, TPBO-Limited na PST watapanda ulingoni Machi 29 kwenye ukumbi waq PTA-Sabasaba jijini Dar es Salaam kuwania mkanda wa UBO-Afrika.
Pambano hilo litakalosindikizwa na michezo zaidi ya mitano ya utangulizi limeandaliwa na promota maarufu kutokea mjini Tanga, Ally Mwazoa chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania (PST).
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa mabondia hao kukutana ulingoni, huku kila mmoja akitamba kuwa ataibuka na ushindi kutokana na maandalizi waliyofanya kwenye kambi zao.
Mashali ambaye amepoteza mapambano mawili tu akipigwa na bingwa asiyepigika nchini, Francis Cheka na jingine la kimataifa dhidi ya Arif Magomedov wa Russia mwishoni mwa mwaka jana, ametamba kuwa Kaseba hana ubavu wa kumsimamisha kwa vile mpinzani wake huyo amelowea kwenye mchezo wa kick boxing.
"Tunamkaribisha kwenye ngumi na Machi 29 haitakuwa salama kwake kama alizoea kupigana na mabondia wepesi, safari hii anakutana na wakali wenyewe, asitarajie mteremko," alisema Mashali.
Mashali ametamba kuwa atamtia adabu mpinzani wake aliyewahi kuwa bingwa wa dunia wa kick boxing wa WCK na WKL kabla ya kurejea kwenye ngumi na kunyakua ubingwa wa PST dhidi ya Osward Maneno 'Mtambo wa Gongo'.
Hata hivyo Kaseba kwa upande wake aliliambia gazeti hili kuwa, amejiandaa kushinda pambano hilo ili kutwaa mkanda huo wa kimataifa ikiwa ni ndoto zake za muda mrefu.
"Kwanza nimefurahi kupata nafasi hii ya kuwania mkanda wa UBO Afrika, ni taji kubwa na nimekuwa na ndoto za muda mrefu za kunyakua mataji ya kimataifa baada ya kutamba kwenye kick boxing hivyo ni nafasi yangu," alisema
Kaseba, alisema ingawa hajajua atampiga Mashali katika raundi ya ngapi, lakini itakuwa ni mapema mno na kumtahadharisha mpinzani wake kuwa, ajiandae kupokea kipigo kwa sababu anataka kunyakua taji la kwanza la kimataifa baada ya kurejea katika ngumi.
Hata hivyo bondia huyo alikiri kwamba Mashali ni mmoja wa mabondia hodari na anamkubali kwa uwezo wake kwenye ulingo, lakini alisema amejipanga kumtandika ili kutimiza lengo lake la kutwaa taji hilo lililo wazi.
Mabondia hao wanakutana Jumamosi kila mmoja akiwa na rekodi yake, Kaseba anajivunia kucheza mapambano nane na kushinda matano, matatu yakiwa na KO na kupoteza matatu, huku mpinzani wake akiwa amecheza michezo 12 akishinda 9, mitano kwa KO na kupoteza mawili na kuambulia droo moja.
Mashali anayeshikilia pia ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mara ya mwisho kupanda ulingoni ilikuwa Novemba mwaka jana nchini Russia na kupigwa kwa KO ya raundi ya pili dhidi ya Arif Magomedov wa Russia, huku Kaseba alishinda pambano lake la mwisho dhidi ya Alibaba Ramadhani baada ya kutoka kupokea kipigo cha KO ya raundi ya pili dhidi ya Jeremy van Diemen nchini Australia.
Hivyo kukutana kwao kwenye pambano hilo ni nafasi ya kila mmoja kutaka kuonyesha umahiri wake na kunyakua mkanda huo UBO.
Kuhusu maandalizi ya pambano hilo mratibu Ally Mwazoa alisema kila kitu kimekaa sawa na mashabiki wa ngumi wanapaswa kujitokeza ukumbini kupata uhondo kwani kutakuwa na mapambano matatu ya ubingwa, miwili ya kimataifa na mmoja wa Taifa-PST.
Mwazoa anayetokea mkoani Tanga, alisema mbali na pambano kuu la Kaseba na Mashali pia siku hiyo kutakuwa na pigano la kuwania ubingwa wa kimataifa wa UBO kati ya Allan Kamote dhidi ya Karage Suga katika uzito wa kilo 61.
Awali Kamote alikuwa amepangiwa kupigana na Fadhil Awadh ambaye alikumbwa na mauti siku chache baada ya kuugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Mwananyamala alipokumbwa na mauti huku mkanda aliokuwa augombanie na Kamote ukiwa umetua nchini.
"Baada ya Awadh kufariki, Allan Kamote sasa atapambana na Karage Suba kuwania ubingwa wa Kimataifa wa UBO, pia siku hiyo kutakuwa na mchezo wa kuwania ubingwa wa taifa-PST kati ya Rajab Mhoja dhidi ya Fred Sayuni," alisema Mwazoa.
Mratibu huyo aliyataja mapambano mengine yatakayochezwa siuku hiyo ni pamoja na lile la  Haji Juma dhidi ya Juma Fundi, Zuberi Kitandula atakayepimana ubavu na Issa Omar na Baina Mazola dhidi ya Bakar Dunda.
Michezo mingine itawakutanisha Jumanne Mohammed atakayechapana na Shaaban Mtengela, wakongwe Said Chaku na Jocky Hamis wataonyeshana nao kazi na Majid atapimana ubavu dhidi ya Frank.
Mwazoa alisema wamejipanga katika kuhakikisha mashabiki watakaoenda ukumbini hapo kupata burudani bila bughudha kwa kuweka ulinzi madhubuti ukiongozwa na askari kanzu, kamera maalum na walinzi wengine shiriki ndani na nje ya ukumbi wa PTA.
"Tunafanya hivi kwa kutambua mabondia Kaseba na Mashali wana mashabiki wengi, tunashukuru Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova ambaye ni Mlezi wa ngumi ametuhakikishia kila kitu kitakuwa sawa, hivyo mashabiki waje kwa wingi bila ya hofu," alisema Mwazoa.
Je, ni Japhet Kaseba au Thomas Mashali atakayecheka au kulia Jumamosi PTA? Tusubiri tuone.

MMJKT MABINGWA WA NGUMI MKOA WA DAR ES SALAAM


Bondia Hamisi Mputeni kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Victor Njaiti wakati wa mpambano wao katika mashindano ya klabu bingwa mkoa wa Dar es salaam juzi Njaiti alishinda kwa pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Mohamed Chibumbuli kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdul Rashid  wakati wa mchezo wao katika mashindano ya klabu bingwa mkoa wa Dar es salaam Chibumbuli alishinda kwa pointi mchezo huo juzi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya MMJKT jana imeibuka mabigwa wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam baada ya kuvipiku vilabu nane vilivyoweza kujitokeza kushiliki mashindano hayo

na kutawazwa kuwa bingwa wa mkoa baadhi ya mabondia waliocheza fainal za mashindano hayo ni Hamisi Mrisho wa 'MMJKT' alisambalatishwa kwa pointi na bondia Oscar Richard wa 'Urafiki'   na Omari Mohamed wa urafiki akichezea kichapo kutoka kwa mwenzie John Mwambinga, na bondia anaekuja kwa kasi ya ali ya juu akitokea timu ya Ashanti ya ilala kwa sasa akichezea timu ya 'MMJKT'  alifanikiwa kumpiga John Christian wa 'Mgulani' Saleh Abdallah wa mgulani alishindwa kutamba mbele ya  Undule Langson wa Magereza

nae Jacobo Agusteno wa 'mgulani' alishindwa kufulukuta mbele ya Bosco Bakari wa 'MMJKT' katika mpambano mwingine uliowakutaniasha Festo Ngabo wa Magereza alishindwa kutamba mbele ya Victor Njaiti wa 'mmjkt' nae bondia Mohamedi Chibumbuli wa magereza alimsambalatisha vibaya bondia Said Saleh wa 'mavituzi'
 akizungumzia maandalizi ya mabondia wa mkoa wa Mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa Dar es salaam 'DABA' Akaroli Godfrey amesema
kwa sasa mabondia wa timu ya mkoa wa Dar es salaam wapo kambini wakijiandaa na mashindano ya majiji yatakayoanza Kampala Uganda April 2 mwaka huu 

timu hiyo ambayo ipo na makocha wazoefu wakiongozwa na David Yombayomba ,Ferdnand Nyagawa mazoezi yanayofanyika kila siku mgulani JKT, wakisaidiwa na Mazimbo Ally na Kameda Antony 

timu hiyo ina maitaji mbalimbalio ikiwemo kambi pamoja na kupeleka timu Uganda ambayo itagalimu milioni 16 kwa ajili ya kwenda kwenye mashindano
hayo ambapo mpaka sasa wamenda sehemu mbalimbali ikiwemo makampuni na kwa watu binafsi

ata hivyo akuna mafanikio yoyote hivyo kuwaomba wadau wa mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kusaidia timu hiyo ambayo inakabiliwa na mashindano ya majiji

Wednesday, March 26, 2014

SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION


MABONDIA KUPIMA UZITO IJUMAA


Mabondia wanaotegemea kupigana jumamosi kugombea ubingwa wa UBO international katika ukumbi wa Karume zamani PTA hall, wakiongozwa na Thomas Mashali na Japhet kaseba wanategemea kupima uzito  siku ya ijumaa katika  hotel ya National hotel iliyopo maeneo ya keko kuanzia saa tatu asubuhi. Akizungumza na wanahabari hizi bw Ibrahim kamwe amesema kuwa mabondia wote wanaocheza mapambano ya utangulizi wapo katika hali nzuri na wale mabondia  wa mikoani wanategemea kuingia kesho alhamis wakiongozwa na alan kamote atakaecheza pambano la ubingwa wa Africa dhidi ya karage suba ambae amekuwa mbadala wa bondia fadhili awadh aliyefariki kwa ugonjwa wa malaria kali iliyomkuta kipindi akijiandaa na mapambano haya ya ubingwa, mapambano mengine yatakayopigwa siku hiyo yatakuwa kama ifuatavyo fredy sayuni motto wa keko atazipiga na Rajab mahoja wa tanga kugombe ubingwa wa taifa wa PST mabondia hawa walishawahi kuzipiga mkwakwani tanga na sayuni kuchezea kichapo kikali, safari hii Fredy sayuni anakutana nae tena kwao akitaka kulipa kisasi. Baina Mazola wa mzazi atapambana na Bakari dunda, huku dogo anayekuja juu kwa kasi na wengi humpenda kwa staili ya uchezaji wake Issa omar Nampepeche au “peche boy” atapimana ubavu na bondia mkongwe bingwa wa bantam Zuberi kitandula pia kutakuwepo na mapambano mengine mengi tu pamoja na lile la juma fundi na haji juma, shaban mtengela na jumanne Mohamed, jocky hamis na said chaku pambano la wakongwe hili .nao watakuja kupima afya zao na uzito kwa mara ya mwisho wakisubiri hukumu ya ulingoni

MASHINDANO YA KLABU BINGWA YA NGUMI ZA RIDHAA MKOA WA DAR YANAENDELEA PANANDI PANANDI ILALA BUNGONI

Bondia Mussa Mchopanga kushoto akionesha ufandi wa kutupa makonde kwa Azizi Swalehe wakati wa michuano ya mashindano ya Klabu bingwa ya ngumi mkoa wa Dar es salaam Mchopanga alishinda kwa K,O ya raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Azizi Swalehe akiwa chini baada ya kupigwa konde zito na Mussa Mchopanga aliyesimama Mchopanga alishinda kwa K,O ya raundi ya kwanza picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Maulidi Athumani kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na John Christia wakati wa mashindano ya klab bingwa ya mkoa wa Dar es salaam Christian alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Monday, March 24, 2014

Floyd Mayweather Jr Mbabe anayetaraji kuhitimisha zama zake A. KusiniFloyd Mayweather Jr
Mbabe anayetaraji kuhitimisha zama zake A. Kusini
*Ni mwanamichezo anayeongoza kwa fedha, matumizi
LEO katika maisha ya wenzetu tutakuwa na mbabe Floyd Mayweather Jr ‘Money’ anayetokea katika ukoo wababe waliowahi kutikisa dunia kwa kutwaa ubingwa wa ngumi wa duniani ambao ni baba yake mkubwa Floyd Mayweather Sr na baba zake wadogo, Jeff Mayweather na Roger Mayweather.
Mbabe huyo ambaye ametangaza kwa mara nyingine kwamba anamipango ya kucheza pambano lake la mwisho Septemba 2015, nchini Afrika Kusini.
Bingwa huyo aliyabainisha hayo wakati alipokuwa nchini Afrika kusini katika ziara yake ya kutangaza mchezo huo nchini humo katika majimbo sita ikiwamo miji ya  Bloemfontein, East London na Cape Town.
Bondia huyo ambaye ni rafiki wa karibu wa rapper 50 Cent ana rekodi ya kushinda mara 45 na hajawahi kupigwa hata pambano moja tangu aanze mchezo huo mwaka 1996, huku akishinda kwa ‘KO’ (26). 
Ujio wa mwakani wa bondia huyo utakuwa wa pili baada ya ule wa kwanza ambao mbabe huyo alifanikiwa kupewa heshima ya kuwa mgeni rasmi wa utoaji wa tuzo wa mwanamichezo bora wa mwaka wa Afrika Kusini.
USICHOKIJUA
Floyd Mayweather amefuata nyayo za baba yake mzazi Floyd Mayweather aliyekuwa bingwa wa dunia, baba yake mdogo Jeff Mayweather alikuwa bingwa wa uzito wa juu wa IBO na baba yake mwingine, Roger Mayweather alikuwa bingwa wa dunia mara mbili, kabla ya kuacha na kuwa kocha wa kijana huyo.
Ngumi za ridhaa alizocheza takribani mapambano 84 yalimuwezesha Floyd, kung’aa na kuonesha kipaji chake kutokana na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa taifa nchini Marekani ‘National Golden Gloves’ kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 1993, hadi 1996.
Floyd kutokana na ugumu wake wa kutopigika, aliokuwa nao, wenzake walimpachika jina la utani ‘Bitch Boy’ kutoka na usugu wa uso wake, uliokuwa hauchubuki wala kuchanika akiwa ulingoni.
Sifa yake kubwa ni ukwepaji wa makonde akifananishwa na enzi za baba yake, Floyd Mayweather Sr na baba yake mdogo, Roger Mayweather, ambao ndio wamekuwa makocha wake.
Baba yake mdogo, Roger Mayweather alichukua jukumu la kumfundisha baada ya baba yake mzazi, Floyd Mayweather Sr. kuhukumiwa kifungo jela baada ya kukutwa na dawa za kulevya ndani ya gari lake mwaka 1993.
Baada ya Mayweather Sr. kutoka jela alimchukua tena mwanawe na kumuendeleza kumfundiusha na kumuwezesha kumshinda kwa KO, Sam Girard.
Mwaka 2006, akiwa na miaka 29 pekee, Mayweather aliviita vyombo vya habari na kuvieleza nia yake ya kutaka kustafu baada ya kucheza na Oscar De La Hoya.
Hatimaye Mei 5, 2007 pambano kati yake na bingwa wa WBC, Light Middle, De La Hoya na kufanikiwa kushinda lakini alibatilisha uamuzi wake wa kustaafu ngumi.
FEDHA
Floyd Mayweather anamiliki utajiri unaofikia kiasi cha dola milioni 216 (sawa na shilingi milioni 216).
MATUMIZI YA FEDHA
Mbabe huyo ambaye ndiye mwanamichezo anayelipwa zaidi amekuwa akielezwa kutumia fedha kwa fujo zaidi kuliko wanamichezo wengine, kwani hata katika pambano lake lililopita la Septemba alilpwa kiasi cha dola milioni  41.5. 
Kutokana na matumizi yake makubwa ya fedha mbabe huyo amepewa jina la utani la ‘Money’.
Tofauti na nyota wengine Mayweather amekuwa na mpambe anayebeba mikoba ya mamilioni ya fedha katika matumizi yake na kulipa kwa fedha taslim badala ya kulipa kwa hundi kama ilivyo kwa nyota wengine.
Hupendelea kuvaa viatu vya hali ya juu na hata nguo zake za ndani amekuwa akivaa mara moja na kutupa.
Wapambe wake na hata wafanyabiashara zake wamepewa jina la ‘The Money Team’ alilalamikiwa kutumia fedha vibaya kiasi cha kutokuwa na fedha benki hali iliyomfanya amuonesha mwandishi wa ESPN kitabu chake cha benki kilichokuwa na dola milioni 123 na kumwambia kwamba hiyo ni akaunti moja tu badoi nyingine.
Kwa kuonesha kwamba anatumia fedha kufuru mbabe huyo alipokuwa katika moja ya ziara yake nchini Marekani alikuwa akitumia ndege binafsi akiwa amempakia kinyozi wake pekee ingawa mara zote anakuwa amenyoa kipara huku wapambe wake wengine akiwa amewakodia ndege nyingine.
Akiwa jijini New York alitumia karibu dola 250,000 (shilingi miloni 400) kwa kununua vito vya mwanaye, Iyanna mwenye umri wa miaka 13 ambavyo ni Hereni na mikufu.
USAFIRI   
Hutumia kiasi kikubwa cha fedha katika ununuzi wa magari ambako anaelezwa amekuwa akinunua magari ya kifahari mawili mawili kwa rangi tofauti kwa nia ya kutumia katika majiji mbalimbali ya Marekani.
Inaelezwa kwamba kununua magari ya rangi tofauti yamekuwa yakimuwezesha kutambua jiji analokuwa amefika kwa mfano anapokuwa Las Vegas hutumia gari jeupe na anapokuwa Miami anatumia jeusi.
MAKAZI
Floyd Mayweather anaishi Las Vegas katika jumba ambalo alilinunua na kulikarabati kwa dola milioni 9. Jumba hilo lipo kwenye eneo lenye ukubwa wa futi za mraba 22,000. Vyumba vitano vya kulala, vyumba saba vya kuoga, baa ndogo, chumba cha kuonea sinema, ukumbi wa mikutano, eneo la kucheza gofu, gereji.
WASIFU
JINA: Floyd Mayweather Jr ‘Money’
UMRI: 37
KIMO: mita 1.73
UZITO: kilogramu 68
Makala hii imendaliwa na Shabani Matutu kwa msaada wa mashirika mbalimbali ya kimataifa
.DVD MPYA KUTOKA KWA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION AMBAZO ZINATARAJIWA KUWA HEWANI WIKI IJAYO NA MAPAMBANO YOTE YA NGUMI YATAKAYOFANYIKA WIKI IJAYO ZAIDI FIKA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO PIGA SIMU 0713406938

Sunday, March 23, 2014

IDDY BONGE AMGALAGAZA SHOKA YA BUCHA

Bondia Amani Bariki 'Manny chuga' kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Selemani Moto wakati wa mpambano wao Many chuga alishinda kwa TKO ya raundi ya nne picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Kasimu Gamboo kulia akipambana na mohamed babeshi wakati wa mpambano wao Ganmboo alishinda kwa k,o ya raundi ya tatu ya mpambano huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
REFARII OMARI YAZIDU AKIMWINUA MKONO JUU BONDIA KASSIMU GAMBOO

bONDIA aLi Bugingo kushoto akioneshabna umwamba wa kutupiana makonde na Hassani Mandula mandula alishinda kwa pointi

Bondia Fadhili Majia kulia akimtupia konde Juma Selemani wakati wa mpambano waio uliofanyika manzese majia alishinda kwa k,o ya raundi ya tatu
Bondia iddi bonge akiwa ulingoni
Refarii Pembe Ndava akiwapatia maelezo mabondia Idd Bonge na Bernard Mwakasanga kabla ya mpambano wao uliofanyika Manzese
Bondia Iddi Bonge kushoto akimtwika Bernard Mwakasanga ngumi wakati wa mpambano wao uliofanyika manzese Dar es salaam Bonge alishinda kwa k,o ya raundi ya kwanza katika mpambanio huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Iddi Kipandu .Iddi Bonge' mwishoni mwa wiki iliyopita alikata ngebe za Bernard Mwakasanga 'Shoka ya Bucha; baada ya kumtwanga kwa K,O ya raundi ya kwanza katika mpambano wao wa uzito wa juu uliofanyika Manzese Dar es salaam

mpambano huo uliokuwa na mashabiki wengi wa kike na kiume ulivuta hisia za watu mbalimbali ambapo baadhi ya mashabiki walikuwa wakisema hapa K,O tu ata hivyo mashabiki wengi walikuwa upande wa Bonge ambao walikuja kumshangilia na ngoma pamoja na filimbi

Bonge alipiga ngumi ya kwanza na kumfanya 'Shoka ya Bucha ' kwenda chini kama pakacha alipo hesabiwa na kusimama aijapita mda akapigwa ngumi nyingine na kudondoka kama mnazi hapo hapo refarii pembe ndava akakatiza mpambano na kumpatia ushindi bonge akimwacha mwakasanga anagalagala kwa ngumi nzito ngumi ya kushiba ya uzito wa juu

mara baada ya mpambano huo bondia Iddi Bonge alijigamba kwa sasa ana mpinzani ila anasikia tu jina la bondia Alphonce Mchumiatumbo ambapo amemtahadhalisha ole wake akutane na mikono ya mwanaume mchumiatumbo anacheza na wachovu ndio mana anawakaslisha mapema tu raundi ya kwanza na ya pili mimi nikikutana nae nitakuwa sina msalie mtume nae nitahakikisha namsambalatisha raundi za awari tu

katika mpambano huo uliosindikizwa na mabondia mbalimbali ambapo bondia Salum Kombe alimpiga kwa pointi Ally Jagalaga uku Amani Bariki ' Manny Chuga' akimsambaratisha kwa TKO ya raundi ya nne Selemani Motto na Kassimu Gamboo akimpiga bila huruma bondia  Mohamed Babeshi kwa K,O ya raundi ya tatu na Ally Ramadhani akitoa droo na Ashrafu Selemani katika mpambano wea uzito wa juu bondia halidi manjee alishindwa kufurukuta kwa Shabani Mtengera baada ya kupigwa kwa point na Hassani Mandula alimtwanga Ally Bugingo kwa point wakati Fadhili Majia akimpiga bila huruma Juma Selemani kwa K,O ya raundi ya nne

Mchezo huo wa masumbwi uliokuwa ukisimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa nchini PST chini ya Emanuel Mlundwa

MABONDIA KUMALIZA UBISHI LEO MANZESE

Bondia Amani Bariki Manny Chuga kushoto akitunishiana misuli na Selemani Motto baada ya kupima uzito ambapo mpambano wao wa kumaliza kubishi unafanyika leo

Mabondia Wa uzito wa Juu I ddi Bonge kushoto na Bernard Mwakasanga wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito jana na mpambano wao unafanyika leo manzese katika ukumbi wa frends corne

Promota Waziri Rosra katikati akiwatambulisha mabondia Iddi bonge na bernard mwakasanga ambapo leo wanamaliza ubishi wa nani zaid

Mabondia Wa uzito wa Juu I ddi Bonge kushoto na Bernard Mwakasanga wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito jana na mpambano wao unafanyika leo manzese katika ukumbi wa frends corne
Ally Bugingo akipima uzito jana kwa ajili ya mpambano wake na hasani mandula kushoto mpambano wao unafanyika leo march 23 katika ukumbi wa frends corner manzese

Hassani Mandula na Ali bugingo wakitunishiana kisuli

Promota waziri rosta baada ya kupromoti ngimi sasa na yeye ataingia ulingoni hivi karibuni kwa kudhaminiwa na kampuni ya kizarendo ya SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION