Tangazo

Pages

Friday, January 29, 2016

BONDIA OMARI KIMWERI KUPANDA TENA UWANJANI FEB 26 AUSTRALIABONDIA mzaliwa wa Tanzania Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatalajia kucheza mpambano wake mwingine  feb 26 akizipiga na  Michael Camellion kutoka Philippines mpambano wa raundi kumi ubingwa wa WBA Pan African light flyweight title  utakaopigwa katika ukumbi wa
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia
 
Kimweri mpaka sasa amepanda uringoni mara 17 tangia aanze kucheza ngumi za kulipwa mwaka 2007 akiwa ameshinda michezo 14 na kupoteza michezo 3
 
bondia huyo mtanzania anaefanya shughuli zake uko amewaomba watanzania kumuombea duwa kwa ajili ya mpambano huo ili afanye vizuri mana akishinda mchezo uho 
 
atakuwa na uwezo wa kupigania ubingwa wa Dunia wa WBA 
 
kwa kuwa maandalizi anayoyafanya kwa sasa ni mazuri na sapoti anayoipata ni nzuri sana 
 
na akishinda mchezo uho itabadilisha maisha ya mchezo wake wa masumbwi na kuwa na kipato kikubwa wakati akipigania mikanda mikubwa inayotambulika Duniani akianzia na mkanda wa WBA ambao ameaidiwa kucheza baada ya kushinda mechi yake hii ya feb 26
 
Kimweri alitoa shukrani za kumsapoti kwa makocha wa Tanzania aliokwisha fanya nao kazi ambapo mpaka sasa anawakumbuka kwa mchango wao mkubwa katika mchezo wa masumbwi ni Baba yake mzazi Idd Kimweri, kaka yake Riadha Kimweri, Habibu Kinyogoli , Rajabu Mhamila 'Super D' 
 
Kocha wa Tanzania Prison Remmy Ngabo,Kameda Antony pamoja na mabondia wa mkoa wa Tanga na Antony Edoa pamoja na kaka zake wote katika mchezo wa masumbwi Twalib Kimweri Mzonge Hassan, Ibrahimu Mashi, na mama zake wote kutoka mkoa wa Tanga 
 
ambao amekuwa chachu katika mchezo wa ngumi mpaka amefikia hatua ya kuwa hapo alipofikia na ata kama anaishi nje ya Tanzania ato sahau asili yake kwa kuwa kitovu chake ndipo kilipozikiwa
 
 
Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto) akimkabidhi vifaa vya mchezo wa masumbwi  kocha wa  Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, mwaka jana walipotembelea nchini

Mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania (kushoto)   kocha   Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam, mwaka jana walipotembelea nchini

MABONDIA KUTWANGANA DAR LIVE MARCH 12

Mabondia Iddi Mnyeke kushoto na Mohamed Kashinde wakiangaliana kwa usongo wakati wa utambuklisho wa mpambano wao utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Iddi Mnyeke kushoto akitunishiana misuli na Mohamed kashinde wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana katika GYM Uhuru viwanja vya basket mpambano utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Iddi Mnyeke kushoto akitunishiana misuli na Mohamed kashinde wakati wa utambulisho wa mpambano wao jana katika GYM Uhuru viwanja vya basket mpambano utakaofanyika march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu

MABONDIA mbalimbali watazitwanga march 12 katika ukumbi wa Dar live mbagala akizungumza mbele ya waandishi wa habari mratibu wa mpambano uho

Rajabu Mhamila 'Super D' amewasainisha mabondia mbalimbali kuzipiga siku hiyo ambapo bondia Ibrahimu Maokola 'Simba wa Mbagala' atazipiga na Joseph Sinkala kutoka Mbeya mpambano wa ubingwa raundi kumi kg 74 utakaosimamiwa na kamisheni ya ngumi za kulipwa 'TPBC'  kinachongozwa na Rais Chaurembo Palasa

aliendelea kwa kusema siku hiyo bondia Iddi Mnyeke kg 61 atamenyana na Mohamed Kashinde wakati Pius Kazaula kutoka Morogoro atakumbana na Karage Suba katika uzito wa kg 66

wakati Shabani Kaoneka atakumbana na Said Seleman mpambano wa raundi sita kg 72 na Ambokile Chusa atavaana na Seleman Galile katika mpambano wa raundi sita kg 74

 pia kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayo sindikiza mpambano uho 

siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed AliMAYWEATHER, PACQUIAO WAKUTANA USO KWA USO NA KUSALIMIANA Pacquiao na Mayweather Mayweather akisalimiana na Manny Pacquiao Mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wameudhihirishia ulimwengu kuwa uhasama uliopo kati yao ni wa ulingoni na sio sehemu nyingine, hiyo ni baada ya kukutana uso kwa uso na kusalimiana kama vile sio mahasimu wakubwa. Mabondia hao wanaoshikilia mataji makubwa ya ndondi, walikutana katika uwanja wa American Airlines usiku wa kuamkia leo(Jan27) wakati wa mchezo kati ya timu ya mpira ya Miami Heat na Milwaukee Bucks katika mchezo uliomaliza kwa Bucks kushinda kwa jumla ya vikapu 109 – 102 dhidi ya Heat. Mbali na mchezo huo, mashabiki na wapenzi wa masumbwi Duniani kote wamekuwa wakisubira kwa hamu mpambano wa wawili hao ambao wamekuwa wakitambiana kwa kipindi kirefu unaotajwa kufanyika mwezi Mei mwaka huu. Watazame hapo chini wakisalimiana Posted by Richard Mwaikenda at Thursday, January 29, 2015 0 comments Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest 2FACE ANASWA NA MCHEPUKO Mwanamuziki wa Nigeria, Innocent Idibia ‘2face’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya picha zinazomuonyesha akifanya mambo ya chumbani na mwanamke mwengine katika klabu yake ya usiku kuzagaa kama njugu kwenye mitandao mbalimbali. 2face na Annie siku ya harusi yao 2face na Annie siku ya harusi yao Kwa mujibu wa tovuti moja ya udaku nchini humo, imedai mwanamke anayeoneka katika picha hiyo ni mama wa watoto wa tatu wa 2face anayeitwa Pero Adeniyi, ambaye amekuwa akipigwa vita mara kwa mara na mke wa ndoa wa mwanamuziki huyo ‘Annie Idibia’ aliyezaa nae watoto wawili wa kike. 2face mwenye umri wa miaka 39, ameamua kuzima soo hilo kwa ku-post picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mke wake katika siku yao ya harusi na kuwataka watu wasipende kuingilia mapenzi yao kwani watakuja kuujua ukweli na utawaweka huru. ”Our love does not have 2 make sense 2 u. pls go on with your perfect life and know the true story behind something before u judge and start making nasty comments based on an orchestrated story by some blog.U shall know the truth and the truth shall set u free.LYTID uwana idibia”,aliandika 2face 2face Idibia 2face na katika mapozi tofauti ya kimahaba na mzazi mwenzie,Pero Adeniyi. Posted by Richard Mwaikenda at Thursday, January 29, 2015 0 comments Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest MAGAZETI YA LEO ALHAMISI . . . . . . . . . . . . . . . DSC08790 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . DSC08804 . . . . DSC08807 . . . DSC08811 . . . . . DSC08810 . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Posted by Richard Mwaikenda at Thursday, January 29, 2015 0 comments Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest Newer Posts Older Posts Home Wanaotembelea Blogu hii Sparkline 2141575 MATOKEO YA KIDATO CHA PILI MATOKEO YA KIDATO CHA PILI BOFYA HAPA KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013 HAYA HAPA Tanzania National Flag Tanzania National Flag Time Dar es Salaam The Digital Company The Digital Company Mtayarishaji: Mtayarishaji: Richard Mwaikenda BONGO HITS Find more music like this on GongaMx Blog Archive

Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin

Monday, January 25, 2016

BONDIA FRANSIC CHEKA ATUA NCHINI NA KUMPIGIA MIKWALA MSERBIA GEARD AJOTOVIC

Bondia Fransic Cheka 'kulia' akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani juu ya maandalizi yake ya mchezo wa ngumi ambapo aliweka kambi nchi ya Zambia kwa wiki mbili kwa ajili ya kumkabili Mserbia Geard Ajetovic
kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 kushoto ni
meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Fransic Cheka 'kulia' akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani juu ya maandalizi yake ya mchezo wa ngumi ambapo aliweka kambi nchi ya Zambia kwa wiki mbili kwa ajili ya kumkabili Mserbia Geard Ajetovic
kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 kushoto ni
meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited Picha na SUPER D BOXING NEWSNa Mwandishi wetu

Dar es Salaam.  Bondia  Francis Cheka amerejea nchini kutoka Zambia na kusema Mserbia Geard Ajetovic aiandae kupokea kipigo kikali katika pambano lao la mabara la uzito wa super middle la  Shirikisho la Masumbwi ya  Kulipwa Duniani (WBF).

Cheka na Ajetovic watapambana kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 katika pambano lililoandaliwa na kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion.

Akizungumza jana, Cheka alimpongeza  meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited kwa kumwezesha kuweka kambi nje ya nchi ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo kwa upande wake.

Alisema kuwa Ndambile na kampuni yake imeonyesha kuwa wanajali na wanamalengo makubwa ya kumwendeleza kutokana na ukweli kuwa amekaa katika kambi ya kisasa yenye mabondia na makocha wazuri nchini Zambia.

“Kwanza naishukuru kampuni ya Advanced Security Limited kwa kufanikisha kambi hii, nimejifua vya kutosha nchini Zambia, mazoezi yalikuwa magumu na yalihitaji uvulivu mkubwa, kwa kutambua lengo langu ni nini, nilifanya kwa juhudu zote na sasa nipo tayari kwa pambano, hata kesho (leo) nipo tayari kwa bondia yoyote duniani,” alisema Cheka.

Alisema kuwa kutokana na siku kuwa nyingi, ataendelea na mazoezi hapa hapa nchini huku akisubiri mipango mengine ya meneja wake kwa upande wa maandalizi.

Meneja wa Cheka, Juma Ndambile ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advanced Security Limited alisema kuwa  lengo la kampuni yao ni kufanya mapinduzi na kuleta maendeleo katika mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini.

Ndambile alisema kuwa Cheka ni bondia mwenye kipaji na hakuwa tayari kuona kipaji hicho kinapotea na kuchukua jukumu la kumwendeleza. “Mimi na kampuni yangu tuna mipango ya kuwamiliki mabondia wengi hapa nchini, kama ilivyo kwa Cheka, nao watapata fursa ya kufanya mazoezi nje ya nchi na kupata mapambano ya kimataifa ya ubingwa ili kuiletea sifa taifa,” alisema Ndambile.

Alisema kuwa wanataka kutumia vizuri fursa waliyopewa na WBF ambayo inamtaka Cheka ashinde pambano hilo ili aweze kuwania ubingwa wa Dunia hapa hapa nchini.


Sunday, January 24, 2016

BONDIA VICENT MBILINYI AENDELEA KUJIFUA NA KUTAFUTA WAPINZANI

VICENT MBILINYI KG 63 TANZANIA 2016

Bondia Vicent Mbilinyi akielekezwa jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi yake yakawaida Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea kujifua baada ya kumchakaza bondia mkongwe wa siku nyingi Deo Njiku sasa anaendelea na mazoezi ya nguvu kwa aji ya kuwasambalatisha mabondia wengine watakaopita mbele yake

bondia huyo mpaka sasa ameshacheza michezo tisa na kushinda 7 kupoteza  na droo 1 ambapo imemuweka katika rekodi nzuri ya mchezo uho kwa mwaka jana

akizungumza na mwandishi wa habari hizo Mbilinyi amesema kwa sasa yupo fiti kucheza na mtu yoyote kwa keshaiva kikamilifu baada ya kupata mazoezi ya aina mbalimbali yanayo mjengea kujiamini katika mchezo wa masumbwi akiwa chini ya kocha wa kimataifa wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D'

aliendelea kwa kusema kuwa nilingia katika ngumi za kulipwa kama najitolea lakini siku zinavyozidi kwenda ndio najijengea mashabiki na kujulikana zaidi katika mchezo niupendao hivyo na ahidi sito waangusha na wala sito lewa sifa wanazonipa nitaendelea kujifua ili niendelee kupambana zaidi katika mchezo

nae kocha anaemnowa bondia huyo Super D amesema kuwa Mbilinyi ana moyo wa kufika mbali hivyo ameonesha nia ya kucheza mchezo uhu katika mazingila magumu hivyo kwa mwaka 2016 ni wake wa kutoka katika mchezo wa ngumi

na naisi katika uzito wake kwa sasa akuna wa kumsumbua kwa sababu amekutana na mabondia wa lika zote ambao wanatamba na waliotamba

Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa sasa anawasimamia mabondia wake akiwemo Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Shabani Kaoneka, Shomari Milundi, Vicent Mbilinyi Mwenyewe na mwanadada Lulu Kayage ambao wote wapo chini ya Super D Boxing Promotio ambayo kazi yake kubwa ni kuwafundisha na kuwatafutia mipambano mbalimbali  ya nje na ndani

MABONDIA ABDALLAH PAZI NA GORGER DIMOSO WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 BAGAMOYO MKOA WA PWANI

Bondia Georger Dimoso kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi baada ya kutia saini za makubaliano ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa tasuba Bagamoyo mkoa wa pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Geoger Dimoso akisaini mkataba wa kuzipiga na Abdallah Pazi wa pili kushoto kulia ni mlatibu wa mpambano huo Pembe Ndava na kushoto ni kocha Mbaruku Heri

Mabondia Georger Dimoso kushoto akitunishiana misuli na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani katikati ni mratibu wa mpambano uho Pembe Ndava Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Abdallah Pazzi na Gerger Dimoso wamesaini mkataba wa kuzipiga Bagamoyo mkoa wa Pwani March 5 katika uzito wa kg 74

akizungumza wakati wa kutiliana saini Promota wa mpambano uho Muhusin Sharif amesema kuwa wameamua kupeleka mpambano uho Bagamoyo kwa ajili ya wakazi wa mkoa wa pwani wapate burudani ya masumbwi siku hiyo

aliongeza kwa kusema kuwa anaomba makampuni mbalimbali kutoa sapoti kwa ajili ya udhamini wa mapambano hayo kwa kuwa Bagamoyo mchezo huo unapendwa na ndio unachipukia hivyo anaomba sapoti kwa makampuni na taasisi mbalimbali kusaidia mchezo uho ili uendelee kukua hapa nchini

ambapo kwa Bagamoyo atuna jukwaa 'ring' la ngumi ata moja mpaka tukodishe kutoka Dar es salaam yaje hapa ndio vijana wapate kucheza hivyo naomba wadau mbalimbali wajitokeze kuchangia upatikanaji wa jukwaa hiro kwa ajili ya mchezo wa ngumi ili zisonge mbele

siku hiyo mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia Sadiq Momba atakumbana na Baina Mazola katika uzito wa kg 59 na Adam Yahaya atakumbana na Selemani Bagaiza katika uzito wa kg 49 na Juma Khan atapambana na Bruno Vivuaviwili na Abdallah Zamba atakumbana na Twalibu Tuwa

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha


Wednesday, January 20, 2016

MABONDIA SADIQ MOMBA NA BAINA M,AZOLA WASAINI KUZIPIGA MARCH 5 TASUBA BAGAMOYO

Mabondia Sadiq Momba kushoto wakitambiana na Baina Mazola baada ya kutia saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa pwani katikati ni promota Muhusin Sharif Picha na SUPER D BOXING NEWS

Promota wa mchezo wa masumbwi Muhusin Shsharif katikati akiwa pamoja na mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola mara baada ya mabondia hawo kutiliana saini ya kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS
KIONGOZI TOKA SHIRIKISHO LA MASUMBWI PST PEMBE NDAVA KATIKATI AKISAINI MKATABA WA KUKUBALI KUPIGANA BONDIA BAINA MAZOLA KUSHOTO NA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU


Promota wa masumbwi nchini Muhusini Sharif Katyikati akiwainuwa mikono juu mabondia Sadiq Momba kushoto na Baina Mazola wakati wa kutambulisha mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo mkoa wa Pwani Picha na SUPER D BOXING NEWS
BONDIA SADIQ MOBA AKITIA SAIN YA KUZIPIGA NA BAINA MAZOLA MARCH 5 KATIKA UKUMBI WA TASUBA BAGAMOYO MKOA WA PWANI WANAOSHUDIA KULIA NI PROMOTA MUHUSINI SHARIFU NA KIONGOZI TOKA SHIRIKISHO LA MASUMBWI PST PEMBE NDAVA

Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Sadiq Momba na Baina Mazola jana wamesaini mkataba wa kuzipiga march 5 katika ukumbi wa Tasuba Bagamoyo Mkoa wa Pwani uzito kwa kg 59
akizungumza wakati wa kutiliana saini kwa ajili ya mpambano huo promota Muhusini Sharif amesema ameamua kuwapambanisha mabondia hawo wanaotamba kwa sasa kwenye uzito uho kwa ajili ya kuleta chachu ya mchezo wa ngumi nchini

unajua Sadiq Momba ni bondia maarufu ambaye anakwenda sana nje ya nchi kwa ajili ya mapambano mbali mbali na amekuwa anafanya vizuri awapo nje ata hivyo mpambano wake wa mwisho nchini Thailand amepigwa kwa T.K.O ya raundi ya tatu na kurudi nyumbani hivyo anacho itaji ni ushindi na kupigana na mtu mwenye point za kutosha kumrudisha kileleni

na Baina Mazola katika uzito wake yeye  ni namba tatu katika boxrec nchini hivyo nae anataka kuwa zaidi ya bondia Momba na ndio anatishia amani katika uzito uho kwa sasa

nae bondia Momba amesema baada ya kupoteza mpambano wake nje ya nchi sasa wadogo zake wanamtaka kucheza nae kwani inaonekana kiwango changu kimepungua na kudiliki watoto wadogo kunitaka mimi ata ivyo nashukuru uhu mchezo mimi ni kazi yangu naitegemea ivyo nitaakikisha simpi nafasi ata chembe kwa kumpiga kipigo kibaya sana ambacho ajawai kupigwa tanga aanze mchezo wa masumbwi nchini 

nae bondia Mazola amesema kwa sasa yupo vizuri sana na anawaomba mashabiki zake kuwa na moli ya kwenda bagamoyo ambapo promota kafanya vizuri sana klupereka mpambao huu uko sisi mabondia wote wawili tuna umarufu mkubwa sana maeneo ya manzese na vitongoji vyake ata hivyo nita akikisha nampiga Momba kama begi kwa kuwa sasa ana jipya nimeona stail zake zote anazotumia kupigana sijaona jipya hivyo ajiandae kwa kipigo tu

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi

pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Monday, January 11, 2016

MCHUMIATUMBO ASAINI KUPIGANA NA BENK MWAKALEBELA JANUARY 30

Bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto akipokea mkataba alio saini kutoka kwa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kwa ajili ya kupambana na Benk Mwakalebela wa Mbeya Picha na SUPER D BOXING NEWS


 Na Mwandishi Wetu

BONDIA Alphonce Mchumiatumbo amesaini mkataba wa kuzipiga na Benki Mwakalebelajanuary 30 katika ukumbi wa sativa Kyela Mbeya mpambano uho wa raundi nane wa uzito wa juu utafanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa uho

akisaini mkataba uho mbele ya Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa amesema ata akikisha kuwa mabondia wa uzito wa juu wanakuwa juu zaidi kwa mapambano hayo katika uzito uho

Mchumiatumbo alisema kuwa kwa sasa yupo katika mazoezi mazito chini ya kocha wake
Juma Urungu 'Mkebezi' 


ambapo kwa siku amekuwa akifanya mazoezi mara mbili au tatu kwa ajili ya kujiandaa na mpambano uho

nae Rais wa  TPBC Chaurembo Palasa ameongeza kwa kusema chama chao kimejizatiti kuinua mchezo wa ngumi kwa kufata taratibu na sheria za mchezo uho wa masumbwi nchini

kwanza wata akikisha kila bondia anapima afya na uzito wake kwa usalama wa mabondia wenyewe na usalama wao wawapo mchezoni

aliongeza kwa kusema kuwa watapima afya siku tano kabla ya mpambano huo ili kujilidhisha na afya za mabondia hawo wenye uzito wa juu nchini ambapo mabondia hawo wamekuwa adimu sana hapa nchini

BONDIA MCHUMIATUMBO KUMKABILI BENK MWAKALEBELA JANUARY 30 KYELA MBEYA

Bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto akipokea mkataba alio saini kutoka kwa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kwa ajili ya kupambana na Benk Mwakalebela wa Mbeya Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Alphonce Mchumiatumbo kulia akisoma mkataba wake na kocha wake Juma Urungu 'Mkebezi'

Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kulia akizungumza na promota juu ya mpambano wa Alphonce Mchumiatumbo katikati

Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC), Chaurembo Palasa kulia akimpatia kiasi cha fedha bondia Alphonce Mchumiatumbo kushoto ni

Bondia Alphonce Mchumiatumbo akisaini mkataba wa kupambana na Benki Mwakalebela January 30Friday, January 8, 2016

MABONDIA KAONEKA NA MAPAMBANO KUZICHAPA FEB 14 TANDIKA

Mabondia Shabani Kaoneka kushoto akitunishiana misuli na Imani Mapambano baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kupambana feb 14 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe katikati ni mdau wa mchezo wa masumbwi Zahoro Maganga 'Super Diego'  picha na SUPER D BOXING NEWS
Mdau wa mchezo wa masumbwi nchini Zahoro Maganga 'Super Diego'  kushoto akimsainisha bondia Shabani Kaoneka kwa ajili ya mpambano wake na Imani Mapambano feb 14 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe kulia ni Rais wa TPBO Yassin Abdallah
picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu
Mabondia Shabani Kaoneka na Imani Mapambano wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya feb 14  uzito wa kg 74 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe

mpambano huo wa raundi nane utasimamiwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa TPBO chini ya rais wake Yassin Abdallah 'ostadhi' mpambano huo wenye kugombaniwa kwa kila mmoja kuwa juu ya mwenzie ambapo bondia Kaoneka ni namba 11 katika viwango vya ubora nchini ambapo amepigana mapambano 13 akishinda 5 kupigwa 5 na sale 3

 atakuwa na kibarua kizito cha ku lilia namba yake kwa mtu wa chini yake Imani Mapambano anaeshikilia nafasi ya 12 ya ubora kwa mabondia wa Tanzania akiwa amecheza mapambano 7 akishinda 4 na kupoteza 3

katika mpambano mwingine utawakutanisha mabondia Hassan Mwakinyo atakae pambana na Salumu Salumu kg 72 katika mpambano wa raundi sita 


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

Sunday, January 3, 2016

CHEKA KUPANDA URINGONI FEB 23 DAR ES SALAAM

Promota Juma Msangi kushoto akitambulisha mpambano wa bondia Fransic Cheka atakaepambana na Geard Ajetovic wa Serbia mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana mpambano utakaofanyika feb 27 katika uwanja wa leaders club wengine ni Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' pamoja na Meneja msaidizi wa bondia  Faransic Cheka  Picha na Picha na SUPER D BOXING NEWS
Promota Juma Msangi kushoto akitambulisha mpambano wa bondia Fransic Cheka atakaepambana na Geard Ajetovic wa Serbia mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam jana mpambano utakaofanyika feb 27 katika uwanja wa leaders club wengine ni Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' pamoja na Meneja msaidizi wa bondia  Faransic Cheka  Picha na Picha na SUPER D BOXING NEWS
 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Saturday, January 2, 2016

MABONDIA WATIFUANA KATIKAS KUFUNGUA MWAKA

Mabondia Shedrack Ignas kushoto akipambana na Abdallah Luwanje wakati wa mpambano wa kufungulia mwaka uliofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese Luwanje alishinda kwa point katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Abdallah Luwanje akinyooshwa mkono kuashilia ushindi

Bondia Hassani Mgos kushoto akipambana na Hassani Kitango wakati wa mpambano wao Kitango alishinda kwa point katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Hassan Kitango akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi

Mohamed Kashinde akipambana na Mwinyi Mzengela masbondioa hawo walitoka droo

matokeo ni drooo


Hussein Mbonde akipambana na Shomari milundi katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Hussein Mbonde akipambana na Shomari milundi katika mpambano uho wa kufungulia mwaka 2016 Picha na SUPER D BOXING NEWS

MABONDIA KUNYUKANA LEO MANZESE FRENDS CORNER

Mabondia Mwinyi Mzengela akitunishiana misuli na Mohamed Kashinde  baada ya kupima uzito jana kwa ajili ya mpambano wao wa leo litakalofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese leo jumanmosi ya january 2 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Shomari Milundi akipima uzito kwa ajili ya mpambano wa leo kushoto ni mpinzani wake Hussein Mbonde mpambano wao wa leo litakalofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese leo jumanmosi ya january 2 Picha na SUPER D BOXING NEWS