Tangazo

Pages

Tuesday, December 15, 2020

SUPER D AMSAINISHA BONDIA HAMISI MAYA KUZIPIGA NA MMISRI FEB 14 SABA SABA HALL

Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiwa na bondia Hamisi Maya baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga 14 february 2021 katika ukumbi wa Saba saba Hall uliopo katika viwanja vya maonesha Saba saba Maya atacheza na Ahmed Hendy kutoka Egypt

Bondia Hamisi Maya kulia akisaini mkataba wa kuzipiga na Ahmd Hendy kutoka Egpty mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa sabasaba hall uliopo katika viwanja vya maonesho ya biashara Saba Saba kushoto ni promota wa mpambano huo Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka katika kampuni ya Super D Boxing Promotion

 Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wa pili kushoto akibadilishana mkataba na bondia Hamisi Maya baada ya usaini mkataba uho kushoto ni kocha wa Maya              Salum LusasiNa Mwandishi Wetu


PROMOTA wa mchezo wa masumbwi nchni Rajabu Mhamila 'Super D' amemsainisha bondia Hamisi Maya kwa ajili ya kuzipiga na Ahmed Hendy kutoka Egyty mpambano wa raundi 8 utakaofanyika katika ukumbi wa saba saba hall uliopo katika viwanja vya maonesha vya sabasaba


akizungumza mara baada ya kutiliana saini katika mkataba wa kuzipiga promota Super D amesema kuwa Maya ni bondia bora mchini ambapo mwaka jana alinyakuwa ubingwa wa mabara wa GBC aliounyakuwa nchini Ujerumani


na kufanikiwa kurudi na ubingwa uho hata hivyo mpaka sasa ajautetea hivyo kampuni ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion tumeamua sasa kumuinua kwa kumuandalia mpambano wa kimataifa hapa hapa nyumbani ili aoneshe uwezo wake na kipaji alicho nacho

hili apate kukionesha mbele ya jamii bondia huyo bingwa wa Ulaya atazipiga nchini kwake mara ya kwanza baada ya kunyakuwa ubingwa uho


nae Maya ameshukuru kwa kampuni ya Super D Boxing Promotion kumsainisha kwa ajili ya mpambano wake mwingine wa kimataifa utakaofanyika hapa nchini 


hivyo naomba mashabiki wangu waje kwa wingi ili niwaoneshe radha ya mchezo wa masumbwi walio ikosa kwa muda mrefu sasa nitacheza kwa kujivunia kwa kuwa nitakuwa katika uwanja wa nyumbambani alisema Maya