Tangazo

Pages

Sunday, April 29, 2012

CHEKA ALIVYOMGALAGAZA MAUGO BILA HURUMA


MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA MPAMBANO WA CHEKA NA MAUGO

 Baadhi ya Maraisi wa vyama vya mchezo wa Masumbwi Nchini wakiangalia mchezo wa Mada Maugo na Francis Cheka ubingwa wa IBF AFRIKA kutoka kushoto ni Rais wa TPBO,Onesmo Ngowi wa TPBC pamoja na Emanuel Mlundwa wa PSTwww.superdboxingcoach,blogspot.com

 Ibrahimu Maokola kulia akipambana na Saidi Mbelwa Maokola alishinda kwa Point.Picha na www.superdboxingcoach,blwww.superdboxingcoach,blogspot.comogspot.com

Baadhi ya Marefarii kutoka Nnje ya nchi wakisubili kuchezasha mpambano wa ubingwa wa IBF Arika kati ya Mada Maugo na Francis Cheka jana.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya mashabiki waliokuwa wamekaa katika VIP wakiangalia mpambano
Mada maugo kushoto na Francis Cheka wakioneshana umwamba wa kutupiana masumbwiwww.superdboxingcoach,blogspot.com

Cheka akipiga ngumi bila mafanikio uku mada akiludi nyuma kujiami.www.superdboxingcoach,blogspot.com
Meya wa Manspaa ya Ilala Jery Slaa akimkabidhi funguo ya gari bondia Francis Cheka baada ya kuibuka na ubingwa wa k.o raundi ya 6 jana.www.superdboxingcoach,blogspot.com

CHEKA AGALAGAZA MAUGO


 

MAUGO ADUNDWA NA CHEKA


BONDIA Francis Cheka ‘SMG’ kutoka Morogoro, kwa mara ya tatu mfululizo Jana Usiku amempiga mpinzani wake Mada Maugo kwa Technical Knockout (TKO) raundi ya saba katika pambano lililokuwa la raundi 12, kwenye ukumbi wa PTA, Saba Saba, Dar es Salaam.
Maugo baada ya kupigwa ngumi nyingi katika raundi tatu mfululizo, kiasi cha kutabiriwa kukaa chini wakati wowote, mwanzoni mwa raundi ya saba hakurejea ulingoni.
Msaidizi wake, Karama Nyilawila alitupa taulo ulingoni akisema bondia wake hataendelea na pambano.
Refa John Shipanuka kutoka Zambia aliyelimudu pambano hilo, alimuinua mkono Cheka kumtangaza mshindi kwa TKO raundi ya saba.
Baada ya hapo, Maugo aliinuka kwenye kona yake na kwenda kumkumbatia Cheka na kocha wake, akisema kwamba amesalimu amri baada ya kuishiwa pumzi.
“Pumzi imekata, siwezi kuendelea,”alisema Maugo ambaye leo alionekana muungwana ingawa hakuwa tayari kusema atahitaji pambano la nne au la.
Akiwa mwenye furaha, Cheka alisema kwamba anamshukuru Mungu amemuwezesha kuendeleza ubabe wake kwa mabondia wa Tanzania na sasa anageuzia makali yake kwa Japhet Kaseba ambaye naye ameomba pambano la marudiano.
Katika pambano la jana, refa Shipanuka alimdhibitu Maugo mwenye desturi ya kuwakumbatia wapinzani wake ili kukwepa kupigwa na pia kupumzikia kwenye miili yao.
Kila alipokuwa akimkumbatia Cheka, Shipanuka alikuwa akifika na kuwaachanisha na kufanya mabondia hao watumie muda mwingi kupigana.
Pamoja na hayo, Maugo alilianza pambano hilo vizuri na katika raundi ya pili almanusra ashinde kwa Knockout (KO) baada ya kumkalisha mpinzani wake kwa ngumi kali.
Lakini SMG aliinuka na kuendelea na pambano, ingawa limchukua hadi raundi ya nne kuanza kuutawala mchezo.
Raundi ya kwanza hadi ya tatu, Maugo alifanya vizuri, lakini baada ya hapo mambo yalikuwa magumu na tangu hapo wengi walijua angepigwa wakati wowote.
Katika  mapambano ya utangulizi, mdogo wake Cheka, Cosmass Cheka alipigwa kwa pointi na Sadiki Momba katika pambano la uzito wa Light, wakati Hajji Juma alimpiga kwa pointi Emmilio Naffat uzito wa bantam.
Simba Watunduru alimpiga kwa KO raundi ya sita Mohamed Kashinde katika pambano la uzito wa Feather, wakati Amos Mwamakala alimpiga kwa pointi Said Muhiddin uzito wa Light.

CHEKA ‘AMPOLA’ GARI MAUGO AENDA KULIACHA POLISI Gari la Cheka likiwa Kituoa cha Polisi Magomeni baada ya kupata ajali jana usiku.
***************************
*Furaha ya ushindi wa Cheka kumchapa maugo yaishia kituo cha Polisi
*Alala Oysterbay Polisi adhaminiwa leo
 BAADA ya Bondia mahiri  Francis Cheka kuibuka na ushindi mnono wa TKO dhidi ya mpinzani wake Mada maugo na kukabidhiwa mkanda wa ubingwa wa Afrika Mashariki IBF na Gari lenye thamani ya Sh. Milioni 8, katika pambano lao lililofanyika jana usiku katika Ukumbi wa PTA, furaha ya bondia huyo iliishia mikononi mwa Polisi.
Ikiwa ni siku moja tu baada ya kuvishwa taji la ubingwa huo na kukabidhiwa mchuma wake, Cheka alikamatwa na Polisi masaa machache tu baada ya kukabidhiwa gari na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake ambayo iliishia mitaa ya Manzese baada ya kupata ajali kwa kugonga Pikipiki na kuwajeruhi dereva wa pikipiki hiyo na abiria wake ambao walikimbizwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu.
Pikipiki iliyogongana na gari la Cheka
Leo asubuhi baada ya kupata taarifa ya tukio hilo mtandao huu wa  ulifanya jitihada za kupata dondoo za tukio hilo na kufika Kituo cha Polisi Oysterbay ambako alikuwa ameshikiliwa Bondia huyo na kupata taarifa kuwa muda mchache tu uliopita kabla ya kuwasili mahala hapo aliondoka akiwa ameongozana na nduguze baada ya kupata dhamana.
Baada ya kupishana na bondia huyo mtandao ulitinga Kituo cha Polisi Magomeni na kufanikiwa kuliona gari hilo likiwa limeharibika na kuvunjika kioo huku Pikipiki hiyo iliyogongwa yenye namba za usajiri T507 BYR, ikiwa mahala hapo.
Akizungumza na Mtandao huu kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea jana usiku majira ya saa nane maeneo ya Manzese na kuwajeruhi dereva na abiria wake waliokuwa katika pikipiki hiyo.
Aidha Kenyela, alisema kuwa baada ya ajali hiyo Dereva wa gari hilo lenye namba za usajiri T 321 AAU, aliyefahamika kwa jina la Francis Cheka, alifikishwa kituo cha Polisi Oysterbay na kushikiliwa hadi asubuhi ya leo walipofika ndugu zake na kumuwekea dhamana.
Akielezea tukio hilo Kenyela, alisema kuwa Gari la Cheka lilikuwa likitokea maeneo ya Manzese kuelekea Ubungo na Pikipiki ikitokea Ubungo kuelekea Manzese na walipofika maeneo ya Tip Top Manzese, dereva wa pikipiki aliutan na kuhamia barabara ya pili ili kuelekea Ubungo na kugongana na gari hilo.
Aidha alisema kuwa dereva huyo wa pikipiki bado amelazwa katika Hospitali ya Mwananyamala akiendelea na matibabu huku abiria wake akitibiwa usiku wa jana na kuruhusiwa.
 Kenyela aliwataka madereva wa pikipiki kufuata na kuheshimu sheria za usalama Barabarani ili kuepuka ajali za kizembe za kila siku zinazokatisha maisha yao.HABARI NA PICHA KWA HISANI YA www.sufianimafoto.blogspot.com,
You might also like:

Friday, April 27, 2012

NANI KUIBUKA MBABE KESHO PTA


 CHEKA AKIWA NA WAPAMBE WAKE
 MADA MAUGO NA CHEKA WAKINYOOSHWA MIKONO JUU NA PROMOTA
 PROMOTA AKIWA NA MABONDIA HAO
Bondia Mada Maugo akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa wa IBF na Francis Cheka kushoto mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba kesho na mshindi atanyakua zawadi ya gari.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MAUGO VS CHEKA WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO KESHONa Mwandishi Wetu
WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wamewapima uzito   na bondia  Mada Maugo  na  Na Francis Cheka wote wamekutwa na KG.
KG.76.5 ambapo mpambano wao utafanyika Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.

Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.

“Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.

--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Thursday, April 26, 2012

FRANSIC CHEKA ASAINI MKATABA WA KUPAMBANA NA JAPHET KASEBA SIKU YA SABASABA Bondia Fransic Cheka kushoto akisaini mkataba wa makubaliano ya kupambana na Japhet Kaseba siku ya sabasaba wanaoshughudia kushoto ni Mshauli wake Oscar George na Promota wa mpambano huo Kaike Silaju .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
f
BONDIA JAPHET KASEBA KATIKATI AKISAINI MKATABA WA KUPAMBANA NA FRANSIC CHEKA

BONDIA FRANSIC CHEKA AKIWA KATIKA POZI

Bondia Fransic Cheka kushoto akisaini mkataba wa makubaliano ya kupambana na Japhet Kaseba siku ya sabasaba Dar es salaam leo wanaoshughudia kushoto ni Mshauli wake Oscar George na Promota wa mpambano huo Kaike Silaju .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

CHEKA VS KASEBA WASINI KUPAMBANA SIKU YA SABASABA

Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro  amesaini mkataba wa kupigana na  bingwa wa kick Boxing. Japhet  Kaseba   katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya sabasaba jijini Dar es Salaam

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Cheka amesema anashukulu kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mchezo wa masumbwi na mabondia wengi wanamtaka   kupigana  na yeye.

Cheka akinia saini picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
;Najua mabondia wa hapa bongo kila mtu anataka kucheza na mimi tu wanajua mimi ndio nalipa kwa soko la bongo na nitahakikisha kila anaekuja mbele yangu namtandika kifupi Tanzania akuna bondia mwenye uwezo zaidi yangu alisema Cheka.Kaseba nilimpiga kwa K.O tareha 3 October 2009 nilimpinga anataka tena wembe kwa ngua ngumi ni sehemu ya maisha yangu siwezi kukataa na mimi ndio napata ridhiki yangu humu hivyo nitahakikisha anaekuja mbele yangu namtwanga tu bila huruma nitaanza na Mada Maugo 28 April na huyo namuweka kama kipolo

kaseba akitia saini picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com  Nae Promota wa mpambano huo Kaike Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam siku ya sabasaba utakuwa ni mpambano ambao aujawai kutokea kwa kuwa mabondia hao wanakubalika na mashabiki wa ndani na nje ya Nchi

Mbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae;

Wednesday, April 25, 2012

CHEKA AJIFUA KUMKABILI MAUGO JUMAMOSI


 kocha wa ngumi Abdallah  Ilamba 'Komando'  akimsimamia
Bondia Francis Cheka kufanya mazoezi ya tumbo Dar es Salaam leo mazoezi hayo ya mwisho kwa ajili ya mpambano wake na Mada Maugo wa kugombea mkanda wa I.B.F pamoja na gari utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba, jumamosi hii

Tuesday, April 24, 2012

Francis Cheka na Japhet Kaseba uso kwa uso siku ya sabasaba


 Bondia Japhert Kaseba wa pili kulia akiangalia mkataba wake Dar es salaam leo  wa kucheza na Francis Cheka mara baada ya kusaini kushoto ni Khalifa Kiumbemoto na promota wa mpambano Kaike Siraju kulia ni Kharifa Kipao.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Japhert Kaseba akisaini mkataba wa kucheza na Francis Cheka siku ya Sabasaba kushoto ni promota Kaike Siraju.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Japhert Kaseba wa pili kulia akiangalia mkataba wake Dar es salaam leo  wa kucheza na Francis Cheka mara baada ya kusaini kushoto ni Khalifa Kiumbemoto na promota wa mpambano Kaike Siraju kulia ni Kharifa Kipao.picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

FRANCIS CHEKA NA JAPHET KASEBA KUPAMBANA TENA SIKU YA SABASABA


Francis Cheka na Japhet Kaseba uso kwa uso siku ya sabasabaNa Mwandishi Wetu

BINGWA wa kick Boxing. Japhet  Kaseba amesaini mkataba wa kucheza na
Bingwa wa dunia wa ndondi mkanda unaomilikiwa na IBC, Francis Cheka wa Morogoro  katika uzani wa KG 75 utakaofanyika siku ya sabasaba jijini Dar es Salaam
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Kaseba amesema anashukulu kupata mpambano huo na atahakikisha anaonesha uwezo wake wote katika mchezo huo kwani yeye ni bingwa wa mapambano

;Najua mabondia wa hapa bongo wananikwepa sana kwa kuwa nimeshakuwa bingwa wa ngumi za mateke lakini awajui mimi ni bingwa katika mapigano yote alisema Kaseba;


Nitahakikisha naweka kambi ya kutosha na kukata ngebe za cheka ni mtoto mdogo sana katika masumbwi kwa kweli bingwa wa kweli ni Rashidi Matumla ambaye ninamuheshimu mpaka sasa cheka kanikimbia mda mrefu tu tangia tupambane 3 October 2009  ambapo alipewa ubingwa kwa kusingizia mshabiki wangu alikuja kumtupa nje ya uwanja kazi yake yeye anarudiana na Mada Maugo kila siku lakini kwa sasa kakanyaga miwaya zamu yake imefika,

Nae Promota wa mpambano huo Kaike Siraju amesema mpambano huo utakaofanyika Dar es salaam siku ya sabasaba utakuwa ni mpambano ambao aujawai kutokea kwa kuwa mabondia hao wanakubalika na mashabiki wa ndani na nje ya Nchi


Mbali na mpambano huo pia kutakua na mapambano ya utangulizi na burudani mbalimbali ambazo mtatangaziwa baadae;

Monday, April 23, 2012

NANI KUONDOKA NA GARI HILI JUMAMOSI MADA AU CHEKA


Na Mwandishi Wetu

WAANDAAJI wa pambano la ubingwa wa IBF kati ya Francis Cheka na Mada Maugo leo wameonesha rasmi gari watakalogombania  Mabondia Mada Maugo Na Francis Cheka  Aprili 28 mwaka huu katika ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.

Pambano hilo linatarajiwa kuwa katika uzito wa kg 75 la raundi 12 la Kimataifa ambapo linatarajiwa kuwa chini ya Kamisheni ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) huku majaji wa pambano hilo wakitegemewa kutoka nje ya nchi.
Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa mpambano huo Yasini Abdallah alisema kuanikwa kwa mkanda huo na Gari kuwekwa Hadharani kutaashiria kupamba moto kwa pambano hilo ambalo linatarajia kuwa katika ngazi ya Kimataifa ili kuweza kupatikana kwa mshindi wa halali na pia itafuta hisia za kuwepo na ubabaishaji katika pambano hilo.

“Tunauanika Gari na mkanda ili kuwathibitishia wadau wa ngumi na mashabiki kwa ujumla kuwa tupo makini na pambano hili na sio la kibabaishaji na kama tulivyosema awali kuwa majaji watoka nje ya nchi na hiyo yote ni kutaka mchezo uchezeshwe kulingana na hadhi ya mkanda,” alisema Kaike.
Alisema, maandalizi kwa ujumla ya pambano hilo yanaendelea vizuri na zawadi ya gari kwa mshindi iko pale pale ambapo mshindi atakabidhiwa siku hio hio ya pambano baada a kutangazwa mshindi na kupewa mkanda itafuatiwa na zawadi hiyo ya gari.
Awali mabondia hao walishakutana mara mbili ulingoni ambapo katika pambano la kwanza lilofanika PTA Cheka alishinda kwa pointi ambapo Maugo hakukubali matokeo hao na kuandaliwa pambano la marudiano lilofanyika Uwanja wa Jamuhuri Morogoro ambapo Cheka aliibuka mshindi tena kwa kumtwanga kwa pointi.
Baada ya kumalizika kwa pambano hilo kila bondia aligoma kucheza na mwenzake tena lakini baada ya kuandaliwa pambano hilo la ubingwa kila mmoja alibadilisha nia na kuamua kurudi ulingoni kuwania mkanda huo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano la Cheka na Maugo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.

--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

GARI LA CHEKA MAUGO ILI HAPA

Msemaji wa Mpambano wa Ngumi kati ya Mada Maugo na Francis Cheka , Yasini Abdallah akionesha mkana na gari atakalopewa mshindi wa mpambano huo
  1. Johannes Lugenge kushoto na Promota wa Mpambano wa Mada Maugo na Francsis Cheka, Lucas Rutainurrwa wakionesha mkana wa Ubingwa wa I.B.F Afrika na gari atakalochukua bingwa wa mchezo huo Dar es salaam

Sunday, April 22, 2012

MWAKILISHI wa Wanawake na Maendeleo ya Vijana, Ajira wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Zuwena Kibena' Mama Kanari Kipingu' ametembelea kambi ya timu ya ngumi ya Taifa
Na MWANDISHI WETU

MWAKILISHI wa Wanawake na Maendeleo ya Vijana, Ajira wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Zuwena Kibena' Mama  Kanari Kipingu' ametembelea kambi ya timu ya ngumi ya Taifa na kuwaasa wawe makini wanapokwenda kwenye michuano ya kufuzu mashindano ya Olimpiki.


Akizungumza na mabondia hao kambini kwao Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani jana,' Mama  Kanari Kipingu' alisema licha ya kwamba  kambi ilikuwa na ugumu wa aina fulani lakini wahakikishe wanarudi na medali kwa watu wote watakaokwenda katika mashindano hayo.

Alisema anajua mabondia wote wapo katika hali nzuri na pia nafasi za kufuzu michuano hiyo ni chache hivyo wanatakiwa kufanya mazoezi kwa bidii kwani siku zilizobaki ni chache.

"Nimeamua kuja kuwatembelea ili kuwapa hamasa na mjue kama tupo nyuma yenu, lakini sitaondoka bure ninawapa hii sh. 50,000 kwa ajili ya kununulia maji na vitu vingine vidogo vidogo na kwamba bondia atakayerudia na medali ataandaliwa zawadi maalum na BFT," alisema' Mama  Kanari Kipingu'
Alisema kesho jumatatu  watakuwa na kikao ambacho kitajadili ni zawadi gani watakayotoa kwa bondia atakayerudi na medali na pia aliahidi kuisaidia BFT kulipa deni wanalodaiwa na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (AIBA).

Katika hatua nyingine, Zuwena ambaye anaupenda sana mchezo huo, alisema yupo mbioni kutoa tuzo kwa makocha ambao walifanya vizuri katika miaka iliyopita lakini bado mpaka hivi sasa wanauendeleza mchezo huo

MRS KANARI KIPINGU ATEMBELEA KAMBI YA NGUMI KIBAHA NA KUTOA AHADIMWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. Zuwena Kibena ' Mama Kanari Kipingu' katikati akiwa katika picha ya pamoja na mabondia.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
MWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. Zuwena Kibena ' Mama Kanari Kipingu' akikabidhi pesa ya maji  kwa Nahodha wa timu ya Taifa ya masumbwi Selemani Kidunda wachezaji wa timu hiyo jana

MWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. zUWENA Kibena ' Mama Kanari Kipingu' kushoto akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya Masumbwi alipotembelea kambi yao iliypo Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani juzi na kutoa ahadi mbalimbali kwa mabondia hawo.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
MWAKILISHI wanawake maendeleo ya vijana ajira kwa wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT. zUWENA Kibena ' Mama Kanari Kipingu' kushoto akizungumza na wachezaji wa timu ya taifa ya Masumbwi alipotembelea kambi yao iliypo Kibaha Mkuza Mkoa wa Pwani juzi na kutoa ahadi mbalimbali kwa mabondia hawo.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com