Tangazo

Pages

Monday, June 30, 2014

NGUMI ZILIVYOPIGWA MWANANYAMALA NDANI YA MFUNGO WA RAMADHANI



Bondia JuliasKisarawe kushoto akipambana na Patrick Nne wakati wa mchezo wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Kisarawe alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mwinyi Mzengela  kushoto akimtupia konde la kushoto bondia Georege Manywele wakati wa mpambano wao wa kumaliza ubishi uliofanyika katika ukumbi wa CCM Mwijuma Mwananyamala mwishoni mwa wiki iliyopita Mzengela alishinda kwa K,O ya raundi ya nne picha na 
Bondia Josepher Mbowe akipambana na Mfaume Alkaida wakati wa mpambano wao mbowe alishinda katika raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Sunday, June 29, 2014

NGUMI ZILIVYPIGWA MANZESE KATIKA UKUMBI WA KOBELO PUB


Bondia Mohamed Mussa kushoto akipambana na Shomary Punzi wakati wa mchezo wao uliofanyika katika ukumbi wa Kobelo Pub Manzese Dar es salaam Punzi alishinda kwa point Mchezo huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mvukeni, Muhidini Kassimu kulia akimkabizi kiongozi wa mabondia, Ramadhanu Uhadi pesa kwa ajili ya mabondia kununua maji wakati wa mashindano yaliyofanyika katika ukumbi wa Kobelo Pub
Bondia Omary Gumbo kushoto akimrushia konde Japhert Pascar wakati wa mchezo wao uliofanyika katika ukumbi wa Kobelo manzese Gumbo alishinda kwa point mpambano huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mwenyekiti wa Sertikali ya Mtaa wa Mvuleni, Muhidini Kassimu akiwapatia zawadi mabondia Omary Gumbo na Japhert Pascar

Bondia Shomari Punzi kushoto akipambana na Mohamed Mussa wakati wa Mpambano wao Punzi alishinda mpambano huo kwa point picha na
www.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, June 27, 2014

NGUMI KUPIGWA JUMAMOSI PUGU KIRUMBA ZULU PARADAISE


Bondia Jems Martn kushoto akitunishiana misuli na Hamza Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumamosi utakaofanyika katika ukumbi wa Zulu Paradaise uliopo Pugu Kirumba Road Picha na www.superdboxing coach.blogspot.com


Dr, Mohamed Hassani 'Bula' akimpima Afya bondia Twalibu Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano na Adamu Ngange jumamosi hii
Bondia Twalibu Mchanjo akipima uzito

Wednesday, June 25, 2014

NGUMI ZA VUNJA JUNGU KUPIGWA PUGU KILUMBA JUNE 28 UKUMBI WA ZULU PARADIES

Twalibu Mchanjo
MPAMBANO mkali wa masumbwi utafanyika katika ukumbi wa Zulu Paradais siku ya Jyne 28 mpambano uho utakaowakutanisha mabondia machachali na wenye uwezo wa ali ya juu kwa sasa ni kati ya Adamu Ngange atakaepambana na Twalibu Mchanjo mpambano wa raundi nane siku hiyo

mabondia watakaosindikiza mpambano huo kwa kucheza utangulizi ni Mussa Shuza atakaezichapa na Hassani Mgosi na Mohamed Kashinde atapambana na Ally Bugingo wakati Jems Martin ataoneshana umwamba na Hamza Mchanjo

mratibu wa mapambano hayo Said Mbelwa amesema ameamua kuwainua vijana kwa namna moja au nyingine ili nawo waweze kunufaika na mchezo wa masumbwi kwa kucheza na kupata mapato katika michezo watakaocheza na kujiwekea rekodi nzuri katika ngumi

MPAMBANO WA NGUMI KUFANYIKA KOBELO PUB MANZESE JUNI 28

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMIMPAMBANO wa masumbwi utafanyika juni 28 katika ukumbi wa kobelo pub uliopo manzese akizungumzia maandalizi ya mpambano huo Ramadhani Uhadi 'Rama Jah' kuwa yameshakamilika hivyo wanasubili siku ya siku tu ila mambo yawe haharani

mapambano hayo kwa ajili ya kuweka rekodi kwa vijana wanaotamba katika mchezo wa ngumi na wapya ili wawe chachu ya kuinua mchezo huo siku hiyo bondia Inocent Zombi atapambana na Mfaume Master wakati Koba Dodati atacheza na Hassani Mussa na Rashid Lugaira atapambana na Azizi Ally Fadhili Athumani atamkabili All Libaba mpambano mwingine utawakutanisha Amani Juma na Omari Rajabu

mapambano yote hayo yataanza saa kumi na moja jioni kwa kingilio cha 5000, tu

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' AWASHUKURU VIONGOZI WA NGUMI NCHINI


Na Mwandishi wetu

BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amewashukuru viongozi wa ngumi nchini kwa sapoti yao wanayo mpa tangu ahanze ngumi mpaka sasa kwani yeye malengo yake ni k
ufika mbali zaidi baada ya kunyakuwa mkanda wa ubingwa unaotambuliwa na WPBF Africa Welterweight Title 

aliyasema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa DDC Keko kulipokuwa na mkutano mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini cha TPBC ambapo alikutana na viongozi mbalimbali na kupongezwa kwa kunyakuwa mkanda huo wa ubingwa alioupata Zambia kwa kumpiga bondia Mwansa Kabinga kwa TKO ya raundi ya tisa katika uwanja wa Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia

bondia huyo mwenye ndoto za kuwa mmoja wa mabondia watakotamba duniani ambapo mwanzoni mwa mwaka huu aliteuliwa kuwa bondia bora wa mwaka 2013 katika uzito wake tuzo zilizoanza kufanyika mwaka huu

fikra zake kwa sasa ni kuwa bingwa wa mikanda mbalimbali inayotambulika Duniani katika uzito wake fikra zake siku moja ni kupambana katika mapambano makubwa za
idi hususani katika ukumbi wa MGM Gland nchini Marekani

bondia huyo mwenye rekodi ya kushinda mapambano 11 na kupoteza mpambano mmoja wakati ananza mchezo huo

bondia huyo anawashukurujopo la makocha wake wa kambi ya ilala linalo ongozwa na kocha mkongwe wa mchezo huo Habibi Kinyogoli 'Masta',kondo Nassoro,Sakwe Mtulya na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kwa kumsimamia na kumpa ushari anapokuwa ulingoni akipambana

bila kuwasahau mashabiki wake waliojaa kila kona ya jiji la Dar es salaam na Tanzania nzima kwa ujumla

Sunday, June 22, 2014

BONDIA KING CLASS MAWE AONESHA MKANDA WAKE KWA VIONGOZI WA NGUMI WA TPBC PAMOJA NA WADAU MBALIMBALI KWENYE MKUTANO

Mdau wa mchezo wa masumbwi nchini Ally Bakari 'Champion' kulia akimpongeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ambaye ni bingwa wa Afrika anayetambuliwa na chama cha WPBF ambao aliupata ubingwa huo nchini Zambia hivi karibuni  katikati ni Bondia Kassimu Gamboo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mwenyekiti wa mda wa chama cha ngumi za kulipwa nchini TPBC Chaurembo Palasa akizungumza wakati wa kufungua mkutano kwa wadau wa mchezo wa ngumi uliofanyika jumapili katika ukumbi wa DDC Keko wengine kushoto ni Chuku Duso,Habibu Kinyogoli,Hamisi Kimanga na Buchato Michael picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mdau wa mchezo wa masumbwi nchini Ally Bakari 'Champion' kushoto akimpongeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ambaye ni bingwa wa Afrika anayetambuliwa na chama cha WPBF ambao aliupata ubingwa huo nchini Zambia hivi karibuni  kulia ni Mwenyekiti wa TPBC Chaurembo Palasa  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mjumbe Habibu Kinyogoli akizungumza wakati wa mkutano huo
wajumbe mblalimbali wakifatilia mkutano huo leo kutoka kushoto ni Aga Peter,Maneno Osward na Ernest Bujiku
Rais wa PST Emanuel Mlundwa akichangia moja ya mada za mkutano huo
 Mjumbe Ally Bakari akichangia wakati wa mkutano huo
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ' Super D' aliyekaa kulia akiwa na mabondia mbalimbali wakati wa mkutano mkuu wa TPBC

VIONGOZI WAKIPITIA MAKABRASHA MBALIMBALI
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' katikati akiwa na ubingwa wake wa chama cha WPBF Africa alioupata hivi karibuni nchini Zambia wengine kushoto ni Habibu Kinyogoli,Hamisi Kimanga,Chaurembo Palasa na Michael Buchato picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com






Saturday, June 21, 2014

NGUMI ZILIVYOPIGWA ULONGONI A GONGOLAMBOTO




Bondia Said Uwezo kulia akioneshana umwamba na Thobias Adaut wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa swai pub ulongoni 'B'  gongolamboto Uwezo alishinda kwa point mpambano huo wa raundi nne  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ambokile Chusa kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Shujaa Keyakeya wakati wa mpambano wao uliofanyika Ulongoni Gangolamboto Keyakeya alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mbaruku Kheri kushoto akioneshana umwamba na Stevin Mwalitwanga wakati wa mpambano wao kheri alishinda kwa K,O ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Mbaruku Kheri kulia akioneshana umwamba na Stevin Mwalitwanga wakati wa mpambano wao kheri alishinda kwa K,O ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Thursday, June 19, 2014

Dula mbabe kuzipiga vunja jungu


Bondia  machachali wa ngumi za kulipwa nchini Abdallah Paziwapazi  kiroba au kama anavyojulikana na wengi” Dula mbabe’ anategemea kupanda uling
oni tarehe 29/6/2014 katika ukumbi wa ccm mwinjuma-mwananyamala kuzipiga na Hamis Juma ambae amekuwa mbadala wa maneno osward. Mpambano huo ambao utakuwa wa vunja jungu yaani  wa kuikaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani ,kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi yakiwemo mawili ya kumaliza uhasama wa wababe wa kitaa,yaani mbabe wa mwananyamala kwa mama zakaria  Mwinyi mzengera”mambwa”  na mbabe wa mwananyamala kwa kopa George manywele “G-mawe”.nae mbabe wa mwananyamala kisiwani joseph piter “mbowe” atazipiga na zumba kukwe, pia kutakuwa na pambano kali la vijana wanaocheza ngumi zenye uwezo wa hali ya juu Issa Omar Nampepeche”peche boy” atakae zipiga na Ramadhani kumbele katika pambano la raundi nane,hili pambano linategemewa kuwa zuri kutokana na mabondia wote kuwa na spidi kubwa wawapo ulingoni. Ukiachilia na  mapambano haya yenye vibweka pia kutakuwepo na mapambano mengine ya utangulizi kama vile Yule mwimbaji maarufu wa mapacha watatu khareed chokolaa atakapozipiga na daud giligili, chidi  mbishi  atamvaa Ramadhan hamis, dj kulwa atazipiga na alex kado na e masango komakoma ataminyana na Mohamed amir”alkaida”
Mapambano haya yameandaliwa na bigright promotion,chini ya kiongozi wake wake Ibrahim kamwe ambae siku zote amejitahidi kuwa mstari wa mbele kuhakikisha michezo ina kuwa ajira kwa vijana na inachezwa mara kwa mara kuweka ufanisi zaidi. Akizungumza na vyombo vya habari bw Ibrahim kamwe alisema maandalizi kwa kiasi kikubwa yamekamilika na mabondia wapo katika hali nzuri ya ushindani na kuwasihi watu wajitokeze waje kuangalia ngumi za kali zenye ushindani ukizingatia kuwa ukumbi umekarabatiwa na kila mtu atakaa katika kiti chake na ulinzi mkali utakuwepo ili kuboresha mchezo wa ngumi usiwe sehemu ya mchezo wa fujo na kila atakaekuja kwa nia ya kufanya fujo atachukuliwa hatua kali za kisheria mojakwamoja bila kusita

Wednesday, June 18, 2014

NGUMI KUPIGWA ULONGONI B JUNI 21 GONGOLAMBOTO

Bondia Abdallah Mbela kushoto akipangua ngumi ya Said Uwezo wakati wa mazoezi ya kujianda kupambana juni 21 Uwzo atapambana na Thobias Adaut katika ukumbi wa swai pub ulongoni 'B'  gongolamboto
 Bondia Said Uwezo kushoto akifundishwa jinsi ya kutupa makonde na Shujaa Keyakeya wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa kupambana na Thobias Adaut katika ukumbi wa Swai pub ulongoni 'B' gongolamboto picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Abdallah Mbela kushoto akipiga ngumi kwa Said Uwezo wakati wa mazoezi ya kujianda kupambana juni 21 Uwzo atapambana na Thobias Adaut katika ukumbi wa swai pub ulongoni 'B'  gongolamboto picha na Rajabu mhamila

Haye wants comeback fight in Dubai, targeting Klitschko rematch in future

 david haye By Scott Gilfoid: Former WBA heavyweight strap holder David Haye (26-2, 24 KO’s) says he wants one of his comeback fights to take place in Dubai. It’s unclear why he wants the fight to be staged there, but it’s a great place in terms of taxes. There are regions that are tax free, and it would seem like an ideal place to stage a fight for that reason.
Haye hasn’t fought in two years since 2012, and he’s slowly rehabbing his right shoulder that he tore up last year while training for a fight against Tyson Fury. Haye expects his shoulder to be ready by next September for him to fight

Monday, June 16, 2014

MASHABIKI WATAKA MPAMBANO KATI YA SAUL ALVAREZ NA MIGUEL COTTO

Baada ya mapambano yao ya mwisho kushinda kila mmoja tena kwa k,o kila mmoja sasa mabondia hawo kukutanishwa hivi punde

Saturday, June 14, 2014

PICHA ZA MAZIKO YA BONDIA MAREHEMU IRAQ HUDU KIMBUNGA 'MKUMWENA' ALIVYO



Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Iraq Hudu 'Mkumwena' wakipeleka mwili kuzika katika makaburi ya Kisutu Dar es salaam kwa ajili ya kumuhifadhi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya waombelezaji wakitia udongo katika kaburi la marehemu Iraq Hudu wakati wa maziko yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kisutu Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya waombelezaji na mabondia wakiwa nyumbani kwa marehemu Iraq Hudu kutoka kushoto ni bondia Adwer George, Rashidi Matumla, Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini Yasini Abdallah na Mwenyekiti wa Shiwata Cassim Twalibu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mtoto wa Marehemu Iraq Hudu, Daniel Hudu  kushoto akisalimiana mabondia Adrwe George,Rashidi Matumla na Rais wa TPBO Yassin Abdallah
Mtoto wa Marehemu Iraq Hudu, Daniel Hudu  kushoto akisalimiana mabondia Adrwe George,Rashidi Matumla na Rais wa TPBO Yassin Abdallah
Mashekhe wakisoma duwa kabla ya kwenda kuzika
Meneja wa bendi ya msondo ngoma Said Kibiriti akisalimiana na mabondia
Baadhi ya waombelezaji waliojitokeza
Mtangazaji Maulid Baraka Kitenge akizungumza na mabondia mbalimbali wakati wa msiba wa bondia Iraq Hudu
Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Maulid Baraka Kitenge akisalimiana na bondia mkongwe ambaye kwa sasa ni kocha wa MKoa wa Tanga katika wilaya ya Muheza Chales Muhilu 'Spins'
Bondia Marehemu Iraq Hudu 'Kimbunga' kulia enzi za uhai wake katikati ni marehemu bondia Papa Upanga
Bondia Iraq Hudu' Kimbunga kulia akipambana na Stanley Mabesi katika mpambano wao
IRAQ HUDU
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU
Mmoja wa waombelezaji kulia akimpa pole bondia Chuku Duso katika msiba wa bondia Iraq Hudu
Ibrahimu Kamwe na Said Chaku
wadau mbalimbali wa mchezo wa ngumi
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU


WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KWENYE KABURI LA MAREHEMU IRAQ HUDU
WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KATIKA KABURI LA IRAQ HUDU
WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KATIKA KABURI LA IRAQ HUDU PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com

ZIKWA KATIKA MAKABURI YA KISUTU