Tangazo

Pages

Tuesday, June 3, 2014

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' HAPATA LESENI YA BOXING


 Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi' kushoto akimkabidhi leseni ya ngumi bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ambayo anaweza kutumiha Dunia nzima kwa ajili ya kutambulika kitaifa na kimataifa ambayo inaweka rekodi mbalimbali za bondia pindi anapocheza mchezo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini T.P.B.O Yassin Abdalla 'Ostadhi' kushoto akimkabidhi leseni ya ngumi pamoja na kitambulisho na nyaraka mbalimbali za bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kwa ajili ya shughuli zake lesini hiyo inayotumika kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kuhifadhia kumbukumbu mbalimbali za michezo aliyo shiliki hafla ya makabidhiano hayo zimefanyika katika ofisi ya ngumi za kulipwa nchini jana  Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto  akiwa na nyaraka mbalimbali alizo kabidhiwa na Rais wa TPBO Yassini Abdallah
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto  akiwa na nyaraka mbalimbali alizo kabidhiwa

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' amekabidhiwa leseni kwa ajili ya ngumi pamoja na kitambulisho na nyaraka mbalimbali za kumtambua kitaifa na kimataifa 

akizungumza wakati wa utoaji wa leseni kwa bondia huyo Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini Yassini Abdalla 'Ostadhi' amesema leseni ni jambo la muhimu sana kuwa nayo bondia kitu ambacho kila bondia anatakiwa kuwa nayo ambapo ndio hinaweka kumbukumbu yako ya mapambano yako yote uliocheza ndani na nje ya nchi kitaifa na kimataifa 

hivyo ni kitu muhimu sana leo hii natoa leseni kwa bondia Class kwa kuwa natambua kazi yake na uwezo wake akiwa katika uringo ambapo itamsaidia kwa ajili ya kazi yake kumbuka hii ni ajira hapa kajiajiri mwenyewe' mtaji wa masikini nui nguvu zake mwenyewe'

nae bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' alishukulu kwa kusema leseni itamuongezea chachu ya kupigana vizuri zaidi awapo uringoni kwani ngumi ndio mchezo anao upenda na ndio anaucheza hivyo atafanya jitiada ili aweze kufika mbali kupitia mchezo wa ngumi

bondia huyo anaenolewa na jopo la makocha kutoka kambi ya Ilala likiongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta'  Kondo Nassoro, Sako Mtulya na Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye ana msimamia katika mapambano yake mbalimbali na kumpatia ushauri  wa jinsi gani ya kupigana na watu anaokabiliana nao awapo uringoni

No comments:

Post a Comment