Tangazo

Pages

Tuesday, July 24, 2018

MABONDIA WA KIKE KUZITWANGA SIKU YA NANE NANE DAR LIVE MBAGALA

Mabondia wa kike Maimuna Hashimu kushoto akitunishiana misuli na Happy Daudi mara baada ya kusaini makataba wa makubaliano wa kuzipiga siku ya tarehe nane mwezi wa 8 sikukuu ya nanenane katika ukumbi wa Dar Live uliopo mbagala Dara es salaam wakisindikiza mpambano wa Said Mbelwa 'Moto wa Gesi' na Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' siku hiyo Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

PROMOTA wa ngumi za kulipwa Zahoro Maganga amewasainisha mabondia wa kike Maimuna Hashimu pamoja na Happy Daudi kuzipiga siku ya sikkuu ya nane nae katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam

Maganga amesema kuwa ameamuwa kuwa sapoti wanawake kwa kuwa wanafanya sana mazoezi kwa mda mrefu na wapo wachache katika mchezo uho hivyo ameamuwa kuwachezesha siku hiyo ili kuinua ngumi za wanawake nchini

haidha siku hiyo kutakuwa na mapambano mengi ya kukata na shoka likiwa lile linalo subiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini ni kati ya Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi' na Abdalla Pazi' Dula Mbabe' watakaozipiga siku hiyo

na Shomari Milundi atazipiga na Ramadhani Migwede  wakati Shabani Kaoneka ataonesheana umwamba na Paul Kamata siku hiyo mbali ya mchezo wa masumbwi kutakuwa na burudani mbalimbali za michezo

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo zilizo tahalishwa na kocha mahiri katika mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D'  ndani yake pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi zilizopiganwa nchini 

Friday, July 13, 2018

MABONDIA SHOMARI MILUNDI RAMADHANI MIGWEDE WASAINI KUZIPIGA DAR LIVE SIKU YA NANENANE

Promota wa mpambano wa ngumi Zahoro Maganga katikati akiwanuwa mikono juu kuwatambulisha mabondia Ramadhani Migwede 'kushoto' na Shomari Milundi kulia kwa ajili ya mpambano wao wa agost 8 utakaofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Ramadhani Migwede Kushoto akitunishiana misuli na Sgomari Milundi baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Agost 8 katika ukumbi wa Dar Live Mbagala katikati ni Promota wa mpambano uho Zahoro Maganga Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Sgomari Milundi akisaini mkataba kwa ajili ya kuzipiga na Ramadhani Migwede siku ya nane nane Mabondia atika  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ramadhani Migwede akisaini mkaraba wa kuzipiga na Shomari Milundi siku ya nanenane katika ukumbi wa Dar Live Mbagala  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA  Shomari Milundi na Ramadhani Migwede wamesaini kuzipiga Agost 8 katika ukumbi wa Dar live Mbagala mpambano wa raundi sita mabondia hawo wenye mashabiki lukuki watapanda ulingoni kusindikiza mpambano wa mahasimu wawili litakalopigwa siku hiyo

watakutana bondia Abdallah Pazi 'Dulla Mbabe' na Saidi Mbelwa 'Moto wa Gesi' watazipiga kwa raundi kumi zisizo na ubingwa
 mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi pamoja na burudani mbalimbali zitakazo kuwepo siku hiyo

akizungumza kuhusu mpambano huo Promota Zahoro Maganga amesema siku hiyo kutakuwa na burudani za kutosha hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuja kushidia mpambano uho uliokuwa unasubiliwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa mchezo wa ngumi

ujue mabondia hawa walikuwa wakitafutana mda mrefu na walitaka kupigana ila mpambano wao aujafanyika sasa mimi nikamuwa kuwakutanisha ili wazipige kwa ajili ya kujua nani zaidi katika mpambano wa masumbwi alisema Maganga;

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd

Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani