Tangazo

Pages

Thursday, January 30, 2014

SUPER D AMPONGEZA BONDIA MUSSA MCHOMANGA NA KUMZAWADIA

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi clip bandeji na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa bondia Mussa Mchopanga baada ya kumdunda Anton Idoa kwa K,o ya raundi ya pili bondia huyo ndie bingwa kwa sasa wa mkoa wa Dar ers salaam na anajiandaa na mashindano ya Majiji yatakayofanyika katikati ya mwaka huu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Anton Idoa akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mussa mchopanga wakati wa mashindano ya Mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Panandi panandi Ilala Mchopanga alishinda raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Anton Idoa kushoto akirusha konde ambalo alijareta madhala kwa mpinzani wake ambae anamwangalia Mussa Mchopanga wakati wa Mashindano ya Mkoa wa Dar es salaam Mchopanga alishinda kwa K,O ya raundi ya pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Kocha Mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kushoto akimwinua mkono juu bondia Mussa Mchopanga baada ya kumvalisha medali ya Dhaabu baada ya kuibuka mshindi wa mkoa wa Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi clip bandeji na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa bondia Mussa Mchopanga baada ya kumdunda Anton Idoa kwa K,o ya raundi ya pili bondia huyo ndie bingwa kwa sasa wa mkoa wa Dar ers salaam na anajiandaa na mashindano ya Majiji yatakayofanyika katikati ya mwaka huu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.comKocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi cheti kwa bondia Mohamed Chibumbuli mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi cheti kwa bondia Mohamed Chibumbuli mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimvisha medali ya dhaabu bondia Mohamed Chibumbuli mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimvisha medali ya Fedha bondia Abdul Rashidi  mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Wednesday, January 29, 2014

KING CLASS MAWE ASAINI MKATABA WA KUPAMBANA NA CHEKA FEB 8 PTA SABASABA


BONDIA bora wa mwaka 2013,2014 katika uzito wa  KG 63  Ibrahimu Class 'King Class Mawe' ame saini mkataba wa kupambana na Cosmas Cheka Feb 8 mwaka huu katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam
Mara baada ya kusaini mkataba huo wa kucheza raundi 10 za ubingwa wa Taifa kg,60 amesema atafanya mazoezi ya kutosha kuhakikisha ana msambalatisha mpinzani wake raundi za awali kwa kuwa alikuwa anachonga sana juu yake

mpambano huo uliodhaminiwa na Promota Maarufu nchini Jay Msangi utakuwa na msisimko wa aina yake kutokana na mabondia hawo kuwa gumzo katika ulimwengu wa masumbwi ndani na nje ya nchi ya tanzania

King Class aliongeza kwa kusema kuwa nipo fiti nimejiandaa na ninasubili tu kuvishwa ubingwa huo wa taifa kwani Cheka ana ujanja kwangu mbinu zake zote nimesha zikamata

King Class Mawe anae nolewa na jopo la makocha wanao ongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta' Rajabu Mhamila 'Super D' Kondo Nasoro 

Bondio huyo amewashukulu wadau wa mchezo wa ngumi kwa kumuwezesha kuchaguliwa kuwa bondia bora wa mwaka katika uzito wake kwa kuwapita mabondia wengine wanne na yeye kuibuka kidedea katika kin'yan'gan'yiro hicho

MASHINDANO YA NGUMI MKOA WA DAR ES SALAAM YAPAMBA MOTO

Bondia Cosmas Peter kushoto akipambana na Hfidhi Bamtula wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana kwenye mashindano ya Mkoa ambayo yanachagua bondia atakaewakilisha Mkoa wa Dar es salaam Bamtula alishinda kwa Point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Hafidhi Bamtula kushoto akitupa ngumi ambayo imenda hewani bila mafanikio alipokuwa akipambana na Cosmas Peter wakati wa Mashindano ya Mkoa wa Dar es salaa ambayo wanachagua mabondia wa mkoa huo Bamtula aklishinda kwa point mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Emillian  Patrick kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hamad Furahisha wakati wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam Patrick alishinda kwa point mpambano huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Kasimu Mbutike kushoto akimtupia konde la mkono wa kushoto Yusufu Said wakati wa mashindano ya mkoa Wa Dar es salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa panandi panandi Ilala Bungoni Said alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

DVD MPYA KUTOKA KWA SUPER D BOXING COACH HIZI HAPAMPAMBANO AMBAO ULIWAKESHESHA WATU MACHO MIMI NIKIWA NI MMOJA WAO kwa MAHITAJI YA DVD WASILIANA 
Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania
Saul 'canelo' alverez bondia mkari kwenye dvd hii unapata gem zake nne pamoja na historia yake ya ngumi na ndie bondia anaekubalika zaidi mexico


DVD ILIYOBEBA WABABE WA ZAMA HIZO MUHAMMAD ALI NA SUGAR RAY LEONARD


DVID MPYA ZA MASUMBWI KWA SASA ZIPO TAYARI KWA AJIRI KUPATA BURUDANI UKIWA NYUMBANI ZAID TUWASILIANE 0713406938 AU TEMBELEA www.superdboxingcoach.blogspot.com
 
 DVD YA MANNY PAQUAIO ALIYOPIGWA KIUTATA IPO INAPATIKANA
  1. DVD YA FLOYD MAYWEATHE MPAMBANO WAKE WA MWISHO KABLA YA KWENDA JELA NAYO INAPATIKANA KWA MAELEZO ZAIDI PIGA NAMBA 0713 406938,0787 406938,0754 406938 NA 0774 406938 AU FIKA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI ULIZA SUPER D AU FIKA KLABU YA ASHANTI ILALA AU AMANA
 

Tuesday, January 28, 2014

YASSIN ABDALLAH ASHUKURU KAMATI YA UTENDAJI YA E&CAPBA

NDG ZANGU
    HIVI KARIBUNI VYOMBO VYENU KARIBU VYOTE VIMEWAFAHAMISHA WANANCHI WA TANZANIA JUU YA UTEUZI WANGU     WA  KUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SHIRIKISHO KUBWA LA NGUMI ZA KULIPWA LA AFRIKA MASHARIKI .

NAPENDA KUTUMIA NAFASI HII KUISHUKURU KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO HILO ILIYOKUTANA JIJINI KIGALI-RWANDA KWA KUNIPATIA NAFASI YA KUWA MMOJA WA VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU KATIKA SHIRIKISHO HILO,PIA NINAUPOKEA UTEUZI WANGU HUU KWA FURAHA KUBWA SANA.

NINA IMANI KUBWA SANA KUWA KAMATI YA UTENDAJI YA SHIRIKISHO HILO IMETHAMINI MCHANGO WANGU AMBAO NIMEKUWA NIKIJITAHIDI SANA KUUTOWA KATIKA MCHEZO WA NGUMI KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI,PIA MAHUSIANO MAZURI MIONGONI MWA VIONGOZI MBALIMBALI WA MASHIRIRIKA TOFAUTI YA NGUMI ZA KULIPWA KOTE DUNIANI.

NIAAHIDI KWA UWEZO WA MWENYEZI MUNGU ATAKAONIJAALIA ,NITAJITAHIDI KUIMARISHA MAHUSIANO MEMA BAINA YA NCHI YANGU TANZANIA NA NCHI ZOTE ZA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KAMA AMBAVYO TAYARI VIONGOZI WETU WA JUU KITAIFA WAMESHAUANZISHA KWA KUUNDA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

WENZETU WA MPIRA WA MIGUU TAYARI WAMESHATUTANGULIA KWA KUUNDA CECAFA,NA TAYARI WANAFANYA MASHINDANO MAKUBWA YANAYOSIMIMIWA NA CECAFA ,NA YAMEONYESHA MAFANIKIO MAKUBWA SANA KWA UHUSIANO BAINA YA NCHI NA NCHI.

NITAJITAHIDI KUSHAURIANA NA VIONGOZI WENZANGU WA SHIRIKISHO ILI KUANGALIA KWA UNDANI ZAIDI NI JINSI GANI TUNAWEZA KUUBORESHA ZAIDI MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA ILI UWE NI AJIRA YA UHAKIKA KWA VIJANA WA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KUPITIA MICHEZO.

                               MATATIZO YA VIJANA

TATHMINI INAONYESHA WAZI KWAMBA VIJANA NDIYO WAMEKUWA WAKITUMIWA KATIKA KUFANIKISHA MAMBO MENGI YA WATU,NA HATA KISIASA.KOTE DUNIANI

VIJANA WAMEKUWA WAKIHAMASISHWA KUSHIRIKI KATIKA MAANDAMANO YA KUZIPINGA SERIKALI ZILIZOKO MADARAKANI,NA WENGINE KUFIKIA KUPATA VILEMA VYA KUDUMU NA HATA KUPOTEZA MAISHA KWA FAIDA YA WANASIASA ,NA WAKISHAPATA MADHARA HAO WANAOWATUMIA HAWAWAPATII MISAADA YEYOTE NA HUISHIA MAGEREZANI,NA KUFANYISHWA KAZI AMBAZO URAIANI WANGEZIFANYA ,NA KUJIPATIA RIZIKI.KAMA WANGEWEZESHWA.

IKO HAJA KUBWA SASA KWA MAKAMPUNI MAKUBWA YA BIASHARA YA KUUTUMIA MCHEZO HUU WA NGUMI ZA KULIPWA AMBAZO ZIMEWATAJIRISHA SANA BAADHI YA MABONDIA DUNIANI NA KUWAPATIA UMAARUFU MKUBWA SANA KUTANGAZIA BIASHARA ZAO KWAKUUDHAMINI,MFANO; FLOYD MAYWEATHER NI MWANAMASUMBWI TAJIRI MIONGONI MWA WANAMICHEZO DUNIANI ,MANNY PAQUIAO YEYE NI MBUNGE WA PHILIPINES ,NA SASA VITALY KLYTCHKO HIVI SASA AMEINGIA KATIKA KINYANGANYILO CHA URAIS CHINI KWAKE UKREANE ,NA ANAITIKISA SERIKALI ILYOKO MADARAKANI .

NCHINI UGANDA BONDIA BINGWA WA ZAMANI WA WBF AMOT NYAKANA AMESHAWAHI KUSHIKA NYADHFA MBALIMBALI HATA YA UMEYA WA JIJI LA KAMPALA.

WOTE HAO NILIOWATAJA WAMEPATA UMAARUFU NA NAFASI WALIZONAZO  KUPITIA MCHEZO WA NGUMI.

PIA NAPENDA KUVISHUKURU VYOMBO VYENU VYA HABARI KWA USHIRIKIANO AMBAO MMEKUWA MKINIPATIA KATIKA UPASHANAJI HABARI ZA MCHEZO KWA MUDA WOTE NINAPOKUWA NA TAARIFA LAKINI PIA MNAPOTAKA TAARIFA KUTOKA KWANGU , MMENISAIDIA KUNIFANYA NIJULIKANE HATA NJE YA MIPAKA YA TANZANIA ,NA NINAKIRI KABISA YAWEZEKANA NYINYI NDIYO MMENITENGENEZEA NAFASI HII,MWENYEZIM MUNGU AWABARIKI WOTE.

KATIKA NAFASI HII MPYA NILIYONAYO HIVI SASA BADO NITAENDELEA KUVIHESHIMU VYOMBO VYOTE VILIVYOPEWA MAMLAKA YA KUSIMIMIA MICHEZO NCHINI TANZANIA ,IKIWEMO WIZARA YA HABARI UTAMADUNI ,VIJANA NA MICHEZO,KURUGENZI YA MICHEZO NCHINI ,NA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA[BMT] NA VIONGOZI WAKE WOTE, KAMWE SITOACHA KUOMBA USHAURI WAO KWA JAMBO LOLOTE LIHUSULO MICHEZO ,LIWE LA MAFANIKIO AU LA MATATIZO .


                                         imeletwa kwenu nami;
                                 yassin abdallah mwaipaya- ustaadh

Monday, January 27, 2014

MASHINDANO YA MKOA DAR ES SALAAM YAANZA ILALA


Bondia Husein Pendeza  wa Klabu ya Ashanti Ilala kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde kiufundi na Ayubu Ibrahimu wa Green House wakati wa ufunguzi wa mashindan ya  wazi mkoa wa Dar es salaam yanayoenderea katika ukumbi wa panandi pasnandi Ilala Bungoni Ibrahimu alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mwenyekiti wa Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Dar es salaam DABA akimkabidhi risara Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu wakati wa mashindano ya wazi yaliyoanza jumatatu

Bondia Husein Pendeza  wa Klabu ya Ashanti Ilala kulia  akimtupiana makonde kiufundi na Ayubu Ibrahimu wa Green House wakati wa ufunguzi wa mashindano ya wazi mkoa wa Dar es salaam yanayoenderea katika ukumbi wa panandi pasnandi Ilala Bungoni Ibrahimu alishinda kwa point Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

 Mbunge wa Ilala Mussa Zungu akifatilia mchezo wa ngumi
Na Mwandishi Wetu
SHILIKISHO la ngumi za ridhaa Mkoa wa Dar es salaam umezindua rasmi mashindano yake ya kwanza tangia waingi Madarakani mashindano hayo yalifunguliwa jana na mgeni rasmi

Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu ambayo imekutanisha zaidi ya timu ishirini na mabondia 60 wa mkoa huu akisoma risala kwa mgeni rasmi 

Mwenyekidi wa ngumi mkoa wa Dar Akaroli Godfrey amesema mbali na mashindano hayo kuwa na changanmoto mbalimbali wameamua kuyafanya kwa kuwa yapo kwenye karenda yao ata hivyo akuna zawadi zozote kwa mabondia watakaopigana hivyo kama mbunge wa jimbo la ilala tunaomba utupatie angarau medali kwa mabondia aidha vifaa tulivyo navyo avikizi kimchezo

akijibu lisara hiyo mbunge huyo ame haidi kutoa zawadi pamoja na kuwa mlezi wa ngumi za ridhaa mkoa wa Dar es salaam na kuwasaidia kutafuta wadhamini mbalimbali watakaojitokeza kuinua mchezo wa masumbwi nchini ili ngumi zisonge mbele 

katika ufunguzi huo mabondia Anton Idoa alimtwanga kwa K,O ya raundi ya pili bondia Mohamed Mzeru huku John Cristian akimsambaratisha Omar Said, na shabani Alimasi akimdunda Saidi Kondo na bondia pekee kutoka timu ya shanti ya Ilala,Hussein Pendeza alipoteza kwa pointi na Ayubu Ibrahimu  

MABONDIA WA KIKE WAFURUMUSHANA MAKONDE URINGONI

Mabondia wa kike wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde walipokuwa wakicheza mchezo huo jana kushoto ni Halima Ramadhani na Zulfa Macho mchezo huo ulifutia mashabiki wengi waliojitokeza Macho alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Halima Ramadhani akitafuta njia ya kumpiga mwenzie ngumi Zulfa Macho wakati wa mpambano wao jana

Bondia Zulfa macho akimpiga mpinzani wake Halima Ramadhani ngumi ya kolomelo wakati wa mchezo wao uliofanyika Dar es salaam jana macho alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Idd Athumani akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Shabani Madilu wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Athumani alishinda kwa point

Bondia Mussa Chitepete akimrushia ngumi bondia Ramadhani shauli wakati wa mpambano wao wa kirafiki uliofanyika jana Shauli alishinda kwa K,O ya raundi ya saba baada ya refarii kumtoa nje ya mchezo chitepete picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Mussa Chitepete akioneshana umwamba wa kutupia ngumi na bondia Ramadhani shauli wakati wa mpambano wao wa kirafiki uliofanyika jana Shauli alishinda kwa K,O ya raundi ya saba baada ya refarii kumtoa nje ya mchezo chitepete picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Sunday, January 26, 2014

PSPF WALIVYO NOGESHA TUZO ZA MABONDIA

Meneja Mpango wa Uchangiaij wa hiyari kutoka PSPF ,Mwanjaa Sembe kushoto akimpatia ya upiga picha bora wa mchezo wa masumbwi pamoja na uhamasishaji mchezo huo Rajabu Mhamila 'Super D' wakati wa utoaji wa Tuzo hizo kwa mabondia zilizofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es  salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia akimkabidhi tuzo ya bondia bora wa mwaka 2013 kwa ngumi za ridhaa  Gelvars Rogasian wakati wa utoaji tuzo za PSPF BOXING AWARDS zilizofanyiaka katika ukumbi wa PTS Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia akimkabidhi tuzo ya bondia bora wa mwaka 2013 kwa ngumi za kulipwa  Francsis Cheka wakati wa utoaji tuzo za PSPF BOXING AWARDS zilizofanyiaka katika ukumbi wa PTS Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia akiwa na Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Mkamia
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia akiwa na Fransic Cheka
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia ajkiwa na Zuwena Kipingu ambaye ni Mjumbe wa shilikisho la ngumi za ridhaaa nchini BFT picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuzo iliyochukuliwa na Rajabu Mhamila Super d
Rais wa PST Emanuel Mlundwa kushoto akimpatia tuzo ya Bondia bora wa mwaka Bilali Ngonyani kwa niaba ya Ibrahimu Class King Class Mawe

Aga Peter akimpatia tuzo Franscis Cheka

Mdau wa masumbwi Aga Peter akimkabidhi tuzo Fadhili Majia kulia ni Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Promota wa masumbwi Mohamed Bawazir akimpatia tuzo ya uandishi bora wa mchezo wa masumbwi Mwali Ibrahimu katikati ni Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Rashidi Matumla akimpatia tuzo Fadhili Majia


Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kulia ajkiwa na Zuwena Kipingu ambaye ni Mjumbe wa shilikisho la ngumi za ridhaaa nchini BFT wakipiga picha ya pamoja na hadija Khopa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

kocha wa timu ya Taifa Jonas Mwakipesile akimkabidhi tuzo Selemani Kidunda
picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis kushoto akimkabidhi tuzo kocha wa timu ya Taifa Jonas Mwakipesile picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya PSPF TANZANIA BOXING AWARDS wakiwa katika picha ya pamoja na naibu waziri wakati wa utoaji wa tuzo hizo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com