Tangazo

Pages

Thursday, February 18, 2021

BONDIA JEMS KIBAZANGE AMTILIA MKWALA MZITO HAMIDU KWATA WATAZIPIGA APRIL 2 P.T.A SABA SABA

JEMS KIBAZANGE 'DOG LA KIVITA'
 Na Mwandishi Wetu


BONDIA Jems Kibazange 'Dog la Kivita' ameapa kuwa lazima amsambalatishe Hamidu Kwata ifikapo April 2 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba mpambano uho uliopewa jina la 'No Pain No Gain Nigth Fight' kuwa ana uwakika wa kumchakaza Kwata kama mfuko wa mazoezi

akizungumza wakati wa mazoezi yake katika     GYM, ya kocha Maneno iliyopo Manzese Midizini amesema kuwa mimi ndio kiboko ya mbwa koko na kwata ajakutana na viama mimi nimesha wapiga mabondia wote waliopo katika uzito wangu ndio
mana natamba na kwa Tanzania hii mimi sina mpinzani kwani mabondia wote kwangu ni viande nashangaa huyu amekubali vipi kupigana na mimi

naisi njaa tu inamsumbua hivyo naona pesa zake atakazo zipata zitaisha katika matibabu yake kwa kuwa nitampiga bila ya huruma kwani mimi ni kamanda katika mchezo huu wa masumbwi na akuna mtu asiejua uwezo wangu niwapo ulingoni

nakuwa mtu mwingine kabisa ndio mana mtaani kwetu wananita Dog la Kivita na vita hii itaenda kumwangamiza Kwata na kumsababishia kilema cha maisha kwani ngumi ni mchezo wangu nilio uwekea nadhiri ya kuendesha maisha yangu hivyo sito kubali bondia mdogo kama huyu aje kuniaribia kiraisi tu

Nae Promota wa Mpambano Uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia


vicent Mbilinyi vs Deo samweli rd 10
Ramadhani Mbegu "Migwede" vs Albano Clement Rd 8
4.Daudi Mwita vs Abdul Ubaya Rd 6
5. Hamidu kwata vs James kibazange 10 rd
6.Mustafa Khalidi vs Mrisho mzezele rd 6
7.kassim Ahmad vs Gabriel Chola rd 8
8.Juma Abdul vs Hamza Mchanjo rd6
9.Veronika Thomas vs Fatima Yazidu rd6
10.Frank Lucian vs Juma Kaiza rd8

pia kutakuwa na burudani mbalimbali kwa ajili ya kusapoti mchezo uho utakao kuwa siku ya Ijumaa kuu ya Pasaka


Wednesday, February 17, 2021

SUPER D AWASAINISHA MABONDIA MAONO ALLY KUZIPIGA NA MESHACK MWANKEMWA APRIL 2

 

MAONO ALLY

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Maono Ally kutoka Bagamoyo mkoa wa Pwani amesaini mkataba wa kuzipiga na Meshack Mwankemwa kutoka Mbeya mpambano utakaofanyika April 2 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba mpambano wa raundi kumi uzito wa kg69 kutafuta nani zaidi kati yao

mpambano uliopewa jina la No Pain No Gain Fight Night mabondia hawo watazipiga siku hiyo katika mpambano ulio andaliwa na kiampuni Tanzu ya Kizarendo ya Super D Boxing Promotion


Maono amesema kuwa katika mpambano uho atokuwa na msalia mtume kwani ngumi kwake ni kazi kwa kuwa mabondia wengi wamekuwa wakimkimbia pindi wanapo pangiwa mapambano na yeye hivyo Mwankemwa akae tayari kwa kipigo tu


Na afanye mazoezi ili apunguziwe kipigo ingawa kipigo kipo pale pale nitampiga mwankemwa kama mfuko wa mazoezi kwani nimejiandaa vya kutosha na sina wasiwasi na pambano hilo


kwa upande wa Mwankemwa amesema asnashukuru kupata mpambano uho utakaofanyika Dar hivyo nipo vizuri na nategemea ushindi ambao sito washirikisha majaji ambapo nitampiga K,O mbaya sana aikuwai kutokea

Nae Promota wa Mpambano Uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia


vicent Mbilinyi vs Deo samweli rd 10
Ramadhani Mbegu "Migwede" vs Albano Clement Rd 8
4.Daudi Mwita vs Abdul Ubaya Rd 6
5. Hamidu kwata vs James kibazange 10 rd
6.Mustafa Khalidi vs Mrisho mzezele rd 6
7.kassim Ahmad vs Gabriel Chola rd 8
8.Juma Abdul vs Hamza Mchanjo rd6
9.Veronika Thomas vs Fatima Yazidu rd6
10.Frank Lucian vs Juma Kaiza rd8

pia kutakuwa na burudani mbalimbali kwa ajili ya kusapoti mchezo uho utakao kuwa siku ya Ijumaa kuu ya Pasaka

Tuesday, February 9, 2021

SUPER D AMSAINISHA DEO SAMWELI KUZIPIGA NA VICENTI MBILINYI APRIL 2 P.T.A SABA SABA


Bondia Deo Samweli kushoto akibadilishana mkataba na Promota wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga na Vicent Mbilinyi mpambano utakaofanyika April 2 katika ukumbi wa P.T.A SABASABA siku ya Ijumaa kuu ya Pasaka

Bondia Deo Samweli akisaini mkataba wa kuzipiga na Vicent Mbilinyi mbele ya promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' mpambano utakaofanyika April 2 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba


Na Mwandishi Wetu


BONDIA DEO SAMWELI amesaini mkataba wa kuzipiga na Vicenti Mbilinyi mpambano wa raundi kumi kumi utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Saba saba siku ya Ijumaa Kuu  April 2

Akisaini mkataba uho mbele ya mkurugenzi wa kampuni Tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa amekuja kufanya kazi hivyo mashabiki waje kwa wingi kwani kazi atakayo ifanya siku hiyo si ya kitoto

aliongeza kwa kuserma kwa sasa anarudi upya katika masumbwi kwani mwishoni mwa mwaka jana alijeruhiwa kidogo hivyo ame mtahadharisha mbilinyi kufanya mazoezi kweli kweli kwani siku hiyo akuto kuwa na msalie mtume

Katika mpambano uho atampiga kipigo cha mwana ukome ambapo mbilinyi ato weza tena kumtaka Deo Samweli warudiane nae tena

Nae Promota wa mpambano uho Super D amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na burudani ya masumbwi ni vitasa kwa kwenda mbele katika mpambano uliopewa jina la 'No Pain No Gain Fight Nigth'

pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ya mabondia mbalimbali ambapo Jemsi Kibazange atazipiga na Hamidu Kwata wakati kassim ahamdi atazidunda na Gabriel Chola na Ramadhani Migwede atazichapa na Albano Clement na mpambano mwingine wa kutisha utakuwa kati ya Maono Ally kutoka bagamoyo atazipiga na Meshacki Mwankemwa kutoka Mbeya na Abdul Ubaya kutoka Mlandizi atazidunda na Daudi Mwita wa Dar