Tangazo

Pages

Wednesday, February 17, 2021

SUPER D AWASAINISHA MABONDIA MAONO ALLY KUZIPIGA NA MESHACK MWANKEMWA APRIL 2

 

MAONO ALLY

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Maono Ally kutoka Bagamoyo mkoa wa Pwani amesaini mkataba wa kuzipiga na Meshack Mwankemwa kutoka Mbeya mpambano utakaofanyika April 2 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba mpambano wa raundi kumi uzito wa kg69 kutafuta nani zaidi kati yao

mpambano uliopewa jina la No Pain No Gain Fight Night mabondia hawo watazipiga siku hiyo katika mpambano ulio andaliwa na kiampuni Tanzu ya Kizarendo ya Super D Boxing Promotion


Maono amesema kuwa katika mpambano uho atokuwa na msalia mtume kwani ngumi kwake ni kazi kwa kuwa mabondia wengi wamekuwa wakimkimbia pindi wanapo pangiwa mapambano na yeye hivyo Mwankemwa akae tayari kwa kipigo tu


Na afanye mazoezi ili apunguziwe kipigo ingawa kipigo kipo pale pale nitampiga mwankemwa kama mfuko wa mazoezi kwani nimejiandaa vya kutosha na sina wasiwasi na pambano hilo


kwa upande wa Mwankemwa amesema asnashukuru kupata mpambano uho utakaofanyika Dar hivyo nipo vizuri na nategemea ushindi ambao sito washirikisha majaji ambapo nitampiga K,O mbaya sana aikuwai kutokea

Nae Promota wa Mpambano Uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia


vicent Mbilinyi vs Deo samweli rd 10
Ramadhani Mbegu "Migwede" vs Albano Clement Rd 8
4.Daudi Mwita vs Abdul Ubaya Rd 6
5. Hamidu kwata vs James kibazange 10 rd
6.Mustafa Khalidi vs Mrisho mzezele rd 6
7.kassim Ahmad vs Gabriel Chola rd 8
8.Juma Abdul vs Hamza Mchanjo rd6
9.Veronika Thomas vs Fatima Yazidu rd6
10.Frank Lucian vs Juma Kaiza rd8

pia kutakuwa na burudani mbalimbali kwa ajili ya kusapoti mchezo uho utakao kuwa siku ya Ijumaa kuu ya Pasaka

No comments:

Post a Comment