Tangazo

Pages

Wednesday, July 30, 2014

NGUMI ZILIVYOPIGWA MANZESE SIKU YA IDDI PILI

Bondia Sadick Nuru kushoto akioneshana umwamba na Baraka Mchonge wakati wa mpambano wao ulifanyika Mazese Dar es salaam wakati wa sikukuu ya iddi pili Nuru alishinda kwa point mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Stevin Kobelo kushoto akirusha ngumi kumpiga Karim Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya iddi pili katika ukumbi wa Manyara park manzese Dar es salaam mpambano huo walitoka droo ya kufungana point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia Joseph Gili kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Ibrahimu Tamba wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa manyara park manzese Dar es salaam Tamba aklishinda kwa T.K.O  ya raundi ya nne Picha na www.superdboxingcoach .blogspot.com
Bondia Julius Kisalawe kushoto akipambana na Ramadhani Kumbele wajkati wa mpambano wao wa ubingwa wa TPBC uliofanyika siku ya Iddi pili katika ukumbi wa Manyara Park Manzese Dar es salaam Kumbele alishinda kwa point na kufanikiwa kuchukua ubingwa picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha mkongwe wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli 'Masta' kulia akimvisha mkanda wa ubingwa bondia ramadhani Kumbele baada ya kumdunda Julius Kisalawe kwa point kushoto ni Refarii Ally Bakari picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, July 29, 2014

MPAMBANO WA NGUMI ULIVYOFANYIKA MBEZI

Bondia Nenge Juma kushoto akipambana na Said Mohamed wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya sikukuu ya iddi mosi mbezi mwisho juma alishinda kwa TKO ya raundi ya tatu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Lugano Mwaikambo akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Michael Chinyama wakati wa mpambano wao uliofanyika siku ya sikukuu ya idi mosi mbezi mwisho jijini Dar es salaam Chinyama alishinda kwa point picha  na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MABONDIA WAPIMA UZITO KUPIGANA IDDI PILI MANYARA PARK

Bondia Peter Mbowe akioneshana umwamba wa kutunishiana misuli na Ibrahimu Tamba baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao yutakaofanyika katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM siku ya Iddi pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Karim Ramadhani akipima uzito
Bondia Karim Ramadhani kushoto akitunishiana misuli na bondia Stevin Kobelo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya iddi pili katika ukumbi wa Manyara Park manzese CCM wa pili kushoto ni bondia Nassibu Ramadhani na Kocha Jafari Ndame picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mjumbe wa kamati ya utendaji wa chama cha ngumi za kulipwa nchini Ally Bakari ' Champion' akiwakumbusha mabondia na wasaidizi wao sheria mbalimbali za mchezo wa ngumi kabla ya mpambano wao
Rais wa TPBO cHAUREMBO pALASA AKISISITIZA JAMBO


Bondia Peter Mbowe akioneshana umwamba wa kutunishiana misuli na Ibrahimu Tamba baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao yutakaofanyika katika ukumbi wa Manyara Park Tandale CCM siku ya Iddi pili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Monday, July 28, 2014

BONDIA WA KIKEKE LULU KAYAGE ANAYEWAZA KUWA NA MATUMAINI KIBAO KATIKA NGUMI


Bondia wa kike,Lulu Kayege akiwa katika pozi bondia huyo  anaenolewa katika Kambi ya Ilala na Makocha wazowefu wa mchezo wa Masumbwi Nchini Habibu Kinyogoli 'Masta, Rajabu Mhamila 'Super D' na Kondo Nassoro kwa sasa yupo fiti kwa ajili ya masindano mbalimbali nchiniwww,superdboxingcoach.
blogspot.com
 
Na Mwandishi Wetu
 Ukizungumzia mchezo wa masumbwi ulivyompatia hamasa mpaka kuanza mazoezi katika kambi ya ilala ya mchezo wa masumbwi bondia Lulu Kayage anasema mchezo anaupenda na pia unamjenga kiafya na ki mwili kwani amekuwa akishiriki mazoezi tangia mwaka 2012 mwezi April na maendeleo yake ni mazuri akiwa chini ya uwangalizi wa makocha wake hawo

Bondia huyo wa kike aliyezaliwa 1990 anamatarajio makubwa ya kuwa ingwa wa dunia katika masumbwi ususani upande wa wanawake 

bondia huyo anaye vutiwa na uchezaji wa mkongwe wa masumbwi nchini Rashidi Matumla 'Snake Man'  ambapo kwa nje anavutiwa na mabondia toafauti ambapo mmoja wapo ni Mbunge wa Filpino Manny Paquaio na bondia asiyepigika ambaye kwa sasa anatumikia kifingo cha siku 90 kwa kosa la kumshambulia aliyekuwa mpenzi wake na mama watoto wake
Katika mazoezi anayofanya na kambi ya Ilala ambayo wanawake wapo wawili ambapo anaendelea kujisikia faraja kwa kuwa wapo katika mazoezi pamoja kama ndugu na nidhamu ya ali ya juu iliyopo hapo katika kambi hiyo

aliwataka wanawake wajitokeze katika mchezo wa masumbwi kwani ni mchezo kama michezo mingine ambapo ata ukiangalia mchezo watu wanapopigana wakimaliza wanakubatiana kwa furaha ni kwa ajili ya kutambua mchezo wa masumbwi si uadui bali ni mchezo


Vikwazo ambavyo amewai kukutana navyo ni pamoja na kukatishwa tamaa kwa watu ambao awapendi michezo kwani wanasema mwanamke mzima unacheza ngumi uogopi kutolewa manundu kuaribiwa sura ehee uzuri wote huo hizo ni sehemu tu za watu wasiopenda michezo kwani kuna vikwazo
 vingi ambavyo tuna vipata mabondia wa kike 

kwa mara ya kwanza nilipotokea kwenye magazeti tu watu walinifata na kunishauli niachane na mchezo lakini kwa sasa nimeshaiva na nipo tayali kwa mapambano mbalimbali yatakayojitokeza

kwa kuwa mimi ni bondia bora pekee wa kike nchini na ninaetoka katika kambi bora kabisa ya mchezo wa masumbwi nchini naisi cheche zangu mtaanza kuziona mwazi agost kwa kuwa kwa sasa nipo kwenye mazoezi makari ambayo yananipa uwezo wa ali ya juu katika masumbwi 

Aliongeza kuwa kwa kufundishwa na kocha wa kimataifa Super D anaefundisha mafundisho hayo kupitia DVD zake ambazo  amechanganya na clips za mabondia mabingwa wa dunia akiwemo Manny Paquaio,floyd Mayweather, Roy Jones, Mohamedi Ali, Mike Taysoni na wengine ameziona na kuzifanyia kazi ambapo kwa sasa anajua mbinu za Ndani na nje ya nchi kutokana na Supe D kumpatia uwezo wa kina katika maswala ya mchezo wa Masumbwi Duniani

Katika mchezo uhu siwezi kukata tamaa katika mazoezi na nawambia mashabiki wa mchezo wa masumbwi watarajie mafanikio yangu katika masumbwi

BONDIA SELEMANI KIDUNDA WA TANZANIA APOTEZA MCHEZO JUMUIYA YA MADOLA


Selemani Kidunda
Bondia Selemani Kidunda amepoteza mchezo wake dhidi ya bondia kutoka nchini Nigeria Kehinde Ademuyiyiwa uzito wa kilo 69 na hivyo kupoteza nafasi ya kusonga katika hatua inayofuata katika michezo ya jumuiya ya Madola inayofanyika Glasgow nchini Scotland.
Akiongea na mtandao wa rockersports kocha mzalendo wa timu ya ngumi John Mwakipesile amesema mchezo ulikuwa ni mzuri kwa upende wa Kidunda kwa roundi zote tatu za mchezo na mpaka kufikia mwisho walikuwa wakijua Kidunda ameshinda lakini ikawa ni ajabu kwa watu wengi kutangazwa Ademuyiyiwa kutangazwa mshindi.
Amesema mpianzani wake alikuwa akitumia mbinu chafu ya kumpiga vichwa Kidunda katika sehemu kubwa ya mchezo huo kitu ambacho waamuzi wa mchezo walikuwa wakikiona na kushindwa kukemea hilo.
Kuondolewa kwa Kidunda ni pigo kubwa kwa Tanzania ambayo ilikuwa imeweka matumaini makubwa kwa nahodha huyo wa Tanzania katika michezo hiyo ya Madola.
Kesho bondia mwingine Nasser Mafuru atapanda ulingoni kucheza dhidi ya Jessie Lartey wa Ghana ambapo mwenye Mafuru ametamba kumchapa mpinzani wake huyo.

Saturday, July 26, 2014

Korean boxing heroine Ju Hee Kim,new WPBF World ChampionBy WPBF-USBC.ORG. December 16,2012.  [PHOTO BY YONHAP]

         
The 26-year-old Korean boxing heroine Ju Hee Kim scored a spectacular 10th round TKO over her Thai opponent Ploynapa Sakrungrueng to claim the Vacant World Professional Boxing Federation Women's World Light Flyweight Title on Saturday at Yeongdeungpo Girls High School in Seoul. Kim Ju-hee improved her record to (17-1-1,8 KOs). The event was promoted by Geoin Promotion.   

Friday, July 25, 2014

CHAMA CHA NGUMI ZA KULIPWA TPBC CHATOA MAFUNZO KWA MAREFARII


Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' kushoto akiwaelekeza baadhi ya marefarii waliojitokeza katika mafunzo hayo yaliyo andaliwa na chama cha ngumi za kulipwa TPBC yaliyoanza Ilala CCM Dar es salaam juzi na kumalizika jumamosi  hii picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' kulia akisisitiza jambo kwa wakati wa mafunzo hayo uku marefarii waliojitokeza wakimsikiliza kwa makini kutoka kushoto ni Kondo Nassoro, Sako Mtulya na Buchato Michael picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mkufuzi wa mafunzo ya waamuzi wa mchezo wa masumbwi Ally Bakari 'Champion' akitoa maelekezo kwa mabondia na marefarii kabla ya kupigana wakati wa mafunzo kwa vitendo ya urefarii wa mchezo huo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

BAADHI YA MAREFARII WALIOSHILIKI KATIKA KOZI HIYO KUTOKA KUSHOTO NI BUCHATO MICHAEL,PEMBE NDAVA,HAMISI KIMANGA,RAJABU MHAMILA 'SUPER D' ALLY BAKARI,Ayubu Tezikoma NA SAKO MTULYA

Wednesday, July 23, 2014

BONDIA IBRAHIMU MAOKOLA AJIFUA KUMKABIRI SELEMANI MKALAKAL AGOUST 9 AMENYA PUB MBAGALABondia Ibrahimu Maokola akipiga beg zito wakati akijifua katika GYM ya okaido iliyopo Mbagala Charambe  kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Mkalakala pambano litakalofanyika agost 9 katika ukumbi wa amenya pub uliopo mbagala picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Maokola akijifua Okaido GYM iliyopo Mbagala Charambe kwa ajili ya kujitaharisha na mpambano wake wa ubingwa wa taifa na Selemani Mkalakala mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub uliopo mbagala augoust 9 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Maokola akijifua Okaido GYM iliyopo Mbagala Charambe kwa ajili ya kujitaharisha na mpambano wake wa ubingwa wa taifa na Selemani Mkalakala mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub uliopo mbagala augoust 9 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Maokola akifanya mazoezi ya kuimalisha misuli ya tumbo kwa ajili ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Mkalakala litakalofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub uliopo mbagala siku ya ya augoust 9 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akielekezwa kupiga ngumi na Ayubu Tezikoma wakati wa mazoezi yake kwa ajili ya kujiandaa kupambana na Selemani Mkalakali mpambano wa ubingwa raundi kumi utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub Augost 9 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akielekezwa kupiga ngumi na Ayubu Tezikoma wakati wa mazoezi yake kwa ajili ya kujiandaa kupambana na Selemani Mkalakali mpambano wa ubingwa raundi kumi utakaofanyika katika ukumbi wa Amenya Pub Augost 9 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Ibrahimu Maokola
Bondia Ibrahimu Maokola kushoto akipiga beg kubwa kwa kusimamiwa na Athumani Magambo wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Selemani Mkalakali litakalofanyika Augoust 9 katika ukumbi wa Amenya pub mbagala Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Sunday, July 20, 2014

DAH! FLOYD MAYWEATHER NGUMI 221 ZAMFANYA ARUDI TENA KUZIPIGA NA MAIDANANA ALLY KAMWE.
RASMI!  Floyd ‘Money’ Mayweather atapanda tena ulingoni September 13 pale MGM Grand hotel, Las Vegas  kucheza pambano la marudiano na bondia Marcos Maidana. Kwa sasa ulimwengu wa masumbwi unaonekana kulihitaji zaidi pambano hili  kuliko pambano la Myweather na Mphilipino Manny Pacquiao.
Mayweather Maidana 2 Mayweather vs. Maidana 2  marcos rene maidana floyd mayweather jr Hii ni mara ya pili kwa Mayweather mwenye rekodi ya kushinda mapambano yote 46 aliyocheza mpaka sasa kukubali kucheza pambano la marudiano! Si kawaida ya Mayweather kupigana kwa mara ya pili na mpinzani aliyekwishampiga awali, lakini sasa imekua tofauti na imemlazimu kukubali  kutokana na utata uliopo baada ya matokea ya pambano la awali baina yake na Maidana ambapo Mayweather aliibuka mshindi kwa tofauti ya pointi.
Pamoja na matokeo kuonyesha kuwa Mayweather alishinda kwa tofauti ya pointi lakini wadau wengi wa mchezo huo wanaamini Mayweather alipoteza pambano lile kulingana na namna Maidana alivyoweza kucheza na kummiliki Mayweather katika raundi zote 12 za pambano lile.
Baada ya kukubali kucheza pambano hili  Floyd Mayweather  anayetafuta rekodi ya dunia ya kucheza mapambano 50 bila kupoteza alitoa sababu muhimu ambazo kwa kiasi kikubwa zimemfanya kutofikiria mara mbili katika uamuzi wake wa kucheza tena pambano la marudiano na Maidana.
NGUMI 221 ALIZOPIGWA NA MAIDANA ZAMCHANGANYA!
Huenda wengi wasilijue hili, lakini ndicho alichokisema bondia huyu sugu wa Kimarekani  kuwa makonde 221 aliyopigwa na Maidana katika pambano lao la kwanza  ndio yamemfanya kukubali tena kupanda tena ulingoni na mkali huyo kutoka Argentina.
Mayweather alisema kuwa idadi hiyo ya ngumi alizopigwa na Maidana ni idadi kubwa zaidi kupigwa katika historia yake ya masumbwi hali inayomfanya kujiuliza kila mara ni vipi Maidana alipata nafasi ya kumpiga idadi hiyo kubwa ya makonde.
Takwimu zimekua zikionyesha kuwa katika jumla ya makonde 858 yaliyotupwa na Maidana ambayo ni sawa na asilimia 26, makonde 221 yalifika katika mwili wa Mayweather. Hiki ndicho kinachompa wazimu Floyd Mayweather
“Alishinda kwa raundi tatu mpaka nne dhidi yangu, haijawahi kuwa hivyo kabla. Ni lazima nijiulize ni vipi hali hiyo ilijitokeza”  Alisema Mayweather
 
MASHABIKI WANAMPA ‘STRESS’,
Heshima imeshuka! Ndivyo anavyoamini Mayweather baada ya kuwepo kwa minong’ono mingi ya watu kudai kuwa alipendelewa katika pambano lake la awali. Wadau wengi wa mchezo huo wamekuwa wakiamini kuwa Mayweather alibebwa na majaji  wakati wa ugawaji pointi katika pambano lao la awali jambo linaloonekana kumnyima raha bondia huyo.
“ watu wameshindwa kuulewa mchezo wa ngumi, wametazama kwenye raundi tatu za mwanzo na kutoka maamuzi yao, hakuna anayejua nini kiliendelea  kwenye raundi 9 zilizobaki. Nilishinda, na nitashinda tena ili kumaliza utata huu” alisema  Mayweather kuonyeshwa kukerwa na maneno ya watu.
 “ Sirudi tena ulingoni kwa ajili yake, narudi kwa ajili ya mashabiki. Mashabiki wameonyesha kuhitaji sana hili pambano hivyo sinabudi kukubali. Sikubebwa wala sikubahatisha na nitalithibitisha hilo September 3”  aliongezea mwanamasumbwi huyo anayeongoza kwa kuwa na mkwanja mrefu zaidi duniani kwa sasa kwa upande wa wanamichezo
NGEBE ZA MAIDANA ZAMKOSESHA USINGIZI
Dogo anachonga sana! Tangu kumalizika kwa pambano la awali May 3 mwaka huu, bondia Marcos Maidana amekuwa akijitapa na kutangaza kuwa yeye ndie aliyestahili kutangazwa mshindi. Kama wengi wanavyoamini ndivyo Maidana anavyoamini  kuwa alimpiga Mayweather.
Jambo hili linaoneka kumkera sana Mayweather kiasi cha kuamini kuwa bila kurudi ulingoni kuzichapa tena na Maidana huenda akawa ameacha dosari katika rekodi zake za masumbwi duniani. Ni lazima aje amfunge mdomo Maidana katika hili
“ ametaka mechi nyingine, nimekubali. Silalamiki tena kuhusu ‘gloves’ zake. Anadai alishinda pambano la kwanza, hivyo ni bora aje afanye tena na ‘gloves’ zake zilezile” alisema Mayweather kuonyesha kuchukizwa na tambo za Maidana.
Awali Mayweather alionekana kulalamika juu ya ‘gloves’ alizokuwa akizitumia Maidana kuwa zimetengenezwa maalumu kwa ajili ya kuongeza uzito wa ngumi lakini sasa mkali huyo amekubali Maidana arudi tena ulingoni na ‘gloves’ zake zilezile alizotumia awali.
MAYWEATHER BWANA! ETI ATATUMIA MBINU ZA WAJERUMANI KWENYE ‘WORLD CUP’.
Haishi mikwara huyu! Baada ya kuwaangalia Wajerumani wakiwaangamiza Waargentina kwenye dimba la Estadio do Maracana pale nchini Brazil, Floyd Mayweather amesema safari hii atatumia mfumo uleule wa Wajerumani katika kumchakaza mpinzani wake Maidana anayetokea kwenye taifa la Argentina.
“ kama walivyofanya Wajerumani, ndicho nitakachokifanya kwa Muargentina mwingine (akimmaanisha Marcos Maidana)” alitamba Mayweather!
Ni Pambano muhimu kwa Mayweather kwa ajili ya kuzima ngebe za Maidana, ni pambano muhimu kwa Maidana pia kwa ajili ya kuionyesha dunia kuwa ni kweli alionewa kwenye mpambano wa awali. Dunia ya masubwi inasubiri kufika September 13 mwaka huu pale Las Vegas.
Nisisahau, hili pia ni pambano muhimu kwa rafiki yangu Yassin Ustadh kwa ajili ya kuwaonyesha vijana wake kuwa kupigwa ni sehemu ya changamoto ya mchezo. Lini Maugo amewahi kuzisifia ngumi alizopigwa na Mashali ama Mashali kuzisifia ngumi alizopokea kwa  Francis Cheka?  Ustadh, ngumi 221 alizopigwa Mayweather zimemrudisha ulingoni tena huku akijilaumu na kujishangaa! Vipi vijana wako, wanasemaga haya?
 
MATOKEO YA POINTI ZA MAJAJI ZILIZOZUA UTATA PAMBANO LA AWALI
                             MAYWEATHER VS MAIDANA
JAJI NAMBA 1               JAJI NAMBA 2                        JAJI NAMBA 3
117-111,                         116-112                                         114-114
kwa hisani ya gazeti la dimba
 .

JUMAPILI YA JULAI 20/ 2014

Saturday, July 19, 2014

MABONDIA WAKUTANA NA KUUNDA UMOJA WA KUSAIDIANA KATIKA MAMBO MBALIMBALI

Bondia Japhert Kaseba kushoto akizungumza katika mkutano wa kwanza wa umoja wa kusaidiana katika mambo mbalimbali kwa mabondia wengine ni Habibu Kinyogoli 'masta' Fransic Miyeyusho na Thomas Mashali picha na www.superdboxing coach.blogspot.com

www.superdboxing coach.blogspot.com

mmoja wa wapiganani wa kick boxing Mkali Kaizum akichangia mada
Mmoja wa mabondia Crispian Kisinini akichangia mada
mmoja wa mabondia akichangia mada
Bondia Japhert Kaseba akizungumza kabla ya kufunga mkutano huo aliouitisha kwa ajili ya kuunda umoja wa mabondia kusaidiana kwa mambo mbalimbali picha na

www.superdboxing coach.blogspot.com

Friday, July 18, 2014

SUPER D AWAKUTANISHA MABONDIA WAKE NA WADAU KATIKA FUTARI


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akifuturu pamoja na mabondia na wadau wa mchezo huo wa pili kushoto ni Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Birali Ngonyani, Shomari Mirundi, Raymond Mbwago wakati wa futari iliyoandaliwa na kucha huyo nyumbani kwake Rozana Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Baadhi ya waumini wa dini ya kislam wakiomba duwa baada ya kufuturu katika futari iliyoandaliwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' mwenye kibagarashia na kanzu picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia na wadau mbalimbali wakifurahia futari iliyoandaliwa na kocha Super D
Watoto nao awakuwa nyuma wakifuturu pamoja wakati wa futari iliyoandaliwa na kocha super d
Futari ikienderea
Kocha Rasjabu Mhamila 'Super D' katikati mwenye kibagarashia na kanzu akiwa katika picha na baadhi ya mabondia na wadau wa mchezo wa masumbwi baada ya kufuturu nyumbani kwake rozana Dar es salaam
Kocha Rasjabu Mhamila 'Super D' katikati mwenye kibagarashia na kanzu akiwa katika picha na baadhi ya mabondia na wadau wa mchezo wa masumbwi baada ya kufuturu nyumbani kwake rozana Dar es salaam kutoka kulia ni Birali Ngonyani,Ibrahimu Class, Mohamed Sadiq, Raymondi Mwago wa pili kushoto na aliyechuchumaa ni Shomari Mirundi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
WADAU WAKIPIGA PICHA YA KUMBUKUMBU NA KOCHA SUPER D
WADAU WAKIPIGA PICHA YA KUMBUKUMBU NA KOCHA SUPER D