Tangazo

Pages

Saturday, May 31, 2014

COSMAS CHEKA KUTETEA MKANDA WAKE WA UBINGWA LEO JUMAPILI YA JUNE 1


Bondia Cosmas Cheka akipima uzito
  
 

BONDIA Cosmas Cheka anatarajia kupanda ulingoni juni mosi kwa ajili ya kutetea taji lake la ubingwa wa TPBO anaoshikilia kwa kupambana na Suma Ninja katika ukumbi wa vijana social hall  wa Morogoro
 
Akizungumzia mpambano huo Cheka amesema amejiandaa kupigana kwa raundi kumi hivyo mashabiki waje kuona kazi anayoifanya akiwa ulingoni.
Bondia huyo ambaye anatamba sambamba na kaka yake Fransic Cheka  aliyekuwa bingwa wa WBF ambao alivuliwa kizembe amesema  yeye anataka afike mbali zaidi ya kaka yake huyo.
 
Pambano hilo linalosimamiwa na TPBO  litasindikizwa na mapambano ya utangulizi kati ya Kudura Tamimu atakaeevaana na Sadiki Yusufu,  wakati Mohamed Matimbwa ataoneshana umwamba na Twaha Kassimu 
 
Siku hiyo pia kutakuwa na uuzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama Mohamed Matumla vs Fransic,  Miyeyusho, Japhert Kaseba Vs Thomas Mashali , Floyd Mayweathar, Manny Paquaio, Saul ‘canelo’ alverez , Mike Tyson, Mohamed Ali, Ferex Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi
  
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’
 
Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kutakuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ameahidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta, Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakaoonesha uwezo wa hali ya juu wa kutupiana masumbwi.

TANGAZO BUJINGA TRADERS


Machinga complex (Karume stadium)
3rd floor, E4
P.O. Box 43063, Dar es Salaam
Tel: +255 754 623320 / +255 784 623320

Deals with: Promotional Materials as Large format printing (flex & rigid), embroidery, screen printing, heat press, graphics & design, corporate giveaways, vehicle branding, offset printing & sign boards

Thursday, May 29, 2014

BUJINGA TRADERS WATENGENEZAJI WA FLIERS,POSTERS,CARDS & CARENDERBUJINGA TRADERS WATENGENEZAJI WA  FLIERS,POSTERS,CARDS & CARENDER WAPO MACHINGA COMPLEX  4TH FLOOR E4, EAST WING
Email; johnson@bujingatradere.com,info@bujingatraders.com
www.bujingatraders.com
P.O. BOX 43064
Dar es Salaam Tanzania 
Cell+255765224522 Tel;+255773623320
Tanzania East Africa


BUJINGA TRADERS WATENGENEZAJI WA  FLIERS,POSTERS,CARDS & CARENDER WAPO MACHINGA COMPLEX  4TH FLOOR E4, EAST WING
Email; johnson@bujingatradere.com,info@bujingatraders.com
www.bujingatraders.com
P.O. BOX 43064
Dar es Salaam Tanzania 
Cell+255765224522 Tel;+255773623320
Tanzania East Africa

COSMAS CHEKA KUTETEA MKANDA WAKE WA UBINGWA JUMAPILI YA JUNE 1


Bondia Cosmas Cheka akipima uzito
  
 

BONDIA Cosmas Cheka anatarajia kupanda ulingoni juni mosi kwa ajili ya kutetea taji lake la ubingwa wa TPBO anaoshikilia kwa kupambana na Suma Ninja katika ukumbi wa vijana social hall  wa Morogoro
 
Akizungumzia mpambano huo Cheka amesema amejiandaa kupigana kwa raundi kumi hivyo mashabiki waje kuona kazi anayoifanya akiwa ulingoni.
Bondia huyo ambaye anatamba sambamba na kaka yake Fransic Cheka  aliyekuwa bingwa wa WBF ambao alivuliwa kizembe amesema  yeye anataka afike mbali zaidi ya kaka yake huyo.
 
Pambano hilo linalosimamiwa na TPBO  litasindikizwa na mapambano ya utangulizi kati ya Kudura Tamimu atakaeevaana na Sadiki Yusufu,  wakati Mohamed Matimbwa ataoneshana umwamba na Twaha Kassimu 
 
Siku hiyo pia kutakuwa na uuzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama Mohamed Matumla vs Fransic,  Miyeyusho, Japhert Kaseba Vs Thomas Mashali , Floyd Mayweathar, Manny Paquaio, Saul ‘canelo’ alverez , Mike Tyson, Mohamed Ali, Ferex Trinidad, Miguel Cotto na wengine wengi
  
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’
 
Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kutakuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ameahidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta, Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakaoonesha uwezo wa hali ya juu wa kutupiana masumbwi.

Wednesday, May 28, 2014

BONDIA KING CLASS MAWE AWAKEMEA MABONDIA WALEVI

Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimfua bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi
BONDIA namba moja katika uzito wake wa  light welterweight ,  Ibrahimu Class 'King class Mawe' ameibuka na kukemea vikali tabia ya mabondia kwenda katika ngumi kuangali na kuona ni kama wanakwenda kwenye starehe 'picnic'

aliyazungumza hayo katika ukurasa wake wa facebook mapema hivi karibuni akipinga matukio yanayofanywa na mabondia wakubwa nchini tanzania kwa kuingia ukumbini uku wakiwa wanakunywa pombe wakiwa wameshika chupa mbilimbili

bondia huyo alienda mbali zaini kwa kuwaeleza kuwa bondia anapo kwenda kwenye ngumi yupo kazini kwa kuwa ni kazi kama kazi nyingine hivyo anapokwenda aijalishi anacheza au achezi kwa siku hiyo hivyo lazima uwe na nidhamu kwa mashabiki ili upate wapenzi wapya zaidi

mana wapenzi wa ngumi wanapatikana kwenye ngumi uwezi mpenzi anaekujua kukutambulisha kwa mwingine ohoo 'King Class Mawe' yule ameshika bia awezi kukubali hata siku moja sana sana atakwambia mbona bondia mwenyewe mlevi namna hile ile inapoteza mwelekeo wa mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini

Class aliongea hayo hivi karibuni baada ya mabondia Mada Maugo na Thomasi Mashali kuamua kuzipiga kavu kavu kwa kitu kilichotambulika kuwa wao ni walevi tena wakiwa katika ukumbi wa ngumi frends corner manzese

kitendo hiki cha kupigana ovyo sikiingi mkono hata siku moja wakati walishapigana uringoni sasa watafute promota ili wapigane tena

kitendo chao cha kupigana ovyo kinatukosesha thamani sisi mabondia chipkizi ambapo mchezo huu wa masumbwi tunautegemea na tunaupenda kwa kuwa tuna malengo nao

ushauli wangu kwa mabondia wasifanye kuwa kwenda kwenye ngumi wanaenda kwenye starehe na kama unajiona wewe mlevi bora ubaki nyumbani kwako unywe basi na si vinginevyo kwa kulewa mbele ya mashabiki wa mchezo wa masumbwi nchini tunaonekana mabondia wote walevi tafadhalini mabondia wenzangu na samahani kama nitakuwa nimekukwadha kwa habari hizi yote tufanye tushilikiane ili mchezo wa masumbwi usonge mbele
Sunday, May 25, 2014

KOCHA WA MCHEZO WA NGUMI SUPER D KUFUNDISHA KWA NJIA YA DVD NCHI NZIMA


BAADHI ya wanamichezo hapa nchini hupitia hatua ngumu hadi kuyapata mafanikio na pia ni wachache kati yao wanapata mafanikio kwa nia rahisi kutokana na asili ya mazingira wanakoishi na michezo wanayocheza.
Mmoja wa mabondia na kocha maarufu nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akizungumza na Gazeti hili hivi karibuni anaelezea mikakati aliyojiwekea baada ya kucheza mchezo huo kwa muda mrefu kabla ya kuachana nao na kuamua kujitosa kuwa kocha kuwawezesha vijana.

Akielezea historia yake Super D anasema alianza kujihusisha na mchezo wa ngumi mwaka 1984 baada ya familia yake kupitia baba Mohamed Mhamila 'Checknolis' kuwataka watoto wote kufanya mazoezi kujiepusha na magonjwa kutokana na miili yao kuwa na asili ya unene.

"Baba wakati huo alikuwa ni baunsa akifanya kazi katika kumbi mbalimbali baada ya mazoezi mazito kwa hiyo alipenda na familia yake tuige mfano wake kufanya mazoezi kuweka miili safi tukabukabliana naye.," alisema Super D.

Anasema akiwa Shule ya msingi mwaka 1984 alianza mazoezi katika klabu ya ngumi ya Simba ambako alikutana na watoto wengi wa umri wake na kupata moyo wa kuendelea kuwa hivyo hata mara baada ya kumaliza shule ya msingi na kuwa bondia mkubwa akiwa katika klabu hiyo.

Anasema baba yake huyo ambaye alikuwa ni mpenda mchezo wa mieleka alitoa hamasa kwa watoto wote kufanya mazoezi bila kuchoka na kujikuta wakikubali na kuwa mabondia. wengine ni kaka yake Shaban Mhamila "Star boy, Rashid Mhamila 'Nature Fire' na 'Mohamed Hemed' 'Kadogo Ninja'. 

Anasema mjomba wake aliyeitwa Ilak Hudu ambaye alikuwa bondia wa zamani wa mchezo wa ngumi alikuwa akiwavusha barabara ya  Msimbazi kwenda katika klabu ya Simba kufanya mazoezi kila siku baada ya muda wa masomo na yeye akiwa miongoni mwao.

Anasema baada ya kupata mafanikio na kucheza akiwa na klabu ya Simba kwa mda mrefu aliamua kujiunga na klabu ya Reli kabla ya kujiunga na Amana lakini kwa wakati huo kipato hakuweza kupata mafanikio makubwa kutokana na msukumo wa mchezo huo kuwa mdogo. 

Super D anasema akiwa katika klabu hizo aliweza kucheza na mabondia mbalimbali na kufanikiwa kuwachapa na kuweka rekodi yake vizuri ambao ni Alfred Ngalomba, Husein Pazi, Oscar Manyuka, Safari Benard, Hajibu Salumu, Rajabu Mshindo, Rashid Ally, Mbwana Matum
la,Iddi Hamisi, na wengine wengi.
"Lakini pia nilichapwa na mabondia bondia Roja Mtagwa kichapo ambacho sitaweza kukisahau na alistahiri kunichapa kwa sababu jamaa anajua na mpambano ulikuwa na upinzani mkari ambapo katika raundi ya kwanza roja nilimdondosha chini na ilipofika raundi ya nne kwenda ya tano nikashindwa kwenda kutokana na kuumia taya hivi sasa anacheza mchezo huu nchini Marekani,." alisema Super D.

Super D aliongeza " Mimi kitaaluma ni mpiga picha nikaamua kujiweka kando kwa muda kufanya mambo mengine kwa sababu mchezo wa ngumi kama ilivyo mingine unahitaji uvumilivu hasa hapa nchini kwetu.," anasema.

Anasema aliacha kucheza mchezo huo mwaka 2002 kutokana na maisha na mchezo wa ngumi kuwa hauna maslahi ya kutosha ukimsababishia kufanya kazi zingine kabla ya kujiunga na kampuni ya Business Times inayochapisha magazeti ya Majira, Spoti Starehe, Maisha, Dar Leo na Business Times akiwa kama mpiga picha akianzia na gazeti la maisha.

Anasema miaka mitatu baadaye alikutana na aliyekuwa kocha wake wa zamani ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kinyogori Foundation, Habibu Kinyogoli ambaye alimshauri aendelee kujihusisha na mchezo huo ndipo alipojiunga kuwa kocha wa klabu ya Ashanti ya Ilala Dar es Salaam baada ya kupata kozi ya awali ya ukocha.

"Nikiwa Ashanti nafundisha watoto wadogo na wakubwa na nashukuru kwa sababu wazazi wa vijana wengi wanauelewa mchezo huu na kuwaleta watoto wao na natumaini watafanya hivyo zaidi.," anasema Super D.

Anasema alijiunga na klabu hiyo miaka miwili iliyopita na mpaka sasa ameweza kufundisha kwa mafanikio ambapo mabondia wake wameweza kushiriki mashindano mbalimbali yakiwemo ya ubingwa wa taifa wa mchezo huo na kufanya vizuri.

Super D anasema kutokana na juhudi zake alizozionyesha Shirikisho la Ngumi za Ridhaa nchini (BFT) kupitia Kaimu Rais wake Michael Changalawe amemtaka kuhakikisha mabondia anaowafundisha wanafikia viwango kwa sababu klabu yake ni miongoni mwa zinazotegemewa.

"Kutokana na jukumu hilo nililopewa na BFT nimeamua kupanua wigo wa kufanya kazi zangu kuhakikisha nawafikia wa
tanzania wengi na kuelewa mchezo huo wapate kuhamasika ambapo nimeandaa Video CD inayozungumzia maisha yangu nikishiriki mchezo huu zaidi ya mikaka 20 iliyopita na tayari ipo sokoni.," anasema.
Anasema CD hiyo iitwayo Super D Boxing Coach imeanza kuuzwa mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu katika mikoa ya Arusha, Tanga na Dar es Salaam ambapo hadi sasa ameuza nakala mbalimbali katika mikoa hiyo na kwamba anafikiria kusambaza katika mikoa mingine.

Anasema anaamini kuwa kupitia CD hiyo ataweza kufikia lengo la kuwapata mabondia wengi vijana ambao watashiriki mashindano mabalimbali yakiwemo ya Olimpiki ambayo yanatarajiwa kufanyika mwakani London nchini Uingereza.

Anasema video hiyo inaonyesha matukio mbalimbali yanayomhusu tangu alipoanza kucheza mchezo huo mwaka 1984, mapambano aliyocheza na kozi mbalimbali za ukocha wa mchezo huo alizoshiriki wakati akisomea mafunzo ya ukocha miaka michache iliyopita.

Super D amesema pia katika video hiyo amejumuisha matukio mbalimbali ya mabondia maarufu duniani wakiwemo Mike Tyson wa Marekani,Floyd Mayweather, Man Paquaio, Mohamed Ali wakiwa ulingoni kutokana na kwamba watakaoshuhudia video hiyo watapata fursa ya kujionea mbinu wanazozitumia mabondia hao wa kimataifa.

Amesema upatikanaji wa Video hiyo ni rahisi ambapo kwa Dar es Salaam inapatikana katika mtaa wa Uhuru na Msimbazi na pia zinauzwa mkononi katika mapambano mbalimbali ya ngumi yanayofanyika Jijini na kuongeza kuwa mabondia wengi maarufu akiwemo Japhet Kaseba, Mada Maugo, Maneno Osward wamenunua na kuiangalia video hiyo.

Super D anasema mbali na filamu hiyo kwa sasa ameanza mpango mwingine ambao kwa kushirikiana na taasisi ya Kinyogori Foundation iliyo chini ya kocha wake Habibu Kinyogoli wameandaa programu maalumu ya kuandaa matamasha kila wiki yanayohusisha mabondia mbalimbali ili kuhamasisha mchezo wa ngumi.

Anasema wanaamini kuwa kupitia programu hiyo vijana wengi wataweza kupata msaukumo kujifunza mchezo huo ambapo kwa sasa programu inaendelea katika Wilaya ya Ilala."Tunazifanya kwa sababu mpira katika soka utakuta watoto wanacheza mpira uwanjani lakini katika ngumi hiki kitu hakipo ndio maana tunaendesha matamasha haya.," anasema Super D.

Bondia huyo alizaliwa mwaka 1977 Ilala Jijini katika hosiptali Ya Ocean Road akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao ya watoto sita na kusoma shule za msingi na Sekondari kabla ya kuendelea na masomo ya juu Jijini Dar es Salaam.

BINGWA WA KUTUNISHA MISULI HAPATIKANA

Baadhi ya watunisha misuli wakionesha misuli yao wakati wa mashindano hayo
Katibu mkuu wa wizara ya habari, vijana utamaduni na michezo, Sihaba Nkinga (kushoto) akimkabidhi Muhammad Nauman cheti cha ubingwa wa michuano ya kutunisha misuli (katikati) Mwenyekiti wa Mashindano hayo Muhammad Ally,yaliofanyika juzi katika Ukumbi wa AT. Pj uliopo kinondoni jijini Dar es Salaam juzi. Picha na John Dande

Saturday, May 24, 2014

VURUGU ZATAWALA KATIKA NGUMI MSHINDI ASHINDWA KUTANGAZWA

Bondia Said Mbelwa kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Karama Nyilawila wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa UBO uliofanyika katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam hata hivyo mshindi ajapatikana kutokana na fujo zilizotokea katika raundi ya nane picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Zumba Kukwe kushoto akioneshana umwamba na Josef Njelekela wakati wa mpambano wao waliotoka droo picha na  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Zumba Kukwe kushoto akioneshana umwamba na Josef Njelekela wakati wa mpambano wao waliotoka droo picha na  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimpongeza khalid chokolaa baada ya kuibuka mshindi katika mpambano wake
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimpongeza khalid chokolaa baada ya kuibuka mshindi katika mpambano wake
Bondia Tasha Mjuaji kushoto akipambana na Rajabu Mahoja wakati wa mpambano wao

Bondia Mada Maugo kushoto akiwa anapigana na Thomas Mahali mwenye rasta
Bondia Mada Maugo akiwa anazipanga kavukavu na bondia Thomas Mashali walipiokutana katika ukumbi wa Frends Corner Manzese picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu

MPAMBANO wa ubingwa wa UBO umekosa kutangazwa mshindi mbele ya mashabiki baada ya vurugu kubwa kutokea katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita

ubingwa huo uliokuwa ukigombaniwa na mabondia Said Mbelwa na Karama Nyilawila alishindikana kupatikana mshindi baada ya raundi ya nane bondia Karama kumpiga kichwa Mbelwa cha wazawazi na kusababisha Mbelwa kuamaki kwa kulipiza kisasi na kumsukuma nje pia kumrukia kama ninja wakati alipotoka nje ya uwanja mpambano huo wa raundi kumi ulijikuta ukishia kwa raundi nane

na refarii pamoja na majaji wake kukimbia ukumbini wakiwaacha mashabiki bila kureta majibu ya mpambano huo hata hivyo mbelwa alirudi uringoni kwa ajili ya kuenderea kupambana na mpinzani waka alikimbia moja kwa moja kutokana na kuona kihama cha ngumi za mtaani zilivyuoanza

wakati huohuo bondia Mada Maugo alimpiga mwenzake Thomas Mashali kwa ngumi tatu mfululizo kavuvu 
bila kufata sheria ambapo ni kinyume na taratibu za mchezo wa masumbwi duniani kote mabondia hawo ambao wote walionekana wamelewa walipishana kiswahili mbele ya promota Ally Mwazoa ambaye ame haidi kabla ya kumaliza mwaka mabondia hawo wawe wameshapanda uringoni 
ambapo mpambano wao wa kwanza Thomas Mashali alimgalagaza kwa point Mada Maugo
katika mapambano ya utangulizi yaliyochezwa siku hiyo bondia Khalid Chokoraa ambaye ni mwanamuziki alimpiga kwa k,o ya raundi ya kwanza  Abdul Manyenza na Mwaite juma alimpiga Athumani Rashid wa Tanga kwa point wakati Selemani Galile alipigwa kwa point na Abdalah Pazi

Friday, May 23, 2014

MABONDIA WAPIMA UZITO KUTWANGANA JUMAMOSI MAY 24 MANZESEBondia Said Mbelwa akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake  leo na Karama Nyilawila wa kugombania ubingwa wa UBO katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mabondia Abdalla Pazi kushoto na Seleman Galile wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambani wao wa leo jumambosi ya may 24 katika ukumbi wa frend corner manzese dar ea salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
BONDIA SELEMAN GALILE AKIPIMA UZITO
Mabondia Abdalla Pazi kushoto na Seleman Galile wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambani wao wa leo jumambosi ya may 24 katika ukumbi wa frend corner manzese dar ea salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

 BONDIA SELEMAN GALILE
  BONDIA SELEMAN GALILE AKIPIMA AFYA KWA DAKTARI
BONDIA SELEMAN GALILE AKIPIMA AFYA KWA DAKTARI
Bondia Khalid Chokolaa kushoto akitunishiana misuli na Abdul Manyenza wakati wa upimaji uzito kwa ajili ya mpambano wao leo jumamosi ya may 24 katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es saklaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Wednesday, May 21, 2014

MABONDIA SAID MBELWA NA KALAMA NYILAWILA WAJIFUA KWA AJILI YA MPAMBANO WAO MAY 24

Bondia Said Mbelwa akipiga bag zito kwa ngumi nzito wakati akijiandaa na mpambano wake na Karama Nyilawila wa kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia wa siku nyingi Rashid Matumla kushoto akimnoa bondia Karama Nyilawila wakati wa mazoezi yake ya mwisho kabla ya kumkabili Said Mbelwa may 24 katika ukumbi frends corner manzese Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


Bondia Said Mbelwa akipiga bag zito kwa ngumi nzito wakati akijiandaa na mpambano wake na Karama Nyilawila wa kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frends corner manzese Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia wa siku nyingi Rashid Matumla kulia akimnoa bondia Karama Nyilawila wakati wa mazoezi yake ya mwisho kabla ya kumkabili Said Mbelwa may 24 katika ukumbi frends corner manzese Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Tuesday, May 20, 2014

Floyd Mayweather we acha tu!
Floyd Mayweather we acha tu! FLOYD Joy Sinclair Mayweather ni bondia anayetamba sasa, akiwa hajapigwa hata pambano moja la ngumi za kulipwa.
Siku hizi jina lake lililozoeleka ni Floyd Mayweather, Jr. japokuwa mashabiki wake wamezoea kumwita ‘Pretty Boy’ yaani kijana mtanashati.
Mmarekani huyu mwenye umri sawa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) japokuwa kidogo kinamtangulia kwani yeye alizaliwa Februari 24, 1977 ni bingwa wa madaraja matano.
Floyd, kumwita kwa urahisi zaidi jina lake, amepata ushindi mara nane katika mashirika mbalimbali ya ndondi duniani kwenye uzani wa aina tatu tofauti.

Anatikisa ulimwengu wa ndondi sasa hivi, ambapo anasema kwa vile yeye ni sawa na shoka lisiloogopa gogo, mundu usiochagua msitu, basi mpinzani wake ajaye hana haja ya kumjua.
Wiki chache zilizopita, Mayweather alishinda kwa pointi pambano dhidi ya Marcos Maidana mjini Las Vegas na kuunganisha mataji ya uzito wa Welter, akifikisha mapambano 46 ya ndondi za kulipwa bila kupoteza hata moja.

Maidana (30) kabla ya pambano la Mayweather alikuwa na rekodi nzuri, hivyo si mbaya wala mzuri sana, maana katika mapambano 38 ameshinda 35 na kukung’utwa matatu, lakini rekodi muhimu hapa alipigana na Khan 2011.
Mayweather ni mtu ambaye jarida maarufu la ‘Ring’ katika mwaka 1998 na 2007 limemwelezea kwamba ni mwanandondi bora. Kadhalika alichaguliwa na Chama cha Waandishi wa habari za Ngumi Marekani (BWAA) kuwa mpiganaji wa mwaka 2007, 2008, 2010, 2012 na 2013.
Huyu ndiye anashikilia mkanda wa WBC wa uzani wa Welter; mkanda wa WBA uzani wa Super Welter, ubingwa wa WBC Super Welter na mpokezi wa mkanda wa WBC Diamond Super Welter.
Kwa sasa kwenye ulingo ndiye anashikilia rekodi ya namba moja kwenye uzani wa Welter na kwa Uingereza wanasema ndiye ‘Pound-for-Pound Boxer’ duniani.
Hata hivyo hayo ni majigambo ya kawaida ya kizalendo ya Waingereza, lakini tovuti mbalimbali zimemtaja kuwa mkali sana ikiwa ni pamoja na majarida - Ring, Sports Illustrated, ESPN, BoxRec, Fox Sports na Yahoo!
Ni Floyd huyu huyu pia ambaye alishika nafasi ya kwanza kwenye orodha za jarida la Forbes na Sports Illustrated kama mmoja wa wanamichezo 50 wanaolipwa vyema zaidi 2012 na 2013 na madai zaidi ni kwamba ndiye anayelipwa vyema zaidi.
Kwa maana hiyo, hata kujidai kwake huko ulingoni si bure kwa sababu hata kifedha anajiweza sana na hata akistaafu katika umri wake huu hana cha kupoteza.
Pengine angependa kuacha simulizi ya kutopigwa kwake katika historia japokuwa linaonekana si jambo linalompa shida sana, kwani wengine wamefika mahali sasa wanamwita ‘Money Mayweather’.
Amedumu ulingoni kwa miaka 17 akiwa anajichotea ‘pesa ndefu ndefu’ tu na inasemwa mwaka juzi alivuta mkwanja wa pauni milioni 45 katika pambano moja dhidi ya Miguel Cotto.
Katika miaka yake ya masumbwi, Floyd amejikusanyia dola za Marekani zaidi ya milioni 350 Kwenye mitandao ya jamii, imeonekana kukiwa na ushindani au utupianaji maneno kati ya mashabiki wa Floyd na wa mwanasoka mahiri wa Hispania, Cristiano Ronaldo.
Kama alivyo Floyd kwenye ngumi katika uzani huo, Ronaldo sasa ndiye mwanasoka bora duniani baada ya kumvua ukuu huo Lionel Messi.
Floyd alizaliwa Grand Rapids, Michigan kwenye familia ya mabondia, ambapo baba yake, Floyd Mayweather Sr., alikuwa mwanamasumbwi katika uzito wa Welter na alipambana na watu sampuli ya akina Sugar Ray Leonard.
Ndugu za baba yake, Jeff Mayweather na Roger Mayweather pia walikuwa mabondia wa kulipwa ambapo Roger ndiye kocha wa Floyd kwa sasa.
Ni kana kwamba Floyd alichaguliwa kwa ajili ya ngumi, kwani alianza hayo tangu akiwa mdogo, na alipokua akamwambia bibiye:
“Nadhani bibi yangu ndiye alikiona kipaji changu kwanza. Wakati nakua nilimwambia; ‘bibi nadhani natakiwa sasa nitafute kazi’. Yeye alinijibu; ‘hapana, endelea kupigana tu’,” Floyd anatanabaisha.
Anaongeza kwamba alipofikisha umri wa miaka tisa alikuwa akiishi kwenye viunga vya New Jersey katika nyumba ya watu wa hali ya chini na wakati mwingine hawakuwa hata na umeme na ndani ya chumba walikuwa kama watu saba hivi.
“Watu wanaponiona ninayomiliki sasa hawawezi hata kufikiria nilikotoka na nilivyokuwa kwa shida lakini mie siwezi kusahau kamwe,” anasema Floyd.
Cio…


HIZI NI DVD ZA AINA MBALIMBALI ZINAZOTOLEWA NA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION DVD MPYA KUTOKA KWA SUPER D BOXING COACH AND PROMOTION AMBAZO ZINATARAJIWA KUWA HEWANI WIKI IJAYO NA MAPAMBANO YOTE YA NGUMI YATAKAYOFANYIKA WIKI IJAYO ZAIDI FIKA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI KARIAKOO PIGA SIMU 0713406938

TANGAZA NA BOZEN MAGAZINE UJULIKANE NA WENGI


JARIDA LA BOZEN LINALOTOKA KILA MWEZI LIKIWA LIMESHEHENI HABARI MBALIMBALI ZA MICHEZIO NA BURUDANI KILA KONA INAKARIBISHA MATANGAZO AMBAYO YATATOKA KWA RANGI NZURI NA YAKUPENDEZA NA MVUTO WA ALI YA JUU ZAIDI WASILIANA KWA NAMBA ZA SIMU PAMOJA NA E MAIL HAPO JUU

KHALID CHOKORAA KUPANDA ULINGONI MAY 24 KUZIPIGA NA ABDUL MANYENZAMwanamuziki na kiongozi wa bendi ya Mapacha watatu Khalid chokoraa anategemea kupanda ulingoni jumamosi ya tarehe 24 katika ukumbi wa friends corner  kuzipiga na bondia chipukizi mwenye uchu wa ushindi  muda wote awpo ulingoni Abdul manyenza. Chokoraa alisema muda mrefu amekuwa akifanya mazoezi ya  kujenga mwili na ya ngumi kwa muda mrefu na amekuwa akipigana na mabondia tofautitofauti mazoezini na kuona uwezo wao ni wa kawaida, hivyo anataka kuwaonesha kama ana kipaji kingine zaidi ya kuimbia, kwa sasa amekuwa akijifua katika gym ya bigright boxing ya mwananyamala  chini ya mwalimu wake bondia  mkongwe omar athuman ‘van dame’ kwa lengo la kumsambaratisha mpinzani wake ambae amekuwa akijitapa kumfukuza chokoraaa kwa kipondo kikali arudi kuimba. Siku hiyo ya jumamosi kutakuwa na mapambano ya ubingwa kati ya Karama nyilawila na Said Mbelwa  wakigombea ubingwa wa UBO-AFRICA ,wakisindikizwa na kina chokoraa na Abdul manyenza, Suleiman Galile akimkabili Abdala Pazi ‘kiroba’ nae  bingwa wa afrika Alan kamote wataoneshana umwamba na Adam ngange, Ramadhan kumbele atazipiga na Hassan kiwale”morobest” , idd athuman na julias kisarawe, nao wababe wa majigambo Zumba kukwe wataoneshana kazi na Kamanda wa makamanda, pia kutakuwa na pambano mengine mengi tu ya utangulizi ya mabondia wa tanga watazipiga na mabondia wa dare es salaam. Kama vile Athuman boxa wa tanga atazipiga na waite juma wa chalinze, Rajabu mahoja wa tanga atazipiga na kaisi wa darn a mengineyo yenye kuleta hamasa na burudani za mchezo wa ngumi, kwa vijana kuonesha vipaji vyao.

Monday, May 19, 2014

MAZOEZI YA KARAMA YAMTISHA THOMAS MASHALIMabondia Karama Nyilawila kushoto na Said Mbelwa wakitambiana wakati wa utambulisho wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa UBO may 24 katika ukumbi wa frende corner manzese katikati ni katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini PST Antony Rutta picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Karama nyilawila ni bondia anayetegemea kupanda ulingoni jumamosi ya tarehe 24 may kuzichapa na Said Mbelwa kuwania ubingwa wa UBO (universal boxing organisation) katika ukumbi wa friends corner – manzese. Hapo awali karama alikuwa azipige na Thomas mashali alievunja mkataba wa pambano kwa kutokuwa vema kwa pambano hilo na badala yake nafasi hiyo ikadondokea kwa said mbelwa ambaye ana vigezo vyote vya kugombania ubingwa. Karama Nyilawila akiwa katika mazoezi ya mwishomwisho alisema” Mashali ananiogopa baada ya kusikia mazoezi ninayofanya ni magumu na hatari kwa bondia atakae katiza mbele yangu, kwani kila siku asubuhi lazima nikimbie kutoka sinza ilipo gym yetu mpaka kibaha maili moja kwenda na kurudi na jioni napiga mfuko wa mazoezi(bag) raundi sita za dakika kumikumi na nacheza sparing raundi 15, aliposikia hivyo mdogo wangu mashali ikabidi achomoe kwa kutafuta visingizio mbalimbali na pambano limekuwa likibadirishwa tarehe kwa ajili yake na mwishowe akaweka wazi kuwa ananiogopa.karama aliendelea kwa kusema huyu mbelwa kavamia adhabu ambayo sio yake,asuburi tarehe ifike apate cha kumuhadithia mashali.
Nae kiongozi na mratibu wa pambano hilo Ibrahim kamwe amesema siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengi makali ya utangulizi yakiwemo ya  Suleiman tall akizipiga na Abdala pazi, ramadhan kumbele akimvaa morobest, zumba kukwe wakioneshana ubabe  na kamanda wa makamanda, idi athuman na julias kisarawe.
Wakati huohuo ndio tunamalizia makubaliano ya mwisho ya bondia chipukizi na mwanamuziki  mashuhuri wa bendi ya mapacha watatu Halid Chokoraa ambae amekubali kuzipiga na Abdul manyenza katika pambano la raundi nne kilogram 63. chokoraa kwa sasa yupo vizuri sana kwa mchezo wa ngumi na ana uwezo wa kumkabili bondia yoyote wa uzito wake.

TANGAZO LA SAHEL TRADING CO.LTD


Sunday, May 18, 2014

BONDIA COSMAS CHEKA AHAIDI KUTETEA TAJI LAKE VIZURI


 
Cosmas Cheka 'kulia' 
 
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Cosmas Cheka anatarajia kupanda ulingoni juni mosi kwa ajili ya kutetea taji lake la ubingwa wa TPBO anaoshikilia kwa kupambana na Suma Ninja katika ukumbi wa vijana socil hall  wa Morogoro

akizungumzia mpambano huo Cheka amesema amejiandaa kupigana kawa raundi kumi hivyo mashabiki waje kuona kazi anayoifanya akiwa ulingoni bondia huoyo ambaye anatamba sambamba na kaka yake Fransic Cheka ambaye alikuwa bingwa wa WBF ambao alivuliwa kizembe amesema yeye anataka afike mbali zaidi ya kaka yake huyo

mpambano huo utakaosimamiwa na TPBO utasindikizwa na mapambano ya utangulizi kati ya Kudura Tamimu atakae vaana na Sadiki Yusufu wakati Mohamed Matimbwa ataoneshana umwamba na Twaha Kassimu 

Siku hiyo kutakuwa pia na huzwaji wa DVD kali za ngumi wakiwemo mabondia wakali wanaotamba Duniani na hapa nchini kama Mohamed Matumla vs Fransic Miyeyusho,Japhert Kaseba Vs Thomas Mashali .Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
 
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'
 
Pamoja na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa  zawadi kwa mabondia na Kocha Super D  ambaye ame haidi kutoa, Gum Shit ,Clip Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali kwa mabondia watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi