Tangazo

Pages

Thursday, November 18, 2021

BONDIA RAMADHANI MIGWENE AMUWEKEA MIKWALA ALBANO CLEMENT BAADA YA KUKIMBIWA NA HABIBU PENGO

BONDIA RAMADHANI MIGWEDE baada ya kukimbiwa na mpinzani wake Habibu Pengo aliesaini nae kuzipiga mara ya kwanza sasa amebadilishiwa mpinzani na atacheza na bondia machachali kutoka mlandizi Albano Clement Desema 3 mpambano wa raundi nae utakaofanyika katika uwanja wa Kinesi uliopo Shekilango jijini Dsar es salaam akiongea wakati wa kutambulisha mpambano wa rasmi Migwede amesema kuwa yeye ni bondia hivyo uwezo wake una mruhusu kucheza na mtu yoyote atakaekuwa mbele yake ili mradi walingane uzito tu aliongeza kwa kusema unajua mimi ni bondia hivyo kazi yangu mimi ni kupigana hivyo siwezi kuacha kupigana kwa sababu Pengo kanikimbia hii ni kazi kama kazi nyingine nimepewa kazi na Albano hivyo ajipange kwa kuwa kipigo nitakachompa ni cha mbwa mwizi mimi ni mtu mwingine kabisa niwapo ulingoni hivyo ajitahalishe sasa sijui mwenzie kaona nini mpaka kakimbia na mimi naishi huyu kadandia treni kwa mbele sasa kipigo nitakachompatia atashindwa kuhadithia nae Clement amesema kuwa yeye ni bondia na ngumi ni kazi yake hivyo kazi kazi watakutana ulingoni sdiku hiyo mimi nimewapiga mabondia wakubwa kuliko yeye nimempiga Saidi Mundi kutoka Tanga bondia ambaye ni hatari sana kwa tanzania lakini nimemkalisha na cha moto kakiona nimemtwanga bila huruma bondia Seba Temba kutoka Morogoro na yeye alikuwepo katika mpambano huo sasa sidhani katika raundi nane hizo hatamaliza yote kwa yote mikono yangu ndio itakayo amua mpambano uho mbali na mpambano uho unaosubiliwa kwa hamu siku hiyo pambano ilingine kali litawakutanisha mabondia machachali Muksin Swalehe ;Alkasusu; na Cosmas cheka mabondia ambao walikuwa wakitafutana kwa mda mrefu sasa kumaliza ubishi Desemba 3 katika uwanja wa kinesi https://1.bp.blogspot.com/-RbPkG_taxIc/XRcPKNLqbvI/AAAAAAAAJ_c/XlGkZZvR4548IL8TEwRMKz7SJDTe-rPIACLcBGAs/s1600/IMG_7446.JPG

Monday, October 11, 2021

BONDIA RAMADHANI MIGWEDE ASAINI KUZIPIGA NA HABIBU PENGO OKTOBA 12 AWAITA MASHABIKI WA CHANIKA KUJITOKEZA SIKU HIYO

NA MWANDISHI WETU BONDIA RAMADHANI MIGWEDE amesaini mkataba wa kuzipiga na Habibu Pengo Novemba 12 mpambnano wa raundi kumi utakaofanyika jijini Dar es salaam akizungumza na wahandishi wa habari kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa Migede kasaini mkataba uho mbele ya katibu wa kamisheni ya ngumi za kulipwa Yahya Poli mpambano utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao bondia huyo mwenye maskani yake chanika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam atapambana na Pengo mpambano ambao utakuwa autabiliki kwani mabondia wote hawo wana uzoefu mkubwa katika mchezo wa masumbwi mbali na uzoefu waliokuwa nao pia wamekuwa wakiwapa vipondo wapinzani wao kadri wakutanapo nao ulingoni ambapo bondia migwede hivi karibuni alimchakaza vibaya tena bila huruma bondia keis ally kwa k,o ya raundi za awali nae Pengo amekuwa tishio katika kipindi cha hivi karibuni kwani alikuwa akicheza mapambano makubwa na yenye msisimko zaidi na kufurahisha mashabiki awapo ulingoni Pengo mwenye mashabiki luluki katika kitongoji cha mabibo na viunga vyake vya jirani amewataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuja kuangalia mchezo uho bila ya kukosa nae Migwede amesema alikuwa anamtafuta sana Pengo kwa udi na uvumba hivyo kwa sasa kaingia katika choo cha watoto hivyo kaingia katika 18 zangu hivyo nawaomba mashabiki wake wote wajitokeze kwani siku hiyo atafanya atakachotumwa na mashabiki zake wa chanika pamoja na vitongoji vya jirani hivyo wasikose kuja

Monday, October 4, 2021

DULA MBABE ULINGONI TENA OKTOBA 9 P.T.A SABASABA CHEKA NDANI NAE SIKU HIYO

NA MWANDISHI BONDIA ABDALLAH PAZI 'DULLA MBABE' atapanda ulingoni kwa ajili ya mpambano wake mwingine zidi ya Alex Kabangu kutoka DRC YA kONGo katika mpambano wa Raundi kumi akizungumza jijini Dar es salaam promota wa mpambano uho Kaike Siraju amesema kuwa pambano hilo la kimataifa litafanyika katika ukumbi wa P.T.A Saba saba siku ya kumamosi hivyo wapenzi na mashabiki wa mchezo wa masumbwi wanapaswa kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwani wameandaa ngumi zitakazoleta burudani ya kutosha siku ya Oktoba 9 Kaike aliongeza kwa kusema kuwa siku ya jumatano bondia kutoka Kongo Alex Kabangu atapokelewa na kufanya mahojiano na wahandishi wa habari za michezo siku hiyo hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa hivyo amewaomba mashabiki kujitokeza katika mpambano uho aliongeza kwa kusema kuwa siku ya ijumaa itakuwa ni kwa ajili ya kupima uzito na afya kwa mabondia hawo ambapo eneo la kupimia uzito ni katika viwanja vya Las Vegas vilivyopo mabibo sokoni hivyo mashabiki wotenaopmbwa kuja kushudia tukio hilo la upimaji uzito pamoja na Afya kwa mabondia ambapo tutaanza saa nne kamili asubui mpaka saa sita na nusu tutakuwa tumesha maliza mbali na mpambano uho kutakuwa na pambano lingine machachali litakalo wakutanisha bondia Cosmas Cheka kutoka Morogoro na Issa Nampepeche kutoka Dar es salaam wakizungu8mza kuhusu mpambano wake uho bondia Nampepeche amesema yeye ni bondi hivyo amejiandaa vizuri na matarajio yake ni ukushinda kwa .K.O ambayo aita wapa tabu majaji nae cheka amesema kuwa yeye ana wasiwasi kwani mazoezi kwake kama dawa kutwa mara tatu hivyo mpinzani wake ajipange

Monday, August 30, 2021

BONDIA IBRAHIMU CLASS AMTAMBIA NASSIBU RAMADHANI KUWA SEPTEMBA 24 ATAMPIGA KWA K,O

 

NA MWANDISHI WETU

 

BONDIA Ibrahimu Class ‘king Class Mawe’ amesema kuelekea katika mpambano wake na Nasibu Ramadhani Septemba 24 atokuwa na msalie mtume kutokana na Nasibu kuwa na maneno sana hivyo baasi anataka akate ngebe kwa kumpiga K.O mbaya sana ambayo aijawai kutokea

 

Katika maisha ya ngumi kwani ndio itakuwa mwisho wake wa kucheza mchezo wa masumbwi nchini hivyo basi naomba wapenzi wa mchezo wa masumbwi waje kuangalia mpambano wa kihistoria nitakaopambana na nasibu mana nimepania kucheza mchezo mzuri ambao utawafurahisha na kuwaburudisha wapenzi wa mchezo wa masumbwi nchini

 

Alijimwambafai Class ata hivyo mpambano uho wa raindi kumi unaosubiliwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa ngumi nchini umekuwa ukoingelewa kila kukicha na wapenzi mbalimbali wa mchezo huo wa masumbwi

Nae bondia Nassibu Ramadhani alijibumapigo kwa kusema kuwa kwa sasa Class atoboi kwani mpambano wa mara ya kwanza alibebwa na majaji hivyo kwa sasa nimemuandalia kipigo kitakatifu ambacho ato kisaau maishani mwake

 

Na mimi uwaga kwangu ni vitendo tu sinaga mambo mengi katika mchezo wa  ngumi mimi ndio sinaga mda wa kuongea ongea kumaliza maneno na kubwabwaja hovyo

 

Nae promota wa mpambano huo Rajabu Mhamila ‘Super D’ kutoka katika kampuni Tanzu ya Kizalendo ya Super D Boxing Promotion wamejipanga kuwaletea mapambano yenye tija kwa mabondia na yenye upinzani mkubwa ili wapenzi wa mchezo wa masumbwi wapate burudani

 

Aliongeza kwa kusema kuwa siku hiyo wameandaa mapambano saba yatakayopigwa siku hiyo uku tukiwa tumesha wasainisha mabondia Juma Choki atakaezipiga na Issa Nampepecvh mpambano wa raundi nane

 

Na tatali wamesha wasainisha mabondia vicent mbalinyi atakaezipiga na Shedrack Ignas wakati Waziri Rosta atakuwa akizipiga na Anuary Mlawa na Albano Clement atazipiga na Ramadhani Migwede na kwa upande wa kina dada bondia Agnes Kayange atazichapa na Lulu Kayage mpambano wa raundi siti na bondia Daudi Mwita atakuwa akizipiga na Saidi Ndilimo

Tuesday, August 3, 2021

MABONDIA CLASS NA NASSIBU WAPIGWA PINI NA SUPER D BOXING PROMOTION

 


NA MWANDISHI WETU


PROMOTA wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amewapiga pini mabondia Ibrahimu class na Nasibu Ramadhani kwa kuingia nao Mkataba wa kuzipiga Septemba 24 jijini Dar esa Salaam 


Akizungumza baada ya kuingia mkataba na mabondia hao uliotiwa saini mbele ya rais wa kamisheni ya ngumi za kulipwa TPBRC Agapeter Basili zilizopo keko Dar 


Super D amesema kuwa anapenda kufungua milango kwa wafadhili mbalimbali kujitokeza kudhamili mpambano uhu kwani mpambano ulikuwa unasubiliwa kwa hamu kubwa sana na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kwa kuwa hii ni dabi ambayo ina kila kitu katika mchezo wa masumbwi mana mabondia wana uwelewa wa mchezo wa ngumi pamoja na kujulikana kimataifa zaidi


aliongeza kwa kusema kuwa mchezo wa masumbwi sio uhadui kwani michezo ujenga urafiki pamoja na kujenga udugu, mabondia hawa ambao wamekuwa wakifanya kazi za uchambuzi wa mchezo wa ngumi katika TV 


ata hivyo kwa sasa wanaingia katika vita ya kutafuta heshima katika mchezo wa ngumi ambao wanaupambania kila kukicha


mbali na mabondia hao mabondia wengine waliokwisha saini mkataba kupitia kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ni Issa Nampepeche ambaye atavaana na Juma Choki katika mpambano wa kugombania ubingwa wa taifa

SUPER D AWACHONGANISHA TENA IBRAHIMU CLASS NA NASIBU RAMADHANI KUZIPIGA SEPTEMBA 24


Promota wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiwanyoosha mikono juu mabondia Nasibu Ramadhani kushoto na Ibrahimu Class mara baada ya kusaini mkataba wa kuzichapa Septemba 24 jijini Dar esa Salaam

 Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Nassibu Ramadhani wamesaini mkataba wa kuzipiga kwa mara nyingine tena kupitia kampuni tanzu ya kizarendo ya Super D Boxing Promotion mpambano unaotarajia kuzipiga septembar 24 jijini Dar es salaam akizungumza mara baada ya kuwasainisha mikataba mabondia hawo promota wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' 


Amesema kuwa mpambano uho unakwenda kuweka historia mpya ya mchezo wa masumbwi nchini Tanzania kwa kuwa viwango vya mabondia hawo ni vya kimataifa hata hivyo mabondia hawo wenye wa penzi wengi wa mchezo huo kwa kuwa na vigezo vikubwa vya kujua mchezo wa ngumi

Katika mpambano wa kwanza uliopigwa miaka kadhaa iliyopita Class alibuka na ushindi wa point na Nassibu akakubali mpambano uho ameshindwa hivyo alikuwa anaomba marudiano


ahidha kampuni hiyo imeingia mkataba wa mpambano mwingine tena kati ya Issa Nampepecha na Juma choki ikiwa pia mpambano huo ni wa marudiano


hata hivyo katika mpambano wa kwanza katika chezo uho Choki alishinda kwa T.K.O ya raundi ya tatu na kuibuka na ushindi mara ya Nampepeche kupigwa na kuvuja Damu nyingi sana katika mchezo huo


ambapo mpambano uhuo ulikuwas ukichezeshwa na refarii Antoni Ruta wakigombania mkanda wa ubingwa wa P.S,T mpambano uliokuwa uchezwe kwa raundi kumi


Thursday, June 17, 2021

HAMADI FURAHISHA KUZIPIGA NA KOCHA WAKE GODFREY POLINO JUNE 27 KIFA MBURAHATI

HAMAD FURAHISHA

BONDIA HAMAD FURAHISHA ambaye ya sasa ameingia katika ngumi za kulipwa kwa mara ya kwanza june 27  atapanda ulingoni kuzichapa na Godfrey  Polino mpambano wa raund 4 kg 55 katika uwanja wa Kifa uliopo Mburahati

Mpambano huo utafanyika katika uwanja wa kifa uliopo Mburahati umekuwa ukisubiliwa kwa hamu kubwa sana ambapo mabondia hawo ni mtu na kocha wake zamani wakati Polino alikuwa kocha uku Furahisha alikuwa bondia katika ngumi za Ridhaa wote wakiwa katika kam,bi ya JKT

Mabondia hawo watapigana kwa mara ya kwanza wakiwa na historia kubwa ya mchezo wa masumbwi katika ngumi za ridhaa na kuliletea sifa Taifa lakini kwa sasa watapigana katika ngumi za kulipwa uku kila mmoja akitaka kukuonesha

Umwamba wake katika ulingo jinsi anavyozipiga kwa ufundi zaidi majina ya Polino na Furahisha sio mageni katika ulimwengu wa masumbwi nchini ila ni mageni katika ngumi za kulipwa ambapo kupitia mabondia hawo mashabiki watapata burudani ya kutosha ya mchezo wa masumbwi nchini

akizungumza na mwandishi wa habari hizo Hamadi Furahisha anasema kuwa ngumi alianza mwaka 2009 Yombo dovya boxing Clab iliyopo chini ya kocha haji Pela ambaye mpaka leo hii wapo pamoja 

alishiriki katika mashindano mbalimbali ya masumbwi ya Ridhaa yakiwemo mashindano ya clab bingwa pamoja na ya taifa na kufanikiwa kuchaguliwa na timu ya Taifa ya ngumi  mwaka 2016 ambapo alidumu katika timu ya Taifa mpaka mwaka 2018 ambapo alipata nafasi ya kujiunga na JKT hata hivyo baada ya miaka kazaa akakosa ajira na sasa yupo mtaani na ameamua na kujiunga na ngumi za kulipwa 

anakumbuka kipindi hicho yupo JKT walipita mabondia ambao ni maarufu na mashughuli kwa sasa akiwepo Hassani Mwakinyo Salim Matango na wengine ambao nao waliachana na JKT na kujiunga na ngumi za kulipwa mara moja 

katika mchezo wa masumbwi yeye alivutiwa zaidi na Ismail Galiatano ambae nae ni bondia wa jeshi mpaka hivi sasa ndio aliekuwa akimpenda tangu anaanza ngumi mpaka sasa na kwa nje anamkubali zaidi

Bondia Manny Paquai ambaye amekuwa akimkubali zaidi kwa mapigo yake ya kasi na jinsi anavyo zitendea aki ngumi apiganapo ulingoni

Furahisha amemwambia Polino kuwa supu aitiwi nazi ikitiwa nazi inakuwa mchuzi hivyo kipigo atakachompa ni cha pekee kwani kipigo hicho akijawai kutokea tangu aanze mchezo wa masumbwi nchini

akizungumza mabondia wa Tanzania amewasii mabondia wasiwe wanaingia mitini pindi wanapopewa mapambano na yeye kwani yeye anamikono miwili na wao miwili 

pia ilitoa wito kwa wazazi kuwaruhusu vijana wao pamoja na watoto kuwapa sapoti ili wacheze mchezo wa masumbwi kwani kwa sasa ni ajira na inaweza kukutoa sehemu moja kwenda nyingine hii ni kazi kama zilivyo kazi zingine wanazofanya watu maofisini

aliongeza kwa kusema anampiga kocha wake pia mabondia wengine wajipange foleni ambao watakuwa katika uzito wa kg 55 kuwa hizi ni salam kwao

asesema anawaomba sapoti kwa mashabiki zake wote wa dabo kibini wakionozwa na Habib Othumanbig kuja kumunga mkono na kumsapoti kwa ali na mali

mpambano huo ulioratibiwa na Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka kampuni Tanzu ya Kizalendo ya Super D Boxing Promotion umeandaliwa na Kwame Sports Promotion chini ya Promota mkuzaji wa Vipaji Kwame Hamisi Matwani mpambano utafanyika june 27

 

Friday, March 12, 2021

BONDIA JONAS SEGE NA TWAHA KIDUKU KUPANDA ULINGO MMOJA MARCH 19 NA MABONDIA WA MATAIFA MENGINE


 Na Mwandishi Wetu


BONDIA Jonas Segu 'Black Mamba' ametamba kumpiga mpinzani wake Hanock Phili kutoka Malawi akizungumza mbele ya wahandishi wa habari kusiana na mpambano wake uho utakaofanyika March 19 katika ukumbi wa Ubungo Plaza


Segu amesema kuwa yeye alienda nchini Africa ya kusini na kuhishi uko kwa ajili ya mchezo wa ngumi na kufanikiwa kuchukuwa ubingwa wa  WBF ambao ata utetea siku hiyo ata hivyo amekuwa apati mapambano ya ndani kutokana na mabondia wengi kumkwepa baada ya kutembeza kipigo kwa mabondia kadhaa wa Tanzania

ambapo alishawai kumchapa Habibu Pengo Idd Pialali na alifanikiwa kumchapa Mfaume Mfaume ata hivyo kutokana na Figisu majaji wakatoa Droo sasa nimeruni nchini Tanzania na mpambano huu ndio utakuwa wa kwanza kwangu kucheza baada ya miaka mitano iliyopita ambapo sijacheza katika ardhi ya Tanzania naomba mashabiki wa ngumi morogoro dar es salaam pwani Tanga na mikoa mingine yote waje kuona ngumi ambazo zenye radha na manufaa katika mchezo huu wa tarehe 19 march


nae promota wa mpambano huo Evalist Elnest 'Mopao' amesema mbali na mpambano huo kutakuwa pia na mpambano wa Twaha Kiduku na Tishibangu Kayembe wa Kongo na mpambano wa kina dada utakao wakutanisha  Najma Isike na Halima Bandola pia kutakuwa na takribani jumla ya mapambano nane tu kwa siku hiyo


hivyo naomba wapenzi wa ngumi waje mapema kuangalia ngumi nzuri zilizo andaliwa vema kabisa kwa galama nafuu kabisa

Thursday, February 18, 2021

BONDIA JEMS KIBAZANGE AMTILIA MKWALA MZITO HAMIDU KWATA WATAZIPIGA APRIL 2 P.T.A SABA SABA

JEMS KIBAZANGE 'DOG LA KIVITA'
 Na Mwandishi Wetu


BONDIA Jems Kibazange 'Dog la Kivita' ameapa kuwa lazima amsambalatishe Hamidu Kwata ifikapo April 2 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba mpambano uho uliopewa jina la 'No Pain No Gain Nigth Fight' kuwa ana uwakika wa kumchakaza Kwata kama mfuko wa mazoezi

akizungumza wakati wa mazoezi yake katika     GYM, ya kocha Maneno iliyopo Manzese Midizini amesema kuwa mimi ndio kiboko ya mbwa koko na kwata ajakutana na viama mimi nimesha wapiga mabondia wote waliopo katika uzito wangu ndio
mana natamba na kwa Tanzania hii mimi sina mpinzani kwani mabondia wote kwangu ni viande nashangaa huyu amekubali vipi kupigana na mimi

naisi njaa tu inamsumbua hivyo naona pesa zake atakazo zipata zitaisha katika matibabu yake kwa kuwa nitampiga bila ya huruma kwani mimi ni kamanda katika mchezo huu wa masumbwi na akuna mtu asiejua uwezo wangu niwapo ulingoni

nakuwa mtu mwingine kabisa ndio mana mtaani kwetu wananita Dog la Kivita na vita hii itaenda kumwangamiza Kwata na kumsababishia kilema cha maisha kwani ngumi ni mchezo wangu nilio uwekea nadhiri ya kuendesha maisha yangu hivyo sito kubali bondia mdogo kama huyu aje kuniaribia kiraisi tu

Nae Promota wa Mpambano Uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia


vicent Mbilinyi vs Deo samweli rd 10
Ramadhani Mbegu "Migwede" vs Albano Clement Rd 8
4.Daudi Mwita vs Abdul Ubaya Rd 6
5. Hamidu kwata vs James kibazange 10 rd
6.Mustafa Khalidi vs Mrisho mzezele rd 6
7.kassim Ahmad vs Gabriel Chola rd 8
8.Juma Abdul vs Hamza Mchanjo rd6
9.Veronika Thomas vs Fatima Yazidu rd6
10.Frank Lucian vs Juma Kaiza rd8

pia kutakuwa na burudani mbalimbali kwa ajili ya kusapoti mchezo uho utakao kuwa siku ya Ijumaa kuu ya Pasaka


Wednesday, February 17, 2021

SUPER D AWASAINISHA MABONDIA MAONO ALLY KUZIPIGA NA MESHACK MWANKEMWA APRIL 2

 

MAONO ALLY

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Maono Ally kutoka Bagamoyo mkoa wa Pwani amesaini mkataba wa kuzipiga na Meshack Mwankemwa kutoka Mbeya mpambano utakaofanyika April 2 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba mpambano wa raundi kumi uzito wa kg69 kutafuta nani zaidi kati yao

mpambano uliopewa jina la No Pain No Gain Fight Night mabondia hawo watazipiga siku hiyo katika mpambano ulio andaliwa na kiampuni Tanzu ya Kizarendo ya Super D Boxing Promotion


Maono amesema kuwa katika mpambano uho atokuwa na msalia mtume kwani ngumi kwake ni kazi kwa kuwa mabondia wengi wamekuwa wakimkimbia pindi wanapo pangiwa mapambano na yeye hivyo Mwankemwa akae tayari kwa kipigo tu


Na afanye mazoezi ili apunguziwe kipigo ingawa kipigo kipo pale pale nitampiga mwankemwa kama mfuko wa mazoezi kwani nimejiandaa vya kutosha na sina wasiwasi na pambano hilo


kwa upande wa Mwankemwa amesema asnashukuru kupata mpambano uho utakaofanyika Dar hivyo nipo vizuri na nategemea ushindi ambao sito washirikisha majaji ambapo nitampiga K,O mbaya sana aikuwai kutokea

Nae Promota wa Mpambano Uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia


vicent Mbilinyi vs Deo samweli rd 10
Ramadhani Mbegu "Migwede" vs Albano Clement Rd 8
4.Daudi Mwita vs Abdul Ubaya Rd 6
5. Hamidu kwata vs James kibazange 10 rd
6.Mustafa Khalidi vs Mrisho mzezele rd 6
7.kassim Ahmad vs Gabriel Chola rd 8
8.Juma Abdul vs Hamza Mchanjo rd6
9.Veronika Thomas vs Fatima Yazidu rd6
10.Frank Lucian vs Juma Kaiza rd8

pia kutakuwa na burudani mbalimbali kwa ajili ya kusapoti mchezo uho utakao kuwa siku ya Ijumaa kuu ya Pasaka

Tuesday, February 9, 2021

SUPER D AMSAINISHA DEO SAMWELI KUZIPIGA NA VICENTI MBILINYI APRIL 2 P.T.A SABA SABA


Bondia Deo Samweli kushoto akibadilishana mkataba na Promota wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga na Vicent Mbilinyi mpambano utakaofanyika April 2 katika ukumbi wa P.T.A SABASABA siku ya Ijumaa kuu ya Pasaka

Bondia Deo Samweli akisaini mkataba wa kuzipiga na Vicent Mbilinyi mbele ya promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' mpambano utakaofanyika April 2 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba


Na Mwandishi Wetu


BONDIA DEO SAMWELI amesaini mkataba wa kuzipiga na Vicenti Mbilinyi mpambano wa raundi kumi kumi utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Saba saba siku ya Ijumaa Kuu  April 2

Akisaini mkataba uho mbele ya mkurugenzi wa kampuni Tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa amekuja kufanya kazi hivyo mashabiki waje kwa wingi kwani kazi atakayo ifanya siku hiyo si ya kitoto

aliongeza kwa kuserma kwa sasa anarudi upya katika masumbwi kwani mwishoni mwa mwaka jana alijeruhiwa kidogo hivyo ame mtahadharisha mbilinyi kufanya mazoezi kweli kweli kwani siku hiyo akuto kuwa na msalie mtume

Katika mpambano uho atampiga kipigo cha mwana ukome ambapo mbilinyi ato weza tena kumtaka Deo Samweli warudiane nae tena

Nae Promota wa mpambano uho Super D amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na burudani ya masumbwi ni vitasa kwa kwenda mbele katika mpambano uliopewa jina la 'No Pain No Gain Fight Nigth'

pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi ya mabondia mbalimbali ambapo Jemsi Kibazange atazipiga na Hamidu Kwata wakati kassim ahamdi atazidunda na Gabriel Chola na Ramadhani Migwede atazichapa na Albano Clement na mpambano mwingine wa kutisha utakuwa kati ya Maono Ally kutoka bagamoyo atazipiga na Meshacki Mwankemwa kutoka Mbeya na Abdul Ubaya kutoka Mlandizi atazidunda na Daudi Mwita wa Dar

 

Saturday, January 9, 2021

BONDIA AMOSI MWAMAKULA KURUDI KIVINGINE KUZIPIGA FEB 6

Kocha wa mchezo wa masumbwi na mateke /kicki Boxing Esmail Abdallah 'Van Dame' kushoto akimwinua mkono juu bondia Amosi Mwamakula kwa ajili ya kumtambulisha katika mpambano wake wa kuzipiga Feb 6 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na Hashimu Kilaga

 Kocha wa mchezo wa masumbwi na mateke /kicki Boxing Esmail Abdallah 'Van Dame' kushoto akimtambulisha bondia Amosi Mwamakula kwa ajili ya  mpambanmo wake wa kuzipiga Feb 6 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba na Hashimu Kilaga


Na Mwandishi Wetu


BONDIA AMOSI MWAMAKULA ametambulisha mpambano wake wa kuzipiga na Hashimu Kilaga mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Saba saba SIKU YA FEB 6 Dar es salaam


akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpambano uho kocha wa masumbwi na Mateke Kicki Boxing Esmail Abdallah 'Van Dame' amesema kuwa mwamakula amejiandaa vya kutosha hivyo mpinzani wake nae ajiandae vya kutosha kwani kwa sasa amerudi kivingine


ameongeza kwa kusema kwa sasa wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya pambano hilo ambalo linandaliwa kwa ubora wa aina yake kwani maandalizi ya mpambano uho sasa yamepamba moto


alieleza kuwa mbali na pambano hilo la masumbwi pia kutakuwa na mapambano mengine ya ngumi ambapo bondia Lulu Kayage atazipiga na Agnes Kayange na Jitu Rajabu kutoka kwa Super D Coach atazipiga na Daniel Mwakafyale na Shabani kaoneka atazipiga na Butel Obedi mambano huo unaletwa na Jamukaya kwa kushilikiana na Black Panda utakuwa na kingilio cha shilingi 10,000 TU kwa siku hiyo 


pia kutakuwa na ngumi za mateke kick Boxing na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa Sanaa Michezo Na Utamaduni 

Friday, January 1, 2021

SUPER D BOXING PROMOTIOBN KUMRUDISHA HAMISI MAYA ULINGONI APRIL 2 SABASABA


                                                  BONDIA HAMISI MAYA


 

Hamisi Maya ambaye ni bingwa wa GBC mkanda unaotambulika Duniani  akwa amevalishwa mkanda baada ya kumdunda Piergiulio Ruhe wa ujerumani na kufanikiwa kurudi na mkanda

NA MWANDISHI WETU

BONDIA HAMISI MAYA sasa kupanda ulingoni rasmi April 2 katika ukumbi wa Sabasaba Hall uliopo katika viwanja vya Sabasaba akimvaa bondia Alvin Omondi wa Kenya mpambano wa Raundi 8 utakaopigwa katika uzito wa KG 66


Akizungumza kuusu mpambano uho Mratibu wa pambano hilo Chaurembo Palasa amesema kuwa baada ya muda mrefu kukaa kimya kwa bondia huyo sasa anaibuliwa upya na kampuni tanzu ya kizarendo ya Super D Boxing Promotion ambao ndio waandaaji wa mpambano uho kwa sasa


Hamisi Maya ambaye ni bingwa wa GBC mkanda unaotambulika Duniani ambapo mpaka sasa anasifika kwa kuwapiga mabondia mbalimbali akiwa nje ya nchi ambapo alishawai kumpiga K,O mbaya sana Jems Onyango wa Kenya mpambano uliofanyika Charter Hall, Nairobi  Kenya na kurudi na ubingwa wa Afrika na kumgalagaza bila ya huruma bondia Piergiulio Ruhe wa ujerumani na kufanikiwa kurudi na mkanda


Alisema Palasa ata hivyo mapromota wengi wamekuwa wakimkwepa Maya kutokana na uchezaji wake awapo ulingoni ni kama bondia aliyekusudia kuuwa mtu akiwa mchezoni ndio mana ajapata mapambano tangu mwaka 2019 hata hivyo kupitia kampuni yetu ya Super D Promotion tunampa nafasi ya kuonesha Kipaji chake kwa mara nyingine kwa mwaka uhu 2021

aliongeza kwa kusema kuwa mbali na mpambano uho pia kutakuwa na mapambano mengine ya lkukata na shoka ambapo bondia machachali awapo ulingoni Vicent Mbilinyi atazipiga na George Onyango na Fransic Miyeyusho atazipiga na Gabriel Chola wakati Hamidu Kwata atazidunda na Jems Kibazange na juma Abdul wataoneshana kazi na Hamza Mchanjo na Bakari Magona atazipiga na Emanuel Mwakyembe


SUPER D BOXING PROMOTIOBN KUMRUDISHA HAMISI MAYA ULINGONI APRIL 2

 NA MWANDISHI WETU

BONDIA HAMISI MAYA sasa kupanda ulingoni rasmi April 2 katika ukumbi wa Sabasaba Hall uliopo katika viwanja vya Sabasaba akimvaa bondia Alvin Omondi wa Kenya mpambano wa Raundi 8 utakaopigwa katika uzito wa KG 66


Akizungumza kuusu mpambano uho Mratibu wa pambano hilo Chaurembo Palasa amesema kuwa baada ya muda mrefu kukaa kimya kwa bondia huyo sasa anaibuliwa upya na kampuni tanzu ya kizarendo ya Super D Boxing Promotion ambao ndio waandaaji wa mpambano uho kwa sasa


Hamisi Maya ambaye ni bingwa wa GBC mkanda unaotambulika Duniani ambapo mpaka sasa anasifika kwa kuwapiga mabondia mbalimbali akiwa nje ya nchi ambapo alishawai kumpiga K,O mbaya sana Jems Onyango wa Kenya mpambano uliofanyika Charter Hall, Nairobi  Kenya na kurudi na ubingwa wa Afrika na kumgalagaza bila ya huruma bondia Piergiulio Ruhe wa ujerumani na kufanikiwa kuruni na mkanda


Alisema Palasa ata hivyo mapromota wengi wamekuwa wakimkwepa Maya kutokana na uchezaji wake awapo ulingoni ni kama bondia aliyekusudia kuuwa mtu akiwa mchezoni ndio mana ajapata mapambano tangu mwaka 2019 hata hivyo kupitia kampuni yetu ya Super D Promotion tunampa nafasi ya kuonesha Kipaji chake kwa mara nyingine kwa mwaka uhu 2021

aliongeza kwa kusema kuwa mbali na mpambano uho pia kutakuwa na mapambano mengine ya lkukata na shoka ambapo bondia machachali awapo ulingoni Vicent Mbilinyi atazipiga na George Onyango na Fransic Miyeyusho atazipiga na Gabriel Chola wakati Hamidu Kwata atazidunda na Jems Kibazange na juma Abdul wataoneshana kazi na Hamza Mchanjo na Bakari Magona atazipiga na Emanuel Mwakyembe