Tangazo

Pages

Friday, November 29, 2013

PIKI PIKI YA MABONDIA NASSIBU RAMADHANI NA MOHAMED MATUMLA YAONESHWA


Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25 katika ukumbi wa friends corner wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mlatibu wa mpambano uho Kaike Siraju Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mratibu wa mpambano wa ndondi Kaike Siraju akiojiwa akiwa juu ya pikipiki itakayogombaniwa na mabondia Mohamed Matumla na Nassibu Ramadhani siku ya Desemba 25 Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana  na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25  wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mlatibu wa mpambano uho Kaike Siraju Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Meneja Masoko wa kampuni ya haojue,Wawa Laida kulia akiwaonesha pikipiki itakayogombaniwa Dar es salaam jana  na mabondia Nassibu Ramadhani kushoto na Mohamed Matumla siku ya Desemba 25  wengine wa pili kushoto ni Rashidi Matumla,Christopher Mzazi na mlatibu wa mpambano uho Kaike Siraju Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MABONDIA JAPHET KASEBA, ALIBABA KUZIPIGA DESEMBA 21 FRIENDS CORNER HOTEL DARMabondia Japhet Kaseba wa jijini Dar es Salaam, na Alibaba Ramadhan wa jijini Arusha, wanategemea kupanda ulingoni siku ya jumamosi ya tarehe 21 Decemba, mwaka huu katika ukumbi wa friends corner hotel,kuzichapa katika pambano la kirafiki lisilo la ubingwa..
Pambano hilo liloandaliwa na Promota Ibrahim Kamwe chini ya  BigRight Promotion kwa usimamizi wa PST, pia litakuwa na mapambano  mengine tisa ya utangulizi ambayo yatawakutanisha mabondia kama Karage Suba na Fadhil Awadh, watakaozichapa kuwania ubingwa wa Mkoa katika uzito wa wealter Kg66 pambano la raundi kumi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe, alisema kuwa  zaidi ya hayo mapambano ya ubingwapia mahasimu wawili wa uzito wa juu Lusekelo Daudi atazipiga na  Mbaruku Kheri (ndota) ikiwa ni marudio ya mchezo wao wa kusisimua uliokosa mshindi. 

Mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni pamoja na Bondia Adam Yahaya (Baby Edo) atazipiga na Harman Richard, mkongwe Enerst Bujiku (Tyson) atacheza na Shah Kassim,  kukumbushia Enzi za akina Stanley Mabesi , Jocky Hamis mkongwe wa zamani atazipiga na bondia sawa na mwanae  mbena Rajabu.

Wengine ni Issa Omar  atazipiga na Haji Juma wa Tanga, Moro Best atapigana na Shafii Ramadhan, huku Shaban Bodykitongoji akizipiga na Mwinyi Mzengera. 

Mabondia wote wameshasaini mikataba ya makubaliano ya mchezo huo na wameshaingia kambini kujiandaa na mechi zao hizo ambazo zina upinzani wa hali ya juu.

kinachoendelea kwa sasa ni kumalizia mchakato wa ulinzi kutoka Kampuni ya Kiwango Security na jeshi la polisi.
 Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo vitakaokuwa vikitolewa na Super D kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha ngumi

Tuesday, November 26, 2013

MBABE WA MASUMBWI MANNY PACQUIAO KUTEMBELEA MJI WA TACLOBAN BAADA YA KUKUMBWA NA KIMBUKA KIKALI TYPHOON HAIYAN!!


Mwana masumbwi Manny Pacquiao ameahidi kutembelea maeneo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino hasa kwenye mji wa Tacloban siku chache zijazo baada ya kutetea ubingwa wake.
Mashindano ya kimataifa ya ngumi za uzani wa kati yametangazwa jana Jumapili kwenye vituo vinne vya wazi mjini Tacloban ili kuwatia moyo wakazi wa maeneo hayo baada ya kukumbwa na kimbunga kilichoathiri maisha yao.

Katika mashindano hayo mbunge Pacquiao akaibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake Brandon Rios kwa raundi 12 huko Maca ,na kutangaza kuwa kipaumbele chake ni kutembelea mji wa Tacloban kama alivyowaahidi wakazi wa mji huo.Pacquiao ameongeza kuwa timu yake inashughulikia kupata taarifa zitakazo mwezesha kusafiri hadi kwenye mji mkuu wa jimbo la Leyte na atakuwa huko ndani ya siku chache zijazo
Baadhi ya wafilipino wakifuatilia mpambano wa manny paquaio

.

WAKIFATISSHA WIMBO WA TAIFA WAKATI UNAPIGWA UKU WAO WAKIANGALIA MPAMBANO HUO KUPITIA LUNINGA

YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH AMPONGEZA CHEKA KUKIMBIA MBIO ZA UHURU MARATHON RAIS -TPBO

                             YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                                                                          RAIS -TPBO  
                  NDG WAANDISHI NA WADAU WA MICHEZO WOTE KWA UJUMLA WETU,

AWALI YA YOTE NAPENDA KUTUMIA FURSA HII KUMPONGEZA BONDIA BINGWA WA DUNIA WA WBF,FRANCIS CHEKA KWA KUKUBALIANA NA WAZO LANGU LA KUMUOMBA AJIUNGE NA KUWA MIONGONI MWA WATANZANIA WATAKOJITOKEZA TAREHE 08-12-2013 JIJINNI DAR-ES0SALAAM KUUNGANA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA MH, JAKAYA MRISHO KIKWETE KUKIMBIA MBIO ZA UHURU MARATHON ZENYE KUADHIMISHA UHURU WA TANGANYIKA.

KWA KWELI NILIKUWA NA MATEGEMEO MAKUBWA SANA KWAMBA FRANCIS CHEKA ANGENIKUBALIA WAZO LANGU HILO ,AKIWA KAMA NI MTANZANIA ANAYEIPENDA KWA DHATI NCHI YAKE KWANI AMESHAIPATIA SIFA KUBWA TANZANIA KWA KUTWAA TAJI LA UBINGWA WA NGUMI WA DUNIA  DHIDI YA MMAREKANI PHILL WILLIAM HAPO TAREHE 30-08-2013 .

NA NILISHAWISHIKA KUMSHAURI CHEKA AINGIE KWENYE MBIO HIZI BAADA YA KUVUTIWA NA TAARIFA ZA WAANDAAJI KWAMBA KATIKA MBIO HIZO YUMO BINGWA WA DUNIA WA MBIO HIZO KUTOKA KENYA, NIKAONA IKO HAJA KWA  MABINGWA WA TASNIA ZISIZOFANANA  WAKANOGESHA MBIO HIZI ZA UHURU MARATHON HAPO 08-12-2013 PALE LEADERS CLUB.

NINAONA WAZI KWAMBA SASA IPO HAJA HATA  KWA MAKAMPUNI MBALIMBALI YAKAMTUMIA FRNCIS CHEKA KATIKA SHUGHULI ZAO MBALIMBALI ZA KIJAMII NA HATA KUWATANGAZIA BIASHARA ZAO.

KWA KWELI HIZI NI MBIO AMBAZO ZINAPASWA KUUMGWA MKONO NA KILA MTANZANIA NA SIYO WANARIADHA PEKEE ,KWANI HAYATI BABA WA TAIFA HILI MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE ALIUPIGANIA UHURU WA NCHI HII KWA MASLAHI YA WATANZANIA WOTE, BILA KUJALI ITKADI ZA KIDINI, ZA KIMICHEZO ,NA HATA UKABILA.

NI JAMBO LA KUTIA MOYO KWAMBA WAMEJITOKEZA WATANZANIA WENYE NIA NJEMA KABISA YA KUUENZI UHURU WA TANGANYIKA KWA NJIA YA MICHEZO [KAMA HAWA WAANDAAJI WA UHURU MARATHON].

NI LAZIMA TUWAUNGE MKONO WAANDAAJI HAWA KWA HALI NA MALI ILI TUUENZI VYEMA UHURU WETU.

NINATUMIA FURSA HII KUWAOMBA MABONDIA WENGINE NA WADAU WA MCHEZO WA NGUMI  WAJIUNGE KWENYE MBIO HIZI KWA LENGO MOJA TU NALO NI KUUENZI UHURU WA NCHI YETU ,KWANI BILA KUWA NA UHURU KTK NCHI YOYOTE , WAZALENDO WA NCHI ILE HUWA HAWANA TOFAUTI NA WATUMWA,KWANI WANAKUWA HAWANA MAAMUZI YAO BINAFSI ,KWA KUWA KILA JAMBO HUAMULIWA  NA WATAWALA WAO BILA KUJALI JAMBO NI ZURI AU BAYA.

KWA KUWA WAANDAAJI WAMETUTANGAZIA KUPITIA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI KWAMBA KUNA MATAIFA ZAIDI YA 21 YAMETHIBITISHA KUSHIRIKI KATIKA UHURU MARATHON ,PIA MHESHIMIWA RAIS,NA WABUNGE , WAMETHIBITISHA USHIRIKI WAO,SIONI KWA NINI WATANZANIA WA KAWAIDA TUSISHIRIKI KATIKA TUKIO HILI LA KIHISTORIA LA UHURU MARATHON.

PIA NINAYAOMBA MAKAMPUNI MBALIMBALI YAZIDHAMINI MBIO HIZI ZA UHURU MARATHON KILA MWAKA ,NA ISIWE MWAKA HUU PEKEE.

NINA IMANI KUBWA SANA KWAMBA WATANZANIA WENGI TUTASHIRIKI MBIO HIZI ZA UHURU MARATHON SIKU HIYO YA TAREHE 08-12-2013 PALE LEADERS CLUB.


              MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE ,NA UDUMISHE UHURU NA AMANI NCHINI KWETU TANZANIA.


                                        IMELETTWA KWENU NAMI;-
                                       YASSIN ABDALLAH -USTAADH
                                       RAIS; TPBO-LTD
                                     +255 713-644974 752 335584

CHEKA KUTETEA TAJI LA WBF APRIL 2014


 1. 22 November 2013
 2.  
 3. Attention:  Mr Kevin Luandes/Mr Yassin Abdallah
 4.  
 5. SANCTION APPROVAL:  FRANCIS CHEKA V TBA
 6. WORLD BOXING FEDERATION WORLD SUPERMIDDLEWEIGHT TITLE – APRIL 2014
 7.  
 8. Dear Sirs
 9.  
 10. This is to confirm that the World Boxing Federation, www.worldboxingfederation.net has officially approved and sanctioned the WBF first world title defense of champion, Francis Cheka against an opponent to be approved by the sanction committee of the WBF.
 11.  
 12. Mr Kevin Luandes has been approved to promote such a defense conditional to the fight taking place before the end of April 2014, and subject to the rules and regulations of the WBF.
 13.  
 14. All sanction fees must be paid in full and in reflect in the WBF account no later than 3 weeks prior to the staging of this fight.  Failure to comply with this may result in the WBF withdrawing its sanction for this fight.
 15.  
 16. The officials assigned to this WBF world title fight are:  Supervisor:  President of the WBF Howard Goldberg, Referee:  Darryl Ribbink, Judges Edward Marshall and two Tanzanian judges.
 17.  
 18. Howard Goldberg
 19. President WBF
 20.  
 21. 00 27 21 5510896
 22. 00 27 845814612
 23. ironfistpro@iafrica.com
 24. manic@iafrica.com
 25. Skype:  wbfpresident
 26. www.worldboxingfederation.net
 27.  
 28.  

Saturday, November 23, 2013

MANNY PACQUAIO AMFANYIA KWELI BRANDON RIOS

Pac Is Back: Manny Manhandles Bam Bam
Bondia Manny Pacquiao  kulia akimrushia konde bondia Brandon Rios wakati wa mpambano wao uliofanyika china manny pacquaio ameshinda kwa point 120-108, 119-109, 118-110 na kumfanya aibuke na ushindi katika mpambano uho uliokuwa wa raundi 12

Friday, November 22, 2013

BONDIA OMARI KIMWERI LION BOY ASEMA YUPO FITI KUNYAKUWA UBINGWA WA DUNIA


OMARI KIMWERI KUGOMBANIA UBINGWA WA DUNIA WA WBC KWA MARA YA KWANZA MTANZANIA

Mpambano huo utakaopigwa nchi ya China   November 30  na bingwa wa dunia wa uzito huo nchini china 
xiong zhao zhong ni bingwa wa dunia WBC minimum weight ambaye anashikilia taji hilo kwa sasa katika uzito huo

Kimweri anakuwa mtanzania wa kwanza kuwania taji kubwa kabisa Duniani akitokea nchini Austalia uku sapoti kubwa akitegemea kutoka Tanzani ambapo alipo zaliwa


na kigezo cha kufanya apate pambano hilo kubwa ni kutokana na rekodi yake pamoja na kutakiwa mtu ambaye anatokea bara la Afrika ambapo kula imemdondokea bondia Omari Kimweri kwa mara ya kwanza mtanzania huyo ataonekana Dunia nzima akijaribu kuwania ubingwa wa WBC 


Omari Kimweri kwa sasa yupo katika mazoezi  ya  mwisho ya kujiandaa na mpambano huo amesema kuwa yeye bindafsi yupo tayali kabisa kwa mpambano huo kwani yeyey pia ni bingwa na katika kuzihirisha hilo ameomba watanzania waendelee kumuombea kwani uwakika wa yeyey kunyakuwa ubingwa huo ni mkubwa sana aliongeza kwa kusema ubingwa huo baada ya kuunyakuwa atakuja nchini Tanzania ili kuwaonesha mkanda huo wa ubingwa wa Dunia mana ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote 
 huku akitegemea zaidi duwa za watanzania kwa kuwa ushindi wake ni ushindi wa watanzania wote Mungu Ibariki Tanzania Mungu Mbariki Bondia Omari Kimweri

Thursday, November 21, 2013

NGUMI KUPIGWA IJUMAA MOROGORO


Na Mwandishi Wetu, Morogoro
MAPAMBANO zaidi ya sita ya ngumi za kulipwa yanatarajiwa kufanyika Ijumaa, wiki hii, katika ukumbi wa Yohana Pub ulioko maeneo ya Msamvu, katika Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza na mtandao huu, msemaji wa mapambano hayo ambayo awali yalipangwa kufanyika Novemba 24 kabla ya kurudishwa nyuma, Mohamed Jeilan alisema maandalizi yanakwenda vizuri na kwamba mabondia wote watakaopanda ulingoni wapo katika mazoezi makali.

Jeilan alisema lengo la mapambano hayo yanayosubiriwa kwa hamu kubwa mjini Morogoro, ni kuibua vipaji vya mabondia chipukizi na kuendeleza mchezo huo kiujumla.

Alisema mbali ya mabondia wa Morogoro, mabondia wachache kutoka jijini Dar es Salaam pia wanatarajiwa kualikwa kwa lengo la kutoa changamoto katika mapambano hayo.

“Kimsingi maandalizi yanakwenda vizuri na mabondia wote hivi sasa wanaendelea kujinoa chini ya makocha wao ili kuhakikisha wanafanya vizuri siku hiyo”, alisema.

Msemaji huyo amewataja baadhi ya mabondia watakaopanda ulingoni siku hiyo kuwa ni George Masawe ‘G Mawe’, Athuman Dame, Miraji Abdallah ‘Kinditi One Power’, Salum Saleh ‘Sure Boy’, Beta Kingalu na Ngoda Stopa.

Jeilan ametoa wito kwa mashabiki wa mchezo wa ngumi mkoani hapa kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya Ijumaa katika ukumbi huo ili kushuhudia mapambano hayo.

“Mapambano yatakuwa makali sana na yenye upinzani wa hali ya juu hivyo napenda kutoa wito kwa mashabiki wa ngumi kujitokeza kwa wingi ili kushuhudia jinsi gani ngumi zinavyopigwa”, alisema

BONDIA KALAMA NYILAWILA AWAASA MABONDIA KUACHA USHILIKINA


BONDIA Kalama Nyilawila 
BONDIA  Karama Nyilawila amewataka mabondia wa Tanzania kuacha imani
za kishirikina na badala yake wafanye mazoezi  ili waweze kufikia mafanikio.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nyilawila alisema  hapendezwi na
vitendo hivyo kwani vinauwa viwango vya michezo nchini.
Alisema mabondia wanatakiwa wasiamini kabisa na kwamba wamekuwa
wakifanya mambo hayo wanapoenda kupambana nje ya nchi.
Nawasihi waachane na imani za kishirikina kwani wanapokwenda huko
huishia kupigwa kwa KO ila naamini wakizingatia mazoezi yatawasaidia
kufanya vema,"alisema.
Alisema mazoezi pekee ndiyo yatakayomsaidia bondia kushinda pambano
lake na si kwenda kwa mganga na kumpa nguvu za giza na badala yake
jitihada zake binafsi  ulingoni ndizo zitakazomfaa.
Alisema watu wasitafute mchawi  aliyesababisha Tanzania isifanye vema
kimataifa kwani wachawi ni wanamichezo wenyewe na wengi wamekuwa
wakiamini imani hizo.
Nyilawila alisema kwa sasa yupo katika mazoezi makali chini ya meneja wake
Seleman Zugo na kwamba  amejipanga kushinda mapambano yake yote yaliyopo mbele yake kwa KO raundi za mwanzoni ambambo hivi karibuni bondia huyo alimshinda kwa K,O  ya raundi ya kwanza bondia Kaminja Ramadhani mpambano ulioandaliwa na Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi  Rajabu Mhamila 'Super D' uliofanyika

NOVEMBA 10

 katika ukumbi wa Zulu Paradise pugu kilumba

TANGAZO LA UPATIKANAJI WA VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI

VIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD  ZA MAFUNZO SASA  ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam TanzaniaVIFAA VYA MCHEZO WA NGUMI PAMOJA NA DVD  ZA MAFUNZO SASA  ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU 0713406938 Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times
Email.superdboxingcoach@gmail.com
mhamila1@gmail.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mob;+255787 406938
+255774406938, +255713406938
Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

BAADA YA KUPATA UBUNGE BONDIA Vitali Klitschko ‘Dr. Ironfist’ SASA ATAMANI URAISKlitschko: Nina kiu ya Ikulu
MIAKA ya hivi karibuni wanamichezo na wasanii nchini ikiwamo na wale wa nje ya nchi wamezinduka wakijitosa kwenye masuala ya kisiasi kama udiwani, ubunge, ugavana na hata ngazi ya juu ya urais. 
Leo katika maisha ya wenzetu tutaangazia maisha ya ya mbabe Vitali Klitschko ‘Dr. Ironfist’ bingwa wa uzito wa juu wa WBC, aliyetangaza azma yake kuwania urais wa nchini Ukraine katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Katika taarifa yake na wanahabari anasema: “Nahitaji kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015, hakuna anayeweza kunizuia kugombea,”
Klitschko (42), anasema: “Ingawa nimekuwa nikiishi nchini Ujerumani, kwangu naona hilo si tatizo la kunizuia kuwania urais wa nchi hiyo kwa mujibu wa Katiba kwani ninabaki kuwa raia wa Ukraine.”
Mbabe huyo yuko katika rekodi ya wababe wa uzito wa juu wanaotambuliwa na WBO kwa kufanikiwa kutwaa mikanda mitatu ya ubingwa wa dunia, wengine wakiwa Muhammad Ali, Evander Holyfield na Lennox Lewis.
Usichokijua
Mbabe huyo mwaka 2006 aliwahi kuwania umeya wa Kiev lakini alijikuta akibwagwa na mwaka 2008 alifanikiwa kutwaa umeya wa halmashauri ya Kiev.
Mwaka jana alifanikiwa kuwa mbunge wa Bunge la Ukraine kupitia chama cha UDAR.
Mwaka 2005 wakati akimchapa Hashim Rahman na kutwaa ubingwa wa WBC alitangaza kustaafu mchezo huo,  lakini Januari 24, 2007 alitangaza kurejea upya.
Ndiye mbabe ambaye anatarajiwa kubadili mawazo ya Lenox Lewis ya kustaafu, kutokana na hivi karibuni Lewis kutangaza kwamba iwapo atatokea mdhamini mwenye dola milioni 100 za kumlipa ataingia kucheza na Vitali.  
Mahusiano
Mbabe huyo na mkewe Natalia Egorova aliyekuwa mwanariadha na mwanamitindo wamebarikiwa kuwa na watoto watatu ambao ni Yegor (Daniel), Elizabeth (Victoria) na Max.
Utajiri
Mbabe Vitali Klitschko anamiliki utajiri unaofikia dola milioni 65; fedha ambazo nyingi zake amezipata kupitia masumbwi, siasa na nyingine katika matangazo ya kampuni ya Ambergo na kampuni ya Shiatzy Chen na kuna wakati alikuwa akivaa nguo ya chini yenye nembo ya D-Star 200.
Vyakula
Mbabe huyo anatumia kiasi cha dola 20 kwa siku kwa ajili ya chakula anachokuwa anakula. Ikiwa ni kaa, mbogamboga na vingine vyenye asili ya Ukraine.
Usafiri
Ana magari kama Cadillac Escalade alilonunua kwa dola 75,000 na pia anayo nyingine inayokwenda kwa jina la 4Porsche Carrera GT aliyonunua kwa dola 440,000.
Nyingine ni Lexus LS 460 Sedan alilonunua kwa dola 60,000. Mercedes-Benz S65 lilomgharimu dola 210,000.
Jengo
BONDIA huyo anamiliki jengo lake katika maeneo ya Berlin, Ujerumani, likiwa limemgharimu kiasi cha dola milioni 11.
Jengo lake jingine liko Ukraine likiwa katika maeneo ya Kiev likiwa limemgharimu kiasi cha dola milioni 5.
Mawasiliano
Kwa masuala ya mawasiliano ya mwanamasumbwi huyo unatakiwa kutembelea website yake ambayo ni www.klitschko.com/vitali.
Wasifu
JINA: Vitali Volodymyrovych Klychko
UZITO: Futi 6 inchi 7
TAIFA: Ukraine
UMRI: 42
Makala hii imeandaliwa na Shabani Matutu kwa msaada wa mitandao.

Sunday, November 17, 2013

YASSIN ABDALLAH AJITOKA KATIKA TUZO BAADA YA KUKOSEKANA KWA JINA LA SUPER D KWENYE ORODHA

YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                                   RAIS -TPBO                               
           taarifa rasmi-vyombo vya habari-michezo.
                       yah;- kujiondowa kuwania TUZO ya boxing award

ninayo hashima kwenu kuwafahamisha yafuatayo;

hivi karibuni kumekuwepo na taarifa ambazo zimetolewa na watu wenye nia njema kabisa ya kutaka kuuenzi mchezo wetu wa masumbwi ya kulipwa na ya ridhaa kwa kujaribu kuwapatia TUZO wanamasumbwi [mabondia] wa pande zote mbili.

lakini inaelekea wale ambao walipelekewa wazo hili hawana nia njema ya kutaka jambo hili lifanikiwe.


kwani kabla ya hata kura zenyewe kuanza kupigiwa washindani ofisi zetu za TPBO tumekuwa tukiletewa malalamiko kutoka kwa baadhi ya mabondia ambao wameachwa kuorodheshwa nan hata wadau wengine pia wameachwa na kuingizwa watu ambao hawastahili ,huu ni ubaguzi ambao sidhani kama ni lengo la waandaaji wa TUZO hizi,.niewasilisha malalamiko hayo kwa wahusika ,nao wanarushiana mpira kwamba ni kiongozi wa juu wa pst ameondowa baadhi ya majina waliyoyaweka katika orodha.


niejaribu kusoma kwa undani sana orodha ya majina ambayo nimetumiwa  ya wanaoshindanishwa katika TUZO hizo,wamo waandishi wa habari ambao TPBO inadhani wana haki ya kupewa tuzo bila kushindanishwa kwa kuwa wao ndiyo wameufanya mchezo wa masumbwi kujulikana sana miaka hii baada ya kuzimia kwa miaka takribani 7 ya nyuma kutokana na viongozi wabinafsi , ambao bado wanataka kuuingiza katika TUZO hizi.


mfano unapoyaandika majina ya watangazaji wa chombo kimoja cha habari [TV REDIO AU GAZETI na ukamuacha mmoja wao kushindania TUZO hii je huoni kama huutambuwi mchango wake ,na tayari umeshajenga matabaka kazini kwake?


nimeshtushwa sana nilipoliona jina langu la yassin abdallah ustaadh,limo kwenye kuwania tuzo ya kiongozi bora,halafu naangalia wanowania tuzo kwa upande wa waamuzi na majaji sioni jina la referii au jaji hata mmoja  kutoka TPBO ina maana hao waliowasaidia waandaaji kuwapatia majina hawawajuwi waamuzi wa tpbo au ndiyo ubaguzi?


nimeangalia pia katika 0rodha ya waandishi sijaliona jina la SUPER D COACH [Rajabu Mhamila]
  ambaye ana miliki mtandao wa habari za masumbwi wa  www.superdboxingcoach.blogspot.com  
mtandao huo umekuwa ukitujuza habari mbalimbali za masumbwi za ndani na nje ya nchi hii

bado najiuliza tena hivi hao waliowasaidia waandaaji wa TUZO hii hawamjuwi SUPER D COACH au hii TUZO imeshafanyiwa hila za kuwatenga watu muhimu katika BOXING? NANI ASIYEJUWA MCHANGO WA SUPER D KATIKA NGUMI ZA KULIPWA,NA NGUMI ZOTE KWA UJUMLA HAPA, NCHINI TANZANIA ? MPAKA ASAHAULIWE KIASI HIKI


KWA MAELEZO HAYA PEKEE INAONYESHA NI JINSI GANI WATU WANAOJIITA VIONGOZI WA NGUMI ZA KULIPWA WANAVYOTAKA KUVURUGA DHAMIRA NJEMA YA WAANDAAJI WA TUZO HIZI KWA KUWABAGUWA WATU KWA CHUKI BINAFSKI.


UAMUZI WANGU BAADA YA HAYO YOTE NINALIONDOWA JINA LANGU RASMI KUWANIA TUZO HIZI PAMOJA NA SABABU ZIFUATAZO;-


[A]TPBO-LIMITED NI KAMPUNI KUBWA [search google] NA MIMI PIA NINAYO HESHIMA KUBWA KWA WATANZANIA KWA KAZI NINAZOWAFANYIA ,HIVYO SIKO TAYARI KUSHINDANISHWA KATIKA TUZO AMBAZO HAZINA VIGEZO VYA KUSHINDANIA.


[B] TPBO-LIMITED SIYO MIMI PEKE YANGU BALI NI PAMOJA NA WAAMUZI NA VIONGOZI WENGINE PIA.


[C] TPBO-LIMITED HAIKO TAYARI KUONA WATU WANATUMIA FURSA HII YA TUZO KUPENDEKEZA MAJINA KWA LENGO LA KUWABAGUWA WENGINE KWA FANI MOJA WAZIFANYAZO NA ZINAZOFANANA.KWA SABABU ZISIZOELEWEKA.


[D] TPBO-LIMITED INAHESHIMU SANA WAZO LA WAANDAAJI WA TUZO HIZO, LAKINI HAIHESHIMU KABISA MFUMO ULIOTUMIWA NA VIONGOZI WA NGUMI WALIOPENDEKEZA MAJINA YA MABONDIA NA WADAU WENGINE ,KWANI YANAANZA KULETA MALUMBANO YASIYO YA LAZIMA.


[E]TPBO-LIMITED BILA KUBAGUWA ITAWAPATIA HATI WADAU WOTE WALIOACHWA  KWA CHUKI BINAFSI AKIWEMO SUPER D COACH KWA KUTAMBUWA MICHANGO YAO MIKUBWA WALIYOITOWA KATIKA NGUMI ZA KULIPWA.

                                AHSANTENI SANA
                             IMELETWA KWENU NAMI
                    YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
                                   RAIS -TPBO

MABONDIA WA TANZANIA WACHEZEA VICHAPO RUSSIA

Ramadhani Shauri
MABONDIA waenderea kuchezea vichapo nje ya nchi ambapo bondia

Ramadhani Shauri kapigwa na Roman Andreev wa Russia kwa k,o raundi ya 7

na Nassibu Ramadhani kapigwa na Nikolay Potapov kwa point

na Thomas Mashali kachezea kichapo kutoka kwa Arif Magomedov wa Russia ko ya raundi ya pili

na bondia Alphonce Mchumiatumbo alipata kipigo kutoka kwa Ruslan Semenov raundi ya 4

Friday, November 15, 2013

MABONDIA WA TANZANIA WACHEZEA KICHAPO CHA K,O AUSTRALIA

KASEBA
 BONDIA Joseph Kaseba  amechezea kichapo kwa kupigwa na Jeremy Van Diemen  wa  Australia, kwa K,O ya raundi ya pili mpambano uliofanyika Metro City, Northbridge nchini Australia 
 nae bondia Jonas Segu alichezea kichapo cha K,O ya raundi ya 5 katika mpambano uliok
uwa wa raundi 6 wakati wa mpambano wa utangulizi michezo ya nchi za nje imekuwa chachu na kuwapatia mabondia wengi nchini kusafili kwenda nchi mbalimbali kwa ajili ya kushiliki mashindano ata hivyo tangia mwaka huu uanze akuna bondia aliyekwishawai kurudi na ushindi nchini kutokana na viwango vyao kuwa vidogo kimchezo na kuto pata sapoti wanapoenda kushiliki mashindano hayo  na taifa wakati wakienda kushiriki michezo hiyo ya masumbwi nje ya nchi


Tuesday, November 12, 2013

MASHINDANO YA NGUMI YA gurudumu la olimpiki YAFIKA TAMATI


Bondia  COSMAS  PETER kulia
 FAINALI
  WATOTO
  Jumanne  Salehe    WA  NDAME
  alimshinda kwa  points  Hamis  Mrisho
  wa  URAFIKI
  INNOCENT  HERMAN  WA  URAFIKI
  ALIMSHINDA  CLAUD  USWEGE  WA
  FUNUAFUNUA  KWA  RSCH
  Issa  Jumanne
  wa   ushirikiano  alipoteza
  kwa  points  dhidi  ya  STEVEN
  ANASTAZIA  WA  NDAME
  WAKUBWA
  UZITO  WA  KILO  49  LIGHTFLY
  MOHAMED  MZERU  WA  JKT
  ALIMSHINDA  KWA POINT  HAJI  SAID
  WA  NDAME

UZITO  WA  KILO  52  FLY

  COSMAS  PETER  WA  JKT  ALIMSHINDA
  KWA  POINTS  JULIUS  THOMAS  WA
> NDAME
>
> UZITO WA  KILO  56  BANTAM
> FRANK  NICHOLUS  WA   JKT
> ALIMSHINDA  KWA  POINTS  CHACHE
> THOMAS  SONNY  WA
> MMJKT
>
> UZITO  WA KILO 60 LIGHTWEIGHT
> ALEX  MICHAEL  WA  MMJKT
> ALIMSHINDA  YOUSOF  SAID  WA JKT
>
> UZITO  WA KILO  64 LIGHTWELTER
> SEIF  RASHID  WA  URAFIKI
> ALIMSHINDA  ABDALLAH NASSOR  WA USHIRIKIANO
 
 KWA RSO

  UZITO  WA  KILO  75  MIDLLE
  IBRAHIMU  TAMBA  WA  NDAME 
  ALIMSHINDA  KWA  POINTS  HAMID  KHALFAN
WA  JKT

  WACHEZAJI  BORA
  WATOTO  JUMANNE  SALEHE  WA  NDAME 


  WAKUBWA ALEX  MICHAEL WA  MMJKT

  WANAWAKE  SARA  ANDREW

  Mashindano  hayo  yaliudhuliwa  na 
  promoter  wa  kimataifa JAY MSANGI  na 
  alifurahi  kuona  viwango  vizuri 
  ambavyo vikiendelezwa  TANZANIA  inaweza 
  kupata  mafanikio  katika  michezo 
  ya  kimataifa.

  pia  wachezaji  waliochaguliwa  katika 
  GURUDUMU  LA  OLIMPIKI  watatangazwa 
  mwishoni  mwa  mwezi  wa  NOVEMBER

Sunday, November 10, 2013

MABONDIA SAID MBWELWA AMSAMBALATISHA SHABANI KAONEKA NA KALAMA NYILAWILA AMKALISHA KAMINJA RAMADHANI RAUNDI YA KWANZA

Bondia Said Uwezo kushoto akipambana na Sindano Paul  wakati wa mchezo wao uliofanyika jumapili katika ukumbi wa Zulu paradaise pugu kulumba Dar es salaam uwezo alishinda kwa point mpambano huo Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Refarii Saidi Chaku katikati akimnyosha mkono juu bondia Said Uwezo baada ya kumshinda kwa point mpinzani wake

Mabondia Kaminja Ramadhani kushoto na Kalama Nyilawila wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili Kalama alishinda kwa K,o ya raundi ya kwanza Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Twalibu Mchanjo kushoto akipambana na Mohamed Kashinde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili Mchanjo alishinda kwa K,o ya raundi ya tatu katika mpambano uho uliokuwa wa kusisimua picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Shabani Kaoneka Kushoto akipambana na Saidi Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika jumapili Mbelwa alishinda kwa K,O ya raundi ya kwanza baada ya kumkalisha chini kwa konde kali na kushindwa kuendelea  picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Shabani kaoneka akiwa chini oi uku akiesabiwa na refarii kulia ni mpinzani wake Said Mbelwa akimsubili kwa hamu hata hivyo mbambano huo ulisha hapo hapo na mbelwa kufanikiwa kushinda kwa k,o ya raundi ya kwanza picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Saturday, November 9, 2013

MABONDIA SAID MBELWA , SHABANI KAONEKA WAPIMA UZITO KUPAMBANA KESHO JUMAPILI NOVEMBA 10 PUGU KILUMBA

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi ambaye ni mratibu wa pambano hilo Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwainua mikono juu mabondia Shabani Kaoneka Kushoto na Said Mbelwa baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Novemba 10 siku ya jumapili katioka ukumbi wa Zulu Paradies Pugu Kilumba kesho picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Kaoneka kushoto na Said Mbelwa kulia wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito katikati ni mratibu wa mpambano huo Rajabu Mhamila 'Super D'
Bondia Said Mbelwa akipima uzito kushoto ni mpinzani wake Shabani Kaoneka na kulia ni mratibu wa mpambano huo Rajabu Mhamila Super D' mpambano utakaofanyika jumapili ya novemba 10 katika ukumbi wa Zulu Paradies pugu kilumba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Shabani Kaoneka akipima uzito kwa ajili ya mpambano huo kushoto ni mpinzani wake said Mbelwa na kulia ni mratibu wa mpambano huo Rajabu Mhamila 'Super D' pICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com

Friday, November 8, 2013

KALAMA NYILAWILA KUZIPIGA NA KAMINJA RAMADHANI JUMAPILI NOVEMBA 10


BONDIA Kalama Nyilawila akifanya mazoezi kabla ya mpambano wake na Kaminja Ramadhani picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com


BONDIA Kalama Nyilawila atapanda ulingoni jumapili ya novemba 10 katika ukumbi wa Zulu Paradise pugu kilumba kupambana na Kaminja Ramahani mpambano huo wa Raundi 6 utakaopigwa kabla ya mpambano mkubwa 

kati ya Shabani Kaoneka 'BSS' na Said Mbelwa 'Moto wa Gesi' awajaoneshana kazi katika mpambano wao wa raundi 8 

akizungumzia mpambano huo kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini ambaye ni mratibu wa mpambano huo Rajabu mhamila 'Super D' amesema mpambano huo ni mahususi kwa wakazi wa vitongoji vya pugu ,chanika,ilala na jiji la Dar es salaam kwa ujumla 

utakaowakutanisha mabondia mbalimbali ambapo watapigana katika mapambano ya utangulizi bondia Chirambo Hemed atavaana na Sharif Mzezele uku Adamu Ngange akioneshana kazi na Shabani Mtengela 'Zunga Boy' ,Hamza mchanjo atamenyana na Tonny King mpambano mwingine utawakutanisha Twaribu Mchanjo atakaepambana na Mohamed Kashinde,Said Uwezo na Sindano Paul

Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo huo vitakaokuwa vikitolewa na Super D kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha ngumi maeneo ya Pugu Kilumba