BONDIA  Karama Nyilawila amewataka mabondia wa Tanzania kuacha imani 
za kishirikina na badala yake wafanye mazoezi  ili waweze kufikia mafanikio.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Nyilawila alisema  hapendezwi na 
vitendo hivyo kwani vinauwa viwango vya michezo nchini.
Alisema mabondia wanatakiwa wasiamini kabisa na kwamba wamekuwa 
wakifanya mambo hayo wanapoenda kupambana nje ya nchi.
Nawasihi waachane na imani za kishirikina kwani wanapokwenda huko
Nawasihi waachane na imani za kishirikina kwani wanapokwenda huko
huishia kupigwa kwa KO ila naamini wakizingatia mazoezi yatawasaidia 
kufanya vema,"alisema.
Alisema mazoezi pekee ndiyo yatakayomsaidia bondia kushinda pambano 
lake na si kwenda kwa mganga na kumpa nguvu za giza na badala yake 
jitihada zake binafsi  ulingoni ndizo zitakazomfaa.
Alisema watu wasitafute mchawi  aliyesababisha Tanzania isifanye vema 
kimataifa kwani wachawi ni wanamichezo wenyewe na wengi wamekuwa 
wakiamini imani hizo.
Nyilawila alisema kwa sasa yupo katika mazoezi makali chini ya meneja wake 
Seleman Zugo na kwamba  amejipanga 
kushinda mapambano yake yote yaliyopo mbele yake kwa KO raundi za 
mwanzoni ambambo hivi karibuni bondia huyo alimshinda kwa K,O  ya raundi
 ya kwanza bondia Kaminja Ramadhani mpambano ulioandaliwa na Kocha wa 
kimataifa wa mchezo wa masumbwi  Rajabu Mhamila 'Super D' uliofanyika 
 
No comments:
Post a Comment