Tangazo

Pages

Thursday, June 12, 2014

mafunzo kwa waamuzi wa ngumi za kulipwa

             taarifa kwa vyombo vya habari-michezo
                        ------------------------------
YASINNI ABDALAH 'OSTADHI' AKIMPONGEZA IBRAHIMU CLASS
---------
          ndugu zangu katika michezo ninayo raha tele kuwajulisheni yafuatayo.

         kwa kuwa mchezo wetu wa ngumi za kulipwa tayari umeshakubalika na kujizolea mashabiki wengi hivi sasa nchini tanzania kote,

oganaizesheni yetu ya ngumi za kulipwa nchini tanzania[TPBO-LTD] kwa kushirikiana na shirikisho la masumbwi ya kulipwa nchini tnzania[PST] Tunaandaa mafunzo kwa ajili ya kupata waamuzi zaidi wa ngumi za kulipwa nchini tanzania.MAFUNZO HAYA YATAENDESHWA NA MKUFUNZI -MTAALAMU NDG EMAUEL MLUNDWA AMBAE AMESHAWAFUDISHA WAAMUZI KARIBU WOTE WA AFRIKA MASHARIKI ,wakati  wakiunda mashirikisho yao ya ngumi za kulipwa nchini mwao.

tunafikia maamuzi haya baada ya kuona kwamba majukumu yametuelemea sana ,kama mjuavyo niTPBO NA PST pekee ambao tumeubeba msalaba mzito wa kuhakikisha kwamba mchezo wa mgumi za kulipwa nchini unaendeshwa vizuri bila migogoro ili mabondia wa kulipwa ambao kwa kawaida na uhalisia wa ukweli kazi yao kubwa ni kupigana ulingoni, na wao kama ilivyo kote duniani hawapaswi kuwa wanachama wa chama chochote cha kusimamia ngumi za kulipwa.

mabondia wanapaswa kupewa mapambano na kampuni yoyote ya masumbwi, na ndiyo maana ukaona FLOYD MONEY MAYWEATHER anahodhi mataji ya mashirikisho mbalambali ya ngumi ya dunia yakiwemo WBC ,WBA,IBF,NA HATA WBO.kwa sababu hakuna chama chochote kinachomkataza kupigania mataji ya chama kingine kwa juwa siyo mwanachama wa chama chochote kati ya hivyo.

hivyo hivyo kwa mabondia wote wa nchi zote wao siyo wanachama wa chama chochote .hivyo wanalopaswa wao ni kuwa leseni tu za kuhifadhia rekodi zao kutoka mashirikisho wanayopenda wao ,na pengine hata yote .

mafunzo hayo tunatajia kuyafanya mwishoni mwa mwezi wa sita ,na yatajuwa ni ya vitendo , pia yatakuwa ya siku 3,kwa maana ya kwamba utafungwa ulingo na vijana watapambana na waamuzi watafundishwa ,jinsi gani point bondia anapata awapo mchezoni na masomo ya ubaoni yatapewa nafasi kubwa sana na waamuzi watauliza ,maswali kama mwanafunzi yeyote awapo darasani. na watakaofuzu watapewa vyeti na wataombewa nafasi ya kuchezesha mapambano nje ya nchi.

Kuwa na waamuzi wengi kutatusaidia pia kuondowa tatizo hili,hebu hata ndg waandishi fikirieni ;-kwa mfano TPBO inao  waamuzi6 [sita]tu na lipo pambano dar-es-salaam na songea inakuwaje? .hali ni hiyo hiyo tene kwa washirika wetu PST ?

Ni budi kwa uchache  kila upande uwe na waamuzi kumi na mbili wenye ujuzi wa kutosha na ufahamu wa hali ya juu ili kuweza kukabiliana na changamoto mabalimbali zitokezapo mchezoni.


HILI NI JAMBO LA MUHIMU SANA KWETU NA TUTAJITAHIDI SANA KUWASILIANA NA WADAU WETU KTK NGUMI ZA KULIPWA WAKIWEMO MAPROMOTA NA MAKAMPUNI AMBAYO TUNAFANYA NAYO KAZI ILI WATUPATIE UDHAMINI KATIKA SUALA HILI NYETI.

KAMA MANBO YAKIENDA VIZURI KAMA TUNAVYOTARAJIA MAFUNZO YETU YATAFUNGULIWA NA KIONGOZI WA NGAZI ZA JUU KUTOKA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, VIJANA NA MICHEZO.

                                  AHSANTENI SANA

                            IMEANDIKWA NA KULETWA KWENU NAMI;-
                                YASSIN ABDALLAH -USTAADH

                                    RAIS-TPBO-LTD

No comments:

Post a Comment