Tangazo

Pages

Friday, January 8, 2016

MABONDIA KAONEKA NA MAPAMBANO KUZICHAPA FEB 14 TANDIKA

Mabondia Shabani Kaoneka kushoto akitunishiana misuli na Imani Mapambano baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kupambana feb 14 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe katikati ni mdau wa mchezo wa masumbwi Zahoro Maganga 'Super Diego'  picha na SUPER D BOXING NEWS
Mdau wa mchezo wa masumbwi nchini Zahoro Maganga 'Super Diego'  kushoto akimsainisha bondia Shabani Kaoneka kwa ajili ya mpambano wake na Imani Mapambano feb 14 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe kulia ni Rais wa TPBO Yassin Abdallah
picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu
Mabondia Shabani Kaoneka na Imani Mapambano wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya feb 14  uzito wa kg 74 katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika maguruwe

mpambano huo wa raundi nane utasimamiwa na oganaizesheni ya ngumi za kulipwa TPBO chini ya rais wake Yassin Abdallah 'ostadhi' mpambano huo wenye kugombaniwa kwa kila mmoja kuwa juu ya mwenzie ambapo bondia Kaoneka ni namba 11 katika viwango vya ubora nchini ambapo amepigana mapambano 13 akishinda 5 kupigwa 5 na sale 3

 atakuwa na kibarua kizito cha ku lilia namba yake kwa mtu wa chini yake Imani Mapambano anaeshikilia nafasi ya 12 ya ubora kwa mabondia wa Tanzania akiwa amecheza mapambano 7 akishinda 4 na kupoteza 3

katika mpambano mwingine utawakutanisha mabondia Hassan Mwakinyo atakae pambana na Salumu Salumu kg 72 katika mpambano wa raundi sita 


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile

Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha

No comments:

Post a Comment