Tangazo

Pages

Thursday, September 20, 2012

IBF YAWAPONGEZA WADAU WANAOSAIDIA KUPROMOTI NGUMI TANZANIA/AFRICA

Shirikisho la Ngumi la Kimataifa IBF lenye makao yake makuu katika jiji la New Jersey, nchini Marekani kupitia ofisi zake za Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba za Uarabu na Uajemi linachukua fursa hii kuwapongeza wadu wote wa ngumi wanaosaidia kuuendeleza mchezo huu hapa Afrika.

IBF inachukua fursa hii kuwapongeza wafuatao kwa juhudi zao binafsi katika kuchangia kuuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa: 

Afrika ya Kusini: (Branco Milenkovic). Zambia: (Captain John Chewe, Anthony Mwamba). Zimbabwe: (Richard Hondo), Ghana: (Henry Mann-Spain, Michael Tetteh), Nigeria: (Ken Biddle), Ivory Coast: (John Ajaba). Misri: (Richard Nwoba), Oman: (Amin Saad Bait-Mabrook), Tanzania: Gabriel Nderumaki, Lucas Rutainurwa, Titus Kadjanji, Fidel Haynes, Yassin Abdallah (Ustaadh), Nemes Kavishe, Boniface Wambura, Godfrey Madaraka Nyerere, Shomari Kimbau pamoja na Msajili wa Wizara ya Mambo ya Ndani, BMT, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, BIDCO, Pepsi, Vyombo vyote vya habari vya magazeti, Radio, Television, Blogs na Websites pamoja na wengine wote ambao wamesaidia kwa njia moja au nyingine. 

IBF inaamini kuwa ushirikiano wetu wote utasaidia kuuendeleza mchezo wa ngumi za kulipwa na kuwezakujenga ajira nyingi kwa vijana wan chi zetu.  

Imetolewa na: 

Onesmo Ngowi

Rais,

IBF Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba za Uarabu na Uajemi

No comments:

Post a Comment