Bondia Yusuph Mkali kushoto akitunishiana misuli na Vicent Mbilinyi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho jumamosi ya march 28 katika ukumbi wa manyara parck uliopo tandale ccm Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Chirstopher Mzazi katikaki akiwainua juu mabondia Julius Kisalawe kushoto na Said Uwezo kwa ajili ya mpambano wao wa kesho jumamosi ya march 28 utakaofanyika katika ukumbi wa manyara parck ccm tandale Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Na Mwandishi Wetu
Mabondia Julius Kisalawe kutoka Ndame Clab na Said Uwezo kutoka Mzazi GYM wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa utakao fanyika katika ukumbi wa manyara parck ccm tandale march 28 jumamosi
mpambano uho utakuwa chini ya oganaizesheni ya mchezo wa ngumi za kulipwa T.P.B.O ambapo msimamizi wa upimaji uzito Ibrahimu Kamwe alitoa taharifa kuwa bondia Uwezo alikuwa kazidi uzito na kumfanya apewe mda wa kukata uzito kwa masaa matano zaidi ili afikie lengo lake la kugombanmia ubingwa uho ambao unashikiliwa na Kisalawe
bondia huyo alikata uzito kwa mda unaotakiwa na kurusiwa kuwania ubingwa uho wa kg 52
mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya kusindikiza mtanange uho ambapo bondia kutoka Super D GYM iliyopo shule ya Uhuru Vicent Mbilinyi atapambana na Yusuph Mkali mpambano wa raundi sita ambapo kiingilio katika mpambano uho ni silingi. 5000 tu na wanawake ni bule kabisa
siku hiyo kutakuwa na ulinzi na usalama wa kutosha kwa watu na mali zao
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether,
Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya
juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super
D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa
ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D . -- Super D Boxing Coach Email.superdboxingcoach@gmail.
Mob;+255787 406938
+255774406938
Po.Box. 15493 Dar es Salaam Tanzania
No comments:
Post a Comment