Tangazo

Pages

Friday, November 11, 2011















Jina: Rashid Matumla

Nafasi Yake: Bingwa wa dunia wa uzito wa kati (WBU)
Historia Fupi

Rashid Matumla alizaliwa mkoani Tanga hapo Mei 6, 1968. Aliingia katika masumbwi mwaka 1979 ambapo ameshiriki mashindano mbali mbali kama vile ile ya olimpiki ya Seoul 1988. Amewahi kuwa bondia bora Afrika mashariki na kati hapo mwaka 1990, na mwaka huo huo alikuwa bingwa wa ridhaa Afrika mashariki na kati .

Mwaka 1997 alitwaa ubingwa wa Afrika na kutwaa taji la mabara linalotambuliwa na WBU mwaka huo huo. Mwaka 1998 alitwaa taji la kimataifa WBU na mwaka hou huo alitwaa ubingwa wa dunia wa WBU uzito wa lightmiddle.

Amecheza michezo 24 katika ndondi za kulipwa na ameshindwa mara moja. Kati ya hiyo 14 ameshinda kwa knockout.


Makutano ya Rockers na familia ya Matumla January 1999
"Mafanikio ya akina Matumla ni jitahada za muda mrefu"

Kitu kilichochukuliwa kama burudani ya kawaida na Mzee Matumla miaka mingi iliyopita leo hii kimegeuka kuwa sifa kwa taifa zima la Tanzania. Bondia huyo wa zamani, Mzee Matumla anasema enzi hizo hakukuwa na chama ngumi hivyo mchjezo huo ulikuwa ni kwa ajili ya burudani hasa kwa siku za jumapili huko katika mashamba ya mkonge Tanga.

Lakini mzee huyo alianza kubadili muelekeo wake katika ndondi pale pale alipoanza kuwafundisha watoto wake mchezo huo. Si kwamba wanawe walikuwa wakiupenda mchezo huo ila nia yake ilikuwa ni kuwaepusha na makundi ya kihuni. Hii iliwafanya wawe na nidhamau na taratibu nao walianza kuvutiwa na mchezo huo. "Ilikuwa ikifika Jumapili kila mtu
anakasirika kwani siku hiyo itamaanisha kukimbia sana na mazoezi" anasema bingwa wa dunia Rashid Matumla. Mzee Matumla aliendelea kuwakazania wanae katika masumbwi.
Lengo lake likiwa siku moja nao waje kuliletea taifa la Tanzania sifa, lengo ambalo limetimia hivi karibuni. Mzee Mataumla anasema katika kupata mafanikio ni lazima rasilimali itumike. "Lazima ugharamie mazoezi ili kupata timu nzuri, mimi niliwagharamia sana hawa vijana kimazoezi, vifaa na kuwapa lishe ya kutosha. Kama huwapatii lisha ya kutosha basi hujengi bali unaumiza". Mzee Matumla anaendelea kusema kuwa siri ya mafanikio katika ngumi ni uvumilivu. "Kumbuka umapompata mwenzio, na yeye anakupata, mvumilivu ndiye anashinda". Mzee Matumla anatoa wito kwa viongozi kuitumia vizuri sera ya michezo vizuri, kuzingatia na kuweka mbele maslahi ya wanamichezo katika maandalizi ya awali ili kutoa mabingwa kila wakati. "Kama hujala vizuri, utatetemeka tu".

Mzee Matumla anavutiwa na juhudi za bondia Marwa chni ya promota Madaraka Nyerere na anasema kuwa vijana wengi wakipatiwa nafasi basi taifa litakuwa na mabondia wegi katika nyanja za taifa na kulipwa.

Mzee Matumla anamshukuru sana promota Jamal Malinzi wa DJB Promotions kwa kuwapeleka wanae katika anga za kimataifa. "Mimi niliwafikisha ngazi ya taifa, yeye kawapeleka ngazi ya kimataifa". Hadi leo pamoja na kuwa Rashidi na Mbwana wanashikilia mikanda ya dunia, Mzee Matumla bado hachoki kukagua mazoezi yao wawapo nyumbani. "Nawakazania kuwa tayari wakati wowote kwani anaweza mtu kuja wakati wowote kutaka kuwa challenge, hivyo lazima wawe tayari wakati wote", anamalizia mzee Matumla.

Rashidi Matumla anasema yeye bado hajaridhika kabisa na mafanikio aliyoyapata hivi karibuni. Anasema lengo lake ni kushinda mataji yanayatambuliwa na vyama vingine kama IBF, WBC au WBA. Anasema bidii yake katika WBU itamwenzesha kucheza WBC au WBO.
"Nikiweza kutetea taji hili mara mbili au tatu naweza kuomba kucheza kupitia vyama vingine kama WBC au WBO" anasema Rashid. Anaendelea kusema kuwa katika ngumi kinachohitajika ni nafasi, bila kupewa nafasi ya kupigana hautaendelea wala kutambulika.

Mafanikio ya akina Matumla yanatokana kwa kiwango kikubwa na kocha wao Norman Hlabane wa Afrika ya Kusini. Rashid anasema wanapokuwa Afrika ya kusini huwa wanapata mazoezi mazito sana. Ansema anapokuwa nje ndio anakuwa makini zaidi hivyo hategemei kuweka kambi yake ya mazoezi
hapa Tanzania. Akiwa Afrika ya Kusikni huwa anakuwa na program nzuri ya mazoezi. Hii yote inatokana na kuwa na kocha mzuri na mwenye kuipenda kazi yake. "Kocha wangu ni mtu mkali sana kuhusu mazoezi" anaongeza Rashid. Kocha huyo huwajenga ki boxing na kisaikolojia. "Tukiwa nyumbani tunakuwa kama watoto wake lakini mazoezini anabadilika kabisa". Rashid anamsifia kocha wake kwa kusema kuwa ni mtu makini na ndio maana ametoa mabingwa wa dunia kama watatu auwnne hivi. "Kila siku atakuotoa makosa, ukifanya vizuri anakwambia na vibaya anakwambia". Kutokana na mazoezi ya kocha wake huyo hivi sasa anajisikia nguvu zaidi tofauti na mwanzo ambapo alikuwa mwepesi lakini hana nguvu. "Ukipata mafunzo Afrika ya kusini una uwezo wa kupigana na mtu yeyote duniani", anasema Rashid.

Anavutiwa na mchezo wa Moses Marwa na ndiye bondia ambaye anamuona anaweza kufanya vizuri katika ndondi za kulipwa, pamoja na umri wake. "Mbona Foreman alirudi kama mtu mzima na alifanya mavitu ?" anauliza Matumla.
Kimataifa alikuwa anavutiwa na Mohammed Alli na Sugar Ray Leonard. Hivi sasa anavutiwa na Roy Jones.

Nukuu muhimu
"Huwa sina makeke. Mimi ni wa vitendo sio mtu wa porojo".

"Ubingwa wa dunia haunifanyi nijione tofauti na watu wengine. Ninafurahia heshima ninayoipata kutoka kwa watanzania wenzangu. Hata hivyo mimi bado ni mtu yule yule, naishi kule kuloe nilikokuwa nikiishi, naongea na watu wale wale na natembelea sehemu zile zile".

"Mbwana ni bondia mzuri anaachohitaji ni nafasi tu. Kule Afrika ya Kusini watu walikua wakihama hata Gym kumkimbia. Ni mwepesi sana."

"Mzee wetu alifanya boxing kama elimu. Akiwa off kazini, tulikuwa tunaenda nae mazoezini, wakati mwingine tulikuwa tunamkimbia. Tulikuwa tukiwasikia akina Nassor Michael na Isangura tulitamani kuwa kama wao na baba yetu alikuwa akitupa moyo sana."

"Jioni tulikuwa tunatembea toka klabu ya Simba mpaka nyumbani (keko) kwa miguu na njia nzima anakuwa akitutoa makosa. Ulikuwa unafanya bidii ili nyumbani usikosolewe".











No comments:

Post a Comment