Thursday, February 28, 2013 -
Dar-Es-Salaam, TANZANIA- Siku kubwa na yenye matumaini mapya katika
maisha ya bondia wa Namibai Albinus Felesianu (9(4)-2(1)-0) itawadia
hivi karibuni wakati atakapokutana na bodia Herbert Quartey
(10(7)-8(6)-0) wa Ghana kugombea ubingwa wa IBF wa dunai uzito wa Unyoya
(Featherweight).
Albinus alipata mshtuko mkubwa sana na kushangzwa na habari za hivi
karubunI kuwa IBF imempa nafasi ya kugombea ubingwa wa dunia wa vijana
jambo lililomfanya apate furaha ya ajabu.
Albinus Felesianu
Albinus (kushoto) akifanya
vitu vyake
Mtu pekee atakayeweza kuzima furaha yake na kumfanya asiweze kufikia
malengo yake katika ngumi ni bondia Herbert Quartey kutoka Ghana ambaye
ni moja kati ya mabondia wenye ujuzi mubwa wa kupigana ulingonI.
Kama inavyosemwa kuwa "mtoto mtukutu aliyepotea kwenye ngumi anapoomba
kurudi kundini na kukaa kufuata kanuni na shaeia za ngumi mchezo wa
ngumi humpokea kwa shangwe na nderemo na kumpa mawaidha na ushauri wa
kumwendeleza" ndivyo hivyo hivyo Albinus Felesianu na Herbert Quartey
watakavyopokelewa na ngumi baada ya pambano lao la tarehe 29 Machi
jijini Windhoek, Namibia.
Bondia Albinus Felesianu yuko chini ya promosheni ya Kinda Nangolo
ambaye anamiliki kampuni tanzu ya Kinda Boxing Promotion na ni promota
anayeinukia kwa kasi sana katika tasnia ya ngumi nchini Namibia na
barani Afrika
No comments:
Post a Comment