Tangazo

Pages

Wednesday, October 12, 2011

BONDIA AMIRI KHAN ATAKA KUREJESHA NGUMI WASHINGTON

Khan ataka kurejesha ngumi Washington

WASHINGTON,Marekani

BONDIA raia wa Uingereza Amir Khan, anajiandaa kurejesha masumbwi katika mji mkuu wa Marekani Washington DC atakapopanda ulingoni Desema 10 mwaka huu, kupambana na mpinzani wake mzaliwa wa mji huo, Lamont Peterson.

Hilo litakuwa ni pambano la kwanza kufanyika katika mji huo, baada ya bingwa wa zamani wa uzani wa juu, Mike Tyson kupigwa na bondia Kevin McBride mwaka 2005.

Pambano hilo pia litakuwa ni la kwanza tangu Khan aongeze ushindi wake wa 26-1 alipomshinda kwa KO, bondia Zab Judah, Julai 23  mwaka huu na kutetea mataji yake ya WBA na IBF.

Bondia huyo alikubali kuzichapa na Peterson mjini Washington, baada ya kufanya ziara mara kadhaa mjini humo, ikiwemo ya Septemba 10 mwaka huu ambapo alikula chakula cha usiku White House dinner.

“Tunataka kurejesha ngumi Washington na ili nadhani litakuwa ni pambano la kwanza kati ya mapambano mengi yatakayofanyika mahali hapa,” alisema  Khan, ambaye atakuwa akitimiza miaka 25 siku mbili kabla ya pambano hilo.

No comments:

Post a Comment