Tangazo

Pages

Friday, October 14, 2011

DAVID HAYE ATUNDIKA GLOVE


LONDON, Uingereza
BONDIA David Haye juzi (Juni 13,2011) alitangaza rasmi kustaafu ngumi wakati wa sherehe yake ya kutimiza miaka 31, huku akisema kuwa anataka kitu kimoja, kufunga mdomo wake zaidi na hana nafasi ya kupigana na Vitali Klitschko ambaye aliagiza kambi yake kumshawishi
Nyota huyo ametangaza kustaafu kucheza ngumu baada ya Alhamisi kutimiza umri wa miaka 31, katika pambano lake la mwisho alipoteza dhidi ya Wladimir Klitschko.
Baada ya kuingia katika uzito wa juu, Haye alikuwa akitoa maneno ya kuwaudhi wapinzani wake, ikiwa ni pamoja na kuvaa fulana ambayo inapicha inayomwonesha ameshika vichwa vya mabondi wa familia ya Klitschko, Wladimir na Vitali.
Pia alitoa maneno makali kabla ya mechi yake dhidi ya Audley Harrison kwa kusema itakuwa kama ni ubakaji.
Badala ya kutumia nafasi yake hiyo ya kustaafu kuomba radho kwa maneno yake mabaye alisema kuwa anaweza kuchonga zaidi kama atakuja kupigana tena.
Bingwa huyo wa zamani wa WBA alitetea tabia yake ya kutoa maneno makali akisema kuwa ilisaidia kuleta msisimko kama ilivyokuwa katika mechi dhidi ya Wladimir na Nikolai Valuev ambapo tiketi nyingi ziliuzwa na wengi kuangalia kupitia televisheni kwa kulipia.
Alisema kwa kupiti mchezo huyo imesaidia kukusanya fedha.
Alisema amestaafu kwa kufuata ahadi yake kuwa atapigana kwa miaka 10 kisha kustaafu akiwa na miaka 31.
Alipigwa na Wladimir Julai na kusema kuwa bingwa wa WBC, Vitali amepoteza nafasi ya kupigana naye kwa kutokubali alipotoa ofa hiyo.
Haye alisema awali hakutaka kupigana na yeye ila kurudiana na kama kaka yake Wladimir, alipotoa wazo hilo hakuonekana kukubali.

No comments:

Post a Comment