Tangazo

Pages

Thursday, August 4, 2011

AMIR KHAN ATAKA KUENDELEZA UBABE WA NGUMI DUNIANIBONDIA Amir Khan anaendelea kutafuta mpinzani wake anayefuatia wa kupigana naye katika uzani light welter kabla ya kuhama uzani huo kwenda welter.

Khan, ambaye ni bingwa wa WBA na IBF wa uwani wa light-welter, anataka kuhamia uzani wa welter baada ya Desemba 25 na amekwua na mtazamo wa kupambana na
Floyd Mayweather mwakani, lakini anataka kupata bonsi wa mwisho wa kupigana naye katika uzito aliopo sasa.

Lamont Peterson anaonekana kuwana nafasi ya kuwania mkanda wa IBF baada ya kumtwanga Victor Cayo wiki iliyopita, ingawa Khan anasema kuwa Mmarekani huyo aliwahi ku kataa ofa katika siku zilizopita.

Mpiganaji huyo wa Bolton karibuni alisema Timothy Bradley amekuwa akiogopa kupigana naye.

Bradley, bingwa wa WBO amepokewa mkanda wake wa WBC, alijitoka katika pambano baada ya kukubaliana kwa mdomo, huku Khan akiwa katika ratiba ya kutwangana na Zab Judah ambapo alimpoka ubingwa wa
IBFbaada ya kutwanga raundi ya tano.

Maingine anayetajwa kuwa anaweza kupigana naye ni bondia wa Mexico, Erik Morales,ambaye anajindaa kutwangahna na Jorge Barrioskwa ajili ya kwuani ubingwa wa WBC Septemba.

"Tulitoa ofa ya pambano dhidi ya Peterson miezi sita iliyopita na walikataa," alisema Khan.

"Niko tayari kutwangana na yeyote katika uzito wa light welter, ni kwamba hawataki kupigana na mimi.


Khan alisema hayo wakati akiwa kwenye gym yake mjini Bolton akiwa chini ya kochaJoe Gallagher.

No comments:

Post a Comment