Tangazo

Pages

Monday, August 8, 2011

SUPER D , KINYOGOLI WAENDELEA KUSAKA VIPAJI VYA MCHEZO WA NGUMI NCHINI

KLABU za ngumi za ridhaa za Ashanti na Amana zimewataka vijana wenye vipaji vya mchezo huo kujitokeza kujiunga na klabu hizo ili kuendelezwa vipaji vyao.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha mkuu wa Klabu ya Ashanti Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kutokana na kugundua kuwepo na vijana wenye uwezo mkubwa wa kucheza ngumi na kukosa watu wa kuwaendeleza hivyo wameona ni fursa pekee ya kuwachukua na kuwaendeleza katika Klabu zao.

Alisema, baada ya mkoa wa kimichezo wa Ilala kuanzisha mapambano ya kuhamasisha mchezo huo wameona vijana wengi waliokuwa na moyo wa kutaka kucheza mchezo huo hivyo wameona watoe nafasi kwa vijana hao kujiunga katika Klabu zao.

"Mimi na kocha wa Klabu ya Amana, Habibu Kinyogoli tumeamua kwa nia moja kuiwaendeleza vijana katika ngumi hizi hivyo tumeona tutoe nafasi kwa vijana wenye kipaji cha ngumi kujitokeza kujiunga na klabu zetu bila gharama zozote ikiwa ni kwa lengo la kuendeleza vipaji vyao," alisema Super D.

Alisema, mabondi hao watapata nafasi ya kupambana ulingoni mbele ya mashabiki huku katika mafunzo wakiwa wananolewa na yeye akiwa pamoja na Kinyogoli na Kondo Nassoro ambapo wote ni makocha wa kambi ya mkoa wa Ilala.

Aliongeza kuwa wakiwa ni waanzilishi wa ligi ya kuhamasisha ngumi hizo kwa mkoa wa Ilala wameamua kuendelea kupanua wigo huo kwa kuongeza idadi ya mabondia pia katika klabu zao.

No comments:

Post a Comment