Tangazo

Pages

Friday, August 5, 2011

SUPER D AACHIA DVD TATU ZA KIMATAIFA KUFUNZIA NGUMINa Mwandishi Wetu

Kocha maarufu wa mchezo wa ngumi nchini, Rajabu Mhamila 'SUPER D' aliyeamua kutumia njia ya DVD kuwafundisha watu mbalimbali kujua na kutambua sheria za mchezo huo ameachia kazi nyingine tatu mpya.

Kazi hizo tatu zinausisha mapambano kadhjaaa ya nyota na mabingwa wa ngumi za kulipwa Duniani, ziliachiwa sokoni zaidi ya wiki moja sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Super D, alisema tofauti na kanda yake ya awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa na zikiwa na mchanganyiko wa 'clips' za michezo ya nyota wa Dunia katika kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.

Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe Habibi Kinyogoli.

''katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd pamoja na CD nyingine tatu tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli Foundition '' alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti  pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia watu wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.


Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa timu ya Ashanti na Amana kujifunza 'live' chini ya makocha Habibu Kinyogoli, Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana mbalimbali

--

No comments:

Post a Comment