Tangazo

Pages

Sunday, August 14, 2011

WADAU WA MASUMBWI WAOMBWA KUJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA



WADAU wa mchezo wa masumbwi nchini wameombwa kujiandaa na kuhudhuria kwa wingi mkutano wa wazi wa kimataifa kuhusu mchezo huo utakaofanyika Agosti 18 hadi 21 Lusaka nchini Zambia.

Mkutano huo umedhaminiwa na Muungano wa Vyama vya Ngumi Afrika, unaofahamika kama African Boxing Union (ABU) na kuandaliwa na wenyeji wa mkutano kupitia Chama cha Ngumi Zambia (BBZ).

Akizungumza na Majira kwa simu juzi akiwa mjini Iringa, Makamu wa Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO) ambao ndio waratibu wa mkutano hapa nchini, Dkt. Fistus Luisa alisema utashirikisha pia semina ambao hawana mafunzo ya kutosha.

"Hii ni nafasi kubwa sana kwa wadau wa mchezo wa ngumi barani Afrika kujifunza kupunguza matatizo tuliyokuwa nayo katika kila eneo linalohusu ngumi, tunawaomba wadau wakiwemo makocha, waamuzi, mabondia wa sasa na wazamani na vyama mbalimbali tujiandaae tukashiriki.," alisema.

Alisema kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chama cha ndondi nchini humo gharama za kwenda na kurudi hoteli na matumizi mengine zinafikia kiasi cha dola 600 ambazo ni sawa na 8,40,000 za kitanzania.

Makamu huyo alisema mkutano utahudhuriwa na Rais wa ABU ambaye pia ni makamu wa kwanza wa raisi wa Chama cha Dunia cha mchezo wa ngumi WBC, Hausin Hauchi, Katibu mkuu wa ABU ambaye pia ni Rais wa chama cha ngumi cha Uganda (UPBC), Selestino Mindra.

Alisema TPBO inaratibu maombi ya wadau watakaohudhuria au katika anwani ya chama cha ngumi cha Zambia ambao ni waandaaji ambapo mwisho wa kuthibitisha kushiriki ni Julai 30 mwakja huu.

Akizungumzia mkutano huo Rais wa TPBO, Yassin Abdallah 'Ustaadhi' alisema ni mhimu kwa nchi kama Tanzania kutokana na mchezo huo kuanza kupoteza imani kwa nchi tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

"Tunatambua kuwa watanzania walio wengi hali ya kifedha sio nzuri lakini nawahakikishia mkutano huu ni mhimu sana na watakaothubutu kuhudhuria watakuwa wamepata darasa kiasi kwamba ujuzi wao utaongezeka.," alisema Yassin.

No comments:

Post a Comment